Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Mohamed,

Sie ni wanadaamu tunaghafilika but sio kutuuita wanafiki hilo sikubaliani nalo. Alichokizungumza Faiza ni cha msingi na kwakweli ana haki ya msingi kutukasirikia kwa kutokuona but sio kutuita wanafiki kwani unafiki ni tabia ya mtu au wasifu wa mtu. Wasifu huo mtume SAW alishatuambia ni watu au mtu wa aina gani kwa kusema mnafiki ana sifa tatu a. Kwanza anasema uongo b. Anafanya hiyana akiaminiwa c. Vile vile hana miadi. Labda tumuuliza tumesema uongo wapi hadi tustahili kuitwa wanafiki? Tumefanya hiyana kwa amana ipi tuliyopewa? Tumevunja miadi ipi.

Lazima tuelewane jamani Quran si kitu cha kuchezea kwani Tafsir ya Quran wanazuoni wanasema kila aya ina maana zaidi ya 50,000. Neno moja laweza kuwa na maana zaidi ya moja mfano hadatha, inaweza kuwa hadithu, inaweza kuwa muhdatha etc. Sasa kama mtu huna elimu nayo si vema ukajiingiza kulisema jambo. Imam Shaffi (R.A) anasema mtu anayesema sijui basi huyo amesema kauli ya kweli. Ndio sababu wengine wetu katika mijadala ya dini tunachangia mara chache sana. Kwani unaweza kupotosha maana ikawa ndivyo sivyo.

Tusamehe kwa kutosema lolote kuhusu Quran lakini hata kama tumeliona hatuwezi kulisemea wengine wetu kwasababu elimu hiyo hatuna. Tunajua kusoma Alif-be basi. Tunajua kuhifadhi quran basi. Lakini maana ya maneno yake wengine ni mafakiri wa elimu hiyo na hilo sio ni unafiki bali ni ujinga wa kutokuwa na elimu hiyo.

FF tuwie radhi kwa kughafilika but sio kutuita wanafiki kwani huo si unafiki bali kughafilika kutokana na uchache wetu wa elimu kuhusu Quran.
Hivi kule Tunisia, Libya, Misri, Yemen, Syria, Lebanon, Somalia,..., Qur'an haipo nini? Hakuna vitabu vimeivuruga dunia kama vitabu hivi viwili, Biblia na Qur'an. Walioviandika hawapo kama ambavyo Mohamed hatokuwepo kitabu chake kikianguka mikononi mwa vichaa fulani wakakifanyia kazi. Kusoma na kuelewa ni vitu viwili tofauti.
 
.

WC,
nafikiri sana unaanza kuchanganya mambo. Naomba ujifunze nini wajibu wa Serikali kwa wananchi wake. Jiulize kwanini miaka 50 tokea uhuru wenu mpaka leo baadhi ya sehemu zimeendelea sana kiuchumi na nyingine bado kabisa. Lakini suala la msingi serikali ilikuwa wapi mpaka sehemu moja inandelea sana kuliko nyingine? kwanini isitoe kipaumbele na kuondoa hiyo gap ya maendeleo kwa jamii au wananchi wake?

Jiulize kwanini makanisa yanaanzissha mashule na mahospital? je kwa fedha zao au wanafadhiliwa? Je umepitia bajeti enu (Tanganyika) ya mwaka 2009/2010 na ile ya 2010/2011 kuona misamaha ya kodi hususan kwa hizi taasisi za kidini? vile vile angalia na Mou ya kanisa na serikali ya tanganyika? Je kuna uwiano hapo? Je serikali inalitazamaje suala hilo hicho ndio mjiulize.

Cha msingi ni serikali enu kuwa sikivu kwaa raia wake hususan wale wanaolalama kuonewa na kudhulumiwa haki yao tena wanaweka malalamiko hayo kimaandishi na kuipa serikali. Kumbukeni kuwa hata mbuyu ulianza kama mchicha.

Hakuna amani wala upende penye dhulma na pasipo na haki. Na sasa dalili zote zipo hewani . sasa sijui mnasubiri kifo.

