Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Hapo umekosea. Nyerere hawezi kuwa Baba wa Taifa kwa Waislamu. Waislamu hatumwiti mtu "Baba" kwa "utakatifu" wake anaopewa na Kanisa.

Waislamu hatuna cheo cha "Baba" unless ni baba yako mzazi. Kwa watu wa Pwani ni TUSI kumwambia mtu amwite mtu fulani "Baba" yake wakati si " Baba" yake mzazi. Kwa hiyo rekebisha hiyo lugha.

Wewe na wenzako wachache mmeshindwa kuelewa lugha tu. Japo huwa mnajishebedua kuwa mnajua kiswahili mpaka mnataka kukihodhi. By the way, kwani Tanzania ina watu wa Pwani tu?
Baba inavyotumika kwenye "baba wa Taifa" haimaniishi "biological father". Ina maanisha "founding father". We umesoma shule gani ambapo unashindwa kuelewa vitu vidogo hivi? Hivi tukisema "'watoto wetu' waende shule" ni lazima watoto hao uwe umewazaa?
Na vipi kuhusu Mohamed Said hapa alipoandika one of the Sykes kama baba yake? Hebu soma posts zake kwenye thread hii ndio utaelewa. Au MS sio muislam? Au sio wa Pwani kwa vile ana asili ya umanyema huko kando ya L.Tanganyika?

Nafikiri wewe ndio urekebishe hiyo lugha.
 
Unayao majibu marefu ya kukariri!
Kama kuna waislam wanamuita Nyerere baba wa taifa na kuna waislam hawamuiti Nyerere baba wa taifa, ni sahihi kweli kusema waislam kwa ujumla wao hawamuiti Nyerere baba wa taifa?

Sweke34,

Upendavyo ndugu yangu hatuna sababu ya kuvutana katika hili.

Mohamed
 
Uislam sio majina ulichotaja wewe ni majina tu..

Uislam ni mfumo wa maisha wa mwanadamu! Una taratibu zake
Wewe si huwa unajiita pagan? anyway kama unaujua Uislam tusaidie.
Nakubaliana na wewe 100% kama Uislam ni mfumo wa maisha.
Wanofuata huo mfumo si ndiyo wanoitwa waislam?
Sasa akitokea mtu akasema hakuna muislam anayemuita Nyerere baba wa taifa ana maana gani?
nisaidie hapo kwanza halafu tusonge mbele!
 
Tunaweza kujiuliza vile vile ni akina nani wanakisoma kitabu cha Salman Rushidie "Satanic Verses" ambacho nacho kimeuzwa na kupendwa sana duniani kote.

Gwalihenzi,

Salman Rushdie ndiye kitabu chake kinakwenda toleo la tatu Tanzania?

Mohamed
 
Wewe na wenzako wachache mmeshindwa kuelewa lugha tu. Japo huwa mnajishebedua kuwa mnajua kiswahili mpaka mnataka kukihodhi. By the way, kwani Tanzania ina watu wa Pwani tu?
Baba inavyotumika kwenye "baba wa Taifa" haimaniishi "biological father". Ina maanisha "founding father". We umesoma shule gani ambapo unashindwa kuelewa vitu vidogo hivi? Hivi tukisema "'watoto wetu' waende shule" ni lazima watoto hao uwe umewazaa?
Na vipi kuhusu Mohamed Said hapa alipoandika one of the Sykes kama baba yake? Hebu soma posts zake kwenye thread hii ndio utaelewa. Au MS sio muislam? Au sio wa Pwani kwa vile ana asili ya umanyema huko kando ya L.Tanganyika?

Nafikiri wewe ndio urekebishe hiyo lugha.
Thanks mkuu. Hapa mpaka unafiki wao utawatoka. Hilo ndilo gogovivu haswa!
 
Nguruvi3,

Mimi nadhani hapa tulipofika panatosha sidhani kama ipo tija itakayopatikana zaidi.
Wewe msimamo wako ni kuwa hukubaliani na kitabu changu.

