Wakuu,
Kwanza kabisa tusimame pamoja na kuwaambia wanaotaka kuligawa taifa, hapana! kila wakileta hoja zao bila kujali imani zetu tuwaambie, hapana!
Tuwaambie sisi ni Watanzania tunaoishi bila kujuana majina, na kwamba majina ni utambulisho na si alama ya imani. Kama ni alama ya imani tunawezaje kuwa na Petro muuaji au Mohamed kibaka!
Lugha ni chombo cha mawasiliano katika kubeba ujumbe wa imani, lakini si imani kama wanavyodhani mashabiki wa dinii.
Tamaduni si sehemu ya imani lakini inaweza kuchukua imani na kuwa sehemu ya tamaduni. Pope pale vatican anavaa kanzu, je amesilimu?
Barua ya Tareq Aziz kwa Sadam ina 'leter head' ya bismillahi, je Tareq ni muislam!
Dini inatumiwa na kundi fulani lenye masilahi yasiyojulikana kutaka kuwafarakanisha Watanzania. Kama yapo matatizo mbona hayazungumzwi na kutolewa mapendekezo? Tumemuuliza Mohamed anashauri nini, yeye akasema hadi serikali itakapo waita ndipo watatoa mapendekezo yao. Huku nyuma anarudi na kutahadharisha hatari ya vita. Usomi maana yake si kusoma ni kutumia elimu kuyakabili mazingira na kutafuta suluhu.
Baada ya dhambi ya kumdhalilisha Nyerere akiwa katika masoksi mareeefu, kupewa vitoweo na pesa za nyama dhambi hiyo hiyo inajirudia na sasa inatafuna kwa yule aliyeitenda. Tumeambiwa Nyerere amekandamiza watu, yaweza kuwa kweli, lakini hakuna mahali popote Mohamed said salum Semtungo ameweka japo nyaraka kuthibitisha madai zaidi ya simulizi za marhumu.
Mohamed akatoa madai kuwa BAKWATA si waislam na ni kama Yuda iskariote(ushahidi upo ukihitajika).
Hapa ana maana waislam wote wakiwemo wazee kama marhum Hemed bin Jumaa ni wasaliti. Inawezekana ana hoja ya nguvu kabisa.
Amedai mfumo kristo ndio unatawala nchi hii, inawezekana ana hoja kabisa.
Mahali ambapo hoja zake zinakuwa kama mabua ya mahindi ni pale anaposhindwa kusema Mwinyi aliyeutumikia mfumo kristo, Kawawa aliyetumikia mfumo kristo, Kikwete anayetumikia mfumo kristo ni wasaliti kama Adam Nasibu na Hemed bin Juma wa BAKWATA. Kwamba wapo wasaliti kwa vigezo vyake na wengine watakatifu kwa vigezo vingine.
Mohamed ana haki ya kutumia vigezo vyake, kibaya sana ni pale vigezo vyake anapovifanya ukweli na ukweli mtupu tena wa kitaifa, na kutumia vigezo hivyo kidini ili kuwaaminisha watu kuhusu kile anachodhani yeye ni sahihi na si kile kilicho sahihi. Ushawaishi wake ni mkubwa na inabidi watu wasimpuuze hata kidogo. Matamshi yake yanayoashiria shari ni ya kukemea mapema sana.
Tusimame na kumwambi, Mohamed tafuta chanzo cha tatizo na si kutoka nje kutafuta mchawi. Mchawi yupo hapo ulipo na chumbani kwako na si jirani aliyebeba jembe lake anakwenda shamba. Unapofundisha watu kuimba bila kuwaambia maana ya tenzi ni kuwapoteza.
Suluhu ya matatizo si mawaziri ni umasikini ulioboboea usiochagua bei ya sukari kwa Pagani, Mwislam au mkristo.
Matatizo ya ANC na kaburu yalimwalizwa mezanii, ya ZAPU/ZANU na Ian Smith yaimalizwa Lancaster house. Ya RENAMO NA FRELIMO yalimalizwa mezani. Matatizo ya Raila na Kibaki yalimalizwa mezani n.k.
Ya kwetu yanaongeleka bila kuwa na upande, yanaongeleka kwa utamaduni wetu wa kitanzania. Tusijenge kambi za kulazimisha ili tukidhi kiu ya matamanio ya nafsi zetu. Nafsi zinatamani kila kitu hata kile kinachomuudhi Mwenyezi mungu.