Jingine pia, nilitoa mfano humu na kuorodhesha idadi ya shule binafsi in 1988, miaka minne kabla ya hiyo so called MoU ndani ya mkoa wa Mbeya. Kulikuwa na shule nyingi binafsi za sekondari zaidi ya mara mbili ya zile zilizokuwa Dar. Wilaya ya Rungwe pekee ilikuwa na Shule nyingi binafsi kuliko Mkoa wa Dar es Salaam. Sasa usipojiuliza kwa nini basi itabakia speculations na hisia ambazo hazitusaidii. Kama we sincerely go deep na kufanya utafiti tutajua tatizo ni nini. Shule za sekondari za serikali zilikuwa chche sana wakati huo hivyo option ikawa shule binafsi, je zilijengwaje na nani na zilijiendeshaje. Na kwa nini Dar kwenye high population, wasomi, wenye hela enzi hizo kulikuwa na shule chache sana?
 
Hivi kule Tunisia, Libya, Misri, Yemen, Syria, Lebanon, Somalia,..., Qur'an haipo nini? Hakuna vitabu vimeivuruga dunia kama vitabu hivi viwili, Biblia na Qur'an. Walioviandika hawapo kama ambavyo Mohamed hatokuwepo kitabu chake kikianguka mikononi mwa vichaa fulani wakakifanyia kazi. Kusoma na kuelewa ni vitu viwili tofauti.

Tafadhali usiseme usichokijua.

Tatizo kote sio dini bali ni ukabila.

Fuatilia hilo kisha utakuja thibitisha kwetu.
 
Wildcard,

Sidhani kama barubaru na wenzake watakuelwa katika hili. Nilisoma makala ya mwanahalisi inayosema Cheza kama pele, panga mipango kama kaanisa katoliki, kuna mdau aliileta hapa JF pia lakini baadhi ya watu wakaishia kumbeza. Ungeipata hiyo na hawa wenzetu wakiisoma wakiwa open minded watajifunza kitu lakini wasipokubali kwamba wanatakiwa kujitathmini wao wenyewe, watakuwa ni watu wa kulalama siku zote. Wasiwasi wangu mkubwa hali itakuwaje kama tutapata raisi asiye muislamu 2015 na kuendelea, maana sasahivi top cream yote yao lakini wananung'unika!

Je ni msaada gani au ufadhili gani wakati mnawabainia kwa kila angle. OIC hamtaki na wakipata pesa zozote mnasema za kigaidi au alqaida. sasa mnategemea nini?

Msibeze kitu pasi na kujua ukweli umesimama wapi?
 
Ukitaka kujua ufadhili umepungua au umezidi ninakupa sehemu ambayo ipo wazi kabisaaaa.

Wewe pitia bajeti za Tz hususan ya 2009/2010 na ile ya 2010/2011 na uangalie misamaha ya kodi hususan kwa taasisi za kidini. Hapo utaona ukweli wa mambo. Jitahidi sana kuwa na sources na takwimu kabla kusema kitu.

Lakini pia kama utajifunza wajibu wa Serikali yoyote ya halali kwa wananchi wake itakuwa na manufaa zaidi. Hiyo MOU ni kielellezo thabiti kwako kwani siku zote kulea mimba si kazi bali kazi na kulea mwana. Kwanini pesa zinazotolewa kutokana na MOU zisielekezwe kwenye shule zenu za kata na zahanati za serikali? Je kunani?

Lakini jiulize kama waliweza kujenga kwnini washindwe kuendeleza na kuchote pesa za Serikali ziendeleze miradi yao?

Lakini mwisho nilikuwa Mtz lakini sasa sipo tena nimerudi kwetu Oman na kuchukua uraia wangu wa asili. Sina uraia pacha.
Barubaru,
Nashukuru umeweka wazi URAIA wako. Kumbe unatusaidia tugongane kwa UDINI halafu tusio na pa kwenda kama wewe tufanyeje! Misamaha unayoisema haina tatizo. Hospitali zinajengwa, vyuovikuu vinachipuka kama uyoga, shule zinajengwa sana tu. Tatizo ni mapesa anayokwapua mtu kama Rostam ambaye naye nadhani yuko mbioni kuukana UTANZANIA.
 
Tafadhali usiseme usichokijua.

Tatizo kote sio dini bali ni ukabila.

Fuatilia hilo kisha utakuja thibitisha kwetu.
Ukabila gani labda Ukoo. DINI, LUGHA moja. Qur'an imeshindwa kusaidia kama Faiza anavyoipamba hapa?
 
Raisi wenu, makamu wa raisi wenu, IGP wenu, CJ wenu, waziri wa elimu wenu, mkurugenzi TISS wenu. Mnataka mpewe nini tena??

