Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Sheikh Mohamed,
..hizi tuhuma zote ulizoweka ulizipeleka kwa wahusika wazijibu kabla hujachapisha kitabu chako?
..kama ulifanya hivyo wahusika walikupa majibu gani?
..kama hukuwasiliana na wahusika unaweza kueleza kwanini hukufanya hivyo?
Wakristo wa dunia nyingine unawaonaje? Unawakubali au wanakukubali? Naona una historia yako mwenzetu! Kwa lipi, UDINI huu?
Kwa kweli mnawaonea wenzenu tu kwa kuwalisha masimulizi ya Uongo. Waislamu wako ndani ya serikali, wako Bungeni, wako wanafurahia maisha katika kila nafasi nchini. Hakuna nafasi yoyote ya ajira ambayo Waislamu huwezi kuwakuta wakiendelea kuijenga nchi yao kwa amani na ushirikiano na ndugu zao. Wapo ma CEO, Majenerali, Makamishna, Maprofesa, n.k Wanaweza kusihi popote na wakifanya kazi zao bila kujihisi kuwa wako oppressed. Mnaowapata ambao hawajui ndio wanaoamini lakini Watanzania hawako oppressed na Kanisa wala na Wakristu. Waislamu wa Tanzania kama walivyo Wapagani na Wakristu wanakandamizwa na mfumo wa Ufisadi ambao umejengwa na ambao watumishi wake ni watu wenye imani mbalimbali hata wenye kumuamini shetani!
S
Yeah of course mtu akitaka hadithi yake inoge lazima uweke na manjonjo humo ndani. Kuna watu walikuwa wakisimulia hadithi hadi watu wanashikwa na midadi. Na nakuambia hujakaa na wazee wakakupigia hadithi utashangaa inavyonogeshwa na hakuna hadithi tamu kama ambayo imewekwa wimbo wa kibwagizo mle ndani. Ndivyo mnavyowafanyia wenzenu hivyo. Mmewapa kibwagizo cha "mfumo Kristu" na wao wanadakia kama watu wanaodakia wimbo ule wa utotoni "Watoto wangu eh!?"...
[/FONT][/URL]
Hao wanaomuita Nyerere Baba wa Kanisa hawajui tu kuwa wanampa hadhi kubwa sana katika historia ya Kanisa Katoliki. Vyeo vya Baba wa Kanisa hakuna mtu yeyote ambaye amepewa kwa karibu miaka 1500 ya Historia ya Kanisa. Kwa hiyo Waislamu wanaomuita Nyerere Baba wa Kanisa wanamkuza kuliko anavyostahili.
Hili nalo ni yale yale ambayo kama watu hawajui ni bora wajifunze kidogo. Nyerere kupewa Uanaheri na baadaye kutangazwa Mtakatifu hakuhusiani na yeye kuwa Rais. Siyo zawadi ambayo mtu anapewa na Kanisa kwa utumishi wake kwa Kanisa! Hili nalo kwa wasomi wangejifunza tu na uzuri wa google siku hizi ipo. Unaweza kuandika neno "canonization process" halafu uone kama huo mchakato unajali kama mtu ni Rais, maskini, tajiri, msomi au nini.
Tukisema lengo lako ni kumdunisha Nyerere hutaki. Unathutu kusema in a hyperbole kuwa heshima na mapenzi ambayo Waislamu walikuwa nayo 'yameondolewa kabisa". Hii ina maana hata ya kwako! Huna heshima wala mapenzi ya aina yoyote kwa Nyerere na unataka Waislamu wengine waamini hivyo. Bahati nzuri Wapo Waislamu kwa mamilioni ambao wanampenda Nyerere na kumheshimu na wamezidi kumpenda sana sasa hivi kwa sababu wamejua ni kwa namna gani walijaliwa kuwa naye kama kiongozi wa Taifa lao. Kikundi kidogo cha Waislamu waliokuwa na udini na waliomchukia Nyerere tangu miaka ya mwanzo ya 1950s ambao sasa wamewaachia wajukuu wao hiyo chuki bado kipo na sidhani kama kitaisha hivi hivi kwani bila ya chuki dhidi ya Nyerere kizazi hicho kitasimamia wapi au nini?
