Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa


Nguruvi3,

Ndugu yangu unaleta hoja nzuri ambazo mimi zinanisisimua tatizo unachukuliwa na hamaki kidogo.

Hii habari ya archive na soksi ndefu ya nini kaka inachafua murua wako isingelikuwa hapo.

Ngoja nikutoa shaka katika hilo la soksi ndefu.

Katika moja ya uzi wangu nilipoona hili suala kaptula linapewa uzito usiostahili nilisema mimi baba yangu akivaa kaptula na stockings akenda kazini. Abdulwahid Sykes akivaa kaptula na stockings akiwa Market Master pale Kariakoo na watu walomuona katika kivazi hicho wu hai. John Iliffe katika "A Modern Histrory of Tanganyika" ameielezea ile picha ya waasisi wa TANU na yeye kenda mbali zaidi kwa kusema kuna tofauti ya mavazi kati ya waasisi waliotoka kwenye majimbo (provinces) na akina Abdulwahid.

Nakuomba sana ndugu yangu tuliache hili la nguo kwa hakika halina tija. Tuzungumze yale yatakayotuongezea ufahamu zaidi wa historia ya nchi yetu.

Nakuomba soma Cranford Pratt, "A Critical Phase in Tanganyika" ameeleza kirefu kuhusu memorandum iliyoandikwa 1950 na TAA Political Sub Comitteee ambayo ilipelekwa kwa Gavana Edward Twinning. Hotuba iliyosomwa Umoja wa Mataifa 1955 imenyambuliwa mle ndani.

Humu ndani nimeeleza kwa kirefu kuhusu jambo hili lakini kama hamuamini wala isiwe tabu hotuba hiyo ni moja tu katika mengi katika historia ya Tanganyika ambayo niko tayari wakati wowote kueleza kwa ajili ya faida ya wanaukumbi.

Kuhusu Nyaraka za Sykes wala usifanye maskhara. Uzione kwa jicho lako ndiyo utaamini. Illife alizitumia hizo kupitia bint yake Abdu, Daisy Sykes kuandika historia ya African Association katika miaka ya katikati ya 1960 wakati Daisy alipokuwa mwanafunzi wake Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Naweka hapa "observations" zangu kuhusu hizi nyaraka kwa faida ya wanaukumbi:

...aliniruhusunisome majalada yake binafsi, barua zake, shajara na kumbukumbu nyinginezo zaukoo wa Sykes. Ally Sykes alinifahamisha kuwa kumbukumbu hizi zilikuwa ndani yasefu ambayo haikupatwa kufunguliwa kwa zaidi ya miaka therathini. Nikiyapitiamajalada yake nilishangazwa na utaratibu wa Ally Sykes wa kupanga kila kitu nakila kipande cha habari mahali pake hata kingekuwa kidogo namna gani wakati ulewa harakati. Ally Sykes ana barua ya mwaka 1954 iliyoandikwa kwa penseli tokakwa Zuberi Mtemvu kwenda kwake akimtaarifu juu ya mazungumzo aliyokuwanayo(Mtemvu) na Nyerere kuhusu yeye na TANU; stakabadhi ya hundi ya posta toka kwaAlly Sykes kwenda kwa Japhet Kirilo wakati wa Mgogoro wa Ardhi ya Wameru;nakala ya barua isiyokuwa na tarehe kutoka TAA kwenda kwa Malkia Elizabethiliyotiwa saini na viongozi wote wa TAA: Rais Julius Nyerere, Makamu wa RaisAbdulwahid Sykes, Katibu Mkuu Dome Okochi, Naibu Katibu Dossa Aziz, MwekaHazina John Rupia, Naibu Mweka Hazina Ally Sykes ikimpongeza Malkia kwakutawazwa; barua ya mwaka 1952 toka kwa Rashid Mfaume Kawawa kutoka Bukobakwenda kwa Ally Sykes ikimfahamisha juu ya hali ya siasa katika Kanda ya Ziwa;barua ya mwaka 1963 toka kwa Lady Judith Listowel, Kenneth Kaunda, Julius Nyerere,Kasela Bantu, Chifu Thomas Marealle ...orodha haina mwisho. Baadaye nilipofanyautafiti kuhusu maisha ya baba yake, Kleist Sykes, nilikuja kufahamu kwambatabia hii ilirithiwa kutoka kwa baba yake ambae alikuwa akiweka ndani ya jaladakila kipande cha karatasi kilichokuwa na habari iliyostahili kukumbukwa. Nijambo la kuhuzunisha kwamba sikuweza kupewa shajara za Abdulwahid ambazonilielezwa kwamba baadhi ziko katika hati-mkato na hadi leo hazijafasiriwa.Shajara hizi nimezioana kwa macho yangu lakini kwa kukosa idhini sikuwezakuzifungua na kuzisoma. Vilevile vilevile sikuweza kupata kumbukumbu halisi zaVita Kuu ya Kwanza zilizoandikwa na Kleist Sykes kwa mkono wake mwenyewe.Hapana shaka yoyote kwamba nyaraka hizi ni hazina zenye thamani isiyo na mfanowake. Ni matumaini yangu kwamba siku moja nchi yetu itakubali na kuthaminimchango wa Abdulwahid katika taifa la Tanzania na nyaraka hizi kama kielelezocha harakati dhidi ya ukoloni, zitakubalika na zitawekwa chini ya hifadhi yaNyaraka za Taifa kwa faida ya vizazi vijavyo."Waungwana hawabanani.