Sasa niambie ni nani anayewabania hiyo OIC. Niliwahi kuisikia siku za mwanzo mwanzo za utawala wa Kikwete lakini baadae ikawa kimyaaaaaaa hadi mlipoibuka na hoja ya mahakama ya kadhi!

tatizo ni mfumo.

Je unajuwa polisi hususan wale rankless wanafuata mfumo gani wa likizo?

Je ma sister wana mfumo gani mkataba wao?
 
tatizo ni mfumo.

Je unajuwa polisi hususan wale rankless wanafuata mfumo gani wa likizo?

Je ma sister wana mfumo gani mkataba wao?
Mfumo ukisukwa barabara( sio barubaru!) hao akina JMK, IGP, ....., wangepenyaje wakafika hapo walipo. Kama ambavyo Mkurya hawezi kumlaumu Mchagga kwa kukosa ELIMU, MWISLAMU naye ni makosa kumlaumu MKRISTO kwa kukosa ELIMU. Haya yana historia ya peke yake.
 
Nimechukua time kama nilivyoahidi na phew ! kuna mengi yamesemwa humu hadi kufikia kuchombeza kuwa Mag3 kakimbia mjadala ! Hili wazushi kama kawaida yao wamelirudia si mara moja, na haya ndiyo ninayoyaita porojo kama anayoyasimulia huyo anayejiita Mohamed Said. Mimi ni binadamu, naenda kibaruani, napumzika, nalala, naugua na ninasafiri - sikeshi hapa JF 24/7 kama FaizaFoxy, yeye yupo kibaruani na kwa mpango maalum, ambao hata hivyo sitasita kuwaambia ukweli, hautafanikiwa. Hautafanikiwa si hapa Tanzania ninayoijua fika toka kabla na baada ya uhuru kwani misingi aliyoijenga Mwalimu Nyerere ya upendo na amani bila kubaguana katu hawataweza kuivunja.

Ni porojo tu na kwa hakika zingeweza kupuuzwa kama tu hazikutolewa wakati huu. Hebu tuanze kwa kujiuliza kidogo tu, why now ? Wakati uongozi wote wa juu umeshikwa na Waislamu, kuna kikundi cha Waislaam wamepewa pasi kupita mikoani kupandikiza chuki miongoni mwa wananchi kwa kuchochea mifarakano ya kidini, why now ? Wakati viongozi wote wa juu wa serikali na chama tawala cha CCM ni Waislaam, kuna mchochezi kwa jina Mohamed Said amepewa pasi anaandika magazetini kuwa Baba wa Taifa kwa kuuchukia Uislaam, kwa makusudi aliwakandamiza Waislaam, why now ? Jibu lililo wazi kabisa hata kwa kipofu ni kwa sababu CCM inaelekea kupoteza imani miongoni mwa wananchi.

FaizaFoxy ni mfano halisi wa hali inayotubidi sisi sote wapenda amani wa nchi hii bila kujali dini wala kabila tupambane nayo bila kurudi nyuma. FaizaFoxy represents a symbol, an institution and a state sponsored legion which has all state resources at its disposal. FaizaFoxy hahitaji kulala, kula hata kwenda uani, anachohitaji ni kubadilisha umbo tu kidogo na naona sasa anatishia hata kuwaumbua kwa majina wachangiaji, mimi namwambia bring it on. Huu mpango waliokuwa nao hawa wachochezi umeanza zamani sana lakini kwa sababu ya taifa letu kujengwa katika misingi imara, kazi ya kuibomoa misingi hiyo imekuwa ngumu ila wamepata kaupenyo kadogo kwa kutumia Udini.

Mohamed Said represents a tool and a very convenient tool kwa sababu ni rahisi kuteka sehemu ya jamii kwa kutumia udini. Fikiria mtu anakubaliana na hoja kuwa serikali inayoongozwa na Waislaam inawadhulumu Waislaam hao hao kwa sababu inaongozwa kwa mfumoKristo ! Huu Mfumo Kristo unaowapa nafasi viongozi wote wa juu serikalini kuwa Waislaam kwa nia ya kuukandamiza Uislaam na kudhulumu Waislaam...!..kwa mtu asiye na upungufu wa akili, mambo mengine ni vigumu kuyaamini. Halafu "scholar" anayetoa madai haya eti sasa ameamua kuandika kitabu cha historia na rejea kuu ikiwa ni masimulizi ya wazee wake ambao kwa madai yao ndio waliopigania uhuru wa Tanganyika, upuuzi mtupu.