Mimi ilivyo na siwezi kubadili ukweli ni kuwa kitabu kipo mitaani kinasomwa toka 1998 na nakala ya Kiswahili sasa tunakwenda tolea la tatu.

Sasa katika hali kama hii mimi na wewe tunafanyaje?

Mohamed
Mzee Mohamed chakufanya ni wewe kuacha tambo na majigambo, badala yake ukubali kuwa wewe kama binadam sio mkamilifu na kwahiyo kukosea na kukosolewa ni jambo la uungwana. Kubali kuwa historia ni matukio yaliyotokea kwa kupangwa au kwa ajali, mwandishi wa historia hawezi kuyaandika yote kwani sio rahisi kuwa aliyashuhudia yote mengi alisimliwa au kusoma kama vile wewe ulivyo fanya. Na sio lazima kuwa uliyosimuliwa yote yalikuwa kweli. Kubali kuwa Nyerere alikuwa na mchango ktk historia ya Tanganyika hata kama wewe humpendi kwa mtizamo wako wa dini. Tuanze kama binadamu tunaoishi ndani ya Tanzania tukipambana kuleta maendeleo na baadae tuangalie imani zetu kujenga uhusiano na Mungu, wala tusijichukulie madaraka kuwa wasemaji wa Mungu dhidi ya watu wengine tunaotofautiana nao kwa imani zetu.
 
Mkiuu naomba unisaidie kidogo...na kwa hili hata Mohamed Saidi au muislam mwingine anisaidie.
Mnaposema 'Waislam' mna maanisha nini??
Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere ni Prof Issa Shivji. Huyu pamoja na waislam wengine kama Salim Ahmed Salimi, Dr Bashiru Ally wa UDSM, Marehemu Prof Haroub Othman + waislam wengi tu wanamuita Nyerere Baba wa Taifa. Hivi hawa waislam wanaomuita Nyerere baba wa taifa siyo waislam??Naomba jibu fupi tu!

Mkuu Sweke34
Hawa watu huwa wana majibu tofauti tofauti hata kama swali ni lile lile. Inategemeana tu muda huo wanatetea hoja gani. Ndio maana hapa chini ritz kakupa jibu hili...

Uislam sio majina ulichotaja wewe ni majina tu..

Uislam ni mfumo wa maisha wa mwanadamu! Una taratibu zake

Hapo ni kuwa waislam wenye mtazamo tofauti na MS et al. pamoja na walioko BAKWATA si waislam for the sake of this argument.

Lakini wanapolalamikia kodi za waislam kwenda kwenye MOU, basi mlipa kodi yeyote mwenye jina la kiislam, anakuwa ni muislam. Na pia wanapotetea kuwa waislam ni wengi Tanzania, na ndio waliopigania uhuru, na wanaonewa, basi wote wenye majina ya Kiislam wanakuwa waislam. Unafiki mtupu!!!
 
Unajua inaonekana wewe unashindwa kuelewa maana ya historia. Hivi unajua historia inavyoandikwa? Hivi unajua ktk kila pande inaandika historia yake?

Pili, unajua maana ya research ktk jambo au mambo? Hapa nyie nyote mnabisha maneno ya MS, lakini hamjawahi kutoa paper/ book yoyote yenye level kama yake. Mie nakushauri, kama unaipenda hii taaluma ya kuwa critics, fanya research, fanya interview na wale waliomo ktk historia ili upate kujua ukweli zaidi.