Once again, HAKUNA kitabu chochote cha historia rasmi ambacho kinafundisha au hata kinaweza kuthubutu kufundisha kuwa Nyerere ndiye "single handedly defeated the British". Nyerere mwenyewe hakuwahi kudai hivyo, hakuna kitabu chenye kauli hiyo na ushahidi wa historia unaonesha wazi kuwa Nyerere hakuongoza harakati za kuwang'oa Waingereza peke yake. HAKUNA KITABU KAMA HICHO.
Here we go again! Hujaandika kuhusu "the forgotten heroes of Indepence Movement". Umeandika kuhusu wanaharakati Waislamu na wengine wote ukawaacha (you also forgot them!). How can one trying to remember the 'forgotten' choose so purposely to forget some of which he vowed to remember?
Ndio tatizo hilo.. ukawaangalia wale Waislamu tu huku ukidai ni "the forgotten heroes". Na Uislamu hapa unaangalia kwa majina tu.
Probably right.. but are you sure it stood naked. Je swali hili linaulizwa kuhusu taasisi nyingine za kidini wakati wa kukomesha utumwa tuone kama nazo zinaweza kuachwa watupu? Uzuri mmoja wa Kanisa Katoliki kwenye haya mambo ya historia ni kuwa halina hofu ya historia yake. Kwa miaka 2000 historia ya Kanisa Katoliki imejaa mazuri na maovu mengi tu. Lakini ni historia ambayo haitaji kurembewa.
Japo hili linaweza kuonekana ni jambo la kina sanalakini ukiliangalia kwa karibu halina kina hicho. Ni lazima ujue mafundisho ya Kanisa ya wakati ule yalikuwaje kwenye suala la mambo ya vita. Lakini vile vile unashindwa kukiri nafasi ya kanisa katika kuponya maeneo ambayo yalikuwa yameharibiwa na Wajerumani na kutoa huduma kwa majeruhi ya vita. Ni kweli yawezekana Kanisa halikufanya mengi (sijui lingefanya nini hasa sijui maana kule Ulaya nako Kanisa linalaumiwa kwa hivi hivi) lakini kwa hakika limefanya mengi mara baada ya vita hiyo na ile ya kwanza ya dunia na ya pili ya dunia.
MM,
Hivi wewe huoni vibaya kuwa kila siku unapiga fidla ya pili?
Niandike tena "paper" we uje nyuma yangu.
Nitoa kwenye kitabu wewe uje nyuma yangu.
Wewe huoni haya?
Unadhani una uwezo wa kupambana na mimi kwa njia hiyo?
Pumzika.
Tafuta mambo mepesi.
Hapa ndipo kikomo cha usomi wako?
Mohamed
Bw. Said ukija kwenye masimulizi tu ya kufabricate historia kwa kweli sikuwezi lakini likija suala la kuangalia vitu kwa mwanga objective na kuwa wakweli katika historia katikahilo wewe husimami. Unaweza kuwavutia watu ambao wamegoma kutumia chembe za ubongo kwenye vichwa vyao vizuri na ambao hufurahishwa na masimulizi kama yale ya Mpiga Filimbi wa Hamlin. Watu wanafuata tu kwa sababu filipimbi inapigwa lakini hawajui mwisho wao ni maangamizi.
Kwa sasa hivi umeshindwa kuandika historia kama ilivyo na hivyo kazi hizi zote ulizozifanya siyo kazi za kihistoria zaidi ya kazi za kihisia ambazo zina lengo la kuonesha tu kitu kisichokuwepo na kutukuza kisichokukwepo. Unajaribu kutengeneza mashujaa wasiokuwepo huku mashujaa wa kweli unawakana. Kwa kutumia dini unajaribu kuwavutia wale ambao kwao dini ndio msingi wa umoja wao na siyo taifa lao. Hawa watakufuata na kukushangilia wao na watoto wao. Wataamini kabisa kuwa filimbi unayowapigia ni ya burudani na watacheza na kukushangilia na wewe ukienda huku unatikisa kichwa kwa mbwembwe na tabasamu motomoto. Lakini unajua unachokifanya.