Nilionya kuwa hatari ya uwongo ukiachwa unarudiwarudiwa sana bila kukemewa, unaweza kujenga hisia potofu katika jamii kulingana na uwezo binafsi kuupokea bila tafakari. Katika huu mjadala tunawashuhudia watu kama hao na utawatambua tu wanavyomeza hizi hadithi za Mohamed Said na FaizaFoxy kuhusu chuki za Mwalimu dhidi ya Uislaam. Fikirieni jamani dai hili la Mwalimu kumwomba Gadafi hela ya kujenga msikiti halafu kukalia hizo hela (alizifisadi) hadi kufa kwake ndio msikiti ujengwe. Fikirieni hili la Mohaned Said kuwa Chifu Mkwawa alikuwa Muislaam na ndio maana alipambana na Wajerumani halafu kuna watu kama mazezeta wanaitikia chorus, huu kama si utumwa ni nini ?

Lakini narudia tena kusema hawa watu tusiwapuuze, wanayo ajenda na hiyo ajenda yao itafanikiwa tu kama Watanzania katika umoja, mshikamano na upendo tulionao bila kujali dini wala kabila (asante Mwalimu), hatutaupiga vita. Tahadhari ni kuwa tukiwapa nafasi wakafanikiwa basi, sisi kama taifa tumekwisha, tunayoyashuhudia yakitokea kwa mfano Somalia na kwingineko tutakuwa tumeyafungulia mlango. Labda tuanze kwa kujiuliza swali moja zito, wakati hizi mbegu za chuki zikipandwa mchana kweupee, usalama wa taifa uko wapi, serikali iko wapi na CCM iko wapi na kwa nini wako kimya ! Jibu mnalo wana jamvi, ukiona vyaelea vyaundwa na sasa vyarembwa.

Adam angeweza kuwa Muislaam sawa lakini si lazima baba yake Sapi alikuwa Muislaam na kama na yeye pia alikuwa Muislaam si lazima babu yake Chifu Mkwawa alikuwa Muislaam, ndivyo tulivyoishi bila kubaguana katika familia. Mfano mzuri mwingine ni Paul Bomani alikuwa Mkristo lakini baba yake mzazi alikuwa Muislaam au Bob Makani Mwenyekiti wa pili wa Chadema alikuwa Muislaam lakini ndudu zake wa kuzaliwa ni Wakristo. Tofauti na pwani huko bara mambo ni tofauti na ndiyo maana mimi nasema mtu wa pwani tena mzaliwa wa Gerezani asithubutu kudai anaandika historia ya wapigania uhuru wa Tanganyika, hapana, anaandika simulizi za wazee wake wa Gerezani, period.

Haya tuendelee........................
ASAnte, kwa ujumbe wako. nikweli MS ana agenda iliyojificha, lazima jambo lifanyike kuzuia utengano kwa WATZ
 
tatizo ni mfumo.

Je unajuwa polisi hususan wale rankless wanafuata mfumo gani wa likizo?

Je ma sister wana mfumo gani mkataba wao?

Tukikubaliana kwamba ni mfumo, nitakuuliza hao ma alhaji wamewezaje kufika kwenye post za juu kitaifa.

Na nitakuuliza, wamefanya nini ama wanafanya juhudi gani kuubadilisha huu mfumo uliopo unaowakandamiza waislamu wenzao?
 
Hapo sasa ndio patamu, nataka wenyewe mnaobisha humu mje na jibu.
Cha msingi ni kujua lini alifunga hiyo safari maana burungutu hilo la kujenga msikiti alipewa wakati anarudi kutoka libya!mwenye kujua??
Hili bandiko hapa chini ni kujaribu kuonyesha jinsi gani Nyerere alivyokuwa mkarimu kwa Waislam ila shukran ya punda ni mateke tu!
Najua MS na wenzake watasema hao mashehe wa butiama ni 'Wasaliti'.
......................

