Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Nyerere alisema hivyo, ok! Mi ckuwahi msikia... Ila wewe unafikiri hili taifa linaongozwa na hiyo gospel??? Wanasheria wa dini mbalimbali wasaidie hapa...
Mbona tunasimamia mambo yasiyo na msingi?????? Utaifa mbele dada, alaaa!!

Micro narudia tena kusema huenda huijui vyema historia ya Waislam na harakati za kudai uhuru. Wazee wetu walikuwa "nationalists" khasa. Kuna kitabu kaandika Mutahaba, "Portrait of a Nationalist The Life of Ali Migeyo." Tafuta kitabu hiki ukisome ikiwa hujakisoma. Waliweka dini pembeni kutaka utaifa leo wamesalitiwa. Hebu soma hii hapa chini:

"Kipindichama badiliko kutoka TAA kuwa TANU kilikwenda vizuri pale makao makuu.Hakukuwa na ya migongano kati ya viongozi wa makao makuu, ukitoa kikundi kidogocha Waislamu wenye msimamo mkali waliokuwa wakipanga kumg'oa Nyerere kwa kuwaalikuwa Mkristo. Hii ilikuwa ni mara ya pili kwa suala la dini kuzuka tanguNyerere achukue uongozi wa chama kwa mara ya kwanza mwaka 1953. Mkutanouliitishwa kuweka hali sawa kuhusu Ukristo ndani ya chama. TANU iliamua kuwachama kitakuwa ni cha kisekula ili kunusuru na kuihifadhi umoja wa kitaifa.Mkutano huu ulifanywa ndani ya nyumba moja katika mtaa wa Pemba na uamuzi wakeuliungwa mkono na Mufti Sheikh Hassan Bin Amir, Sheikh Nurdin Hussein tokaLindi na Sheikh Abdallah Chaurembo wa Dar es Salaam. Mkutano huu ulimfananishana 'Yuda' mwanachama yeyote yule ndani ya TANU atakayembagua Mwafrika mwenzakekwa sababu ya imani yake. [1] Jina la hili 'Yuda' lilikuwa ndilo lile jinala Yuda Iskarioti katika Biblia, mfuasi aliyemsaliti Yesu kwa vipande thelathinivya fedha."

Baada ya uhuru haya yakawekwa pembeni na Nyerere kazi ikawa kulijenga Kanisa Katoliki kama tulivyoonyesha hapa ukumbini kwa rejea nyingi tu.

Mohamed
 
Ok Moha! Mimi inawezekana sijui dini vizuri....
Sasa kama amesema tusikubali kudhulumiwa, na amekataza tusidhulumu tutafanyaje katika hiyo hali???
Tulishadhulumiwa zamani, sasa tunyamaze tusonge mbele tukatae kudhulumiwa hiyo kuanzia sasa. (SIO KUFOCUS KWENYE KUKUMBUSHA PAST). Mfumo wa sasa tuko kila mahala, hilo halifichiki labda kama tunataka nchi iwe ya kiislamu na tujae peke yetu. Mambo taratibu sheikh..., tusomeshe watoto wakacompete. Na tuwafundishe WASIWE WADINI

Micro tukichukua mambo kwa wepesi kiasi hiki iko siku tutakumbwa na tufani tusijue lilikotokea mwishowe ni kulaumiana kwanini wewe hukusema?

Hapa tumeonyesha kwingi tu kuwa Kanisa Katoliki linadhulumu Waislam kupitia mfumokristo.

Hivi hauna habari ya hili vuguvugu la Waislam wa Tanzania nzima kupiga kelele kuhusu udini uliopo katika serikali toka uhuru?

Tarehe 11 Oktoba Waislam walifanya mkutano wa majumuisho Ukumbi wa Diamond baada ya kuzunguka nchi nzima wakizungumzia tatizo la mfumokristo.

Bahati mbaya vyombo vya habari havitaki kutangaza ukweli huu kwa hofu tu kuwa lipo tatizo la udini Tanzania ulimwengu usisikie labda ndiyo maana huna khabari.

Tulia, fikiri na uliza hali ya nchi ikoje utaelezwa upepo unaopepea ni upi.


Mohamed
 
Lakini kwa mujibu wako Nyerere alisema upuuzwe. Kwamba hakuna atakayekuamini. Tunashuhudia hapa majibu ya Nyerere.

