sio inawezekana, huo ndio ukweli, ukirejea historia hata vita ya Mkwawa dhidi ya Germany ilikuwa ya kiuchumi zaidi kuliko ukombozi kasome historia. Ndg yangu ulichpoandika ndio ukweli ila nimeshangaa baadhi ya watu kusema eti MTEMI MKWAWA alipigana kutetea Uislam, aaaah watu wengine bwana their way of thinking is questionable. ANYWAY WANA AGENDA YAO YA SIRI, ninachofurahia imejulikana sasa hawana pa kutokeaMdondoaji,
..inawezekana mahusiano ya MKWAWA na RUMALIZA yalihusu biashara ya WATUMWA na PEMBE ZA NDOVU.
Udini ,ubaguzi chuki ,ndio naona vinajidiliwa kwenye huu mnakasha hongereni wenzenu wamesahau historia zenu , wanajenga vyuo kila mkoa ,Hosp kila mkoa mkija stuka mtaanza sema mfumu kristo unatawala! Kazi mnayo masheikh wetu.
Mdondoaji said:Further investigation by the germans revealed that the letter (Mecca Letter) had originated from Zanzibar. It had been composed by , or written for , the family of Muhammad bin Khalfan bin Khamis Al-Barwani better known as RUMALIZA, a member of the QADIRIYYA tariqa, and famous slave trader and ivory merchant.
sio inawezekana, huo ndio ukweli, ukirejea historia hata vita ya Mkwawa dhidi ya Germany ilikuwa ya kiuchumi zaidi kuliko ukombozi kasome historia. Ndg yangu ulichpoandika ndio ukweli ila nimeshangaa baadhi ya watu kusema eti MTEMI MKWAWA alipigana kutetea Uislam, aaaah watu wengine bwana their way of thinking is questionable. ANYWAY WANA AGENDA YAO YA SIRI, ninachofurahia imejulikana sasa hawana pa kutokea
Mdondoaji,
..kama ulivyosema kwenye posting yako nyingine, na kama nilikuelewa, historia inaweza kufunua mambo ambayo hatuko comfortable kuyasikia.
..sasa haya "madubwana" unayotuletea hapa naogopa in the end tusije tuka-conclude kwamba Mkwawa alikuwa akishiriki biashara ya watumwa. Kwamba ugomvi wake na Wajerumani ulihusu control ya caravan routes zilizokuwa zikipitisha pembe na watumwa.
..kuna mahali nimesoma kwamba, in Angola, Wareno walikuwa wanabatiza Watumwa wao kabla hawajawapakia kwenye meli.
..hapo kwenye kipande ulichotuletea naona prominent members wa tariqa Qadiriyya wanatajwa kuwa vinara wa biashara ya utumwa.
..kuna mambo ya kihistoria hukutana nayo, basi hubaki nikijiuliza WHY, WHY,WHY. kwanini MUNGU alituacha Waafrika tukateswa na ngozi nyeupe kiasi kile? vilevile kwanini Waafrika wenzetu walishirikiana na ngozi nyeupe kutenda unyama ule dhidi ya Waafrika wenzao?
Tunashukuru kwa uchambuzi wa familia ya Mkwawa,
Ila mambo mawili matatu naomba ufafanuzi. Kwanza ilikuwaje hadi Rumaliza alifanikiwa kupenya katika ngome ya wahehe na kupata influence kubwa? Pia BG Martin (1969) (Article nilishaitaja nyuma sina umuhimu wa kuirudia) alisema haya naomba unijibu:-
Mkwawa and Rumaliza became blood-brothers, and Rumaliza doubtless gave his ally advice on rebuilding in stone his earth fortress at Kalenga, near Iringa, against the day of German attack. On 30th October 1894 Rumaliza was in the fort with Mkwawa when it was asaulted by the Germans. Mkwawa commited suicide four years later, while Rumaliza escaped to Zanzibar by fishing boat to evade the Germans.
