Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Hauwezi kuwa mnafiki halafu ukaacha kuwa mwizi. Hizi ni sifa kama pacha wale wa yai moja.

Hatuna ushahid wa nyerere kuiba na kufaidisha jamii yake huo ni ukweli

Kama kuiba labda ni hii ya kupeleka pesa za umma kanisani

Of course mimi nahisi intention yake ni kupata dhawabu kwa mungu wake (udini)

Nashawishika kuamini kuwa hata kuwabagua, kuwatesa waislamu amelifanya akifikiri kufanya hivyo ni kupata dhawabu kwa mungu wake

Ndiyo shida kubwa ya mwalimu alijali dini yake Udini) kupita taifa lake
 
Kama ulikuwepo msikiti basi ni kabla ya kujengwa upya kwa fedha za Gaddafi alizozikalia Nyerere mpaka anakufa. Mama Maria mwenyewe alitangaza kuwa kuna fedha Nyerere alipewa na Gaddafi za kujengea msikiti na utajengwa huko. Kama ni huo umejengwa upya au kuna mwingine umejengwa kwa hizo fedha baada ya kufa Nyerere hilo pia linawezekana. Si sifa yangu kusema uongo na nnauhakika na niyasemayo.
Pengine Faiza anazungumzia msikiti wa Dodoma. Vinginevyo ameamua kupinga mazuri ya Mwalimu kwa kila namna na kila silaha! Ni taabu kidogo kutoyaona mazuri ya Mwalimu. Kuna wakati anajidhalilisha kabisa kwa kuongopa namna hii.
 
Hapana.
Uspotoshe hapa. Msikiti ulikuwepo wakati wa mazishi na nimeenda tena Butiama kumsalimia Madaraka sikuona mabadiliko yeyote uliofanyiwa msikiti ule. Na ukiwa njiani kuelekea Mwitongo kutoka Musoma huwezi kukosa kuuona msikiti ule haujafanyiwa ukarabati, hasa kwa nje. Ni uongo kusema kuwa Nyerere alikalia hela ambazo aliziomba mwenyewe kwa Qadafi kujengea msikiti in the first place. Hivi Bibie umewahi kufika Butiama?
 
Sio "utakatifu" bali muujiza! Mwalimu hakuwa wa kawaida kama mimi na wewe tukibahatika kupewa nafasi alookuwa nayo. Mmekosa cha maana cha kumkosoa mmekimbilia UDINI.
Evidence ndio kila kitu

Waandishi wengi wameonyesha alivyo mdini na athari zake hadi leo tunaziona..church influence is beyond normal to the goverment operations
 
Pengine Faiza anazungumzia msikiti wa Dodoma. Vinginevyo ameamua kupinga mazuri ya Mwalimu kwa kila namna na kila silaha! Ni taabu kidogo kutoyaona mazuri ya Mwalimu. Kuna wakati anajidhalilisha kabisa kwa kuongopa namna hii.
Asichanganye basi. Msikiti wa Dodoma umejengwa majuzi. Unajua ukishakuwa na tabia ya kumchukia mtu hata lile jema analofanya mtu huyo unajitahidi kulionyesha kuwa ni uovu. Hichi ndicho kinachomsukuma Faiza na wapambe wake.
 
Kama ulikuwepo msikiti basi ni kabla ya kujengwa upya kwa fedha za Gaddafi alizozikalia Nyerere mpaka anakufa. Mama Maria mwenyewe alitangaza kuwa kuna fedha Nyerere alipewa na Gaddafi za kujengea msikiti na utajengwa huko. Kama ni huo umejengwa upya au kuna mwingine umejengwa kwa hizo fedha baada ya kufa Nyerere hilo pia linawezekana. Si sifa yangu kusema uongo na nnauhakika na niyasemayo.

Baada ya shughulizi zote hizo, Jaffar alikwenda kwenye msikiti mkubwa uliojengwa na Rais wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi, kwa ajili ya kuswali, kisha kupata chakula cha mchana kwenye Ukumbi wa Joseph Kizurira.

