Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Hotuba iliyosomwa Umoja wa Mataifa 1955 imenyambuliwa mle ndani.

Mohamed,
Ungesema hivi tangu mwanzo tusingekuvalia bango. Hotuba aliyoitoa Mwalimu UN 1955 "imenyambuliwa kutokan memoranda ya 1950" Lakini hukusema hivyo. Jinsi ulivyosema/ulivyoandika ni kwamba hotuba iliandikwa na Sykes na Mwalimu akaisoma word for word. Kumbe ile memorandum ya 1950 ilitumika kama hadidu za rejea? Ndio maana nilikuuliza, lini ulipogundua kuwa kura tatu za Tabora zilikuwa ni uamuzi wa busara? Kwa sababu katika kitabu chako, toleo la kwanza, uliandika kuwa ni ushahidi wa kuwabagua Waislamu. Tuendelee.

Jasusi,

Karibu tena.

Mohamed
 
Hahahahah "Nyundo" zimemlewesha, anaona nyota nyota, si unaona huko juu, mara hii sio historia ni simulizi mara hii ni historia. Ana-haha.

Unajuwa Sheikh Mohamed Said, hii shock si wao tu inaowapata hata sisi Waislaam imetupata kwa kiasi fulani labda sisi imetupata kivingine. Ngoja nikuelezee kwa upande wangu kwa ufupi sana:

Kwanza nnapokisoma ulichokiandika, huwa nnasema hakika Mwenyeezi Mungu ni mwingi wa rehema na shani zote ni zake, huwa nnasema leo angetokea Muislaam mwingine ambae hana mnasaba kabisa na hawa wazee na hakutokea katika jamii na ahli hiyo, sijui hayo matusi yangekuwaje? maana kila wanapotaka kujaribu huwa jibu ni kuwa anaeandika anawafahamu ni wao na anayoyasema ni kweli. Hapo sasa.

Hakuna humu hata mmoja aliyekuja akasema hapana, huyo Mzee uliemtaja hakuwepo na hakuwa na wadhifa huo au hakufanya harakati hizo.

Inayobaki wanaanza, mbona fulani hukumuuliza, mbona fulani hukumuuliza. Hivi ni kweli wao wanashindwa kuwauliza hao wanaowataka wao? Au wanawauliza na majibu ndio hawana pakuyaweka? Hiyo ndio shock inayonipata mimi.

Watu wanakuja na kufanya kila hila kuutowa huu mjadala kutoka kwa wazee na kuupeleka kwenye EPA, wanapoambiwa 83% ni wao, wanaanza kuuliza imetoka wapi, wanashindwa kufanya kautafiti kadogo tu wakaja hapa waseme hapa hiyo asilimia si kweli, asilimia sahihi ni hii hapa kwa ushahidi huu na huu.

Unapowaambia umeiona historia iliyoandikwa Kigamboni na imewasahau wazee waasisi wa AA na TAA na TANU na unapowabainisha kinaga-ubaga, wanashindwa kusema hao wazee si wa ukweli hawakuwepo, kama hilo linawashinda na kweli walikuwepo ni nini zaidi kinachowasumbuwa? Ni rahisi sana kuelewa, ni shock, na masikio yao na bongo zao zimeaminisha kuwa ilikuwa "One man show" sasa kuja kuona si hivyo, inakuwa vigumu sana wao ku "insert" haya ya ukweli.

Shock yangu ni kwanini inawawia vigumu?

IKO HIVYO THEN WHAT?????????????????????? Waislamu tunatakiwa tulipize kisasi au....?? Mbona sasa tuna fursa sawa????
Mimi sioni msingi wa hii historia kusimuliwa sasa kama tunaweka maslahi ya taifa mbele na sio ya dini.
Wanasema hata mbuyu ulianza kama mchicha. Baada ya kusoma haya nimegundua tunawashtaki wao kuwa wadini kwa sababu ya udini wetu.
YEYOTE MWENYE AKILI NA AUONE HUU KAMA USHENZI, UPUUZI NA UPUMBAVU, si kwa sababu ni uongo ila kwa sababu ni hatari kwa amani na umoja wa taifa letu lenye miaka 50 sasa.
Miaka yote hiyo mambo haya yalikuwa wapi kusemwa??????
KIKWETE ANAYEPINGA UDINI DAY & NIGHT YUKO WAPI??? Wanasiasa wanajua fika mambo ya kwenye forums, wanaliokoaje taifa letu na hawa masheikh na mapadre wanaopanda mbegu mbaya kwa vijana wetu??
I can describe this by three (3) words: UPUMBAVU, UPUMBAVU & UPUMBAVU
 
Dhulma haidumu hata kama ni karne moja..