Mohamed
 

Mkapa alikuwepo wakati AA na TAA zina asisiwa? hivi mkapa anaweza kuwa na habari za Abdul Wahid Sykes na ujio wa Nyerere Dar. zaidi ya Ali Sykes? Hivi huyu Mkapa wakati TANU inaanzishwa alikuwa na la kuongelea? Jamani, pumba zingine taratibuni.
 
Mkapa alikuwepo wakati AA na TAA zina asisiwa? hivi mkapa anaweza kuwa na habari za Abdul Wahid Sykes na ujio wa Nyerere Dar. zaidi ya Ali Sykes? Hivi huyu Mkapa wakati TANU inaanzishwa alikuwa na la kuongelea? Jamani, pumba zingine taratibuni.

Someone wrote this before hiyo comment ya Mkjj

 


Kina Mkandara?

a) Simulizi zilizokufanya uwajue wote waliotajwa, simulizi zilizokufanya uelewe kuwa katiba ya TANU ilikuwa ni "COPY and PASTE", simulizi zilizokufanya uamini kuwa Waislaam ndio watakuja kujibu yote haya, simulizi zinazokufanya uulize kuhusu Ndege ya Rais wakati watu wanamuongelea Mshume. Laiti ungeweza kulitafsiri neno "history" kiswahili usingeliita "Historia" the nearest lingekuwa hiyo "simulizi". Simulizi za Mohamed Said zina ushahidi kamili, Jee, Nyerere hakupokelewa na Abdul Wahid Sykes kama alivyosimulia Mohamed Said?

b) Na hao wazee walikuwa dini ipi? Na yeye unaesema si wazee wake, unaweza kutuambia wazee wake ni wepi na kwanini hakuwataja?

c) Tutajie hao watu, ili tuamini huo uhakika wako.

Hayo ni matumaini mema na wote tunaombea iwe hivyo ili waliosahauliwa kwenye Taifa hili wakumbukwe japo kwa majina tu. Mohamed Said kaanzia na wazee wake wa Dar. kwa majina na walipoishi na harakati walizozifanya kabla ya Nyerere kuja na mpaka wakawa nae na mpaka akasahau walikuwa na nyadhifa zipi, na wewe kwa nini usituletee ya wazee wako tuone mchango wao humu au huna wa kuanzia?

Maana pa kuanzia kwa sasa unapo baada ya kazi nzuri ya Mohamed Said, wa kuanzia naona hapo ndio kasheshe, ulianza ukapata jibu lake ukakosa pa kuanza tena ukaja kuanza na EPA, mengine jamani si ya kucheka lakini mnhhhhhh.
 

Kama wale waliowafukuza waumini kanisani kwa kuwa wameichaguwa CCM? Au tumfate Slaa Daktari wa kanoni? mbona huweki wazi? unaficha ficha? zama za kuficha ficha zimekwisha kijana, sasa tupo kwenye kizazi cha dot com. Utaficha nini kisijulikane?
 