DEOGRATIAS MUSHI
Julius Nyerere's process to sainthood widened this week, following a revelation of an extra ordinary thing that Mwalimu did in 1999. The move by the BBC World Service to bring together sons of the two former East African leaders whose hostility toward each other

Jaffer Remo Amin, the son of Uganda's former president, Idi Amin and Madaraka Nyerere, the son of former Tanzanian President Julius Nyerere, met on Thursday at Butiama Village, Mwalimu's birthplace amidst joy and fraternal love. Prior to this encounter, BBC aired programmes that portrayed Mwalimu as a unique leader, doing equally unique things that could accelerate his process to sainthood, according to the Catholic Church's tradition.
Though a devout Catholic himself, Mwalimu is said to have raised $400,000 for the construction of a beautiful mosque at Butiama, to serve the population of about 200 muslims who live in the midst of a predominantly Christian community of at least 10,000 at the time. And who donated that big amount? It was Muammar Gadhafi, the current Libyan leader. According to Vicky Ntetema, a BBC journalist who covered the event in Butiama last week, Mwalimu was approached by the local muslim community, asking him for financial assistance to renovate their mosque that was in bad shape.

The Secretary of Butiama Masjid Rahman Mosque, Mr Suleiman Juma, told the BBC that Mwalimu told the Islamic leaders that he was travelling and that he would give them a reply of their request on return. Mwalimu Nyerere who was by then retired, was travelling to Libya for a meeting where he met Mr Gadhafi and told him to contribute some money for the renovation of a mosque in his home village in Tanzania. According to the BBC, Ghadafi responded to Mwalimu Nyerere's request with the following statement: "I have no money for the renovation, but I will give you money for construction of a new modern mosque in your village."
The following day, as Mwalimu waited for his flight back home at the Tripoli International Airport, Gadhafi aides brought him the $400,000 in hard cash -- for the construction of Butiama mosque. Mwalimu brought the money, handed it over to Muslim leaders in Butiama, who later formed a committee to supervise it. The money was used to build a mosque, a residential house for a sheikh and a hostel to accommodate muslim visitors who visit the place. The late Vice-President, Dr Omar Ali Juma, officially opened the mosque on October 13, 2000.

According to Butiama Mosque chairperson, Swahib Araka Ahepe, Mwalimu lived a saintly life, because he reconciled with Ghadafi and made him a friend, even though he had supported Uganda in the war against Tanzania in 1979. The Auxiliary Bishop of the Catholic Archdiocese of Dar es Salaam, Right Reverend Methodius Kilaini, told the 'Sunday News' on Thursday that Nyerere's process to sainthood was slowly but surely moving ahead. "The formal process of sainthood involves a complicated process taking time, money, testimonies and miracles and the church follows a strict set of rules in the process," he said.

He added that although some people claim to have received some favours after asking Nyerere to intercede for them, the church was taking each step with a lot of care. He added that what the church was interested in was a scientific miracle about Nyerere, that could be believed without some doubts. On Nyerere's predisposition to forgiveness, Bishop Kilaini said he portrayed that virtue, after he also forgave those who wished to oust him from power.
On Mwalimu's readiness to lend a hand to anyone - irrespective of faith or creed -- Bishop Kilaini said Mwalimu was never a religious fanatic. "Though Catholic himself, he made the state take over schools run by the same church, because he wanted equal services to be enjoyed by all people," he added. Mwalimu Nyerere (1922-1999) has already been declared a Servant of God (Mtumishi wa Mungu), as the first step in the process (cause) of canonization.

The official inauguration of the process took place during a eucharistic liturgy that was celebrated by Cardinal Polycarp Pengo at Butiama Parish in Mara region on 21 January, 2006. One of the statements that Nyerere uttered on Independence Day describes his kind of a person. He said: We would like to light a candle and put it on the top of Mount Kilimanjaro, which would shine beyond our borders, giving hope where there is despair, love where there is hate and dignity where before there was only humiliation.
 
Kwa sote.
Nami nashukuru sana kwa darsa yako nzuri sana ambayo ina mazingatio makubwa sana kwa wenye akili na ufahamu.

Barubaru,

Mimi nakusoma na nakuelewa kwa nini umekuwa hivyo na kuweza kunifahamu haraka sana. Nakushukuru sana.

Nasikitika sana nisomapo jamaa zangu humu ndani wanapofanyia istihizai mapokezi ya wazee wangu.
Laiti wangelijua kimo cha ujuzi na elimu wanayopata watu kwa kusikiza darsa tu hata bila ya kushika kitabu sijui wangelisemaje.