Bila shaka ni kuhusu biashara ya watumwa na Pembe za ndovu.Huu ukaribu wa Rumaliza na Mkwawa ulikuwa wa nini mnaweza kufafanua hadi wa kufa na kufaana
Mkwawa alikufa tarehe 19 July 1898. Sasa hapa kwenye Islamisation ya Uhehe na Unyamwezi ni kitu cha kutafakari. Hao waenezaji uislamu walifika Kalenga wakati gani? Aliyeleta uislamu Kalenga ni Sapi Mkwawa akitokea Zanzibar alipoachiwa baada ya baba yao kujiua.Labda nikuongezee nondo nyengine Edward Simpson et.al. (2008) katika kitabu chake kinachoitwa Stuggling with History: Islam and Cosmopolitan in Western Indian Ocean anasema:-
The sultan with help of Qadiriyya movement helped islamisation of uhehe and unyamwezi region during the first decade of the twentieth region and after 1880. (1880-1910).
Hapa nauliza je Mkwawa alikufa mwaka gani?
Na pengine hao wazee watuambie after the Germans defeated Wahehe. Moja ya masharti waliyokubaliana baina ya wahehe na wajerumani ni kuwa Wajerumani watatawala wahehe ila wahehe watabakiwa na mambo yao binafsi (Kama anavyoreport Marcia Wright.). Moja ya masuala hayo ufundishwaji wa lugha ya Kiswahili na UISLAMU (references Marcia Wright, 1968, Local roots in German East Africa, Journal of African History, Cambridge University Press)
Jambo hili lilipingwa sana wamissionary wa kijerumani unaweza kutupatia maelezo ya kwanini walilipinga?
Sipendi mada ambazo zina harufu ya udini,
Mr. Mohamed
Ukitaka kuheshimika jaribu kutafiti kujua ukweli na siyo kudhibitisha hisia, baadhi ya wenzetu wanaimani kuwa dini yao inakandamizwa,
Hii sasa imekuja na sura mpya ya "kuthibitisha" katika historia sijui lengo ni nini? Unataka ugomvi kati ya wakristo na waislamu ndipo utakapofurahi? Ukiono mitaa ya Tanzania imeingia katika ugomvi wa kidini ndipo utakapojua madhara ya makala zako?
Tuna matatizo mengi sana Tanzania ambayo yana hitaji nguvu ya pamoja kuyatatua bila kujali dini,
Vyovyote utakavyojitetea mada hii haina msaada katika kujenga bali kubomoa.
Baada ya mada hii utasikia watu wakisema, Rais ajaye awe muislamu kwa sababu Nyerere alikuwa mkristo akatawala miaka mingi hivyo kulipiza ni lazima....Tuamke usingizi utageuka kifo...
KWANZA nikiri kwamba nilishaaga na kwa kweli ni mara chache sana huwa nazigeuka ahadi zangu na mara zote huwa nafanya hivyo kama kutafuta thawabu kwa muumba wangu na kuweka kumbukumbu njema kwa binadamu wenzangu. Nasisitiza TENA sina nia tena ya kuendelea na mjadala huu, na wote ambao hawakujua kama NILISHAAGA hii ni POST yangu ya mwisho KABISA kwenye THREAD hii.
Wajerumani na Askari wao au "sakarani" kama Mkwawa alivyokuwa anawaita, walielekezwa Kalenga na aliyekuwa askari wa Mkwawa ambaye baba yake aliuawa na Mkwawa kwa maamuzi ya wazee wa baraza la Mkwawa. na Askari huyu kukimbilia eneo la Ilula ya leo. Kwa kweli bado nakusunya maelezo mengi kuhusu Rumaliza. Kwani watu watokanao na Ukoo wa Mkwawa na wale wenye kufahamu historia yake Mkwawa, Rumaliza si jina lililo kwenye kumbukumbu za wahehe wengi na utawala wao. Na mimi najiuliza ni kwa nini wahehe wenyewe hata wale wa ukoo wa Mkwawa hawamchukulii Rumaliza kwa uzito ule ule wa wale walioandika Historia ya Mkwawa. Ni kwa nini Kila nimuulizae kuhus Rumaliza naye ananiuliza mimi "Rumaliza, Ndiyo alikuwa nani?" Kwa kweli MS kaleta changamoto kubwa sana ya kuanza kuchimbua historia ya taifa letu. Si tunakumbuka jinsi wazungu walivyodai kwamba Johannes Rebmann ndiye alikuwa mtu wa KWANZA kuuona Mlima Kilimanjaro!!??