Jasusi,

Swali je, imewezekana kupuuzwa?
Jibu hapana.

Leo historia hii niliyoandika imekuwa maarufu.
Katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru makala zangu za historia hii ndizo zilizopamba gazeti la Mwananchi na kwa hakika zimefungua macho wengi.

Hilo moja pili baada ya kutoka kitabu nimelikwa kwingi ndani na nje ya nchi kuzungumza.

Lakini kubwa ambalo hakika mimi linanisikitisha ni hili hapa chini hebu soma hii:

"Muslims are now organising nationwide mass rallies which openly and inlive broadcasts denounce the church, criticise the government and church agentswithin the ruling party Chama Cha Mapinduzi (CCM) and the Parliament for oppressingMuslims. Seemingly derogatory words like “pandikizi” (singular) and“mapandikizi” (plural) meaning “turncoats;” or the new coined word “MfumoKristo” roughly meaning “Christian dominance” are now part of the Muslim and Swahilivocabulary. These analogies are used freely in the Muslim media and amongMuslims in every day conversation. But what usually thrills Muslims and utterlysignificant showing that times have changed is when in the rallies and innormal discussion Muslims refer to Nyerere hitherto known respectfully as “Babawa Taifa” as “Baba wa Kanisa,” meaning “Church Elder.”[1] The moveby the Catholic Church to make him a saint has not helped matters. More so itproves all the allegations levelled against Nyerere that he never was anationalist but a Catholic zealot. Respect and love which Muslims once had forNyerere has been completely wiped out. The new generation of Muslims no longerbelieve in the official history of TANU and the propaganda that it was Nyererewho single handed defeated the British. Muslims instead are honouring theforgotten heroes of independence movement and in so doing invoking emotionsparticularly in the new generation to stand up against oppression as theirforefathers had done against Germans and the British. Muslim heroes of the MajiMaji War like Suleiman Mamba, Ali Songea Mbano,[2] andMuslim nationalists like Abdulwahid [3] and AllySykes,[4] DossaAziz, Sheikh Hassan bin Amir,[5] SheikhSuleiman Takadir, Sheikh Yusuf Badi, Bibi Titi Mohamed,[6] BibiTatu bint Mzee, Bilali Rehani Waikela,[7] AliMigeyo[8] andothers are now part of nationalist history which was suppressed for many years.[9] Muslimsare demanding the restoration of their history and honour as true liberators ofTanganyika. This is unprecedented. One can only speculate and wonder where thiswould lead to. Can we identify thisphenomenon as corrective and revision of history or is it a lesson of anarchyin recording history?[10] Theresult of all this is that the Church has been made to stand naked. That theChurch did not play any role during Maji Maji[11] orduring the struggle against the British or that it has worked hand in hand withthe government to sabotage Islam and Muslims is now common knowledge."