Hapa ndipo mzee Said unatatiza sana.
Swali langu linalotokana na hoja zako ni kuwa kwa vile sub committee ilishaundwa na tunajua ni ya chama cha TAA, Je, hiyo hotuba iliandikwa ili nani aipeleke kunako husika(kwa gavana kama ni hivyo), nani alikuwa aisome UN? Na hotuba ya uhuru ililenga uhuru wa mwaka gani.
Maana yangu ni kuwa ukinunua mbeleko unajua upo utungo wa mimba kwahiyo yote yalijulikana.
swali ni rahisi na straight forward. Tuache hii ya mwaka 1955 tujibu ile ya 1950
 
Mag3,
Nadiriki kusema kuwa Mohamed ame "hijack" jina na legacy ya Abdulwahid Sykes kwa malengo yake ya kidini. Hata mimi niko karibu na wanae Abdulwahid. They are not exactly thrilled with Mohamed's jihad.

Hao unaojidai upo nao karibu hao ndio wamempa Mohamed Said nyaraka nyingi tu za kitabu chake. Leo nani asiyetaka Baba'ke ajulikane mchango wake katika Historia? unashangaza sana.

Jihad (strive hard in any good cause) ni kujitahidi ni nani asiyependa kujitahidi? wewe?
 

Within One Hour:

 

Nguruvi3,

Niwie radhi kama huwa sifiki katika kimo chako.

Nakupa ushauri mmoja tafuta kitabu chochote cha sheria usome mada ya "the standard of the reasonable man." Utaongeza elimu yako na maswali kama hayo yako utakuwa huniulizi tena.

Sheikh Hassan bin Amir akitumia sana hii mara nyingi likija swali kwake la sampuli hiyo alikuwa akisema, "Tatizo nyinyi hamtaki kusoma laiti ungelisoma isngeliuliza swali kama hilo."

Hata hivyo niakujibu hebu kwanza pata "background" ya jambo lenyewe:
TAA 1950
"Makao Makuu ya TAA mjini Dar es Salaamchini ya Dr Kyaruzi na Abdulwahid ikiungwa mkono na kamati ya siasa sasailikuwa ikiamka kutoka kwenye usingizi mzito. Kilichotakiwa ilikuwa ni kupatamaswala yakutoa changamoto kwa akili za wale wasomi vijana. Uongozi wa chamacha TAA haukuwa na haja ya kuangaza mbali. Changamoto ilikuja kwa sura yaConstitutional Development Committee (Kamati ya Mapendekezo ya Katiba)iliyoundwa na Gavana Edward Twining na mgogoro wa ardhi ya Wameru.
Uingereza ilikuwa ikitawala Tanganyikachini ya kifungu 76 na 77 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Kama mamlaka tawalaUingereza ilitarajiwa kuanzisha na kuendeleza maendeleo ya siasa, uchumi na yakijamii ya Tanganyika hadi kufikia wakati ambao watu wake wangekuwa tayarikujitawala. Lakini Waingereza walifanyakhiyana na hawakutimiza ahadi hiyo. Walijihusisha na kulinda maslahi yaowenyewe ya kikoloni na yale ya watu weupe wachache na wakaendelea kuwapuuzaWaafrika waliokuwa wengi na wenye nchi. [1] Labda kwa kuanua ngomajuani, Gavana Twining alikaribisha mapendekezo kutoka kwa watu mashuhuri, vyamavya ustawi wa jamii na Native Authorities,[1] kutaka mapendekezo yajinsi Tanganyika itakavyotawaliwa. Kamati ya siasa ya TAA ilipeleka mapendekezoyake ambayo yalitiwa sahihi na wajumbe wote wa kamati ya siasa. Sheikh Hassan bin Amir, Abdulwahid Sykes,Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, John Rupia, Stephen Mhando na Said Chaurembo.[1]Katika taarifa yake ya mwaka ya 1950 Abdulwahid aliandika: "Kwa ajili ya maslahi ya Waafrika na kulindamaslahi ya chama hiki na yale ya jumuiya ya Waafrika kwa ujumla, chama kimewekawakili atakayeshauri juu ya mambo ya sheria. Wakili huyo ni Bwana E. E. Seatonwa Moshi. Mara kwa mara amekiandikia chama hiki juu ya masuala mbali mbali yasiasa, na kwa kiasi kikubwa ushauri wake umesaidia wakati chama hiki kilipokuwakikitayarisha mapendekezo juu ya katiba."[1] Abdulwahid alitambua kuwa matatizo mengikuhusu haki za Waafrika yalikuwa masuala ya kisheria ambayo yalihitaji ushauriwa wanasheria. Kwa mara ya kwanza kwa msaada wa Seaton, TAA kilitoa hoja zakezilozotiwa nguvu na ukweli hoja na kwatarakimu zilizoonyesha udhalimu ndani ya mfumo wa kikoloni ambao ulikuwakinyume na Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Memorandum ya TAA kwa ConstitutionalDevelopment Committee ambayo Pratt amesema iliandikwa kwa utaalamu wa hali yajuu na uongozi wa makao makuu ya Tanganyika African Association ilipendekezakuwa ndani ya baraza la kutunga sheria. Waafrika watashika nusu ya vitikwa miaka kumi na mbili na baada ya hapo ipigwe kura kuwachagua wajumbe.[1]"

