Hahahahah "Nyundo" zimemlewesha, anaona nyota nyota, si unaona huko juu, mara hii sio historia ni simulizi mara hii ni historia. Ana-haha.
Unajuwa Sheikh Mohamed Said, hii shock si wao tu inaowapata hata sisi Waislaam imetupata kwa kiasi fulani labda sisi imetupata kivingine. Ngoja nikuelezee kwa upande wangu kwa ufupi sana:
Kwanza nnapokisoma ulichokiandika, huwa nnasema hakika Mwenyeezi Mungu ni mwingi wa rehema na shani zote ni zake, huwa nnasema leo angetokea Muislaam mwingine ambae hana mnasaba kabisa na hawa wazee na hakutokea katika jamii na ahli hiyo, sijui hayo matusi yangekuwaje? maana kila wanapotaka kujaribu huwa jibu ni kuwa anaeandika anawafahamu ni wao na anayoyasema ni kweli. Hapo sasa.
Hakuna humu hata mmoja aliyekuja akasema hapana, huyo Mzee uliemtaja hakuwepo na hakuwa na wadhifa huo au hakufanya harakati hizo.
Inayobaki wanaanza, mbona fulani hukumuuliza, mbona fulani hukumuuliza. Hivi ni kweli wao wanashindwa kuwauliza hao wanaowataka wao? Au wanawauliza na majibu ndio hawana pakuyaweka? Hiyo ndio shock inayonipata mimi.
Watu wanakuja na kufanya kila hila kuutowa huu mjadala kutoka kwa wazee na kuupeleka kwenye EPA, wanapoambiwa 83% ni wao, wanaanza kuuliza imetoka wapi, wanashindwa kufanya kautafiti kadogo tu wakaja hapa waseme hapa hiyo asilimia si kweli, asilimia sahihi ni hii hapa kwa ushahidi huu na huu.
Unapowaambia umeiona historia iliyoandikwa Kigamboni na imewasahau wazee waasisi wa AA na TAA na TANU na unapowabainisha kinaga-ubaga, wanashindwa kusema hao wazee si wa ukweli hawakuwepo, kama hilo linawashinda na kweli walikuwepo ni nini zaidi kinachowasumbuwa? Ni rahisi sana kuelewa, ni shock, na masikio yao na bongo zao zimeaminisha kuwa ilikuwa "One man show" sasa kuja kuona si hivyo, inakuwa vigumu sana wao ku "insert" haya ya ukweli.
Shock yangu ni kwanini inawawia vigumu?