Kupingwa utapingwa na hoja zako zitakataliwa na kuoneshwa jinsi zilivyo dhaifu. Siyo tu zitakatliwa bali zitaendelea kufunuliwa na kuwekwa peupe na kuzionesha kuwa ni hoja zenye udini ulio wazi ambao zina lengo la kuleta mgogoro wa kudumu kati ya vizazi vya Wakristu na Waislamu wa Tanzania. Unaendeleza itikadi ya wale wazee waliomkataa Nyerere mwanzoni mwa miaka 1950 kwa sababu ya Ukatoliki wake na ambao mwishoni mwa 1950s walitaka kuanzisha chama chao cha kidini na anmbao walikataliwa mwanzoni mwa miaka ya 1960s na wengine kuondolewa kabisa katika siasa za Tanzani amwishoni mwa miaka 1960s! Hawa wazee wadini ambao walikuwa wanaongozwa na chuki ya kidini wamewarithisha watoto na watoto wa watoto wao chuki hii na kwa muda waliachwa kutamba bila kuzuiwa au kupingaa.
Bahati nzuri kizazi kipya cha Watanzania Waislamu kwa Wakristu, Vijana kwa Wazee, wabara na wapwani wamesimama kidete kukataa ajenda ya itikadi ya chuki ambayo mjumbe wake wa kudumu ni wewe. Unataka kuwafanya Waislamu wajisikie wanyonge ndani ya nchi yao; unataka watembeee wakiwa wanaamini kuwa wap mo victims wa jinamizi la kuchora liitwalo "Mfumo Kristu". Umewachorea picha hii ya jinamizi na kuliweka manyoya, meno makali, macho ya kutisha na kulifanya lionekane kama linanguruma kweli. Kweli wasiojua wakiliona kwenye picha yako wanashtuka na mioyo yao inawalipuka.
Kwa neema wapo watu ambao wamegundua kuwa ni picha tu! Ni picha ya kuchora kama yule Simba wa Kuchora wa Bw. fulani! Inawatisha wale ambao wanafikiria picha inaweza kuuma na wale watoto ambao labda hawajui tofauti ya picha na kitu halisi. Bw. Said picha yako itaonekana ni picha tu pale Waislamu wa Tanzania na Wakristu wa Tanzania watakapotambua kuwa tatizo lao siyo kanisa wala Wakristu! Watakapotambua kwa tatizo lao ni ufisadi na uongozi wa kisiasa wenye kuendekeza ubinafsi, wizi wa mali za umma, matumizi mabaya ya madaraka na ukosefu wa utu. Watatambua kama walivyotambua Waislamu wa Misri, Yemen, Iran, Syria, Tunisia, Saudia, Oman n.k kuwa mwanadamu ana haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake. Watakapotambua kuwa kudhulumiwa na Muislamu mwenzao siyo haki yao na kuwa wao nao ni binadamu sawa kabisa na wale watawala.
Bahati nzuri hili limeanza kutokea. Ndio maana leo hii Watanzania wanasimama pamoja kama walivyosimama wazee wao miaka hamsini iliyopita. Wanasimama pamoja wakikataa ubaguzi wa aina yoyote kati yao. Leo hii Watanzania wanasimama pamoja kukataa sera mbovu ambazo zimeharibu elimu na nafasi ya watu wetu kufanikiwa. Leo hii Watanzania wanasimama pamoja kudai haki zao na thamani yao kama watu. Naam, kwa pamoja wanakuja kuanza kudai ujenzi wa taifal jipya la kisasa ambamo ndani yake kila Mtanzania (na msisitizo uko kwenye 'kila') anafurahia matunda ya uhuru bila upendeleo wowote wa rangi, nasaba, jinsia, dini, n.k Wanarudia misingi ya taifa lao ambalo leo wanaitamani. Kuwa wao walizaliwa katika umoja na udugu.
Itikadi yako na ya wale wengine wanaomini katika mgongano wenye msingi wa kidini itashindwa kwani tayari imeshindwa
! Tunachojitahidi kufanya hapa sisi wengine ni kukuonesha tu kuwa itikadi hiyo imeshindwa na haina nafasi ya kufanikiwa.
Niliwahi kusema hapo nyuma uwongo ukipewa nafasi ya kurudiwa rudiwa lazima tu wapo watu watanasa na hasa wale wanaoongozwa kwa hisia na mbaya kuliko zote ni hisia za dini. Lakini tatizo lingine ni kuwa hata muongo mwenyewe anaanza kuuamini uwongo alioutunga na kuuona kama ukweli kwa sababu tu wako watu ambao watameza chochote kile mradi dini yao imeguswa. Anayoyahubiri Mohamed Said siyo mageni masikioni mwa wengi wetu kama anavyodhani, wengine tuliyasikia hata kabla ya uhuru wa Tanganyika.