[1] The late Prof. Haroub Othman after reading Sheikh Ali Muhsin’s book Conflict and Harmony in Zanzibar and thewriter’s book The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 -1968 The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialismin Tanganyika, Minerva Press, London 1998 andhaving come across hitherto unknown information on Nyerere was devastatedbecause he was a great admirer of Nyerere as a patriot and a nationalist. Thetwo books had painted him differently. Prof. Haroub confronted Nyerere and toldhim that the allegations in those two works have tarnished his image and headvised him to respond to them. Nyerere never did. Christian lecturers at Dares Salaam University are discouraging students from making references to thosetwo books. Dr. Harith Ghassany’s book KwaheriUkoloni Kwaheri Uhuru, has also come up with more information on Nyererehitherto unknown in the Zanzibar Revolution and the bloodbath which followed.
[2] In all historical references to Maji Maji War hero and Chief of WangoniAli Songea Mbano, his Muslim name “Ali” would be omitted and he would bereferred to as Songea Mbano.
[3] MohamedSaid, The Life and Times of AbdulwahidSykes (1924 –1968), The Untold Story of the Muslim StruggleAgainst British Colonialism in Tanganyika Minerva Publishers, London, 1998.
[4] Mohamed Said, Broken Dreams, TheLife of Ally Kleist Sykes, Phoenix Publishers, Nairobi 2011 (Forthcoming).
[5] Issa Ziddy, Sheikh Hassan bin Ameir (1880-1979). Also See Mohamed Said, “Sheikh Hassan bin Ameir -The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968)” (Paperpresented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly ofMuslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27[SUP]th[/SUP]February – 4[SUP]th[/SUP] March 2004.
[6] Bibi Titi was recruited into TANU by Schneider Abdillah Plantan andbegan to mobilize people particularly women to join the party even before hecame to know Nyerere.
[7] Bilali Rehani Waikela one of the TANU founder members in WesternProvince in 1955 and Regional Secretary of the East African Muslim WelfareSociety (EAMWS) was detained by Nyerere in 1964 for “mixing religion andpolitics.” His personal papers were of great help in understanding the EAMWScrisis of 1968 and the reasons why Nyerere detained prominent sheikhs andbanned the society in 1968. A documentary of his political life has been madeand although not officially recognized as a patriot Muslims now consider him asone of the heroes of the independence movement. For more information seeMohamed Said, “In Praise of Ancestors,” AfricaEvents (London) March/April 1977.
[8] G. Mutahaba, Portrait of aNationalist: The Life of Ali Migeyo, East African Publishing House, 1969.
[9]Maji Maji Museum in Songea which has been greatlydesecrated removing all signs of Muslim symbols during the Maji Maji War withGermans. The Maji Maji Museum at Peramiho under the Catholic Church has closedits doors to young Muslims for fear of criticism for distorting history. AllMuslim symbols in Maji Maji War against Germans have been obliterated in theMaji Maji Museum.
[10] A children’s bookauthored by the current writer, Torch onKilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2007 has been blacklistedand cannot be included as a reader in schools because it contravenes the officialhistory.
[11] Yusuf Halimoja, Historia ya Masasi,East African Literature Bureau, Nairobi, 1977 pp 163 175 gives a narration howChristians fought alongside Gerrmans during Maji Maji. Also see P. GeroldRupper, OSB, Pugu Hadi Peramiho: Miaka100 wa Wamishionari Wabenediktini Katika Tanzania, BenedictinePublications, Ndanda Peramiho, 1980, pp 31- 42.


Kweli mtu anaweza kujilazimisha kukataa ukweli huu lakini mambo yamebadilika sana. Tanzania ile si hii. Waislam wanajiangalia upya kila kuchao.

Mohamed
 
Tatizo la watu wanaishi kwenye 'capital cities' ni kuamini wao ndio taifa na nchi.Mapinduzi ya nchi za kiafrika mengi yaliishia kuteka mji mkuu na nchi inaitwa imepinduliwa fine. Kwa hili la uhuru waislamu wa Dar es Salaam walichangia sana kwa kuotesha mbegu ya uhuru. Mbegu bahati mbaya hufa na ndicho kilichotokea ni maudhui ya dunia hayabadiliki. Viongozi wa bakwata wengi wanatoka dar, je bara hakuna waislamu au demographical reality. Kama tukiangalia kila kitu kwa ubaguzi katu hakuna kitachosimama, hata kile tunachokishikilia karibu na moyo.
 
Somalia dini moja kabila moja, hali ikoje?
Nini malengo ya kufocus kwa wazee wa Kariakoo tu, ukaacha MWANZA, TABORA, DODOMA, IRINGA KANDA ya KASkAZINI , MBEYA. note---I smell something fish is going on behind this thread

Mwakabako,

Karibu.

Ukipitia nyuzi za nyuma utakuta hayo yote uliouliza na kama unataka kuijua historia hii zaidi soma kitabu, "Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes..."

Au fuatilia "serialisation" za kitabu katika gazeti la "Lulu" ambalo wanaadhimisha miaka 50 ya uhuru kwa kuchapa kitabu ndani ya gazeti hilo.

Mohamed
 
Ndugu zangu wapendwa naomba achaneni na huyu MCHOCHEZI hana jipya na lengo lake kwanza halijulikani. Zaidi ni Nyerere tuu sasa anachopaswa kufanya ni kuwaelimisha Waislam wenzake umuhimu wa elimu na aache POROJO NA FITNA ZAKE.
Nchi hii watu hatuulizani DINI WALA KABILA ila juhudi zako ndo zitakubeba. Hivi kweli Nyerere hasingetaifisha shule za madhehebu ya dini sijui sasa tungekuwa tunaongea lugha gani?
HACHA UCHOCHEZI UTAISHIA THE HAGUE KWA OCAMPO SIJUI NAPO UTAMLAUMU MAREHEMU.
 