Lakini kuandika hapa, bila ya hiyo research ni kuleta UBISHI wa Simba na Yanga.
Haya ni maneno ya mtu aliyekata tamaa na sio msomi. Hatuhitaji historia "subjective" kama ya huyu mzee wako. History should be objective for the sake of truth. Tuseme katika historia jambo fulani lilitokea na kweli liwe lilitokea, halafu tupate kulitafakali na kulijadili kwanini lilitokea namna lilivyotokea.
Sasa wewe unakuja "arogantly" kuwashambulia wachangiaji ati hawajui historia kwa kuwa hawajaandika "paper". Huo sio usomi ndugu yangu, usomi ni kuvumilia kukosolewa kwa chochote ulichoweka hadharani. Kama hampendi kukosolewa wewe na huyo mzee wako kwanini mlibandika hoja yenu hapa? Bora mngepeleka kwenye mihadhara yenu mkaimba "takdiri"!
 
Wewe si huwa unajiita pagan? anyway kama unaujua Uislam tusaidie.
Nakubaliana na wewe 100% kama Uislam ni mfumo wa maisha.
Wanofuata huo mfumo si ndiyo wanoitwa waislam?
Sasa akitokea mtu akasema hakuna muislam anayemuita Nyerere baba wa taifa ana maana gani?
nisaidie hapo kwanza halafu tusonge mbele!
Kaka sweke34, ritz huwa hana majibu ya kisomi, yeye anasubiri mzee Mohamed Said aseme neno yeye hulidaka na nakulipamba.
 
Gwalihenzi,

Salman Rushdie ndiye kitabu chake kinakwenda toleo la tatu Tanzania?

Mohamed
Kwani kitabu chako wewe kinasomwa Tanzania tu? Basi Fuatilia utagundua Kuwa Satan Verses pamoja na kwamba kilipigwa marufuku hapaTanzania na muislam mwenzenu alhaj Mwinyi sasa hivi kimepanda chati ile mbaya. Kinapatikana electronicaly.
 
Huu ujuaji utasababisha mtoane macho! Wewe wasema...

Hapo umekosea. Nyerere hawezi kuwa Baba wa Taifa kwa Waislamu. Waislamu hatumwiti mtu "Baba" kwa "utakatifu" wake anaopewa na Kanisa.

Waislamu hatuna cheo cha "Baba" unless ni baba yako mzazi. Kwa watu wa Pwani ni TUSI kumwambia mtu amwite mtu fulani "Baba" yake wakati si " Baba" yake mzazi. Kwa hiyo rekebisha hiyo lugha.

MS, anasema...

Mohamed Said said:
WC,

Wewe si mzungumzaji wangu katika historia ya marehemu Bwana Abdu na Nyerere. Mimi Abdu Sykes ni baba yangu.
Tosheka na hilo tu.

Sina haja ya kubishana na wewe kuhusu historia ya mtu ambae mimi namfahamu vizuri lau kama nilikuwa mtoto mdogo.

Mohamed

Kama Abdu Sykes ni "baba Mzazi" wa Mohamed Said basi kweli hilo "Tusi la pwani" lirekebishwe.
 
Kwani kitabu chako wewe kinasomwa Tanzania tu? Basi Fuatilia utagundua Kuwa Satan Verses pamoja na kwamba kilipigwa marufuku hapaTanzania na muislam mwenzenu alhaj Mwinyi sasa hivi kimepanda chati ile mbaya. Kinapatikana electronicaly.

Gwalihenzi,

Tusishindane kwa jambo ambalo kwa hakika halina manufaa nasi.
Tutosheke na hapa tulipofika.

Mohamed
 
Mzee Mohamed chakufanya ni wewe kuacha tambo na majigambo, badala yake ukubali kuwa wewe kama binadam sio mkamilifu na kwahiyo kukosea na kukosolewa ni jambo la uungwana. Kubali kuwa historia ni matukio yaliyotokea kwa kupangwa au kwa ajali, mwandishi wa historia hawezi kuyaandika yote kwani sio rahisi kuwa aliyashuhudia yote mengi alisimliwa au kusoma kama vile wewe ulivyo fanya. Na sio lazima kuwa uliyosimuliwa yote yalikuwa kweli. Kubali kuwa Nyerere alikuwa na mchango ktk historia ya Tanganyika hata kama wewe humpendi kwa mtizamo wako wa dini. Tuanze kama binadamu tunaoishi ndani ya Tanzania tukipambana kuleta maendeleo na baadae tuangalie imani zetu kujenga uhusiano na Mungu, wala tusijichukulie madaraka kuwa wasemaji wa Mungu dhidi ya watu wengine tunaotofautiana nao kwa imani zetu.