Ni kweli pia mtoto umleavyo ndivyo akuavyo na Mohamed Said anayedai kuwa alipata malezi mema hatuna haja tena ya kujiuliza aina ya malezi aliyoyapata na anayoyaongelea. Lakini historia ina tabia moja ya kujirudia na ninaamini kwa jinsi ile ile Waislaam wema walivyowakataa wachochezi waliotaka kutuvuruga mwaka 1958, wengine wao wakiwa Wazee wa Mohamed Said ndivyo hivyo Waislaam wema wa leo watamkataa Mohamed Said na uchochezi wake kama tunavyoshuhudia humu kutoka kwa Mkandara na Nguruvi3.
Atawapata watu kama Barubaru, watu ambao kisirani chao wanashindwa hata kukificha kwani pamoja na kuukana uraia wa Tanzania bado wanafikiri utawala wa Kisultani utarejea. Nina imani kubwa na Waislaam wema ambao ninashiriki nao kila siku kwa shughuli mbali mbali na hawasiti kuwalaani hawa wachochezi ambao ni vigumu kuelezea hata wanavyoruhusiwa kupanda hizi mbegu za chuki. Mohamed Said kama anavyojisifu, atatembea sehemu nyingi ndani na nje ya nchi akieneza uwongo, lakini kwa watu makini ategemee kukwaa kisiki.
Mimi Mag3 sina haja ya kujibu hoja anazozitoa Mohamed Said kwani naamini kufanya hivyo ni kumpandisha daraja kama mwandishi wa historia na mtafiti, daraja ambalo kama wazee wake, atabaki akiiota tu kwani sifa hiyo kaipoteza kwa kusimulia uwongo. Toka miaka ya mwanzoni baada ya uhuru nimeishi jijini Dar es Salaam, najua nilivyoikuta na ilivyokuwa miaka kumi baadaye na mtu hanidanganyi hata kama alizaliwa Gerezani. Mohamed Said sasa yabidi ajitazame upya na kujiuliza, anataka kulipeleka taifa wapi na hizi porojo zake.
Mohamed Said.
Nikipitia vitabu vyako na makala zako uwa nakutana na haya maneno ya John Dryden..
Uongo, kama vile nyasi juu ya maji huelea;Atafutae Lulu budi kupiga mbizi.
Kuna awa wazee TANU bado wapo hai Dome Okochi, Bilal Rehani Waikela, Yusufu Chembera, Japhet Kirilo?
Mag3,
Ukweli ni kuwa huna uwezo wa kupambana na mimi si kuwa "hutaki" kujibu hoja zangu.
Soma hii hapa chini baadhi ya rejea nilizopitia katikia kitabu changu nionyeshe porojo ilipo:
1. [1]Daisy Sykes Buruku, ëThe Townsman: Kleist Sykesí, katika Iliffe (ed) ModernTanzanians, Nairobi, 1973, uk. 95-114. Angalia A.D. Sykes ëThe Life of Kleist Sykesí, University of Dares Salaam Ref. No. JAN/HIST/143/15.2. [1]M.J. Sichwale kwa Ally Sykes 2 Agosti, 1962. Nyaraka za Sykes.3. [1]Listowel, op. cit. uk.121.4. [1]Listowel kwa Ally Sykes, 12th November 1962. Nyaraka za Sykes.5. [1]Angalia Press Release A/2746/68 IT/1.322 ya 13th October 1968. East Africana,University of Dar es Salaam,6. [1]Sunday News, 20th October 1968.7. [1]Hassan Upeka aliajiriwa na TANU mwaka 1956 mara tu baada ya kumaliza masomoyake Tabora School. TANU ilimpeleka katika mafunzo ya ukachero Israel na nchikadhaa za Ulaya ya Mashariki. Upeka alifanya kazi hiyo kabla na baada ya uhuru.8. [1]Ili kuweza kuelewa matatizo ya historia rasmi angalia makala ya Nikolai Maslov,ëQuestions of History of the Communist Party of Soviet Unioní, katika DailyNews, 24th October, 1987. Kwa kufanya ulingano angalia Historia yaChamaÖop.cit.9. [1]Daily News, 6th October 1988.10. [1]Angalia M. Said, ëIn