Pesa za umma zilizotumika kuendeleza kanisa either zirudi au mfuom mzima wa kugawa fedha za umma uwekwe sawa period..
 
Mwanakijiji,

Unajua kuna baadhi ya hoja nakubaliana na wewe. Ila nasita kuanzishwa kwa Commision for Truth and Unity kwasababu ya historia ya nchi hii. Hembu nikuulize ikianzishwa hiyo commision do you think kweli waislamu wataiamini? If not why? Je unadhani walivyopoteza kumbukumbu za mwanzo sasa hivi ndio watazitokomeza kabisa!!!! Hebu fikiria kwa upande wa pili mwanakijiji. Ndio maana nasema ni vema ikawepo Truth and reconciliation committee kwanza tuwekane sawa na kuombana radhi yaishe. Then turekebishe historia na mwelekeo wa nchi mbele. Vyenginevyo itakuwa ni hadithi ya merry go round!!!!

The problem is that a truth and reconciliation commission presumes some wrongs were done and the facts are indisputable. The historical commission on the other hands inataka kutafuta ukweli wa historia kwanza.. kabla hatujafikia kujua kama kuna wrongs were done.. we need to set the facts straight kwanza.
 
Mwanakijiji,

Uzuri wa utafiti na kuandika ndiyo huu.

Vipi nimetoa changamoto ya wewe na wenzako kuandika historia kujibu kitabu changu.

Je mmeipokea hiyo changamoto au mmetoa mbukwa?

Mohamed

sasa mzee mohamed? wewe uliandika kitabu ili ujibiwe au ili utoe ilmu kwa watanganyika? halafu, nimeambiwa kuwa historia hiyo ndiyo inakusudiwa kuwa mbadala wa hii iliyopo, na kwa kuanza vitabu vitapelekwa kwenye shule za kiislamu, sasa historia itafundishwaje ilhali wewe mwenyewe unasubiri changamoto za akina mwanakijiji na mag3, huoni kuna shaka hapo sheikh?
 
The problem is that a truth and reconciliation commission presumes some wrongs were done and the facts are indisputable. The historical commission on the other hands inataka kutafuta ukweli wa historia kwanza.. kabla hatujafikia kujua kama kuna wrongs were done.. we need to set the facts straight kwanza.

"when the going get tough, let tough get going" hii tafsiri yake inaweza kuwa " safari inapokuwa ngumu, acha walio jasiri waendelee na safari" Wewe Mwanakijiji ni jasiri.

Mohamed Said na wenzake ambao wameingiwa na hofu ya safari kuelekea kwenye nchi isiyo na udini wanataka watu wote tuwe waoga na kubakia kwenye kisiwa cha wapumbavu wanaodhani maendeleo au kutokuendelea kunasababishwa na dini ya mtu. Sasa hivi ukienda Kariakoo au ukichunguza wanaomiliki magari ya usafiri ni waislamu. Sidhani wanamiliki magari hayo kwa sababu "serikali' iliweka mpango maalumu wa kuzuia wakristo kumiliki magari ya kusafirisha abiria.

FaizaFoxy na MS anayemshabikia wote wawili wanakizalilisha kiwango cha kufikiri cha watu wa pwani wanaodai wanawatetea. Uislamu ni dini adhimu sana hata kutetewa katika mtindo anaotumia MS na mashabiki wake ni kuishusha hadhi kufikia kiwango cha kufuru kwa muislamu anayeijali dini yake.

Ushabiki wa kutiana shime kwenye kupotosha kwa maslahi ya matumbo ambayo muda wa kufa ukifika yataoza yakiwa kaburini (iwe baharini au Jangwani) ni kinyume kabisa cha Uislamu. Ghadaffi, Ben Ally, Hussein Mubarak na wengineo wa kariba hiyo walijinasibisha na uislamu hata kudiriki kwenye kuhhiji Macca mara kumi kumi, lakini ufirauni wao umekuwa ni mkubwa sana hata kuliko maajabu ya Mussa.

