Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Hivi kwanini usichukue nafasi hii adimu kwenda Kuwa hoji hao unaosema ili wao nao waje na upande wao wa hadithi alafu utekee hapa tuone kipi kweli na kipi uongo?kukazania kwamba MS ni mzushi hauta eleweka kwani kunabaadhi yetu hapa tunajua ya MS kabla hata yeye hajayaleta.
Kwakua wewe unao watu ambao unadai maelezo yao hata kua "hearsay" nenda upate maelezo yao kwani "angles" tayari MS ameshakupa.baadae kwa kutumia ujuzi wako na ile "radio" sijui podcast yako utatuwekea hata sauti achilia mbali maelezo

Mwanakijiji.

Huo ndio hata mimi ushauri wangu kwako. Kumbuka hapa nia ni kuandika kile kilichojificha na kufichwa iwe kwa kusahaulika au kwa makusudi maalum katika historia ya Tanganyika.
 
Faiza,

Ungelikuwa mwanamme ningelikuvisha kilemba na kukupa kashda
.

Somesha mwanangu somesha...wape urithi wa mtukufu wa darja.

Mimi nikifika hafla yoyote ya Waislam basi wakiniona nyuma hunivuta mbele na kama ni maulid huwekwa
sawasawa na kinara katikati ya masheikh wakubwa ambao mimi siwezi hata kubeba viatu vyao.

Mimi najua kwa nini wanafanya hivi na nashukuru kuwa ndugu zangu wananipenda.

Mimi sijaalikwa na BAKWATA tu hao ndiyo "wasonijua."

Mohamed

Ahsante Sheikh wangu hii sifa ulionipa kwa kuukubali tu mchango wangu ni zaidi ya Kilemba na Kashda. Shukran Sana.
 
Hivi kwanini usichukue nafasi hii adimu kwenda Kuwa hoji hao unaosema ili wao nao waje na upande wao wa hadithi alafu utekee hapa tuone kipi kweli na kipi uongo?kukazania kwamba MS ni mzushi hauta eleweka kwani kunabaadhi yetu hapa tunajua ya MS kabla hata yeye hajayaleta.
Kwakua wewe unao watu ambao unadai maelezo yao hata kua "hearsay" nenda upate maelezo yao kwani "angles" tayari MS ameshakupa.baadae kwa kutumia ujuzi wako na ile "radio" sijui podcast yako utatuwekea hata sauti achilia mbali maelezo

Swali zuri sana lakini unamuuliza mtu asiye sahihi. Miye sijawahi kudai naandika historia ya Tanganyika wala historia ya wale "waliosahauliwa". Siku nikitaka kuandika historia kweli kabisa haiwezi kuwa kama alivyoandika Bw. Said. Sitamtaja mtu ambaye sikumpa nafasi ya kunieleza upande wake na wala sitatumia maneno kama "inasemekana" au "ilionekana" au "inaaminika" nitaandika kile tu ambacho kina ushahidi ambao mtu mwingine anaweza kuupima. So, hili ombi tuungane tumpatie Mzee Said kuwa awahoji hawa wengine ambao yeye kawataja.
 
Mwanakijiji.

Huo ndio hata mimi ushauri wangu kwako. Kumbuka hapa nia ni kuandika kile kilichojificha na kufichwa iwe kwa kusahaulika au kwa makusudi maalum katika historia ya Tanganyika.

Kweli kabisa. Je unaona kuwa ni udhaifu mkubwa kwa Mzee SAid kutowahoji watu waliokuwa hai na ambao anawataja kwa kupitia maneno ya watu wengine? kuwa angefanya vyema sana kuwahoji kama mama Nyerere, Mzee Mwinyi n.k?
 
Kwanini uone kazi ya Mohamed Said kutokuwahoji hao unaowataka wewe ni udhaifu? Je wale wazee wa kigamboni walipoandika historia ya Tanu na Tanganyika mbona hawakuwahoji akina Sykes, Mshume Kiyate, Sheikh Takadir, Sheikh Hassan bin Ameir na wengineo? na historia hii unaikubali wewe ila ya akina Mohamed Said ina udhaifu!!!! Kweli ukipenda bana hata chongo utaita kengeza tu mradi roho yako ifurahi.
 
