Kitu kinacho nishangaza hapa JF aidha kwa Waislaam au Wakristo au wasiokuwa na imani ya upande wowote, ni pale nilipobaini kuwa Mzee Mwanakijii ameipandikiza (ameibandika) aya ya Qur'an isivyo. Si Muislaam wala asiye Muislaam aliyeweza hata kufunguwa mdomo kusema au kushtuka.
Maswali mengi sana kuliko majibu. Huu ndio mshikamano wa Waislaam na wasio Waislaam hata pale tunapoona makosa? hata mmoja kati ya wachangiaji wa JF kusema ni kweli Mzee Mwanakijiji, omba msamaha kwa makosa uliyoyafanya, kama anavyoshinikiza FF. Badala yake kitu nilichokiona ni hata Mohamed Said kumsifu Mzee Mwanakijiji kuwa ni Heavy Weight. Haaa! Ma heavy weight hawana makosa hata wanapokosea? hii ndio JF au huu ndio usomi? Au huu ndio unafik wa Waislaam?
Sasa inanifanya niamini maneno ya Zomba (my cousin) ameni PM na kuniambia hakuna cha Mohamed Said wala Mwanakijiji wote hao ni system na wanawacheza shere.
Ahsante Zomba kwa kunitanabahisha hayo, sasa sitopoteza usingizi wangu. Na nimeona ukweli.
Mohamed Said, nimekutetea sana na ni mwandishi mzuri sana, lakini kweli hukuwa unatetea Uislaam wala Waislaam, unatetea na kuandika Historia ya wazee wako, na hata Uislaam unapoandikwa ndivyo sivyo hukuweza hata kutanabahi na japo kuuweka msimamo wako Kiislaam na wala kusema kweli hapo kuna kosa.
Nilichokitathmini, ni kuwa unataka ieleweke kuwa Wamanyema na Wazulu ndio waliokuja kuwafungua macho wenyeji na wenyeji wote ni hamnapo hakunapo.
Naamini, Waislaam mlichokipanda ndio mnachokivuna. Mmeshindwa hata kuitetea aya ya Qur'an ilivyobandikwa ndivyo sivyo, mtaweza kuutetea Uislaam? Mtabaki kutetea wazee wenu, alifanya hivi walikuwa hivi wakawa vile, na hao wazee wenu kwa unafik wao ndio wakawapa msemo na nguvu watu kama kina Nyerere. Kawawa na Songambele na Mustafa Nyang'anyi walitokea wapi? Uislaam kwa jina tu hautoshi na vitendo na mshikamano wa Waislaam ndio unaoonesha Uislaam wa kweli.
Leo mmeshindwa kutetea aya ya Qur'an inayosimamisha Uislaam, mtaweza kuwateteta Umma wa Kiislam. Wanafik wakubwa.