Sheikh Mohamed siasa na dini havishikamani hata siku moja umenukuu maneno ya Allah umetaka kuyalenga zaidi kwenye siasa hebu angalia matendo ya waislamu wenzetu yanaendana na hayo uliyosema? Waislamu na Wakristo tunadhulumiwa na mfumo wa siasa uliopo, narudia kusema mfumo huu wa siasa uliopo unalinda maslahi ya wachache; wapo mamilioni ya wakristo wanaishi maisha duni sana; ungekuwa mkweli kama ungepigania dhulma wanayotendewa watanzania.

Chama
Gongo la Mboto DSM

Chama usifanye haraka.
Fanya uchunguzi kabla hujatoa uamuzi wa jambo.

Mada hii imeanza mbali sana na naambiwa ni katika mada kali ambazo zimewahi kujadiliwa hapa ukumbini.

Rejea zilizotolewa ni nyingi na nina taarifa kuwa kuna wengi wamepigwa na mstuko kwa yale niloandika humu.

Si jambo la kimzahamzaha.

Yako mengi nishayasikia Insha Allah tutayajadili wakati wake ukifika.

Mohamed
 
Ndugu zangu wapendwa naomba achaneni na huyu MCHOCHEZI hana jipya na lengo lake kwanza halijulikani. Zaidi ni Nyerere tuu sasa anachopaswa kufanya ni kuwaelimisha Waislam wenzake umuhimu wa elimu na aache POROJO NA FITNA ZAKE.
Nchi hii watu hatuulizani DINI WALA KABILA ila juhudi zako ndo zitakubeba. Hivi kweli Nyerere hasingetaifisha shule za madhehebu ya dini sijui sasa tungekuwa tunaongea lugha gani?
HACHA UCHOCHEZI UTAISHIA THE HAGUE KWA OCAMPO SIJUI NAPO UTAMLAUMU MAREHEMU.

JM,

Naweza kuelewa kwa nini unasema hivyo ni kwa kuwa huujui ukweli.

Ushahidi wa dhulma na rejea za kutia nguvu tuhuma za Waislam tumeweka hapa.

Kudai "uchochezi" nk. nk. na kuitana majina mabaya na kupandisha hamaki haiwezi kusaidia mustkbali wa nchi yetu.

Jibu ni tutulize akilia zetu na tuangalie kweli nchi yetu ina tatizo la udini?

Hii ndiyo njia nzuri ya kutatua tatizo tulokuwanalo.

Tatizo hili halitoweza kuondoka lenyewe.

Tusiuogope ukweli.

Mohamed
 
M Waliweka dini pembeni kutaka utaifa leo wamesalitiwa. Hebu soma hii hapa chini:

"Kipindichama badiliko kutoka TAA kuwa TANU kilikwenda vizuri pale makao makuu.Hakukuwa na ya migongano kati ya viongozi wa makao makuu, ukitoa kikundi kidogocha Waislamu wenye msimamo mkali waliokuwa wakipanga kumg'oa Nyerere kwa kuwaalikuwa Mkristo. Hii ilikuwa ni mara ya pili kwa suala la dini kuzuka tanguNyerere achukue uongozi wa chama kwa mara ya kwanza mwaka 1953. Mkutanouliitishwa kuweka hali sawa kuhusu Ukristo ndani ya chama. TANU iliamua kuwachama kitakuwa ni cha kisekula ili kunusuru na kuihifadhi umoja wa kitaifa.Mkutano huu ulifanywa ndani ya nyumba moja katika mtaa wa Pemba na uamuzi wakeuliungwa mkono na Mufti Sheikh Hassan Bin Amir, Sheikh Nurdin Hussein tokaLindi na Sheikh Abdallah Chaurembo wa Dar es Salaam. Mkutano huu ulimfananishana 'Yuda' mwanachama yeyote yule ndani ya TANU atakayembagua Mwafrika mwenzakekwa sababu ya imani yake.

Hiini sehemu ya historia ambayo ningependa urudi kidogo kwa sababu kwenye kitabu chako hukutueleza kwa undani juu ya hili:

a. "Kikundi kidogo cha Waislamu wenye msimamo mkali" kilikuwa na kina nani - je tunawajua majina yao katika historia- ni kina nani hawa waliounda hili 'kundi dogo'?

b. Kikundi hiki kilikuwa kinataka kumng'oa Nyerere kwa sababu Mkristu kuanzia mwaka gani? - yaani hii ilikuwa ni kabla ya kina Mtevu in 1958?

c. Je haki kabisa kusema kuwa lilikuwepo kundi la Waislamu ambalo lilimkataa Nyerere toka mwanzo - alipokuja Dar kwa sababu ya Ukristo wake?

c.
 