Gwalihenzi,

Mimi sitambi ninachokuambia ndicho hicho nilichotenda.

Ama kuhusu ukamilifu aliyekamili ni Allah peke yake.

Nishasema mara nyingi kuwa kazi yoyote ya mkono wa binadamu haikosi makosa.
Lakini kuhusu historia ya Waislam wa Tanganyika ndiyo hiyo niloandika.

Mohamed
 
Uwe unasoma katikati ya mistari na kuelewa.....ndiyo maana watu wanakuuliza mtu akiandika kitabu cha ngono ,uhalifu , mfumo kristo , satanic verses etc na vikachapishwa matoleo mengi ina maana gani?

Sweke34,

Sasa tunafanya nini katika hali hii ambayo kitabu kipo na kinasomwa?

Hivi tuandikapo tunaingia toleo la tatu.

Hiki kitabu kinaweza kikaondoka hivi hivi?

Ndiyo naposema hapa tulipofika si panatosha?
Sasa tunabishana nini?

Asiyekitaka ni bahati mbaya kwake.

Mohamed

Mohamed
 
Nguruvi3,Kumbuka kusoma kitu kisha kukaa kimya nao pia ni adab za msomi.
Si kila kitu unaweza kuchangia kwani hizi tafiti huwezi kuzijibu kwa vijistari viwili vitatu vya JF. Ni vizuri nawe uandike makala yako tuone umahiri wako.tafaku
Mnaoweza kukaa kimya ni ninyi ambao mumeridhika hata kama udanganyifu ni wa wazi kabisa. Hakuna ninachomuuliza Mohamed kutoka nje ya mada zake. Suala la Christian lecturers kalizungumzia mwenye nami nilichofanya ni kumelekeza uandishi usio na ushabiki ambao unamtia matatani sana na kushindwa kutetea kazi zake
Baadhi yenu mnaona dhalili mtafiti anapojibiwa hoja kirahisi na anaposhindwa kujibu hoja kirahisi. Mimi sina adabu za kisomi za kudanganywa. Hivi Mohamed ataongelea mabucha ya nguruwe aseme yana uhusiano na Kigoma nikae kimya kwasababu ni adabu za madrasa. Never! Nimeyaona kwa macho yangu mubashir.

Ninachoshangaa nyinyi manosema kuna tafiti, tunawaonyesha kuwa kama kuna tafiti basi ipo overrided na hisia na ushabiki ndio maana the whole thing inapoteza maana na inakuwa vulnerable to attack.

Nikupe mfano, hebu nijibu suala hili. '........Diamond jubilee hawakuwepo waislam ila BAKWATA. Wakati wa kusalimiana serikali iliumbuka kwasababu waislam hawakutoa mkono kusalimiana na wakristo. Yaani watu wasiokuwepo ukumbini walitoaje mkono wa kusalimiana na wakristo? Hapa utaona ni hadithi iliyopikwa na bila ya uhariri ikaji contradict.
Sasa nyie mnataka tukae kimya tumeze tu kwasababu ni adabu za usomi. Usomi ni uelewa si kumeza kila kitu kwasababu kinasemwa na mtu aliyekwenda ulaya na marekani na anayepokea wazungu.

