Nanren
JF-Expert Member
- May 11, 2009
- 3,135
- 3,392
Hapo umekosea. Nyerere hawezi kuwa Baba wa Taifa kwa Waislamu. Waislamu hatumwiti mtu "Baba" kwa "utakatifu" wake anaopewa na Kanisa.
Waislamu hatuna cheo cha "Baba" unless ni baba yako mzazi. Kwa watu wa Pwani ni TUSI kumwambia mtu amwite mtu fulani "Baba" yake wakati si " Baba" yake mzazi. Kwa hiyo rekebisha hiyo lugha.
Wewe na wenzako wachache mmeshindwa kuelewa lugha tu. Japo huwa mnajishebedua kuwa mnajua kiswahili mpaka mnataka kukihodhi. By the way, kwani Tanzania ina watu wa Pwani tu?
Baba inavyotumika kwenye "baba wa Taifa" haimaniishi "biological father". Ina maanisha "founding father". We umesoma shule gani ambapo unashindwa kuelewa vitu vidogo hivi? Hivi tukisema "'watoto wetu' waende shule" ni lazima watoto hao uwe umewazaa?
Na vipi kuhusu Mohamed Said hapa alipoandika one of the Sykes kama baba yake? Hebu soma posts zake kwenye thread hii ndio utaelewa. Au MS sio muislam? Au sio wa Pwani kwa vile ana asili ya umanyema huko kando ya L.Tanganyika?
Nafikiri wewe ndio urekebishe hiyo lugha.