Lakini sisi tutafanyaje na hao wenzetu hawakujaaliwa nema tulojaliwa sie. Sisi ni wa kushukuru na ikiwezekana na wao wakipenda tuwape yuliyosoma kwa masheikh wetu.

Humu ndani kimeingia kizazaa akili zao zinashindwa kukubali wanayosikia kutoka kwangu ni mambo mapya na mageni kabisa kuwa murid wa Sheikh Mohamed Ramia Khalifa wa Tariqa Kadiriyya wamepewa amri kuwa wakapige kura na wampigie Nyerere.

Wanashindwa kuelewa kuwa Sheikh Hassan bin Amir alikuwa na zawiyya nchi nzima wamepelekewa amri kuwa wapige kura na kura zende kwa Nyerere.

Huu mtandao ni wa asili ulikuwapo hapo labda nenda nyuma miaka mia na zaidi. TANU ilipokuja Waislam walifanya kazi moja tu nayo ni kubadilisha muelekeo na kumpiga tepe mkoloni wakiwatumia watu hawa.

Bahati mbaya ndugu zetu hawakujaaliwa kuwa na neema hii. Sasa mimi kueleza haya wao wameshtuka sana. Hawakuwa wanayajua haya.

Ala kumbe nguvu ya Nyerere ilikuwa inatokana na watu hawa?

Abdulwahid na Dossa peke yao wazingeliweza kuhimili kishindo kile cha Muingereza ndiyo maana walitaka msaada wa wazee na kukawa na Baraza la Wazee wa TANU masheikh na wanazuoni watupu mle ndani.

Sasa changamoto yangu kwao nawaomba wao wafanye utafiti wa haya nisemayo wasikalie kubeza kuwa ati haya nisemayo ni porojo.

Nilikuwa Ujerumani na nimetoa muhadhara Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin haya nisemayo humu yamewavuruga akili. Tayari washeleta wanafunzi (Ph D) kuanza utafiti katika somo hili.

Wanasema wakati wa Vita ya Majimaji Waislam waliwapa shida sana askari wao na wanataka kufanya 'comparison" nini kinawasukuma Waislam kuwa wamoja kila wanapohisi dini na nchi yao iko katika kushambuliwa na Ukristo.

Jamaa zangu wao sana sana watafoka, kukejeli na kutoa matusi.

Mohamed
 
Historia, kwa mtazamo wangu, ni mkusanyiko wa matukio yaliyopita yanayoelezea kilichotokea, wakati wa kutokea, wahusika, na taathira yake. Na kwa vile Tanganyika ni kubwa haitaingia akilini iwapo atajitokeza mtu mmoja peke yake kuandaa machapisho na kudai kuwa ndiyo historia ya tanganyika. Kwa hiyo mkusanyiko wa simulizi na tafiti kutoka kila kona ya nchi ndio unaoweza kuunganishwa na kutengeneza kitu kinachofanana na historia halisi. Hivyo kila mtu ana fursa ya kuchangia katika kuandikwa upya kwa historia sanifu ya Tanganyika ili kuondokana na historia potofu za enzi 'za zidumu fikra za mweyekiti'. Na kuvumiliana kunahitajika wakati wa kusoma mawazo ya wengine ambayo yataenda tofauti na fikra ulizozizoea...
 
Kapongo,
Hakuna anayepinga haya unayoyaeleza hapa. Tatizo linakuja pale mtu anapojaribu kuiandika UPYA kabisa historia yenyewe kwamba yote iliopo imekosewa, imepotoshwa, imebagua, haifai bila kuweka anayotaka yeye ambayo ni simulizi zinazoambatana na chuki, husda, wivu, hisia na vionjo vya KIDINI, KIKABILA,...
Ujanja wa WAMANYEMA wa Kariakoo tunaufahamu sana. Mtu anapoutumia ujanja huo kuibadili historia ya NCHI yetu tutakataa.
 
Barubaru,

Mimi nakusoma na nakuelewa kwa nini umekuwa hivyo na kuweza kunifahamu haraka sana. Nakushukuru sana.

Nasikitika sana nisomapo jamaa zangu humu ndani wanapofanyia istihizai mapokezi ya wazee wangu.
Laiti wangelijua kimo cha ujuzi na elimu wanayopata watu kwa kusikiza darsa tu hata bila ya kushika kitabu sijui wangelisemaje.