Swali zuri sana lakini unamuuliza mtu asiye sahihi. Miye sijawahi kudai naandika historia ya Tanganyika wala historia ya wale "waliosahauliwa". Siku nikitaka kuandika historia kweli kabisa haiwezi kuwa kama alivyoandika Bw. Said. Sitamtaja mtu ambaye sikumpa nafasi ya kunieleza upande wake na wala sitatumia maneno kama "inasemekana" au "ilionekana" au "inaaminika" nitaandika kile tu ambacho kina ushahidi ambao mtu mwingine anaweza kuupima. So, hili ombi tuungane tumpatie Mzee Said kuwa awahoji hawa wengine ambao yeye kawataja.

Hapo itakuwa huandiki Historia unaandika storia, hivi utampata Abdul Wahid Sykes umuulize? au utaenda kwenye "the nearest source"? Hivi Mohamed Said alikuwa akiiandika "biography" au historia? Kama ni historia basi hakuwa na haja ya kumuuliza anaemwandika zilizohitajika ni "reliable sources" na kama angalikuwa anaandika "biography" ya Nyerere na mwenyewe yuko hai hicho ni kitu kingine. Hivi leo uende ukamuulize mama Maria Nyerere "Tunasikia Mumeo alijuana na Abdul Wahid Sykes ni kweli au uongo?" Unategemea jibu lipi? Na ukienda kumuuliza Ali Sykes ambae licha ya kuwa ni ndugu yake Abdul Wahid khalisa alikuwa ni Mwanaharakati mwenzake na isitoshe ana kumbukumbu za nyaraka ambazo nna uhakika hata Maria Nyerere hanazo, unategemea upate zaidi kwa Maria Nyerere au kwa Ali Sykes? kwani Abdul Wahid Sykes kama inavyojionesha alikuwa katika harakati za kisiasa kabla ya Nyerere na mkewe kuja Dar kutokea Butiama. Hivi hapo kuna tatizo lipi la kuelewa?

Nashangaa sana muandishi anaposhindwa kutofautisha "biography", "history", "news" na "article".
 
Mnapomzungumzia Mama Maria Nyerere mnajua amesoma mpaka darasa la ngapi?
Je mnaujua uwezo wake?
Je Nyerere mwenyewe alimuhusisha katika vitu vyake hususan vya kitaaluma na uongozi?
au alikuwa ni mama wa nyumbani wa pika pakua tu?

Kila la kheir.
 
Swali zuri sana lakini unamuuliza mtu asiye sahihi. Miye sijawahi kudai naandika historia ya Tanganyika wala historia ya wale "waliosahauliwa". Siku nikitaka kuandika historia kweli kabisa haiwezi kuwa kama alivyoandika Bw. Said. Sitamtaja mtu ambaye sikumpa nafasi ya kunieleza upande wake na wala sitatumia maneno kama "inasemekana" au "ilionekana" au "inaaminika" nitaandika kile tu ambacho kina ushahidi ambao mtu mwingine anaweza kuupima. So, hili ombi tuungane tumpatie Mzee Said kuwa awahoji hawa wengine ambao yeye kawataja.

Mkuu,

"Kuungana" na wewe ili kumuuliza Bwn.Muhamed Said siwezi,haya aliyo yaleta yeye mimi nayafahamu kitambo na nilishachukua nguvu kuyaleta hapa kwenye mijadara ya zamani iliyo muhusu Nyerere lakini kwakua sikua na "research" zaidi ya hadithi na watu hapa barazani kunishinda kwa HOJA niliachana nalo lakini kama kumbukumbu zako zitakuwa sawa...,ilikuandikia kukupa namba ya simu ya mtu ambaye mimi nilidhani angekuwa source nzuri tu kwa haya ambayo MS ameyaleta lakini hukufatilia.
Sasa sijui unadhani na wewe kuungana na nani hapa kati yako na MS?
 
