Tunashukuru kwa uchambuzi wa familia ya Mkwawa,
KWANZA nikiri kwamba nilishaaga na kwa kweli ni mara chache sana huwa nazigeuka ahadi zangu na mara zote huwa nafanya hivyo kama kutafuta thawabu kwa muumba wangu na kuweka kumbukumbu njema kwa binadamu wenzangu. Nasisitiza
TENA sina nia tena ya kuendelea na mjadala huu, na wote ambao hawakujua kama
NILISHAAGA hii ni
POST yangu ya mwisho
KABISA kwenye
THREAD hii.
Ila mambo mawili matatu naomba ufafanuzi. Kwanza ilikuwaje hadi Rumaliza alifanikiwa kupenya katika ngome ya wahehe na kupata influence kubwa? Pia BG Martin (1969) (Article nilishaitaja nyuma sina umuhimu wa kuirudia) alisema haya naomba unijibu:-
Mkwawa and Rumaliza became blood-brothers, and Rumaliza doubtless gave his ally advice on rebuilding in stone his earth fortress at Kalenga, near Iringa, against the day of German attack. On 30th October 1894 Rumaliza was in the fort with Mkwawa when it was asaulted by the Germans. Mkwawa commited suicide four years later, while Rumaliza escaped to Zanzibar by fishing boat to evade the Germans.
Wajerumani na Askari wao au "sakarani" kama Mkwawa alivyokuwa anawaita, walielekezwa Kalenga na aliyekuwa askari wa Mkwawa ambaye baba yake aliuawa na Mkwawa kwa maamuzi ya wazee wa baraza la Mkwawa. na Askari huyu kukimbilia eneo la Ilula ya leo. Kwa kweli bado nakusunya maelezo mengi kuhusu Rumaliza. Kwani watu watokanao na Ukoo wa Mkwawa na wale wenye kufahamu historia yake Mkwawa, Rumaliza si jina lililo kwenye kumbukumbu za wahehe wengi na utawala wao. Na mimi najiuliza ni kwa nini wahehe wenyewe hata wale wa ukoo wa Mkwawa hawamchukulii Rumaliza kwa uzito ule ule wa wale walioandika Historia ya Mkwawa. Ni kwa nini Kila nimuulizae kuhus Rumaliza naye ananiuliza mimi "Rumaliza, Ndiyo alikuwa nani?" Kwa kweli MS kaleta changamoto kubwa sana ya kuanza kuchimbua historia ya taifa letu. Si tunakumbuka jinsi wazungu walivyodai kwamba Johannes Rebmann ndiye alikuwa mtu wa KWANZA kuuona Mlima Kilimanjaro!!??
Huu ukaribu wa Rumaliza na Mkwawa ulikuwa wa nini mnaweza kufafanua hadi wa kufa na kufaana
Bila shaka ni kuhusu biashara ya watumwa na Pembe za ndovu.
Labda nikuongezee nondo nyengine Edward Simpson et.al. (2008) katika kitabu chake kinachoitwa Stuggling with History: Islam and Cosmopolitan in Western Indian Ocean anasema:-
The sultan with help of Qadiriyya movement helped islamisation of uhehe and unyamwezi region during the first decade of the twentieth region and after 1880. (1880-1910).
Hapa nauliza je Mkwawa alikufa mwaka gani?
Mkwawa alikufa tarehe 19 July 1898. Sasa hapa kwenye Islamisation ya Uhehe na Unyamwezi ni kitu cha kutafakari. Hao waenezaji uislamu walifika Kalenga wakati gani? Aliyeleta uislamu Kalenga ni Sapi Mkwawa akitokea Zanzibar alipoachiwa baada ya baba yao kujiua.
Na pengine hao wazee watuambie after the Germans defeated Wahehe. Moja ya masharti waliyokubaliana baina ya wahehe na wajerumani ni kuwa Wajerumani watatawala wahehe ila wahehe watabakiwa na mambo yao binafsi (Kama anavyoreport Marcia Wright.). Moja ya masuala hayo ufundishwaji wa lugha ya Kiswahili na UISLAMU (references Marcia Wright, 1968, Local roots in German East Africa, Journal of African History, Cambridge University Press)
kwanza tuwe wakweli jamani,hivi wahehe wangependa zaidi haki yao kujifunza Kiswahili na uislamu ilindwe kuliko haki yao ya kutumia Kihehe na mila zao za kijadi? Watoto wa Mkwawa waliporudishwa na wajerumani kutoka Uhamishoni walikubaliana mambo fulani fulani moja wapo ni hilo la Kiswahili na Uislamu. Kwanza uelewe watoto wa Mkwawa waliopelekwa Uhamishoni Bagamoyo na baadaye Zanzibar ndiyo walikuja na hoja ya Kiswahili na Uislamu. Lakini wale waliobakiA Ilala 'Misheni Kota" wao waliporudishwa hawakupangiwa kutawala Kalenga. Hao ndiyo wale Wakristo.
Jambo hili lilipingwa sana wamissionary wa kijerumani unaweza kutupatia maelezo ya kwanini walilipinga?
Hao "wamissionary" hata vitabu vya Historia vya darasa la nne wanaelezewa kama walikuwa ni mawakala wa Ukoloni. Kumbuka kwamba ni Sapi ambaye ndiye aliyerithi utawala wa MKwawa na yeye tayari tangu akiwa Bagamoyo alishasilimu na kuwa Muislamu na alipotoka Zanzibar alirudi na Mwalimu wa dini ya Kiislamu kuja kuwafundisha wahehe wa Kalenga Uislamu.
Kwa hiyo hao wamisheni walijua wao kwa Sapi hawatakuwa na maslahi na hasa kama waislamu watakuwa wengi kwa maana nyingine kuongeza ushawishi wa waarabu Kalenga. Na ujue kwamba eneo alilokuwa anatawala Sapi ndilo kwa leo lina Mbuga ya Ruaha national park na huko ndiko kulikuwa na Tembo wengi.
FaizaFoxy nivizie kwingine swali lako kwenye thread hii sitaweza kulijibu.