Kuna waislamu wengi tu (wengine wakiwa ni ndugu zangu) wamesoma vizuri sana tena zama za Nyerere na wengine wao walikuwa kwenye nyadhifa nzuri zaidi kuliko hata walizokuwa nazo wakristo. Kuna ukweli ambao MS na wenzake hawataki kuusema. kwamba wao wanaisiasisha dini (Religion Politilisation) na wanaijeshishaji dini ( Religion Militarisation) kwa faida ya CCM na siyo jambo la kushangaza kuona mpaka leo Dar es salaam ya waswahli bado CCM imeota mizizi ingawa kwenye maeneo mengi ya nchi inachukiwa kama ukoma.

Siku moja nilikuwa kwenye msikiti wa Magomeni Kagera nikamsikia Sheikh anatangaza kwenye loud Speakers kwamba "Ndugu zangu waislamu lazima tuhakikishe tunapochagua tusichague chama chenye mfumo kristu ndani yake, chama chenye mgombea ambaye aliwahi kuwa Padre." Nikajua hapa hakuna kitu.

Hivi kama bila serikali kuchangia huduma za Afya zinazotolewa na Makanisa kuna mtanzania (achilia mbali waislamu) ambaye atamudu gharama za matibabu kwenye Hospitali za kanisa? Huyo MS anayemtumia Aga Khan kutetea hoja yake kuhusu shule zilizojengwa na naye kwa ajili ya waislamu, leo hii akiumwa huwa anakwenda kwenye Hospitali ya "Muislamu" mwenzake Aga Khan au huwa anakimbilia Amana? HIvi gharama za shule za Aga Khan ni sawa na zile ambazo watoto na wajukuu wa MS wanao uwezo wa kuingia?
 
sasa mzee mohamed? wewe uliandika kitabu ili ujibiwe au ili utoe ilmu kwa watanganyika? halafu, nimeambiwa kuwa historia hiyo ndiyo inakusudiwa kuwa mbadala wa hii iliyopo, na kwa kuanza vitabu vitapelekwa kwenye shule za kiislamu, sasa historia itafundishwaje ilhali wewe mwenyewe unasubiri changamoto za akina mwanakijiji na mag3, huoni kuna shaka hapo sheikh?

M,

Jitulize andika tena vizuri mimi nitakujibu Insha Allah.

Mohamed
 
samahani kama hati yangu inakukwaza. ila kifaa nitumiacho ndio uwezo wake, nivumilie tafadhali!

Mimi ndiyo nimetoa changamoto wao nao waandike kitabu cha kuweza kuwa na hadhi sawa na changu ili ukweli katika historia ya uhuru wa Tanganyika ijulikane.

Shule za Kiislam kwa miaka mingi sasa inasomesha historia hii na hata baadhi wa vijana walimu wa historia katika vyuo vikuu nchini wamevutiwa na kitabu hiki na hukitumia kama rejea katika kufundisha.

Kisa cha mashujaa waliopigania uhuru wa Tanganyika kimevutia wengi.

Mohamed
 
IKO HIVYO THEN WHAT?????????????????????? Waislamu tunatakiwa tulipize kisasi au....?? Mbona sasa tuna fursa sawa????
Mimi sioni msingi wa hii historia kusimuliwa sasa kama tunaweka maslahi ya taifa mbele na sio ya dini.
Wanasema hata mbuyu ulianza kama mchicha. Baada ya kusoma haya nimegundua tunawashtaki wao kuwa wadini kwa sababu ya udini wetu.
YEYOTE MWENYE AKILI NA AUONE HUU KAMA USHENZI, UPUUZI NA UPUMBAVU, si kwa sababu ni uongo ila kwa sababu ni hatari kwa amani na umoja wa taifa letu lenye miaka 50 sasa.
Miaka yote hiyo mambo haya yalikuwa wapi kusemwa??????
KIKWETE ANAYEPINGA UDINI DAY & NIGHT YUKO WAPI??? Wanasiasa wanajua fika mambo ya kwenye forums, wanaliokoaje taifa letu na hawa masheikh na mapadre wanaopanda mbegu mbaya kwa vijana wetu??
I can describe this by three (3) words: UPUMBAVU, UPUMBAVU & UPUMBAVU

nimekugongea thanks yangu hapo..
 
Mimi ndiyo nimetoa changamoto wao nao waandike kitabu cha kuweza kuwa na hadhi sawa na changu ili ukweli katika historia ya uhuru wa Tanganyika ijulikane.