Lakini sisi tutafanyaje na hao wenzetu hawakujaaliwa nema tulojaliwa sie. Sisi ni wa kushukuru na ikiwezekana na wao wakipenda tuwape yuliyosoma kwa masheikh wetu.

Humu ndani kimeingia kizazaa akili zao zinashindwa kukubali wanayosikia kutoka kwangu ni mambo mapya na mageni kabisa kuwa murid wa Sheikh Mohamed Ramia Khalifa wa Tariqa Kadiriyya wamepewa amri kuwa wakapige kura na wampigie Nyerere.

Wanashindwa kuelewa kuwa Sheikh Hassan bin Amir alikuwa na zawiyya nchi nzima wamepelekewa amri kuwa wapige kura na kura zende kwa Nyerere.

Huu mtandao ni wa asili ulikuwapo hapo labda nenda nyuma miaka mia na zaidi. TANU ilipokuja Waislam walifanya kazi moja tu nayo ni kubadilisha muelekeo na kumpiga tepe mkoloni wakiwatumia watu hawa.

Bahati mbaya ndugu zetu hawakujaaliwa kuwa na neema hii. Sasa mimi kueleza haya wao wameshtuka sana. Hawakuwa wanayajua haya.

Ala kumbe nguvu ya Nyerere ilikuwa inatokana na watu hawa?

Abdulwahid na Dossa peke yao wazingeliweza kuhimili kishindo kile cha Muingereza ndiyo maana walitaka msaada wa wazee na kukawa na Baraza la Wazee wa TANU masheikh na wanazuoni watupu mle ndani.

Sasa changamoto yangu kwao nawaomba wao wafanye utafiti wa haya nisemayo wasikalie kubeza kuwa ati haya nisemayo ni porojo.

Nilikuwa Ujerumani na nimetoa muhadhara Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin haya nisemayo humu yamewavuruga akili. Tayari washeleta wanafunzi (Ph D) kuanza utafiti katika somo hili.

Wanasema wakati wa Vita ya Majimaji Waislam waliwapa shida sana askari wao na wanataka kufanya 'comparison" nini kinawasukuma Waislam kuwa wamoja kila wanapohisi dini na nchi yao iko katika kushambuliwa na Ukristo.

Jamaa zangu wao sana sana watafoka, kukejeli na kutoa matusi.

Mohamed
Laiti unge substitute hayo maneno kwenye red na watanganyika/watanzania , watu wengi wangekuelewa!
 
Laiti unge substitute hayo maneno kwenye red na watanganyika/watanzania , watu wengi wangekuelewa!

Sweke34,

Ukoloni haukuwa unafanyakazi kwa namna hiyo hawakuutazama Uislam kwa jicho lilelile walilotazama Ukristo. Sasa ikiwa nitatoa mchango wa Uislam katika via hivi nitakuwa nauogopa ukweli. Hebu soma hiki kipande hapa chini:
"Vita vya Maji Maji vilipoanza kusini yaTanganyika mwaka 1905 kwa nia ya kuwafukuza Wajerumani kutoka Tanganyika, zilesehemu zenye Wakristo wengi zilikataa kujiunga na vita na badala yakewakajiunga na majeshi ya Wajerumani na kupigana bega kwa bega na dhidi ya wazalendo.Hii ilitokana na sababu ya kuwa uasi dhidi ya dhulma wa Wajerumani ulianzakatika maeneo yenye Waislam wengi na vita vikachukua sura ya vita vya Kiislamudhidi ya Wazungu ambao dini yao ni Ukristo. Kwa kuwa wamishonari walikuwawashirika wa wakoloni, walichukuliwa kama maadui na hivyo ikawa vituo vyaovinashambuliwa na wapiganaji wa Maji Maji. Kutokana mashambulizi haya, Wakristowalivichukua Vita Vya Maji Maji kama vita dhidi ya Ukristo. Harakati za MajiMaji zilishindwa na Wajerumani walifanya fisadi kubwa dhidi ya wananchi naviongozi wao. Jambo hili liliacha kovu kubwa katika fikra za wananchi na kwaupande wa Wakristo ambao walinusurika na ghadhabu ya Wajerumani, wengi waowakajiweka mbali na aina yoyote ya kupinga ukoloni. Kufuatia historia hii Waafrika waliokuwakusini ya Tanganyika sasa wakiwa chini ya utawala wa Waingereza na kuwa chiniya himaya ya wamishonari walipupazwa kiasi kiasi kwamba waliogopa siasa. Baadaya Waafrika kushindwa vita kwa silaha kali za Wazungu sasa Kanisa likaona ndaniya fadhaa ile fursa yao kutawala sehemu hiyo kwa kutoa vishawishi kama vileshule na hospitali. Kwa hiyo Wamishionari na Waingereza walionekana kamamabwana wema wenye kuwajali raia zao kinyume na serikali katili na ya kidhalimu ya Wajerumani. Vuguvugu la siasakama ilivyokuwa Vita vya Maji Maji, lilianza katika maeneo ya Waislam kufuatiamfumo ule ule kama ilivyokuwa katika upinzani wa ukoloni wa Wajerumani.Wakristo katika Jimbo la Kusini waliiona TANU kama walivyoviona Vita Vya MajiMaji, kama harakati nyingine za Waislam zilizowa zinakuja tena kwa mara ya pilikuvuruga amani na utulivu. TANU ilipoanza ikawa inavuma kuwa safari hii Waislamwalikuwa wamemua kuanzisha vita dhidi ya Waingereza kama walivyoanzisha vita naWajerumani."