Mwanakijiji.

Huo ndio hata mimi ushauri wangu kwako. Kumbuka hapa nia ni kuandika kile kilichojificha na kufichwa iwe kwa kusahaulika au kwa makusudi maalum katika historia ya Tanganyika.

Barubaru,

Na vile vile akumbuke kuandika source za taarifa zake, tarehe na watu husika ili iwe rahisi na wengine waende kuwauliza je kama ulikuwapo mbona akina Mshume Kiyate wanasema vengine na tarehe zengine nk. Usiandike historia kwa kwenda kuwauliza wazee wa kigamboni tu ukaona umekamilisha historia. Nakutakia kila la kheri Mwanakijiji ila ujue kutofautisha baina ya "jarida", "utafiti", "wasifu" na "makala". Kila tafiti zina limitations zake but la msingi waulizwe hao waliotajwa ili kuendeleza yaliyopatikana katika utafiti. Sasa wewe anzia pale aliposema Mohamed Said kuwa waislamu wamebaguliwa na uje na utafiti unaonyesha kwanini waislamu hawabaguliwi ili tujifunze zaidi. Otherwise, Neither you nor the rest of Pro-nyerere fans have intellectual authority to criticise Mohamed Said work.
 
Mnapomzungumzia Mama Maria Nyerere mnajua amesoma mpaka darasa la ngapi?
Je mnaujua uwezo wake?
Je Nyerere mwenyewe alimuhusisha katika vitu vyake hususan vya kitaaluma na uongozi?
au alikuwa ni mama wa nyumbani wa pika pakua tu?

Kila la kheir.

Mbona hujauliza hawa mashahidi wengine ambao wanatumiwa katika kitabu hicho walisoma mpaka darasa gani? Kwa taarifa tu mama Maria Nyerere ni mwalimu kwa taaluma.
 
Otherwise, Neither you nor the rest of Pro-nyerere fans have intellectual authority to criticise Mohamed Said work.

I hope you include yourself but don't include me. If you consider yourself lacking intellectual authority to criticize Mr. Said, speak so on your own behalf. Some of us do indeed have and are willing to use unsparingly our intellectual authority and prowess to question and criticize what we consider to be a pseudo-history.
 
Hapo itakuwa huandiki Historia unaandika storia, hivi utampata Abdul Wahid Sykes umuulize? au utaenda kwenye "the nearest source"? Hivi Mohamed Said alikuwa akiiandika "biography" au historia? Kama ni historia basi hakuwa na haja ya kumuuliza anaemwandika zilizohitajika ni "reliable sources" na kama angalikuwa anaandika "biography" ya Nyerere na mwenyewe yuko hai hicho ni kitu kingine. Hivi leo uende ukamuulize mama Maria Nyerere "Tunasikia Mumeo alijuana na Abdul Wahid Sykes ni kweli au uongo?" Unategemea jibu lipi? Na ukienda kumuuliza Ali Sykes ambae licha ya kuwa ni ndugu yake Abdul Wahid khalisa alikuwa ni Mwanaharakati mwenzake na isitoshe ana kumbukumbu za nyaraka ambazo nna uhakika hata Maria Nyerere hanazo, unategemea upate zaidi kwa Maria Nyerere au kwa Ali Sykes? kwani Abdul Wahid Sykes kama inavyojionesha alikuwa katika harakati za kisiasa kabla ya Nyerere na mkewe kuja Dar kutokea Butiama. Hivi hapo kuna tatizo lipi la kuelewa?

Nashangaa sana muandishi anaposhindwa kutofautisha "biography", "history", "news" na "article"
.

Well.. nimependa wakati mwingine unazungumza sense. Kitabu cha Abdulwahid Sykes ni nini kati ya hayo manne!?
 