Shule za Kiislam kwa miaka mingi sasa inasomesha historia hii na hata baadhi wa vijana walimu wa historia katika vyuo vikuu nchini wamevutiwa na kitabu hiki na hukitumia kama rejea katika kufundisha.

Kisa cha mashujaa waliopigania uhuru wa Tanganyika kimevutia wengi.

Mohamed

Ni vitabu gani vinatumika kufundishia historia rasmi ambavyo vinaonesha kuwa harakati za Uhuru zilianza na Nyerere?
 
Ni vitabu gani vinatumika kufundishia historia rasmi ambavyo vinaonesha kuwa harakati za Uhuru zilianza na Nyerere?

Kitabu kilichoandikwa Kigamboni, kimetajwa humu rejea post za nyuma. Usigandishe santuri kwa makusudi.
 
Mimi ndiyo nimetoa changamoto wao nao waandike kitabu cha kuweza kuwa na hadhi sawa na changu ili ukweli katika historia ya uhuru wa Tanganyika ijulikane.

Shule za Kiislam kwa miaka mingi sasa inasomesha historia hii na hata baadhi wa vijana walimu wa historia katika vyuo vikuu nchini wamevutiwa na kitabu hiki na hukitumia kama rejea katika kufundisha.

Kisa cha mashujaa waliopigania uhuru wa Tanganyika kimevutia wengi.

Mohamed
Sijui kama MS ni kwa nini unajifanya hujui kwamba kwenye shule zetu kuna aina mbili za vitabu. Vitabu vya kiada na vitabu vya ziada, na hakuna mtu anayekataa kwamba vitabu vyako vinatumika kwenye mashule ya waislamu bali kinachochambuliwa ni yaliyomo ndani ya kitabu chako na madhumuni yake.

Ni wewe mwenyewe uliyeleta makala zako ulizoandika kwenye gazeti la Mwananchi na kuzitundika humu, ulidhani watu wote wanasoma kwenye hizo shule za waislamu kwa hiyo watazikubali kiurahisi hoja zako? Na hapa pia najifunza ni kwa nini shule nyingi za kiislamu somo la Historia wanafeli sana. Maana madarasani wanajifunza kwa kutumia vitabu vyako wakati siku ya mtihani wanapewa maswali kutoka kwenye vitabu vingine kabisa.

Nakushauri ndugu yangu kwanza kabisa vitafutie ithibati vitabu vyako ili visomwe kwenye shule zote hata zile zisizo za "kiislamu" maana shule nyingine zinazoitwa za kiislamu nachelea kuzihusisha na uislamu kutokana na matendo yatendwayo na waalimu pamoja na wanafunzi wao. Basi tuishie kuziita za waislamu ilhali ni miradi ya watu wanaoutumia uislamu kushibisha matumbo yao.
 
Hakuna mpaka sasa aliyesema hao wazee anaowaandika Mohamed Said kuwa walikuwa si wa ukweli na wakubuni.

Kinachopingwa ni nini?
 
Kumejitokeza suala la BAKWATA ambalo linajitikeza na ilitolewi maelezo yanayojitosheleza kama ilivyo kawaida ya kukwepa mada.
Tumeishia kupewa rejea za mwandishi mwenyewe.

Hakuna anayeweza kujitokeza na kusema nje ya BAKWATA , ni chombo gani kinawakilisha waislam. Kuna kamati na taasisi kibao.
Hakuna baraza au kamati inayoshughulikia huduma za jamii kama afya na elimu. Mlolongo wote huo haujulikani upo chini ya mwamvuli gani.
Ni kituko kusema waislam wa Tanzania wamesema! wapi hao? na mtu anatumia kigezo gani kusema hawa ndio waislam wa TZ

Mohamed anasema 17% waisla inadhulumiwa . Wakati huo huo amebeba wadhifa kama kiongozi wa waislam.
Kisichojulikana ni kiongozi wa kundi gani ? Kwanini watu waone ubaguzi wa nje wasione ule ulio ndani ya jamii yao?

Sheikh Mohamed anasema waislam wamepigania uhuru. Kigezo kikubwa anachotumia ni majina.
Ni Sheikh Mohamed amechukua jukumu la kuhukum wanadamu wenzake kwa kusema BAKWATA si waislam.
Endapo alitumia kigezo cha majina kuhalalisha nguvu katika harakati, iweje asitumie kigezo hicho kutambua kuwa BAKWATA ni waislam wenye mtazamo na matatizo tofauti kama zilivyo taasisi nyingine za waislam.