Waliweka dini pembeni kutaka utaifa leo wamesalitiwa.
Hapa MS ndip ugomvi wetu ulipo. unapotaka kuonyesha wazee wako walikuwa wazalendo unasema waliweka dini pembeni, lakini ghafla unakumbuka msingi wa hoja yako ni dini, unaleta madai ya kusalitiwa!

Kuna hoja kwamba Mwalimu baada ya kuwa kiongozi aliwasahau wenzake aliopigania nao uhuru. Lakini wazee kama Mohamed Kisoky na Mustapha Songambele walipewa nyadhifa tena bila hata ya kuwa na ujuzi mkubwa na elimu ya kutosha. Sisi hatutaki kuishi kwenye mzimu wa Mwalimu kwani kuna ushahidi wapo watu ambao walitoa kila walichonacho kwa ajili ya Uhuru lakini baadaye wakafa fukara.

Lazima tukubaliane wapigania Uhuru ambao hapo baadaye hawakushika madaraka ya kidola hali zao hazingeweza kubadilika bila ya kufanya kazi. Hata Afrika ya Kusini wale waliopigania uhuru hali zao za kimaisha haziwezi kufanana na za Mandela hata kama walifungwa pamoja na Mandela kwenye ile jela maarufu ya Robben Island.
 
Hiini sehemu ya historia ambayo ningependa urudi kidogo kwa sababu kwenye kitabu chako hukutueleza kwa undani juu ya hili:

a. "Kikundi kidogo cha Waislamu wenye msimamo mkali" kilikuwa na kina nani - je tunawajua majina yao katika historia- ni kina nani hawa waliounda hili 'kundi dogo'?

b. Kikundi hiki kilikuwa kinataka kumng'oa Nyerere kwa sababu Mkristu kuanzia mwaka gani? - yaani hii ilikuwa ni kabla ya kina Mtevu in 1958?

c. Je haki kabisa kusema kuwa lilikuwepo kundi la Waislamu ambalo lilimkataa Nyerere toka mwanzo - alipokuja Dar kwa sababu ya Ukristo wake?

c.

Hilo kundi inafaa lienziwe na liheshimiwe kwani lilikuwa na muono. Leo wangesikilizwa tusingekuwa hapa tulipo. 83% vs 17%
 
Hilo kundi inafaa lienziwe na liheshimiwe kwani lilikuwa na muono. Leo wangesikilizwa tusingekuwa hapa tulipo. 83% vs 17%
Nadhani unamaanisha maono (Vision) maana muono ni mawazo (Opinion/view) ya mtu juu ya jambo fulani. Kama walikuwa na maono maono yao yalilenga katika nini? Nadhani mimi nakumbuka zamani watu wa pwani (Baadhi yao si wote) watoto wao wakifaulu walikuwa wanawazuia kwa hoja kwamba wanakwenda kulishwa Nguruwe.

Nadhani hata Nyerere alikuwa na maono pia, jiulize shule hizi zilikuwa zinamikiwa na Kanisa kama si yeye kuzitaifisha hali ingekuwaje? Forodhani, Jangwani Girls school, Azania ,kwa hapa Dar. Hakuna waislamu kweli waliosoma kwenye shule hizi?
 
Sheikh Mohamed,

Mara nyingi katika mnakasha huu umekuwa ukiwataka watu wasipige ''back passes''. Lakini mbona wewe unatumia ''tactic'' hiyo hiyo unayo discourage wengine wasiitumie?
 
Nadhani unamaanisha maono (Vision) maana muono ni mawazo (Opinion/view) ya mtu juu ya jambo fulani. Kama walikuwa na maono maono yao yalilenga katika nini? Nadhani mimi nakumbuka zamani watu wa pwani (Baadhi yao si wote) watoto wao wakifaulu walikuwa wanawazuia kwa hoja kwamba wanakwenda kulishwa Nguruwe.