Source: Mtoto wa Amin anguruma Butiama

...Swahiba wetu huyu ati! Ukisoma Majira leo kule mwisho mwisho nimegusia hili. Alimpa Mwalimu pesa tukajenga msikiti Butiama, halafu Mkapa naye akaomba zingine saa hizi msikiti karibu unamalizika Dodoma...
Source: Neno La Leo: Kiongozi Wa Nchi Haui Watu Wake, Gaddafi Amewaua, Hana Aibu! - Wanabidii | Google Groups
 
Evidence ndio kila kitu

Waandishi wengi wameonyesha alivyo mdini na athari zake hadi leo tunaziona..church influence is beyond normal to the goverment operations
Waandishi wengi ndio akina nani? Mbali na Mohamed nitajie wengine ambao wamekuja na uthibitisho kuwa Nyerere alikuwa mdini.
 
Jasusi,

Tutakuwa tunarudia humo kwa humo.

Waislam baada ya kuzunguka nchi nzima wakiuelimisha umma kuhusu mfumokristo wametoa kijitabu kinachoonyesha viwango vya mambo mengi kati ya Waislam na Wakristo.

Bahati mbaya mimi sijakipata lakini katika ugawanajiwa madaraka Wakristo wamehodhi 83% na Waislam wamabakiziwa 17%.

Serikali imeombwa itoe maelezo hali hii imekujaje.

Tusubiri majibu.

Mohamed
Wamegawana Kikristo na Kiislamu? TCC na TEC kwa upande mmoja na BAKWATA upande mwingine wanapeleka majina kwa Rais na anateua kwa namna hiyo? Nadhani hawataishia hapo tu. Wataangalia pia kabila lipi lenye madaraka mengi na wapi. Haya mambo sawasawa na kula nyama ya mtu.
Namshukuru Mungu hayapo. Anayafikiri Mohamed na DINI yake tu. Hizi DINI tuzitumie kufunga ndoa na kuzikana tu.
 
Baada ya shughulizi zote hizo, Jaffar alikwenda kwenye msikiti mkubwa uliojengwa na Rais wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi, kwa ajili ya kuswali, kisha kupata chakula cha mchana kwenye Ukumbi wa Joseph Kizurira.

Source: Mtoto wa Amin anguruma Butiama

...Swahiba wetu huyu ati! Ukisoma Majira leo kule mwisho mwisho nimegusia hili. Alimpa Mwalimu pesa tukajenga msikiti Butiama, halafu Mkapa naye akaomba zingine saa hizi msikiti karibu unamalizika Dodoma...
Source: Neno La Leo: Kiongozi Wa Nchi Haui Watu Wake, Gaddafi Amewaua, Hana Aibu! - Wanabidii | Google Groups
Faiza,
Hapo haujaonyesha kuwa Nyerere alikalia fedha za Qadafi na Mama Maria ndiye aliyezitoa kujenga msikiti huo. Kubali umekosea na uombe msamaha kadamnasi kama ulivyotaka Mwanakijiji awaombe msamaha. Onyesha mfano.
 
Na haya hapa maneno ya mwanae Vincent Nyerere:

...Nakumbuka Mwalimu Nyerere aliwahi kwenda Libya kwa Gaddafi na akaulizwa apewe msaada gani kwa wanakijiji wenzake Butiama, akitambua kuwa hapakuwa na msikiti bora na mzuri, aliomba fedha za ujenzi wa msikiti na ulijengwa na sasa ndiyo msikiti bora zaidi mkoani Mara...
Source: Rudisha Rasilimali kwa Wananchi: Si kweli kwamba hatuwezi kuchimba wenyewe madini

Kumbuka huo msikiti mzuri ulijengwa baada ya Nyerere kufa na si kabla kama ulikuwepo kabla basi ulikuwa si huo mzuri.
 
Sijakosea na sina cha kuomba msamaha, Nyerere alizikalia fedha za msikiti mpaka alivyokufa, baada ya kufa ndio msikiti ukajengwa kama una access na kina Nyerere uliza wakueleze.

Mwambie Mwenzako aje kuomba msamaha kwa kubandika Qur'an isivyo.
 