Kwanini uone kazi ya Mohamed Said kutokuwahoji hao unaowataka wewe ni udhaifu? Je wale wazee wa kigamboni walipoandika historia ya Tanu na Tanganyika mbona hawakuwahoji akina Sykes, Mshume Kiyate, Sheikh Takadir, Sheikh Hassan bin Ameir na wengineo? na historia hii unaikubali wewe ila ya akina Mohamed Said ina udhaifu!!!! Kweli ukipenda bana hata chongo utaita kengeza tu mradi roho yako ifurahi.

sasa two wrongs make it right? kama hao wazee hawakuwahoji wahusika wengine wakati wakiwa hai ni kosa kubwa la uandishi na hivyo historia yao haiwezi kuwa kamili. Ukikubali hili ni lazima ukubali la M. Said vile vile. Je unakubali kuwa kwa kushindwa kuwahoji baadhi ya wahusika anaowataja Bw. Said hajaitendea haki historia anayoidai kutupatia?
 
Barubaru,

Na vile vile akumbuke kuandika source za taarifa zake, tarehe na watu husika ili iwe rahisi na wengine waende kuwauliza je kama ulikuwapo mbona akina Mshume Kiyate wanasema vengine na tarehe zengine nk. Usiandike historia kwa kwenda kuwauliza wazee wa kigamboni tu ukaona umekamilisha historia. Nakutakia kila la kheri Mwanakijiji ila ujue kutofautisha baina ya "jarida", "utafiti", "wasifu" na "makala". Kila tafiti zina limitations zake but la msingi waulizwe hao waliotajwa ili kuendeleza yaliyopatikana katika utafiti. Sasa wewe anzia pale aliposema Mohamed Said kuwa waislamu wamebaguliwa na uje na utafiti unaonyesha kwanini waislamu hawabaguliwi ili tujifunze zaidi. Otherwise, Neither you nor the rest of Pro-nyerere fans have intellectual authority to criticise Mohamed Said work.

Nilimtaka Mag3 pia atueleze yeye ni nani, ameandika kipi? akashindwa kujibu, alichonjibu ni kuwa "Mag3" inatokana na herufi tatu za mwanzo za jina lake. Nilipoulizwa mimi nikawatajia mpaka nyumbani kwetu, sijui kinawashinda nini kuwa wa wazi.

Maswali yangu kwa Mag3 hayana majibu mpaka dakika hii, akajikurupusha kwa kujidai namchekesha, kaingia mitini. Nawashangaa sana. Mwanakijiji hali kadhalika nimemuuliza maswali mawili matatu huko juu, anayakimbia kama ukoma.

Naona hawana hoja wala majibu kwa hiyo Sheikh Mohamed Said, mwaga vitu tufaidike.
 
Mwambieni alete tu lakini atawapa nyie ambao hamna ujasiri wa kufanya intellectual criticism kwa sababu mshakubali prima facie and by doing that your doing all of us a huge disservice. I'm quite sure yeyote kati yenu akiamua tu kidogo kufanya ukosoaji wa madai ya Bw. Said anaweza kujikuta anasikia uchungu. Ila inahitaji ujasiri kweli kumkosoa mtu ambaye tayari umekubali hata kabla hujasikia amesema nini. Na ninaombea kuwa wanaofanya hivyo si wasomi bali wanatumia imani kuamua na siyo uwezo wao waliopewa na Mwenyezi Mungu kuhoji, kuuliza, kusahihisha na hatimaye kuboresha kile wanachosikia.

Ukiona watu wanaoitwa wasomi - au wanaoamini kuwa ni wasomi - wanakubali maelezo ya msomi mwenzio bila kujaribu kuyakosoa basi ujue wana maslahi ambayo ni kinyume na kuutafuta ukweli kwani kwao ukweli siyo kile kinachosemwa bali yule anayesema. A tradegy of sort if you will.
 
FF,

Ahsante na nakushukuru sana.

Sheikh Mohamed Ayoub akiwafunza wanafunzi wake anasema elimu ni amana kwa hiyo mwenyewe akija kutaka amana aliyowekeza kwako ni wajib wako kumkabidhi amana yake.

