Hauwezi kuwa mnafiki halafu ukaacha kuwa mwizi. Hizi ni sifa kama pacha wale wa yai moja.
Pengine Faiza anazungumzia msikiti wa Dodoma. Vinginevyo ameamua kupinga mazuri ya Mwalimu kwa kila namna na kila silaha! Ni taabu kidogo kutoyaona mazuri ya Mwalimu. Kuna wakati anajidhalilisha kabisa kwa kuongopa namna hii.Kama ulikuwepo msikiti basi ni kabla ya kujengwa upya kwa fedha za Gaddafi alizozikalia Nyerere mpaka anakufa. Mama Maria mwenyewe alitangaza kuwa kuna fedha Nyerere alipewa na Gaddafi za kujengea msikiti na utajengwa huko. Kama ni huo umejengwa upya au kuna mwingine umejengwa kwa hizo fedha baada ya kufa Nyerere hilo pia linawezekana. Si sifa yangu kusema uongo na nnauhakika na niyasemayo.
Hapana.Kama ulikuwepo msikiti basi ni kabla ya kujengwa upya kwa fedha za Gaddafi alizozikalia Nyerere mpaka anakufa. Mama Maria mwenyewe alitangaza kuwa kuna fedha Nyerere alipewa na Gaddafi za kujengea msikiti na utajengwa huko. Kama ni huo umejengwa upya au kuna mwingine umejengwa kwa hizo fedha baada ya kufa Nyerere hilo pia linawezekana. Si sifa yangu kusema uongo na nnauhakika na niyasemayo.
Evidence ndio kila kituSio "utakatifu" bali muujiza! Mwalimu hakuwa wa kawaida kama mimi na wewe tukibahatika kupewa nafasi alookuwa nayo. Mmekosa cha maana cha kumkosoa mmekimbilia UDINI.
Asichanganye basi. Msikiti wa Dodoma umejengwa majuzi. Unajua ukishakuwa na tabia ya kumchukia mtu hata lile jema analofanya mtu huyo unajitahidi kulionyesha kuwa ni uovu. Hichi ndicho kinachomsukuma Faiza na wapambe wake.Pengine Faiza anazungumzia msikiti wa Dodoma. Vinginevyo ameamua kupinga mazuri ya Mwalimu kwa kila namna na kila silaha! Ni taabu kidogo kutoyaona mazuri ya Mwalimu. Kuna wakati anajidhalilisha kabisa kwa kuongopa namna hii.
Kama ulikuwepo msikiti basi ni kabla ya kujengwa upya kwa fedha za Gaddafi alizozikalia Nyerere mpaka anakufa. Mama Maria mwenyewe alitangaza kuwa kuna fedha Nyerere alipewa na Gaddafi za kujengea msikiti na utajengwa huko. Kama ni huo umejengwa upya au kuna mwingine umejengwa kwa hizo fedha baada ya kufa Nyerere hilo pia linawezekana. Si sifa yangu kusema uongo na nnauhakika na niyasemayo.
Waandishi wengi ndio akina nani? Mbali na Mohamed nitajie wengine ambao wamekuja na uthibitisho kuwa Nyerere alikuwa mdini.Evidence ndio kila kitu
Waandishi wengi wameonyesha alivyo mdini na athari zake hadi leo tunaziona..church influence is beyond normal to the goverment operations
Wamegawana Kikristo na Kiislamu? TCC na TEC kwa upande mmoja na BAKWATA upande mwingine wanapeleka majina kwa Rais na anateua kwa namna hiyo? Nadhani hawataishia hapo tu. Wataangalia pia kabila lipi lenye madaraka mengi na wapi. Haya mambo sawasawa na kula nyama ya mtu.Jasusi,
Tutakuwa tunarudia humo kwa humo.
Waislam baada ya kuzunguka nchi nzima wakiuelimisha umma kuhusu mfumokristo wametoa kijitabu kinachoonyesha viwango vya mambo mengi kati ya Waislam na Wakristo.
Bahati mbaya mimi sijakipata lakini katika ugawanajiwa madaraka Wakristo wamehodhi 83% na Waislam wamabakiziwa 17%.
Serikali imeombwa itoe maelezo hali hii imekujaje.