Na mwisho, Mohamed anapenda heshima na ni lazima awe tayari kuheshimu wengine kwa kauli na mawazo yao, matusi yake ya kipwani hayamsaidii kujenga hoja na anatakiwa ajibu hoja. Na ni lazima aelewe kuwa hapa si kule anapoweka watu chini na kusema anachotaka, No no! tutamhoji. Kama atatoa majibu ya kutuita wamashomvi hewala, sisi tutachambua makala zake na ikiwezwekana kuzikosoa kama kama kichwa cha habari cha Mada ya Mag3.
 
Huu ujuaji utasababisha mtoane macho! Wewe wasema...

MS, anasema...

Kama Abdu Sykes ni "baba Mzazi" wa Mohamed Said basi kweli hilo "Tusi la pwani" lirekebishwe.

Hakyanani, nyie watu nyie nimewavulia kofia.
Huu mtanange bado unaendelea? Ngoja niendelee kujisomea tu maana naona makamanda mnaonyesha kwamba mna pumzi ndefu!
 
Huu ujuaji utasababisha mtoane macho! Wewe wasema...

MS, anasema...

Kama Abdu Sykes ni "baba Mzazi" wa Mohamed Said basi kweli hilo "Tusi la pwani" lirekebishwe.

Mgalanjuka,

Kwa adabu za kikwetu mtu yeyote mwenye umri sawa na baba yako unamwita "baba" hali kadhalika mwanamke yeyote umri wa mama yako unamwita "mama."

Hakuna jina jingine nje ya hapo.

Na inapokuwa kati ya hao ni rafiki ya baba au mama yako ile heshima ya ubaba na mama huwa juu zaidi.
Huwa hawana jina lingine nje ya hayo.

Utamwita "baba" au "mama."
Hizi ndizo mila, desturi na heshima za watu wa pwani.

Mohamed
 
Wewe na wenzako wachache mmeshindwa kuelewa lugha tu. Japo huwa mnajishebedua kuwa mnajua kiswahili mpaka mnataka kukihodhi. By the way, kwani Tanzania ina watu wa Pwani tu?
Baba inavyotumika kwenye "baba wa Taifa" haimaniishi "biological father". Ina maanisha "founding father". We umesoma shule gani ambapo unashindwa kuelewa vitu vidogo hivi? Hivi tukisema "'watoto wetu' waende shule" ni lazima watoto hao uwe umewazaa?
Na vipi kuhusu Mohamed Said hapa alipoandika one of the Sykes kama baba yake? Hebu soma posts zake kwenye thread hii ndio utaelewa. Au MS sio muislam? Au sio wa Pwani kwa vile ana asili ya umanyema huko kando ya L.Tanganyika?

Nafikiri wewe ndio urekebishe hiyo lugha.

Unashindwa hata kuelewa maana ya hilo neno. Unajua kwanini inaitwa "Founding Father" unajua kwanini inatumika neno "Father" Hiyo idea ya neno "Father" imetokana na Christians Principles.

The Founding Fathers of The United States were Christians who formed a government based on godly principles.

John Adams
The second President (or tenth if you consider John Hanson the first) wrote to Thomas Jefferson on June 28, 1813:
  • The general principles on which the fathers achieved independence were. . . . the general principles of Christianity. . . . I will avow that I then believed, and now believe, that those general principles of Christianity are as eternal and immutable as the existence and attributes of God; and that those principles of liberty are as unalterable as human nature.
 
Mgalanjuka,

Kwa adabu za kikwetu mtu yeyote mwenye umri sawa na baba yako unamwita "baba" hali kadhalika mwanamke yeyote umri wa mama yako unamwita "mama."

Hakuna jina jingine nje ya hapo.

Na inapokuwa kati ya hao ni rafiki ya baba au mama yako ile heshima ya ubaba na mama huwa juu zaidi.
Huwa hawana jina lingine nje ya hayo.

Utamwita "baba" au "mama."
Hizi ndizo mila, desturi na heshima za watu wa pwani.

Mohamed

Shukrani. Huyo Mr. Right kama ni muungwana inatakiwa akuombe msamaha.
 
Back
Top Bottom