Praise of Ancestorsí, Africa Events, London, March/April 1988, uk. 37-41.11. [1]Wakati wa utawala wa Rais Julius Nyerere, Dr Mayanja Kiwanuka kwa hofu yakutambulikana kuwa yeye ni Muislam, alikuwa akijulikana kama Kataroge MayanjaKiwanuka. Baada ya kuondoka Nyerere na kuja kwa utawala wa Rais Ali HassanMwinyi, Dr Kiwanuka akabadili namna ya kuandika majina yake na sasa akawaanaitwa Dr Ahmed Kiwanuka. Huu ni moja ya mifano ya uoga waliokuwanao baadhi yawatu katika kujinasibisha na Uislam. 12. [1]Angalia Africa Events, May 1988 barua ya Dr K. Mayanja Kiwanuka.13. [1]Angalia Africa Events, June/July 1988.14. [1]Angalia Africa Events, September, 1988.15. [1]Kiwanuka, op. cit.16. [1]Angalia Fr. Peter Smith, ëChristian and Islam in Tanzania Development andRelationshipsí katika Islamochristiana, 16 (1990) uk.171-182. Vilevile Smith,ëSome Elements for Understanding Muslim-Christian Relations in Tanzaniaí. 1993(ilitolewa katika semina Dakar, Senegal, ëIslam in Africa South of Saharaí).17. [1]Smith, passim18. [1]Kwa kuelewa nafasi ya utamaduni, makundi ya watu, itikadi etc. katika vyama vyasiasa angalia Maurice Duverger, Political Parties, Their Organisation andActivity in the Modern State, (New York, 1963).19. [1]Angalia Elder Council Section File 376, Maktaba ya CCM, Dodoma.20. [1]Angalia M. Said, ëFounder of a Political Movement: Abdulwahid K. Sykes1924-1968í, Africa Events, London September, 1988, uk. 38-41.21. [1]Angalia Daily News, 23rd October 1988. Vilevile Uhuru, 23 Oktoba 1988.22. [1]ëAn Unsung Hero?í Africa Events, London, November, 1986 uk.
Mohamed
Mlidhani wazee wetu hawataacha kumbukumbu ya khiyana na dhulma zenu?
Mohamed
Tooba Ya'rabi! Yamekuwa hayo Msalie Mtume mzee -.. haya na na miye nina khiyana na dhulma gani kwa Waislamu miye?
Mwislamu mmoja safi kabisa wa aina yako wewe na Mzee Mohamed aliniambia "hamkubaliani" na watu kama Mbowe kuvaa hivo. Nakumbuka pia Hijab ya Mama Fatma Kimario wa Igunga ilivoleta tafrani kule.
Bw. Said ukija kwenye masimulizi tu ya kufabricate historia kwa kweli sikuwezi lakini likija suala la kuangalia vitu kwa mwanga objective na kuwa wakweli katika historia katikahilo wewe husimami. Unaweza kuwavutia watu ambao wamegoma kutumia chembe za ubongo kwenye vichwa vyao vizuri na ambao hufurahishwa na masimulizi kama yale ya Mpiga Filimbi wa Hamlin. Watu wanafuata tu kwa sababu filipimbi inapigwa lakini hawajui mwisho wao ni maangamizi.
Kwa sasa hivi umeshindwa kuandika historia kama ilivyo na hivyo kazi hizi zote ulizozifanya siyo kazi za kihistoria zaidi ya kazi za kihisia ambazo zina lengo la kuonesha tu kitu kisichokuwepo na kutukuza kisichokukwepo. Unajaribu kutengeneza mashujaa wasiokuwepo huku mashujaa wa kweli unawakana. Kwa kutumia dini unajaribu kuwavutia wale ambao kwao dini ndio msingi wa umoja wao na siyo taifa lao. Hawa watakufuata na kukushangilia wao na watoto wao. Wataamini kabisa kuwa filimbi unayowapigia ni ya burudani na watacheza na kukushangilia na wewe ukienda huku unatikisa kichwa kwa mbwembwe na tabasamu motomoto. Lakini unajua unachokifanya.
