Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Hupendi matusi lakini unapenda kutukana sana! tuendelee kuvumiliana mbele ya safari.
Nguruvi3,
Kwa hakika mimi kama mwandishi wa kitabu hicho sina sababu wala haki ya kuvutana sana na wasomaji wa kitabu changu. Kitabu hiki kimependwa sana si hapa Tanzania tu bali kote kinaposomeshwa.
Nakala ya Kiswahili tunakwenda toleo la tatu.
Labda tujiulize nani anasoma kitabu hiki na kwa nini kimepata wasomaji wengi?
Wakija vijana kutoka US au Ulaya kunihoji kwa ajili ya "thesis" zao jambo la kwanza hunambia kuwa wamesoma kitabu changu na kimewasaidia sana kuelewa siasa za Tanzania na nafasi ya Waislam katika nchi hii.
Kwangu mie hicho si kitu kidogo.Waswahili tuna msemo, "Mmashomvi mmoja hafungi soko."Mohamed
Mwandishi wa kitabu anasababu ya kueleza maudhui ya kitabu chake ndivyo wanavyofanya wasomi. Kitabu hiki unachosema kinasomeshwa( si kweli) kwasababu hakipo katika mtaala wa chuo chochote Ulaya na marekani. Kama kipo maktaba basi ni sawa na kile cha mwanadada aliyeandika' Memoir' yake kuhusu maisha ya ukahaba kilivyo pia.
Kama kinatumika ubungo secondary ni sawa lakini si sawa kuseme kinasomeshwa kwingineko.
Mimi nimezichambua hoja zako zisizo na mantiki na ungelikuwa makini ungezijibu, lakini kama ilivyo kawaida yako wanafunzi bora si wale wa Morogoro University au UDSM bali ni kutoka Ulaya na Marekani wanapokuja kuandika thesis. Yaani akili yako inakutuma kuwa ukipata wanafunzi wa kizungu wewe ni bora sana. Inferiority complex ya kiwango cha kutukuka.
Hapa chini nikuonyeshe jinsi gani unavyobabaika na kujikanyaga kwa maandishi yako.
Soma hii
Halafu unatushawishi hiviMohamed Said: Kipindi chama badiliko kutoka TAA kuwa TANU kilikwenda vizuri pale makao makuu.Hakukuwa na ya migongano kati ya viongozi wa makao makuu, ukitoa kikundi kidogo cha Waislamu wenye msimamo mkali waliokuwa wakipanga kumg'oa Nyerere kwa kuwa alikuwa Mkristo. Hii ilikuwa ni mara ya pili kwa suala la dini kuzuka tanguNyerere achukue uongozi wa chama kwa mara ya kwanza mwaka 1953
Kama huko si kujichanganya sijui tuite nini.Mohamed Said Prof. Haroub Ilibidi aende kwa Ahmed Rashad Ali amuulize na Rashad akamuambia na yeye aliwekwa kizuizini kama Muislam pamoja na masheikh wengine wakati wa sakata la EAMWS akaja tolewa kifungoni na Dossa Aziz
Jibu hoja mzee Said, wageni wa marekani na Ulaya ni wakwako they have nothing to do with us. Ulikotembelea tumeshakujua huna haja ya kurudia rudia kwasababu si sehemu ya maudhui ya kitabu. Haya unaweza kuyaongea huko nyumbani kwako faragha, hapa tunajadili hoja ulizoleta na si maisha yako ya ukumbini.
Kama huna jibu au huwezi kufafanua hoja basi nitasema lile neno la makuzi yangu lislopendwa pwani.