Sasa soma hii hapa chini:

TAA/TANU 1954
"Ajenda yakwanza kujadiliwa chini ya TANUtarehe 9 Julai ilikuwa lile suala la uchaguzi wa wajumbe wa Baraza la KutungaSheria. Katika mwaka 1950 itakumbukwa kuwa TAA, chini ya uongozi wa Abdulwahidna Dr Kyaruzi iliwakilisha memorandum kwa Gavana Twining kueleza mapendekezoyake juu ya mabadiliko ya katiba. Ilishauriwa kwamba ili kufikia kiwango fulanicha maendeleo ya siasa, ilikuwa lazima Waafrika wapitie utaratibu wa maendeleohatua kwa hatua kwa kushiriki katika kuitawala nchi yao. Moja ya mapendekezoilikuwa Waafrika waruhusiwe kuchagua wawakilishi wao wenyewe katika Baraza laKutunga Sheria. Ilikisiwa kwamba haya mabadiliko ya hatua kwa hatua yaruhusiwekuendelea kwa kipindi cha miaka kumi na tatu baada ya hapo Waafrika waruhusiwekuunda serikali yao wenyewe iliyo huru.[1] Hii ilikuwa ajenda muhimu sana na Abdulwahidna Rupia ambao walikuwa wajumbe wa kamati ndogo ya siasa ya TAA iliyorasimumapendekezo hayo walieleza mkutano kwa ufupi juu ya upinzani wa serikali katikakukubali mapendekezo hayo. Ilikubaliwa na wote kwa pamoja kuwa suala lakuanzisha kanuni za kidemokrasia katika uchaguzi wa wajumbe kwenye Baraza laKutunga Sheria lilikuwa muhimu sana na watu lazima wafahamishwe juu ya hakihii."

Ikiwa umesoma "the standard of the reasoble man" na umeshindwa kujua majibu ya maswali yako tutafuta msaada wa wanaukumbi wengine watusaidie. Ndiyo maana muulizaji wa "Aga Khan ni Muislam au si Muislam" sikumjibu maana huwa sipendi kuwa "encourage" wanamnakasha kuuliza vitu ambavyo ni "obvious" vinachachua majadiliano. Kwa hakika kama ulivyosema mwenyewe hili ni swali rahisi.

Mohamed

 

Historia haiegemei katika dini pekee.
Ujaribu kuzungumzia historia kwa mapana na si kwa nguzo ya dini pekee.
 

Within One Hour:


Mwanakijiji,

Dawa yangu mimi ni nyinyi mkaandika kitabu basi.
Vinginevyo itakuwa ni hii "merry go round."

Hamuwezi kujibu kitabu changu kwa sentensi.

James Brenan na Jonathan Glassaman walinileta hadi Northwestern University, Chicago Illinois tukafanya mnakasha mkali. Mimi hawa nawaheshimu ndiyo mabingwa wa mambo haya wapige "google" uone moto wao.

Hivi wako njiani kuwaleta wanafunzi wao Ph D kuja kupitia upya historia ya Tangayika na Nyerere husan mle ambamo hatukubaliani.