Kupingwa utapingwa na hoja zako zitakataliwa na kuoneshwa jinsi zilivyo dhaifu. Siyo tu zitakatliwa bali zitaendelea kufunuliwa na kuwekwa peupe na kuzionesha kuwa ni hoja zenye udini ulio wazi ambao zina lengo la kuleta mgogoro wa kudumu kati ya vizazi vya Wakristu na Waislamu wa Tanzania. Unaendeleza itikadi ya wale wazee waliomkataa Nyerere mwanzoni mwa miaka 1950 kwa sababu ya Ukatoliki wake na ambao mwishoni mwa 1950s walitaka kuanzisha chama chao cha kidini na anmbao walikataliwa mwanzoni mwa miaka ya 1960s na wengine kuondolewa kabisa katika siasa za Tanzani amwishoni mwa miaka 1960s! Hawa wazee wadini ambao walikuwa wanaongozwa na chuki ya kidini wamewarithisha watoto na watoto wa watoto wao chuki hii na kwa muda waliachwa kutamba bila kuzuiwa au kupingaa.
Bahati nzuri kizazi kipya cha Watanzania Waislamu kwa Wakristu, Vijana kwa Wazee, wabara na wapwani wamesimama kidete kukataa ajenda ya itikadi ya chuki ambayo mjumbe wake wa kudumu ni wewe. Unataka kuwafanya Waislamu wajisikie wanyonge ndani ya nchi yao; unataka watembeee wakiwa wanaamini kuwa wap mo victims wa jinamizi la kuchora liitwalo "Mfumo Kristu". Umewachorea picha hii ya jinamizi na kuliweka manyoya, meno makali, macho ya kutisha na kulifanya lionekane kama linanguruma kweli. Kweli wasiojua wakiliona kwenye picha yako wanashtuka na mioyo yao inawalipuka.
Kwa neema wapo watu ambao wamegundua kuwa ni picha tu! Ni picha ya kuchora kama yule Simba wa Kuchora wa Bw. fulani! Inawatisha wale ambao wanafikiria picha inaweza kuuma na wale watoto ambao labda hawajui tofauti ya picha na kitu halisi. Bw. Said picha yako itaonekana ni picha tu pale Waislamu wa Tanzania na Wakristu wa Tanzania watakapotambua kuwa tatizo lao siyo kanisa wala Wakristu! Watakapotambua kwa tatizo lao ni ufisadi na uongozi wa kisiasa wenye kuendekeza ubinafsi, wizi wa mali za umma, matumizi mabaya ya madaraka na ukosefu wa utu. Watatambua kama walivyotambua Waislamu wa Misri, Yemen, Iran, Syria, Tunisia, Saudia, Oman n.k kuwa mwanadamu ana haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake. Watakapotambua kuwa kudhulumiwa na Muislamu mwenzao siyo haki yao na kuwa wao nao ni binadamu sawa kabisa na wale watawala.
Bahati nzuri hili limeanza kutokea. Ndio maana leo hii Watanzania wanasimama pamoja kama walivyosimama wazee wao miaka hamsini iliyopita. Wanasimama pamoja wakikataa ubaguzi wa aina yoyote kati yao. Leo hii Watanzania wanasimama pamoja kukataa sera mbovu ambazo zimeharibu elimu na nafasi ya watu wetu kufanikiwa. Leo hii Watanzania wanasimama pamoja kudai haki zao na thamani yao kama watu. Naam, kwa pamoja wanakuja kuanza kudai ujenzi wa taifal jipya la kisasa ambamo ndani yake kila Mtanzania (na msisitizo uko kwenye 'kila') anafurahia matunda ya uhuru bila upendeleo wowote wa rangi, nasaba, jinsia, dini, n.k Wanarudia misingi ya taifa lao ambalo leo wanaitamani. Kuwa wao walizaliwa katika umoja na udugu.
Itikadi yako na ya wale wengine wanaomini katika mgongano wenye msingi wa kidini itashindwa kwani tayari imeshindwa! Tunachojitahidi kufanya hapa sisi wengine ni kukuonesha tu kuwa itikadi hiyo imeshindwa na haina nafasi ya kufanikiwa.
................Kazi za kitafiti ni kazi za kitaaluma zaidi nazo siku zote zinajibiwa kitaaluma na kitafiti na si vinginevyo........
the fact ni kwamba hiyo statement hapo juu haina UKWELI......period
Brother MS anaweza kuwa mtafiti sawa.......lakini kwa hizi hadithi za wazee wake huhitaji.......kuambiwa au kufanya utafiti kuona uongo na uchochezi wake........labda kama maana ya utafiti ya Brother MS au yako ni tofauti na tafiti ambazo zinaeleweka kitaaluma......