Bibie,
Vincent si mtoto wa Mwalimu, ni mtoto wa mdogo wake Mwalimu Nyerere, Kiboko. Bado hujathibitisha kuwa msikiti ulijengwa baada ya Nyerere kufariki. Unaona ugumu gani kuomba msamaha kwa kupotosha umma. Nimekuuliza, ulishafika Butiama? Huna jibu. Mimi mwenyewe nilikuwepo Butiama kwa mazishi ya Mwalimu. Msikiti nimeuona. Unarudi tena hapa na uongo wako eti ulijengwa baada ya Nyerere kufa. Uongo katika dini zote ni dhambi, bibie. Unachokifanya ni kurudia uwongo mara kwa mara ukidhani huko baadaye utaaminika kuwa kweli. Tuombe msamaha!
 
Sio Mwalimu tunayemfahamu! Akataliwe hata na aloowateua akina IGP Hamza Aziz wa Mtoni kwa Aziz Ali? Mwalimu alikuwa mvumilivu na msikivu pia. Ukumbuke pia kwamba kuijenga nchi isiyo na DINI kutoka TANU ya WAISLAMU wa misimamo mikali kama masheikh unaowataja hapo haikuwa kazi ndogo.

WC,

Wala siwezi kufanya manakasha kukupinga jinsi unavyomuelewa Nyerere. Hilo siwezi kanisa kwani nami katika utafiti wangu nimekutana na mengi ambayo baada ya watu kusoma nao waliniuliza kutaka kujua na kupata uhakika zaidi.

Mfano ni huu wa historia hii ambayo tumeizungumza sasa inafika juma la pili.

Wengi wakiniuliza huyu Abdu Sykes alikuwa mtu wa aina gani, uwezo wake ulikuwaje, vipi aliingiliana na watu kwa kiwango kile, kwa nini historia imemsahau nk. nk. na huu nimekupa mfano wa mtu mmoja tu.

Hamza Aziz alikuwa rafiki yangu sana ingawa tulikuwa tumepishana sana umri, akimfahamu baba yangu nk. nk. tukitaniana maana na yeye kazaliwa Kipata kama mimi na wote tukipenda nyimbo za Nat King Cole.

Kanipa mengi mpaka nikawa nashuku anafanya vile kwa makusudi ili nije siku moja nitumie yale alonieleza. Nikashuku ananieleza yale ili siku moja nije niwaeleze watu.

Ntakwambia kabla hajafa nilifuturu kwake na sikuwa peke yangu niliwapeleka watu fulani basi mazungumzo yakanoga akasema msiondoke hapa lazima leo tufuturu pamoja.

Akakirudia kisa cha kukataa kumkamata Sheikh Hassan bin Amir mbele ya wale wageni. Mimi nilikuwa nishakisikia mara nyingi tu. Akasema katika vitu anavyomshukuru Allah ni ile kupata fikra ya kukataa kumkamata Sheikh Hassan bin Amir.

Akasema, "Ningelimkamata mimi Sheikh Hassan bin Amir leo ningeliwatazamaje Waislam mimi?"

Huenda ikawa si rahisi kwa mtu ambaye hakukulia katia mazingira ya Dar es Salaam na ule Uislam kujua hadhi ya Sheikh Hassan bin Amir.

Lakini kukupa picha uweze kuelewa uzito wa jambo ni kama leo, IGP Said Mwema kwenda St. Joseph usiku wa manane na kumtoa Kadinali Pengo chumbani kwake amevaa pajama.

Sheikh Hassan bin Amir likamatwa usiku wa manane na alitolewa ndani kwake kavaa kanga.

Soma hii kidogo:

"Inspekta Jenerali wa Polisi, Hamza Aziz,mdogo wake Dossa alipopokea amri kutoka kwa rais kupitia Waziri wa Mambo yaNdani kuwa amkamate Sheikh Hassan bin Amir, hakuweza kuamini masikio yake.Alitaka afahamishwe sababu za kutaka kukamatwa Mufti ñ kiongozi wa juu kabisakatika safu ya uongozi wa Waislam katika Tanzania. Alipoambiwa kuwa sababu nikuwa anaihujumu serikali, Hamza Aziz alimwambia Waziri wa Mambo ya Ndani kuwahuenda kuna makosa katika amri ile. Alimfahamisha waziri kuwa yeye binafsialikuwa anamfahamu mzee yule toka yeye Hamza alipokuwa mtoto mdogo. AkimfahamuSheikh Hassan bin Amir kama mwalimu na mtu aliyeshiriki katika ukombozi waTanganyika. Msimamo wake heshima nahadhi yake mbele ya Waislam ipo juu kabisa. Inspekta Jenerali wa Polisialimwambia waziri kuwa haitawezekana kwake yeye kutii amri ile kwa sababu yeyehaamini kuwa tuhuma zile dhidi ya Mufti Sheikh Hassan bin Amir ni za kweli.Nyerere alifahamishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani kuwa Inspekta Generali waPolisi, Hamza Aziz amekataa kutii amri yake ya kumkamata Mufti. Nyerere alitoaamri kwa Usalama wa Taifa kumkamata Sheikh Hassan bin Amir. Hii ilikuwa nikinyume na utaratibu kwa kuwa Usalama wa Taifa hawana mamlaka ya kukamata watu.Usiku wa manane siku hiyo hiyo SheikhHassan bin Amir alikamatwa na makachero wa Usalama wa Taifa akapelekwa uwanjawa ndege na kurudishwa Zanzibar. [1]Inaelekea kulikuwa na mpango uliokuwa umetayarishwa kabla ya serikali yaMapinduzi Zanzibar kumpokea Sheikh Hassan bin Amir. Inasemekana mara kadhaaKarume alipata kumueleza Sheikh Hassan bin Amir kuwa Nyerere alikuwa hamtakinchini kwake na akawa anamshauri arudi nyumbani Zanzibar. Sheikh Hassanalikataa ushauri ule hadi alipokamatwa na kurudishwa kwa nguvu. Karume alimpaSheikh Hassan bin Amir hadhi zote alizostahili kama ulamaa na akamruhusukuendesha madras. Lakini Zanzibar ilikuwa imebadilika.Mapinduzi ya mwaka 1964yalikuwa yameingiza katika Zanzibar fikra potofu zilizokuwa zinapinga Uislam.Karume mwenyewe alikuwa ametoa amri ya kuchoma vitabu vyote vya dini. Nakala zaQurían Tukufu zilichomwa moto pamoja na taka za mji. Muslim Academy chuo kilichokuwakikisomesha masomo ya dini kilifungwa. Mashine za kuchapa kwa lugha ya Kiarabuzikatupwa kutoka Government Press. [1]Maulama wengi na wanafunzi wa Sheikh Hassan bin Amir walikuwa wamekimbiaZanzibar kwenda kuishi uhamishoni. Zanzibar haikuwa tena kitovu cha elimu namaarifa ya Kiislam. Sheikh Hassan bin Amir akawa sasa mfungwa katika nchi yakemwenyewe kwa kuwa hakuwa na ruhusa ya kuondoka visiwani hapo na kurejeaTanzania bara. Mara baada ya kukamatwa kwa Sheikh Hassan bin Amir, Adam Nasibuakatangaza kufanyika kwa mkutano ambao ulikuja kujulikana kama Mkutano waWaislam wa Taifa. Mkutano ambao ilitangazwa utafanyika Iringa kuanzia tarehe12-15 Desemba, 1968. Agenda kuu ya mkutano ule ilikuwa kujadili katiba kwaajili ya jumuiya mpya ya Waislam."

Kila ninapoalikwa kuhadhir kuhusu harakati za Waislam hiki ndicho kipande watu humwagikwa na machozi.

Mohamed
 
Sijakosea na sina cha kuomba msamaha, Nyerere alizikalia fedha za msikiti mpaka alivyokufa, baada ya kufa ndio msikiti ukajengwa kama una access na kina Nyerere uliza wakueleze.

Mwambie Mwenzako aje kuomba msamaha kwa kubandika Qur'an isivyo.
Kama wewe unashindwa kuomba msamaha kwa uwongo huu wa mchana kweupe unadhani nitamhimiza Mwanakjj aje hapa kukuomba msamaha? No.
 
Sijakosea na sina cha kuomba msamaha, Nyerere alizikalia fedha za msikiti mpaka alivyokufa, baada ya kufa ndio msikiti ukajengwa kama una access na kina Nyerere uliza wakueleze.