Wanatambua ukweli kuwa njia ya wao kunitoa makosa ni kuja na kitabu kingine cha historia ya uhuru wa Tangnayika.

Hebu na nyie waungeni mkono tupate ukweli.


Mohamed
 
Mzee Said nimekumbuka swali moja niiltaka kuuliza mzee John Rupia ni miongoni mwa "wazee wako"?
 

Umejipambanua sana hapo nilipo RED.

Kuna mifumo mingi sana ya kiutawala inayo tumiwa na watawala katika kutawala. Mmoja ukiwa ule wa gawanya na utawale (divide and rule) na mara nyingi katika mfumo huu utachukua watu wachache sana katika ile jamii husika na kuifanya bora zaidi kwa ajili ya kulinda maslahi yako kwa kuikandamiza ile jamii waliyotokea. ndio maana waswahili wanasema Shoka haliwezi kukata miti mpaka liwekwe kipande cha mti (Mpini)

Sasa tujiulize kama miti yhote itakataa kabisa kuingia kwenye shoka basi shaka hata siku moja halitaweza kukata miti. Ili shoka likate miti ni lazima kitoke kipande cha mti (Mpini) kiwasaliti wenzake na kuingia katika shoka ndipo miti itateketezwa.

Sasa na hao uliowataja na Mpini. Na kumbuka waislam wanatafuta mzizi wa dhulma hizo na hawababaishwi na hiyo Mpini kwani hicho ni kitu kidogo sana kwao wao wanatumia kuelimishna kisha wote kwa pamoja kudai haki yao iliyofichwa na kuporwa.

Kila la kheir
 
Kama wale waliowafukuza waumini kanisani kwa kuwa wameichaguwa CCM? Au tumfate Slaa Daktari wa kanoni? mbona huweki wazi? unaficha ficha? zama za kuficha ficha zimekwisha kijana, sasa tupo kwenye kizazi cha dot com. Utaficha nini kisijulikane?

FF,

Watu waliokuwa na Sheikh Hassan bin Amir Zanzibar baada ya Nyerere kumfukuza Bara walikuwa hawazungumzii mchango wa Sheikh katika kupigania uhuru wala juhudi zake katika kutaka kujenga Chuo Kikuu Cha Waislam kupitia EAMWS walikuwa wakianza historia hiyo Sheikh akijiinamia na kulia.

Walipo jua hivyo wakaacha kabisa.

Hii ikafikia hata baadhi ya wanafunzi wake katika kumuadhimisha wakawa wanasema Sheikh Hassan bin Amir hakuwa mwanasiasa.

Mohamed
 
Mzee Said nimekumbuka swali moja niiltaka kuuliza mzee John Rupia ni miongoni mwa "wazee wako"?

Kuliko unavyoweza kufikiria.

Mwanangu mmoja (mtoto wa kaka yangu) alikuwa anaoa.
Mmoja wa waliotoa hotuba katika harusi ile ni mtoto wa Mzee John Rupia na yeye na mkewe walikuwa meza kuu.

Mohamed
PS: Mwanakijiji hebu niulize maswali ya chemsha bongo haya sasa hayana muhimu katika historia au umechoka? Kama "fatigue" inakunyemelea basi tupumzike sote. Tulochangia hapa jamvini si haba. MS
 
Mohamed,
Wa kutusimulia ili tuandike kama wewe hayupo. Hatuna wazee wetu "Wakristo" waliokuwa TAA ambao wako hai sasa. Mimi ni mmoja wa wanaoogopa sana kuwasemea marehemu. Pili, ukianza simulizi kwa kutumia DINI, KABILA, JINSIA,......, inakuwa sio historia tena.
Halafu, wazee wako hawa, Mohamed hawakuwa na mapungufu hata kidogo kama ulivyomwanika Mwalimu?
 
Historia haiegemei katika dini pekee.
Ujaribu kuzungumzia historia kwa mapana na si kwa nguzo ya dini pekee.

Hili la dini mbona Mohamed Said kisha lijibu sana mpaka sasa inakuwa (kisemeo cha Mohamed Said) "kama santuri iliyokwama". Rudi nyuma uone limejibiwa vipi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…