WC,
Wala siwezi kufanya manakasha kukupinga jinsi unavyomuelewa Nyerere. Hilo siwezi kanisa kwani nami katika utafiti wangu nimekutana na mengi ambayo baada ya watu kusoma nao waliniuliza kutaka kujua na kupata uhakika zaidi.
Mfano ni huu wa historia hii ambayo tumeizungumza sasa inafika juma la pili.
Wengi wakiniuliza huyu Abdu Sykes alikuwa mtu wa aina gani, uwezo wake ulikuwaje, vipi aliingiliana na watu kwa kiwango kile, kwa nini historia imemsahau nk. nk. na huu nimekupa mfano wa mtu mmoja tu.
Hamza Aziz alikuwa rafiki yangu sana ingawa tulikuwa tumepishana sana umri, akimfahamu baba yangu nk. nk. tukitaniana maana na yeye kazaliwa Kipata kama mimi na wote tukipenda nyimbo za Nat King Cole.
Kanipa mengi mpaka nikawa nashuku anafanya vile kwa makusudi ili nije siku moja nitumie yale alonieleza. Nikashuku ananieleza yale ili siku moja nije niwaeleze watu.
Ntakwambia kabla hajafa nilifuturu kwake na sikuwa peke yangu niliwapeleka watu fulani basi mazungumzo yakanoga akasema msiondoke hapa lazima leo tufuturu pamoja.
Akakirudia kisa cha kukataa kumkamata Sheikh Hassan bin Amir mbele ya wale wageni. Mimi nilikuwa nishakisikia mara nyingi tu. Akasema katika vitu anavyomshukuru Allah ni ile kupata fikra ya kukataa kumkamata Sheikh Hassan bin Amir.
Akasema, "Ningelimkamata mimi Sheikh Hassan bin Amir leo ningeliwatazamaje Waislam mimi?"
Huenda ikawa si rahisi kwa mtu ambaye hakukulia katia mazingira ya Dar es Salaam na ule Uislam kujua hadhi ya Sheikh Hassan bin Amir.
Lakini kukupa picha uweze kuelewa uzito wa jambo ni kama leo, IGP Said Mwema kwenda St. Joseph usiku wa manane na kumtoa Kadinali Pengo chumbani kwake amevaa pajama.
Sheikh Hassan bin Amir likamatwa usiku wa manane na alitolewa ndani kwake kavaa kanga.
Soma hii kidogo:
"Inspekta Jenerali wa Polisi, Hamza Aziz,mdogo wake Dossa alipopokea amri kutoka kwa rais kupitia Waziri wa Mambo yaNdani kuwa amkamate Sheikh Hassan bin Amir, hakuweza kuamini masikio yake.Alitaka afahamishwe sababu za kutaka kukamatwa Mufti ñ kiongozi wa juu kabisakatika safu ya uongozi wa Waislam katika Tanzania. Alipoambiwa kuwa sababu nikuwa anaihujumu serikali, Hamza Aziz alimwambia Waziri wa Mambo ya Ndani kuwahuenda kuna makosa katika amri ile. Alimfahamisha waziri kuwa yeye binafsialikuwa anamfahamu mzee yule toka yeye Hamza alipokuwa mtoto mdogo. AkimfahamuSheikh Hassan bin Amir kama mwalimu na mtu aliyeshiriki katika ukombozi waTanganyika. Msimamo wake heshima nahadhi yake mbele ya Waislam ipo juu kabisa. Inspekta Jenerali wa Polisialimwambia waziri kuwa haitawezekana kwake yeye kutii amri ile kwa sababu yeyehaamini kuwa tuhuma zile dhidi ya Mufti Sheikh Hassan bin Amir ni za kweli.Nyerere alifahamishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani kuwa Inspekta Generali waPolisi, Hamza Aziz amekataa kutii amri yake ya kumkamata Mufti. Nyerere alitoaamri kwa Usalama wa Taifa kumkamata Sheikh Hassan bin Amir. Hii ilikuwa nikinyume na utaratibu kwa kuwa Usalama wa Taifa hawana mamlaka ya kukamata watu.Usiku wa manane siku hiyo hiyo SheikhHassan bin Amir alikamatwa na makachero wa Usalama wa Taifa akapelekwa uwanjawa ndege na kurudishwa Zanzibar. [1]Inaelekea kulikuwa na mpango uliokuwa umetayarishwa kabla ya serikali yaMapinduzi Zanzibar kumpokea Sheikh Hassan bin Amir. Inasemekana mara kadhaaKarume alipata kumueleza Sheikh Hassan bin Amir kuwa Nyerere alikuwa hamtakinchini kwake na akawa anamshauri arudi nyumbani Zanzibar. Sheikh Hassanalikataa ushauri ule hadi alipokamatwa na kurudishwa kwa nguvu. Karume alimpaSheikh Hassan bin Amir hadhi zote alizostahili kama ulamaa na akamruhusukuendesha madras. Lakini Zanzibar ilikuwa imebadilika.Mapinduzi ya mwaka 1964yalikuwa yameingiza katika Zanzibar fikra potofu zilizokuwa zinapinga Uislam.Karume mwenyewe alikuwa ametoa amri ya kuchoma vitabu vyote vya dini. Nakala zaQurían Tukufu zilichomwa moto pamoja na taka za mji. Muslim Academy chuo kilichokuwakikisomesha masomo ya dini kilifungwa. Mashine za kuchapa kwa lugha ya Kiarabuzikatupwa kutoka Government Press. [1]Maulama wengi na wanafunzi wa Sheikh Hassan bin Amir walikuwa wamekimbiaZanzibar kwenda kuishi uhamishoni. Zanzibar haikuwa tena kitovu cha elimu namaarifa ya Kiislam. Sheikh Hassan bin Amir akawa sasa mfungwa katika nchi yakemwenyewe kwa kuwa hakuwa na ruhusa ya kuondoka visiwani hapo na kurejeaTanzania bara. Mara baada ya kukamatwa kwa Sheikh Hassan bin Amir, Adam Nasibuakatangaza kufanyika kwa mkutano ambao ulikuja kujulikana kama Mkutano waWaislam wa Taifa. Mkutano ambao ilitangazwa utafanyika Iringa kuanzia tarehe12-15 Desemba, 1968. Agenda kuu ya mkutano ule ilikuwa kujadili katiba kwaajili ya jumuiya mpya ya Waislam."
Kila ninapoalikwa kuhadhir kuhusu harakati za Waislam hiki ndicho kipande watu humwagikwa na machozi.
Mohamed