Tusubiri majibu.
Mohamed
Faiza,
Baada ya shughulizi zote hizo, Jaffar alikwenda kwenye msikiti mkubwa uliojengwa na Rais wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi, kwa ajili ya kuswali, kisha kupata chakula cha mchana kwenye Ukumbi wa Joseph Kizurira.
Source: Mtoto wa Amin anguruma Butiama
...Swahiba wetu huyu ati! Ukisoma Majira leo kule mwisho mwisho nimegusia hili. Alimpa Mwalimu pesa tukajenga msikiti Butiama, halafu Mkapa naye akaomba zingine saa hizi msikiti karibu unamalizika Dodoma...
Source: Neno La Leo: Kiongozi Wa Nchi Haui Watu Wake, Gaddafi Amewaua, Hana Aibu! - Wanabidii | Google Groups
Faiza,
Hapo haujaonyesha kuwa Nyerere alikalia fedha za Qadafi na Mama Maria ndiye aliyezitoa kujenga msikiti huo. Kubali umekosea na uombe msamaha kadamnasi kama ulivyotaka Mwanakijiji awaombe msamaha. Onyesha mfano.
Bibie,Na haya hapa maneno ya mwanae Vincent Nyerere:
...Nakumbuka Mwalimu Nyerere aliwahi kwenda Libya kwa Gaddafi na akaulizwa apewe msaada gani kwa wanakijiji wenzake Butiama, akitambua kuwa hapakuwa na msikiti bora na mzuri, aliomba fedha za ujenzi wa msikiti na ulijengwa na sasa ndiyo msikiti bora zaidi mkoani Mara...
Source: Rudisha Rasilimali kwa Wananchi: Si kweli kwamba hatuwezi kuchimba wenyewe madini
Kumbuka huo msikiti mzuri ulijengwa baada ya Nyerere kufa na si kabla kama ulikuwepo kabla basi ulikuwa si huo mzuri.
Sio Mwalimu tunayemfahamu! Akataliwe hata na aloowateua akina IGP Hamza Aziz wa Mtoni kwa Aziz Ali? Mwalimu alikuwa mvumilivu na msikivu pia. Ukumbuke pia kwamba kuijenga nchi isiyo na DINI kutoka TANU ya WAISLAMU wa misimamo mikali kama masheikh unaowataja hapo haikuwa kazi ndogo.
Kama wewe unashindwa kuomba msamaha kwa uwongo huu wa mchana kweupe unadhani nitamhimiza Mwanakjj aje hapa kukuomba msamaha? No.Sijakosea na sina cha kuomba msamaha, Nyerere alizikalia fedha za msikiti mpaka alivyokufa, baada ya kufa ndio msikiti ukajengwa kama una access na kina Nyerere uliza wakueleze.
Mwambie Mwenzako aje kuomba msamaha kwa kubandika Qur'an isivyo.
Angalau unafahamu Mwalimu alikuwa haabudu pesa. Hizi angezikalia za nini?! Ongopa mengine Faiza. Kama umeishiwa kopa kwa Mohamed ambaye mnaelekea kufanana kwa mambo mawili makubwa. Moja ni udini wenu. La pili ni namna mnavyoweza kuwasuta Marehemu au kujenga hoja ambazo mashahidi ni marehemu tayari.Sijakosea na sina cha kuomba msamaha, Nyerere alizikalia fedha za msikiti mpaka alivyokufa, baada ya kufa ndio msikiti ukajengwa kama una access na kina Nyerere uliza wakueleze.
Mwambie Mwenzako aje kuomba msamaha kwa kubandika Qur'an isivyo.
Sisumbuliwi na ujana wala utoto kama unavyofikiri. TANZANIA KWANZA DINI BAADAE.Mwakaboko,
Sijakutukana.
Uliposema kuwa umezaliwa baada ya uhuru nikajua wewe kwangu ni mdogo na nikatumia lugha tutumiayo watu wa pwani katika kumkanya mtoto mdogo ili awe na heshima.
"Mtoto aliyefunzwa."
Haina maana hukufunzwa.
Huenda umefunzwa lakini unataka kuonyesha ujuba tu, machachari ya ujana na utoto.
