Ahali yangu Mohamed said,
Hakika hizo ni rasharasha tu miongoni mwa makubwa uliyo yaona na kupambana nayo. Mengi nionayo hapa ni mas'khara na mzaha wa wachangiaji ukiangalia kwa undani sana na kusoma utaona wale walioamua kukusoma si kwa nia ya kukuelewa umekusudia nini bali waliokusoma kwa nia ya kukupinga. Hivyo hawawezi kukuelewa.
Lakin ukumbuke wengine tumeona na kupata fahari kubwa kuweza kufanya mnakasha na wewe moja kwa moja mara baada ya kusoma vitabu vyako vingi. Na tunashukuru sana na wewe bila ajizi wala choyo yoyote umekubali kutupa kila kitu unachokijua iwe kutoka kwenye vitabu vyako au nje ya vitabu vyako pasi na kututoza pesa yoyote. Kwani wengine tunajua fika papers zako na hata vitabu vinauzwa. Tunakushukuru sana kwa Hilo na Allah atakuzidishia zaidi na zaidi na kukupa Pepo ya Firdaus.
Lakin pia tupo wengine ambao tunatumia mnakasha huu kujua mengi sana na kuchota busara zako na kila pale inapojilia mush,kira basi tunakuuliza kwa nia ya kuelewa zaidi.
Hivyo napingana na wewe unaposema mnakasha umekwisha. Tunaomba na kuzidi kukuomba utupe mengi na mengi kwani tunakiu kubwa ya kujua mengi. Tunakuomba darsa iendelee tupo tunaofuatilia kwa kina sana kwa nia ya kujua na kufahamu zaidi.
Tunakuomba ubadili maneno yako kwa nia ya kukata kiu yetu tunaofuatilia darsa zako.
maa salaam