Mwambie Mwenzako aje kuomba msamaha kwa kubandika Qur'an isivyo.
Angalau unafahamu Mwalimu alikuwa haabudu pesa. Hizi angezikalia za nini?! Ongopa mengine Faiza. Kama umeishiwa kopa kwa Mohamed ambaye mnaelekea kufanana kwa mambo mawili makubwa. Moja ni udini wenu. La pili ni namna mnavyoweza kuwasuta Marehemu au kujenga hoja ambazo mashahidi ni marehemu tayari.
 
Mwakaboko,

Sijakutukana.

Uliposema kuwa umezaliwa baada ya uhuru nikajua wewe kwangu ni mdogo na nikatumia lugha tutumiayo watu wa pwani katika kumkanya mtoto mdogo ili awe na heshima.

"Mtoto aliyefunzwa."

Haina maana hukufunzwa.
Huenda umefunzwa lakini unataka kuonyesha ujuba tu, machachari ya ujana na utoto.

Lakini kama kweli wewe ni kijana mwenye adabu hutoingia tena humu kwa makeke kama yale.

Mohamed
Sisumbuliwi na ujana wala utoto kama unavyofikiri. TANZANIA KWANZA DINI BAADAE.
Asante kwako wewe mwenye busara ya Kuwatenganisha WATZ kwa misingi ya UDINI.
Mimi sio kijana kama unavyofikiri, ww mwenye busara ya kuwatenganisha WATZ, labda utaniita ni kijana ukinilinganisha na umri wako. Maana ktk lika la vijana tayari nimetoka huko.

Ila siwezi shangaa ukiniita kijana maana watu wa PWANI banaaaaaaa wanapenda sana kuwaita watu wazima vijana. Kama kumbukumbu zako ziko sawa sawa utakumbuka mwaka ule uleeeeeeeeeeeeeeee kwani umesahau, kuna mtu kwa sasa ni maarufu sana akiwa na umri wa zaidi ya miaka 50 mlisema ni kijana, nadhani umekumbuka hata jina lake pia (sina haja ya kulitaja unalijua).

Narudia nimelelewa vema na wazazi wangu wa thamani hawakunipa sumu ya ubaguzi unayotuilisha ww leo, uniambiaye kuwa una busara. Busara uliyonayo ni questionable kuwatenganisha WATYZ ni busara, No MS think twice about this. U have a hidden agenda in this sio bure. Wakati ukifika itakapokuwa dhahiri everyone will remember this
 
Angalau unafahamu Mwalimu alikuwa haabudu pesa. Hizi angezikalia za nini?! Ongopa mengine Faiza. Kama umeishiwa kopa kwa Mohamed ambaye mnaelekea kufanana kwa mambo mawili makubwa. Moja ni udini wenu. La pili ni namna mnavyoweza kuwasuta Marehemu au kujenga hoja ambazo mashahidi ni marehemu tayari.
Wildcard,
Unajua nini. Hawa watu wamedhamiria kweli kum-paint Nyerere in the darkest light possible. Hata pale mazuri yake yanapowasuta wanajaribu kuyapuuza au kuyaweka katika mwanga tofauti. Nitakupa mfano mmoja tu. Kuna kisa kimoja kaelezea Mohamed katika mojawapo ya mabandiko yake juu ya mama mmoja wa Singida aliyemwazima Mwalimu baibui yake kumwezesha Mwalimu asikamatwe na authorities. Mohamed kasimulia jinsi yule mama alivyomfuata Mwalimu Dar-es-Salaam kuulizia baibui yake ( I think this was years later) na Mwalimu alimkumbuka huyu bibi na akamjengea nyumba huko kwao Singida. Lakini hili hutaliona kwenye kitabu cha Mohamed kwamba huyu Nyerere aliyefadhiliwa na Waislamu kumbe kuna wakati alirudisha fadhila? Sasa ni hayo hayo ya msikiti wa Butiama. Faiza hawezi kuamini kwenye akili zake kwamba Nyerere huyu huyu tunayemtuhumu kuwachukia Waislamu, of all things aliwaombea Waislamu wa Butiama hela za kujenga msikiti? Kwao haiingii akilini kabisa kwa sababu ya mindset waliyo nayo. It goes against their grain.
 