Ikiwa sitafanya uchambuzi kama historia ilivyokuwa kwa kuogopa ukweli na kutaka kuwafurahisha watu historia hii itapotea.

Mohamed
 
Mohamed,
Vita ya Majimaji nayo ni ya WAISLAMU? Pindisha tu historia tuone baadae itakuwaje. Akina Kinjekitile walitumwa na UISLAMU wao kuwapiga WAJERUMANI! Papo hapo Vita Kuu ya Pili ya Dunia baadhi ya wazee wako walipigana upande wa WAINGEREZA! Wakausahau UISLAMU wao?
 
Hebu,

Tuambie wewe vita vya maji maji Kinjekitile alitokea wapi? Vita vya Maji Maji vilianza lini na vikaisha lini? Ila mbona umekimbia maswali yangu ya MoU ya ujambazi baina ya kanisa na serikali ya watanzania? Rudi kwanza unijibu Bilioni 91 za nini mnazopewa na serikali?
 
Kapongo,
Hakuna anayepinga haya unayoyaeleza hapa. Tatizo linakuja pale mtu anapojaribu kuiandika UPYA kabisa historia yenyewe kwamba yote iliopo imekosewa, imepotoshwa, imebagua, haifai bila kuweka anayotaka yeye ambayo ni simulizi zinazoambatana na chuki, husda, wivu, hisia na vionjo vya KIDINI, KIKABILA,...
Ujanja wa WAMANYEMA wa Kariakoo tunaufahamu sana. Mtu anapoutumia ujanja huo kuibadili historia ya NCHI yetu tutakataa.

WC,

Mimi ndiyo nishaandika kitabu hiki maktaba zote kubwa duniani kipo pamoja na Library of Congress, Washington.

Vyuo vikuu Ulaya na Marekani ni kimoja katika vitabu vya rejea katika historia ya Tanganyika.

Baadhi ya wahadhiri wa historia ya Afrika nimeonananao na wengine tumefanya minakasha katika vyuo vyao.

Ukweli ni kuwa hiki kitabu kipo njia ya kuweza kukipinga ni moja tu.

Nayo ni nyie kuandika kitabu kitakachopinga hiki changu.
Hakuna njia ya mkato.

Kwa hapa tulipofika ukweli ushajulikana kuwa historia ya uhuru wa Tanganyika iliwatisha baadhi ya watu na hivyo wakaamua kuihujumu.

Si maskhara kitabu hiki kimeninyanyua kwelikweli katika uwanja wa "scholarship."
Haufanyiki mkutano mahali nikaacha kuombwa kutoa "paper."

Hivi sasa tunakwenda kwenye toleo la tatu la kitabu cha Kiswahili.
Penye ukweli uongo hujitenga.

Sheikh Mohammed

Nikuulize vipikuna jitahida za kitabu hiki kutumika katika shule na vyuo vikuu vya za kiislam Tanzania

Unaweza kuangalia pia uwezekano wa kuziweka kwenye library za misikiti yote Tanzania hasa hicho cha kiswahili.

Hii inaweza kutupa fursa sahihi kuelewa mambo mengi yaliyojiri nchini hasa kwa jamii yetu..
 
Back
Top Bottom