Bila shaka ni kuhusu biashara ya watumwa na Pembe za ndovu.
Mkwawa alikufa tarehe 19 July 1898. Sasa hapa kwenye Islamisation ya Uhehe na Unyamwezi ni kitu cha kutafakari. Hao waenezaji uislamu walifika Kalenga wakati gani? Aliyeleta uislamu Kalenga ni Sapi Mkwawa akitokea Zanzibar alipoachiwa baada ya baba yao kujiua.
kwanza tuwe wakweli jamani,hivi wahehe wangependa zaidi haki yao kujifunza Kiswahili na uislamu ilindwe kuliko haki yao ya kutumia Kihehe na mila zao za kijadi? Watoto wa Mkwawa waliporudishwa na wajerumani kutoka Uhamishoni walikubaliana mambo fulani fulani moja wapo ni hilo la Kiswahili na Uislamu. Kwanza uelewe watoto wa Mkwawa waliopelekwa Uhamishoni Bagamoyo na baadaye Zanzibar ndiyo walikuja na hoja ya Kiswahili na Uislamu. Lakini wale waliobakiA Ilala 'Misheni Kota" wao waliporudishwa hawakupangiwa kutawala Kalenga. Hao ndiyo wale Wakristo.
Hao "wamissionary" hata vitabu vya Historia vya darasa la nne wanaelezewa kama walikuwa ni mawakala wa Ukoloni. Kumbuka kwamba ni Sapi ambaye ndiye aliyerithi utawala wa MKwawa na yeye tayari tangu akiwa Bagamoyo alishasilimu na kuwa Muislamu na alipotoka Zanzibar alirudi na Mwalimu wa dini ya Kiislamu kuja kuwafundisha wahehe wa Kalenga Uislamu.
Kwa hiyo hao wamisheni walijua wao kwa Sapi hawatakuwa na maslahi na hasa kama waislamu watakuwa wengi kwa maana nyingine kuongeza ushawishi wa waarabu Kalenga. Na ujue kwamba eneo alilokuwa anatawala Sapi ndilo kwa leo lina Mbuga ya Ruaha national park na huko ndiko kulikuwa na Tembo wengi.
FaizaFoxy nivizie kwingine swali lako kwenye thread hii sitaweza kulijibu.
JK,
Hilo mbona sio siri.
Hivi hukuwa unajua?
Uzuri wa historia ni kuwa lililotokea ndiyo hivyo hivyo huwezi kulibadili ingawa unaweza ukafanya uchambuzi unavyopenda. Nimesema huko nyuma Wazulu, Wanubu na Wamanyema waliingia na Wajerumani kama askari mamluki.
Babu yangu Mkuu alikuwa boma la Wajerumani, Shirati, Musoma.
Mohamed

Likija suala la Uislaam hakuna Mmanyema wala Mpogoro.
Nimekubali kurudi kwa ombi lako!!Kigarama,
Nakuomba urudi tena tena kwani tunajifunza mengi. Kwanza nashukuru kwa kujitahidi kunijibu ila kuna mapungufu katika majibu yako.
a. Rumaliza umesema wazee wako hawamjui hembu waulize kuhusu jina bwana Muhammad bin Khalfan bin Khamis Al-Barwan labda watakuwa wanamjua vizuri.
b. Rumaliza alikuwa mfanyabiashara wa pembe za ndovu, utumwa na pia mtangaza daawa na mfuasi wa madhahabu ya tasawwuff chini ya tariqa ya Qadiriyya. Tariqa ya Qadiriyya walikuwa wakitangaza dini na waliingia Uhehe, unyamwezi kati ya 1880-1910. Kipindi walichokuwa wanashambulia ngome ya Mkwawa 1894, Rumaliza alikuwa bega kwa bega na Mkwawa mpaka kifo chake. Leo wanasema hawamjui kweli???
c. Marcia Wright amenukuliwa pia na David Pizzo (To Devour the Land of Mkwawa, ) anasema hivyo hiyo.