Lakini kama kweli wewe ni kijana mwenye adabu hutoingia tena humu kwa makeke kama yale.
Mohamed
Wildcard,Angalau unafahamu Mwalimu alikuwa haabudu pesa. Hizi angezikalia za nini?! Ongopa mengine Faiza. Kama umeishiwa kopa kwa Mohamed ambaye mnaelekea kufanana kwa mambo mawili makubwa. Moja ni udini wenu. La pili ni namna mnavyoweza kuwasuta Marehemu au kujenga hoja ambazo mashahidi ni marehemu tayari.
Bibie,
Vincent si mtoto wa Mwalimu, ni mtoto wa mdogo wake Mwalimu Nyerere, Kiboko. Bado hujathibitisha kuwa msikiti ulijengwa baada ya Nyerere kufariki. Unaona ugumu gani kuomba msamaha kwa kupotosha umma. Nimekuuliza, ulishafika Butiama? Huna jibu. Mimi mwenyewe nilikuwepo Butiama kwa mazishi ya Mwalimu. Msikiti nimeuona. Unarudi tena hapa na uongo wako eti ulijengwa baada ya Nyerere kufa. Uongo katika dini zote ni dhambi, bibie. Unachokifanya ni kurudia uwongo mara kwa mara ukidhani huko baadaye utaaminika kuwa kweli. Tuombe msamaha!
Kuijenga NCHI isiyo na DINI haikuwa kazi ndogo. Lazima wahanga walikuwepo katika kulitekeleza hili. Kama huyu Sheikh wako alikuwa mmoja wao basi. Hii ndio Tanzania alootuachia Mwalimu. Bahati ni kuwa hakufungwa bali alirudishwa kwao Zanzibar. Kule asilimia99 ni Waislamu. Kulimfaa zaidi.WC,
Wala siwezi kufanya manakasha kukupinga jinsi unavyomuelewa Nyerere. Hilo siwezi kanisa kwani nami katika utafiti wangu nimekutana na mengi ambayo baada ya watu kusoma nao waliniuliza kutaka kujua na kupata uhakika zaidi.
Mfano ni huu wa historia hii ambayo tumeizungumza sasa inafika juma la pili.
Wengi wakiniuliza huyu Abdu Sykes alikuwa mtu wa aina gani, uwezo wake ulikuwaje, vipi aliingiliana na watu kwa kiwango kile, kwa nini historia imemsahau nk. nk. na huu nimekupa mfano wa mtu mmoja tu.
Hamza Aziz alikuwa rafiki yangu sana ingawa tulikuwa tumepishana sana umri, akimfahamu baba yangu nk. nk. tukitaniana maana na yeye kazaliwa Kipata kama mimi na wote tukipenda nyimbo za Nat King Cole.
Kanipa mengi mpaka nikawa nashuku anafanya vile kwa makusudi ili nije siku moja nitumie yale alonieleza. Nikashuku ananieleza yale ili siku moja nije niwaeleze watu.
Ntakwambia kabla hajafa nilifuturu kwake na sikuwa peke yangu niliwapeleka watu fulani basi mazungumzo yakanoga akasema msiondoke hapa lazima leo tufuturu pamoja.
Akakirudia kisa cha kukataa kumkamata Sheikh Hassan bin Amir mbele ya wale wageni. Mimi nilikuwa nishakisikia mara nyingi tu. Akasema katika vitu anavyomshukuru Allah ni ile kupata fikra ya kukataa kumkamata Sheikh Hassan bin Amir.
Akasema, "Ningelimkamata mimi Sheikh Hassan bin Amir leo ningeliwatazamaje Waislam mimi?"
Huenda ikawa si rahisi kwa mtu ambaye hakukulia katia mazingira ya Dar es Salaam na ule Uislam kujua hadhi ya Sheikh Hassan bin Amir.
Lakini kukupa picha uweze kuelewa uzito wa jambo ni kama leo, IGP Said Mwema kwenda St. Joseph usiku wa manane na kumtoa Kadinali Pengo chumbani kwake amevaa pajama.
Sheikh Hassan bin Amir likamatwa usiku wa manane na alitolewa ndani kwake kavaa kanga.