Bibie,
Vincent si mtoto wa Mwalimu, ni mtoto wa mdogo wake Mwalimu Nyerere, Kiboko. Bado hujathibitisha kuwa msikiti ulijengwa baada ya Nyerere kufariki. Unaona ugumu gani kuomba msamaha kwa kupotosha umma. Nimekuuliza, ulishafika Butiama? Huna jibu. Mimi mwenyewe nilikuwepo Butiama kwa mazishi ya Mwalimu. Msikiti nimeuona. Unarudi tena hapa na uongo wako eti ulijengwa baada ya Nyerere kufa. Uongo katika dini zote ni dhambi, bibie. Unachokifanya ni kurudia uwongo mara kwa mara ukidhani huko baadaye utaaminika kuwa kweli. Tuombe msamaha!

Mtoto wa mdogo wake mwalim si mtoto wa Mwalim, huo ndio Utanzania uujawao wewe?

Hakuna cha kuomba msamaha nina uhakika na niyasemayo, wewe si unajidai kuwa una access na kina Nyerere na Butiama uliza huko uelezwe.

Ukipenda amini ukipenda usiamini hivyo ndivyo ilivyo.
 
WC,

Wala siwezi kufanya manakasha kukupinga jinsi unavyomuelewa Nyerere. Hilo siwezi kanisa kwani nami katika utafiti wangu nimekutana na mengi ambayo baada ya watu kusoma nao waliniuliza kutaka kujua na kupata uhakika zaidi.

Mfano ni huu wa historia hii ambayo tumeizungumza sasa inafika juma la pili.

Wengi wakiniuliza huyu Abdu Sykes alikuwa mtu wa aina gani, uwezo wake ulikuwaje, vipi aliingiliana na watu kwa kiwango kile, kwa nini historia imemsahau nk. nk. na huu nimekupa mfano wa mtu mmoja tu.

Hamza Aziz alikuwa rafiki yangu sana ingawa tulikuwa tumepishana sana umri, akimfahamu baba yangu nk. nk. tukitaniana maana na yeye kazaliwa Kipata kama mimi na wote tukipenda nyimbo za Nat King Cole.

Kanipa mengi mpaka nikawa nashuku anafanya vile kwa makusudi ili nije siku moja nitumie yale alonieleza. Nikashuku ananieleza yale ili siku moja nije niwaeleze watu.

Ntakwambia kabla hajafa nilifuturu kwake na sikuwa peke yangu niliwapeleka watu fulani basi mazungumzo yakanoga akasema msiondoke hapa lazima leo tufuturu pamoja.

Akakirudia kisa cha kukataa kumkamata Sheikh Hassan bin Amir mbele ya wale wageni. Mimi nilikuwa nishakisikia mara nyingi tu. Akasema katika vitu anavyomshukuru Allah ni ile kupata fikra ya kukataa kumkamata Sheikh Hassan bin Amir.

Akasema, "Ningelimkamata mimi Sheikh Hassan bin Amir leo ningeliwatazamaje Waislam mimi?"

Huenda ikawa si rahisi kwa mtu ambaye hakukulia katia mazingira ya Dar es Salaam na ule Uislam kujua hadhi ya Sheikh Hassan bin Amir.

Lakini kukupa picha uweze kuelewa uzito wa jambo ni kama leo, IGP Said Mwema kwenda St. Joseph usiku wa manane na kumtoa Kadinali Pengo chumbani kwake amevaa pajama.

Sheikh Hassan bin Amir likamatwa usiku wa manane na alitolewa ndani kwake kavaa kanga.

Soma hii kidogo:

"Inspekta Jenerali wa Polisi, Hamza Aziz,mdogo wake Dossa alipopokea amri kutoka kwa rais kupitia Waziri wa Mambo yaNdani kuwa amkamate Sheikh Hassan bin Amir, hakuweza kuamini masikio yake.Alitaka afahamishwe sababu za kutaka kukamatwa Mufti ñ kiongozi wa juu kabisakatika safu ya uongozi wa Waislam katika Tanzania. Alipoambiwa kuwa sababu nikuwa anaihujumu serikali, Hamza Aziz alimwambia Waziri wa Mambo ya Ndani kuwahuenda kuna makosa katika amri ile. Alimfahamisha waziri kuwa yeye binafsialikuwa anamfahamu mzee yule toka yeye Hamza alipokuwa mtoto mdogo. AkimfahamuSheikh Hassan bin Amir kama mwalimu na mtu aliyeshiriki katika ukombozi waTanganyika. Msimamo wake heshima nahadhi yake mbele ya Waislam ipo juu kabisa. Inspekta Jenerali wa Polisialimwambia waziri kuwa haitawezekana kwake yeye kutii amri ile kwa sababu yeyehaamini kuwa tuhuma zile dhidi ya Mufti Sheikh Hassan bin Amir ni za kweli.Nyerere alifahamishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani kuwa Inspekta Generali waPolisi, Hamza Aziz amekataa kutii amri yake ya kumkamata Mufti. Nyerere alitoaamri kwa Usalama wa Taifa kumkamata Sheikh Hassan bin Amir. Hii ilikuwa nikinyume na utaratibu kwa kuwa Usalama wa Taifa hawana mamlaka ya kukamata watu.Usiku wa manane siku hiyo hiyo SheikhHassan bin Amir alikamatwa na makachero wa Usalama wa Taifa akapelekwa uwanjawa ndege na kurudishwa Zanzibar. [1]Inaelekea kulikuwa na mpango uliokuwa umetayarishwa kabla ya serikali yaMapinduzi Zanzibar kumpokea Sheikh Hassan bin Amir. Inasemekana mara kadhaaKarume alipata kumueleza Sheikh Hassan bin Amir kuwa Nyerere alikuwa hamtakinchini kwake na akawa anamshauri arudi nyumbani Zanzibar. Sheikh Hassanalikataa ushauri ule hadi alipokamatwa na kurudishwa kwa nguvu. Karume alimpaSheikh Hassan bin Amir hadhi zote alizostahili kama ulamaa na akamruhusukuendesha madras. Lakini Zanzibar ilikuwa imebadilika.Mapinduzi ya mwaka 1964yalikuwa yameingiza katika Zanzibar fikra potofu zilizokuwa zinapinga Uislam.Karume mwenyewe alikuwa ametoa amri ya kuchoma vitabu vyote vya dini. Nakala zaQurían Tukufu zilichomwa moto pamoja na taka za mji. Muslim Academy chuo kilichokuwakikisomesha masomo ya dini kilifungwa. Mashine za kuchapa kwa lugha ya Kiarabuzikatupwa kutoka Government Press. [1]Maulama wengi na wanafunzi wa Sheikh Hassan bin Amir walikuwa wamekimbiaZanzibar kwenda kuishi uhamishoni. Zanzibar haikuwa tena kitovu cha elimu namaarifa ya Kiislam. Sheikh Hassan bin Amir akawa sasa mfungwa katika nchi yakemwenyewe kwa kuwa hakuwa na ruhusa ya kuondoka visiwani hapo na kurejeaTanzania bara. Mara baada ya kukamatwa kwa Sheikh Hassan bin Amir, Adam Nasibuakatangaza kufanyika kwa mkutano ambao ulikuja kujulikana kama Mkutano waWaislam wa Taifa. Mkutano ambao ilitangazwa utafanyika Iringa kuanzia tarehe12-15 Desemba, 1968. Agenda kuu ya mkutano ule ilikuwa kujadili katiba kwaajili ya jumuiya mpya ya Waislam."

Kila ninapoalikwa kuhadhir kuhusu harakati za Waislam hiki ndicho kipande watu humwagikwa na machozi.

Mohamed
Kuijenga NCHI isiyo na DINI haikuwa kazi ndogo. Lazima wahanga walikuwepo katika kulitekeleza hili. Kama huyu Sheikh wako alikuwa mmoja wao basi. Hii ndio Tanzania alootuachia Mwalimu. Bahati ni kuwa hakufungwa bali alirudishwa kwao Zanzibar. Kule asilimia99 ni Waislamu. Kulimfaa zaidi.
 
Jasusi,

Mjadala haujafika tamati bana mbona ndio kwanza alfajiri kunakucha au umechoka kujadiliana?? Vp mzee mwenzangu unakimbia jamvi?
 
Back
Top Bottom