Yoda,
Usiandike lugha za kifedhuli, ''bargashia,'' nk. haipendezi.
Hatari yake ni kuwa tutawakaribisha watu hodari kwa matusi mfano wa hayo na tutauharibu mjadala.
Sijui hiyo 99% ya Waislam kuwa walipigania uhuru wewe umeitoa wapi.
Nilichoeleza mimi katika kitabu cha Abdul Sykes na kwa hakika hili liko wazi ni kuwa Waislam walikuwa na mchango mkubwa katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Unaweza kuanza kuisoma historia hii kuanzia mwaka wa 1929 ilipoasisiwa Africa Association.
Na sababu zimeelezwa kwa nini historia imekuwa hivi.
Nadhani unajua kuwa Southern Province Kanisa lilikuwa linawatisha waumini wake wasijiunge, na TANU kwa kudai kuwa TANU ni chama cha Waislam wanataka kuleta Maji Maji nyingine safari hii dhidi ya Waingereza.
Haya yamo katika historia ya safari ya kwanza ya Nyerere Lindi alikofika hadi Mikindani, Masasi na Nachingwea.
Ujumbe makhsusi ulitumwa New Street TANU HQ kuja kueleza uongozi wa TANU matatizo yaliyokuwa yanaikabili TANU Southern Province.
Unaweza kuyasoma haya katika kitabu cha Abdul Sykes (1998) na halikadhalika katika kitabu changu, ''Watu Mashuhuru Katika Uhuru wa Tanganyika 1,'' (2019).
Katika kitabu hiki utawasoma Ali Ibrahim Mnjawale na Salum Mpunga kutoka Lindi waliyokuja Dar es Salaam kuhudhuria mkutano wa kwanza wa TANU 1955 wakiwa na ujumbe kuhusu hii bugdha iliyokuwa inakabili TANU.
TANU ikawapeleka Nyerere, Ali Mwinyi Tambwe na Rajab Diwani Southern Province kwenda kupambana na propaganda hii mbaya.
Kama mtu anaona kuwa mimi naandika propaganda hii ni bahati mbaya kwake lakini ukweli utabakia pale pale kuwa hawa wazalendo walikuwapo na halikadhalika matatizo haya yalikuwapo pia na hawa wazalendo walikuwapo.
View attachment 2168689