Labda nikuongeze nondo nyengine muhimu. David Pizzo anasema hivi kuhusu Mkwawa namnukuu:-
"Mkwawa had Arab advisors, architects, and could call on auxilliaries from a number of dozen communities (such as wabena etc). He also had complex diplomatic relationship with Nyamwezi, and Ngoni. He also had diplomatic relationship with Abushiri rebels of the coasts.
David Pizzo , PhD thesis (2007) To devour the land of Mkwawa. colonial violence and German-Hehe War 1884-1914. University of North Carolina. Book now Lambert Publishind (2010).
Nimekubali kurudi kwa ombi lako!!
Hakuna mahali hao wazee walipokana kumjua Rumaliza ila wanaonyesha kabisa kwamba hawamjui Rumaliza. Lakini Historia ni Historia na hakuna mtu anayeweza kujidai eti yeye ni kamusi ya Hisrtoria fulani. Naendelea na tafiti zangu kwa kuwasiliana na watu mbalimbali hasa wale wazee wa miaka zaidi ya 70 ambao ingawa wametawanyika sana lakini nimepata contacts zao.
Hata mimi inanishangaza sana ni kwa nini wazee zaidi ya watano wenye umri zaidi ya miaka 70 niliofanya nao mahojiano wanasema hawamjui Rumaliza wakati vitabu vingi sana vimemtaja huyu jamaa kama alikuwa ni mshauri wa Mkwawa. Labda tujifunze kwa kisa hiki. Von Zelewski alipotoka kwao Ujerumani alijulikana kwa jina hilo, lakini kwa watu wa Tanganyika ya wakati huo alijulikana kwa jina la Nyundo. Inawezekana kuna jina ambalo wahehe wanamtambua Rumaliza. Rumaliza aliitwa nani na wahehe? Hilo ndilo jambo linalonitatiza kwa sasa.
Nikikamilisha utafiti wangu nitaanzisha thread kuhusu Mkwawa!!
Tanzania sheria za kimila hazijafutwa na ilikuwa hakuna mahakama hizo. Aliofutwa ni Kadhi wa Waislaam tu.@Faiza Foxy
Toa maoni yako
- Kitendo cha kufuta mahakama za kimila na kichief na tawala zao kilikuwa sahihi au nalo ni moja ya ukandamizaji wa Nyerere kulienga kuni la dini au kabila fulani ?
Na hii Bakwata mnayohituhumu kwa nini haijawai kuongozwa na waislam wa ikoa y bara kama Kigoma, Tabora, Kagera, etc ?
- Je Sio wakati kutafuta viongozi wa Kiisalm wa Kweli kutoka mikoa yenye wasomi wa elimu dunia na elimu dini ya juu
Unamjuwa Adam Nasibu katokea mkoa upi? unamjuwa Saleh Masasi katokea Mkoa upi? Unamjuwa Rajabu Kundya katokea wapi? unamjuwa Shaaban Simba anatokea wapi? kama hujui uliza uambiwe, usikurupuke.
Hapa nakuwekea nakuwekea majibu ya mikoa yao, wewe chagua umpendae umpe huo Mkoa: Singida, Kagera, Iringa, Shinyanga.
Fanya ka-"homework" kadogo.
Uhuru wa Kariakoo Gerezani.
Dah, hii nitaiandika kwenye vitabu vyangu vya kumbukumbu ili hata nikafa kesho mwanangu aje kusoma.
Kigarama nimekuuliza:
Usiogope, mimi nakuuliza la kwenye hii post yako: "sakarani" unaijuwa maana yake? na au unaijuwa asili ya hilo neno?