Insha Allah mimi nitatoa kila ninachokijua kwa nia ya kuelimisha na kupata radhi za Allah na masheikh wetu walotufunza na kubwa zaidi wenzetu waelewe ukweli assa kheri huenda tukaliepuka janga linalotunyemelea.

Mohamed
 
I hope you include yourself but don't include me. If you consider yourself lacking intellectual authority to criticize Mr. Said, speak so on your own behalf. Some of us do indeed have and are willing to use unsparingly our intellectual authority and prowess to question and criticize what we consider to be a pseudo-history.

I do not think so may be in your thinking because from what you are writing in this thread

a. You do not have evidence to prove what Mohamed Said found is wrong. Instead you want Mohamed Said to spoon feed you with details why not go and find it for yourself?

b. You are driven by emotional thinking arguing that what actually happened was moderate muslims and nyerere fought for Tanganyika. When did this happened and why it has happened you do not have an answer for that (in short YOU ARE BIASED).

C. Your work has not being edited or proved by intellectuals (meaning historians) to be a worth of contribution to the history. I encourage you to do that.

e. Your work is not yet published nor submitted to any academic or professional body or conference. In SHORT YOU HAVE NO PUBLICATION.

Mie sijamcriticise Mohamed Said nor wale wazee wa kigamboni nachosema kuna tatizo somewhere na hivyo kuna haja ukawepo mjadala wa wazi kujadiliana haya masuala kwa manufaa ya taifa letu mbeleni (truth and reconciliation committee) ingelikuwa Mohamed Said ameingia katika anga zangu za nilichosomea angeona jinsi nilivyotambaa na ningelimcriticise kama kungelikuwa na haja hiyo . Therefore, I will like to conclude that you have no intellectual authority to question Mohamed Said or narudia tena NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK.
 
Mbona hujauliza hawa mashahidi wengine ambao wanatumiwa katika kitabu hicho walisoma mpaka darasa gani? Kwa taarifa tu mama Maria Nyerere ni mwalimu kwa taaluma.

Kwa kuwa ni Mwalim basi atakuwa na data za Abdul Wahid Sykes zaidi ya Ali Sykes?
 
Mwambieni alete tu lakini atawapa nyie ambao hamna ujasiri wa kufanya intellectual criticism kwa sababu mshakubali prima facie and by doing that your doing all of us a huge disservice. I'm quite sure yeyote kati yenu akiamua tu kidogo kufanya ukosoaji wa madai ya Bw. Said anaweza kujikuta anasikia uchungu. Ila inahitaji ujasiri kweli kumkosoa mtu ambaye tayari umekubali hata kabla hujasikia amesema nini. Na ninaombea kuwa wanaofanya hivyo si wasomi bali wanatumia imani kuamua na siyo uwezo wao waliopewa na Mwenyezi Mungu kuhoji, kuuliza, kusahihisha na hatimaye kuboresha kile wanachosikia.

Ukiona watu wanaoitwa wasomi - au wanaoamini kuwa ni wasomi - wanakubali maelezo ya msomi mwenzio bila kujaribu kuyakosoa basi ujue wana maslahi ambayo ni kinyume na kuutafuta ukweli kwani kwao ukweli siyo kile kinachosemwa bali yule anayesema. A tradegy of sort if you will.

Mwanakijiji,

Kosoa bila hofu nami Insha Allah nitajitahidi kujibu pale ninapoweza nikishindwa nitakufahamisha kuwa hilo sijui na tutasonga mbele.

Ningependa sana kusikia kwako kipi umekipata kipya kutoka kwangu.

Mohamed
 
Mnapomzungumzia Mama Maria Nyerere mnajua amesoma mpaka darasa la ngapi?
Je mnaujua uwezo wake?
Je Nyerere mwenyewe alimuhusisha katika vitu vyake hususan vya kitaaluma na uongozi?
au alikuwa ni mama wa nyumbani wa pika pakua tu?

Kila la kheir.

Ukisikia '' kumkoma Nyani Giladi'' ndio huku...sasa ndio nini tena Barubaru!!! hii nayo mppyaaa!
 
Back
Top Bottom