Mohamed amewahi kusema(ushahidi upo) magereza kumejaa waislam. Kama hao ni watoto waliosoma shule za BAKWATA ambazo Mohamed anadhani zina watoto wasio waislam nani alaumiwe.

Na kwanini inapokuja hoja ya shule za kiislam ndipo BAKWATA inaingia lakini hijabu ni suala la kitaifa.
BAKWATA walipotoa tamko kuhusu hijabu waislam wote wakaliunga mkono, lakini hoja ya shule hiyo ni ya BAKWATA.
Hii ni dhambi ya ubaguzi inayowatafuna wale wanaobagua. Baada ya kumalizana na Nyerere sasa wamegeuziana Kibao.

Kwa mantiki hiyo asilimia 17 au 23 ya ajira au nafasi za masomo kwa waislam ni ndogo zaidi ya kiwango anachosema Mohamed.
Ni ndogo kwasababu BAKWATA sio waislam kutokana na kauli za Kiongozi Mohamed.
Ikifika hapo namkumbuka Mkandara na jinsi alivyochambua katika post zilizopita kwa weledi wa hali ya juu.

Asichosema Mohamed ni kuwa Shule za BAKWATA zinaangukia kundi gani la jamii kiimani?
BAKWATA si waislam na tunajua si Wakristo, je yaweza kuwa ni Wapagani au Atheist? Mohamed S.Samtungo amewahi kana uwepo wa wapagani
Mohamed anazungumzia EAMWS shule na chuo kikuu. Asichojibu ni kuwa kile cha Morogoro kisicho cha BAKWATA kinafanya nini tofauti na shule za BAKWATA! Haina mantiki wala maana kuongelea historia ya jengo lisilowahi kuwepo na kutoona kile kilichopo?

BAKWATA wana matatizo makubwa sana, lakini kwa mtu mwenye fikra ni lazima aangalie mambo kiueledi zaid kama kuathirika kwa watoto. Kushindwa kufanya hivyo ni njia rahisi ya kutengeneza data na takwimu ambazo zinaweza kutokea naturally.
Itamchukua mtu mwenye akili kujua tatizo ni nini na si kutafuta mchawi. Kuendelea kuwaaminisha watu uongo ni mwendelezo wa kujidhulumu.

Mohamed ni kiongozi alichaguliwa na nani? narudia aliyechaguliwa na waislam gani.
Nasema aliyechaguliwa kwasababu nina ushahidi wa kutosha kuwa waislam wanachagua viongozi, na nikitakiwa kuuweka hapa jamvini nitauweka.

Watu waanglie chanzo wasiimbie nyimbo au kumtafuta mchawi nje ya nyumba yao.
 
Nguruvi,

Inasikitisha kuwa hayo ya elimu na afya na mengineyo huelewi kuwa yapo chini ya kanisa na hata hiyo BAKWATA unayoieleza ushapewa kisa chake kuwa inafadhiliwa na kanisa. Sijui kwanini unazunguka mbuyu na mambo yako uwanjani.
 
We utalambwa.

Kama wanafadhiliwa na kanisa inamana Wanatumia BIBLIA kuendesha kazi zao za kila siku?
 
We utalambwa.

Kama wanafadhiliwa na kanisa inamana Wanatumia BIBLIA kuendesha kazi zao za kila siku?

Ahsante kwa kunipa sifa njema.

Kwani hata hii nchi inaongozwa kwa kutumia nini? Soma preface ya Mwembechai Killings umsikie Nyerere anajibu nini alipoulizwa, alisema anatumia "Gospel of Jesus", sasa hicho ni nini?
 
Si vibaya hata Jakaya akitumia miongozo ya Quran kuongozea nchi kwani kwenye Quran hakuna mahali kumeandikwa viongozi wanatakiwa kuwalinda mafisadi, badala yake Quran inahimiza kulinda haki na kuwatendea haki wanyonge. Kama Kweli Kikwete angewatendea haki wanyonge na kupambana na mafisadi basi bila shaka wote tungesema Kikwete anatumia Quran kuongoza nchi!!

Halafu kwani Mwalimu alikuwa anajibu kuhusu Mwembechai au kipande hicho cha maneno ya Mwalimu kilichomekwa ili kuweka msisitizo wenu kuhusu Nyerere. Nyie wote mnajua kwamba bila ya kulitaja jina la Nyerere maandiko yenu yote hayatasisimua.
 
Back
Top Bottom