Nadhani hata Nyerere alikuwa na maono pia, jiulize shule hizi zilikuwa zinamikiwa na Kanisa kama si yeye kuzitaifisha hali ingekuwaje? Forodhani, Jangwani Girls school, Azania ,kwa hapa Dar. Hakuna waislamu kweli waliosoma kwenye shule hizi?

Usishangae akakwambia al haji suleiman kova aliposoma azania alikuwa mkristu!
 
true true.. inabidi Mzee Said aje atuambie majina yao ili waweze kuenziwa na kuheshimiwa.

Mbona majina hayana shida, kila anaetajwa katika kitabu cha Mohamed Said inabidi aenziwe, hata wale waliowasaliti Waislaam wenzao, ukisoma vizuri, walikuja kujuta baada ya wao kuyaona.

Wala usihangaike kuhusu majina ya kuenziwa, ni yote.

Na wewe, uombe msamaha kwa kutubandikia Qur'an isivyo na kutaka kupotosha watu kama kawaida yako. Si uungwana, hizo ndio mbinu zinazokufanya hata usiwe na thamani, hata wenzako wanapokubaini kuwa hata Qur'an unaibandika visivyo wanakuwa hawana raha na wewe labda wawe wanafik.
 
Sasa naweza kufahamu kwa uwazi kabisa ni kwanini waislamu wa dsm hawampendi Nyerere na ndio sababu ya kuzunguka nchi nzima kuwahamasisha waislamu wa maeneo mengine wawaunge mkono.

Baadhi ya wazee waislamu wa dsm walimbagua Nyerere tangu mwanzo kwa sababu ya ukristo wake. Walijaribu kumng'oa madarakani TAA na baadae TANU bila mafanikio.

Sasa watoto wao na wajukuu wao wamejitosa kutaka kumchafua Nyerere kwamba aliwadhulumu waislamu kumbe wao ndio wana chuki nae. Hata pale wanapoonyeshwa kwamba chama kinachotuhumiwa kuwadhulmu wao ndio wamekikumbatia wanaanza kumtafuta mchawi Dr. Slaa na chadema.

Naweza kusema kwa uhakika kwamba hawa wanaharakati wa gerezani hawawezi kufanikiwa azma yao ya kuwatumia waislamu wenzao wa bara ili kufikia malengo yao binafsi.

Wazee wao walijaribu wakashindwa vibaya na wao wameanza lakini watashindwa vibaya sana!
 
Nadhani unamaanisha maono (Vision) maana muono ni mawazo (Opinion/view) ya mtu juu ya jambo fulani. Kama walikuwa na maono maono yao yalilenga katika nini? Nadhani mimi nakumbuka zamani watu wa pwani (Baadhi yao si wote) watoto wao wakifaulu walikuwa wanawazuia kwa hoja kwamba wanakwenda kulishwa Nguruwe.

Nadhani hata Nyerere alikuwa na maono pia, jiulize shule hizi zilikuwa zinamikiwa na Kanisa kama si yeye kuzitaifisha hali ingekuwaje? Forodhani, Jangwani Girls school, Azania ,kwa hapa Dar. Hakuna waislamu kweli waliosoma kwenye shule hizi?

Hayo yote unayoyasema ni mawazo yako na ni haki yako. Cha msingi ni kuwa mpaka sasa tunakwenda sambamba, hakuna kati yenu aliyepinga hao wazee wanaoelezewa na Mohamed Said kuwa hawakuwepo na au hawakuwa kama wanaovyolezewa. Hapo sasa.
 
Mbona majina hayana shida, kila anaetajwa katika kitabu cha Mohamed Said inabidi aenziwe, hata wale waliowasaliti Waislaam wenzao, ukisoma vizuri, walikuja kujuta baada ya wao kuyaona.

Wala usihangaike kuhusu majina ya kuenziwa, ni yote.

Na wewe, uombe msamaha kwa kutubandikia Qur'an isivyo na kutaka kupotosha watu kama kawaida yako. Si uungwana, hizo ndio mbinu zinazokufanya hata usiwe na thamani, hata wenzako wanapokubaini kuwa hata Qur'an unaibandika visivyo wanakuwa hawana raha na wewe labda wawe wanafik.

Kama unatambua thamani ya kuomba msamaha, basi kabla hujamshinikiza mwanakijiji kuomba msamaha unatakiwa uanze wewe kwa kuendekeza tabia ya kutukana tukana hapa jukwaani.
 
Back
Top Bottom