Soma hii kidogo:
"Inspekta Jenerali wa Polisi, Hamza Aziz,mdogo wake Dossa alipopokea amri kutoka kwa rais kupitia Waziri wa Mambo yaNdani kuwa amkamate Sheikh Hassan bin Amir, hakuweza kuamini masikio yake.Alitaka afahamishwe sababu za kutaka kukamatwa Mufti ñ kiongozi wa juu kabisakatika safu ya uongozi wa Waislam katika Tanzania. Alipoambiwa kuwa sababu nikuwa anaihujumu serikali, Hamza Aziz alimwambia Waziri wa Mambo ya Ndani kuwahuenda kuna makosa katika amri ile. Alimfahamisha waziri kuwa yeye binafsialikuwa anamfahamu mzee yule toka yeye Hamza alipokuwa mtoto mdogo. AkimfahamuSheikh Hassan bin Amir kama mwalimu na mtu aliyeshiriki katika ukombozi waTanganyika. Msimamo wake heshima nahadhi yake mbele ya Waislam ipo juu kabisa. Inspekta Jenerali wa Polisialimwambia waziri kuwa haitawezekana kwake yeye kutii amri ile kwa sababu yeyehaamini kuwa tuhuma zile dhidi ya Mufti Sheikh Hassan bin Amir ni za kweli.Nyerere alifahamishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani kuwa Inspekta Generali waPolisi, Hamza Aziz amekataa kutii amri yake ya kumkamata Mufti. Nyerere alitoaamri kwa Usalama wa Taifa kumkamata Sheikh Hassan bin Amir. Hii ilikuwa nikinyume na utaratibu kwa kuwa Usalama wa Taifa hawana mamlaka ya kukamata watu.Usiku wa manane siku hiyo hiyo SheikhHassan bin Amir alikamatwa na makachero wa Usalama wa Taifa akapelekwa uwanjawa ndege na kurudishwa Zanzibar. [1]Inaelekea kulikuwa na mpango uliokuwa umetayarishwa kabla ya serikali yaMapinduzi Zanzibar kumpokea Sheikh Hassan bin Amir. Inasemekana mara kadhaaKarume alipata kumueleza Sheikh Hassan bin Amir kuwa Nyerere alikuwa hamtakinchini kwake na akawa anamshauri arudi nyumbani Zanzibar. Sheikh Hassanalikataa ushauri ule hadi alipokamatwa na kurudishwa kwa nguvu. Karume alimpaSheikh Hassan bin Amir hadhi zote alizostahili kama ulamaa na akamruhusukuendesha madras. Lakini Zanzibar ilikuwa imebadilika.Mapinduzi ya mwaka 1964yalikuwa yameingiza katika Zanzibar fikra potofu zilizokuwa zinapinga Uislam.Karume mwenyewe alikuwa ametoa amri ya kuchoma vitabu vyote vya dini. Nakala zaQurían Tukufu zilichomwa moto pamoja na taka za mji. Muslim Academy chuo kilichokuwakikisomesha masomo ya dini kilifungwa. Mashine za kuchapa kwa lugha ya Kiarabuzikatupwa kutoka Government Press. [1]Maulama wengi na wanafunzi wa Sheikh Hassan bin Amir walikuwa wamekimbiaZanzibar kwenda kuishi uhamishoni. Zanzibar haikuwa tena kitovu cha elimu namaarifa ya Kiislam. Sheikh Hassan bin Amir akawa sasa mfungwa katika nchi yakemwenyewe kwa kuwa hakuwa na ruhusa ya kuondoka visiwani hapo na kurejeaTanzania bara. Mara baada ya kukamatwa kwa Sheikh Hassan bin Amir, Adam Nasibuakatangaza kufanyika kwa mkutano ambao ulikuja kujulikana kama Mkutano waWaislam wa Taifa. Mkutano ambao ilitangazwa utafanyika Iringa kuanzia tarehe12-15 Desemba, 1968. Agenda kuu ya mkutano ule ilikuwa kujadili katiba kwaajili ya jumuiya mpya ya Waislam."
Kila ninapoalikwa kuhadhir kuhusu harakati za Waislam hiki ndicho kipande watu humwagikwa na machozi.
Mohamed