Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Nini kinawachoma?
Wangependa kama historia hii nisingeiandika na tukawa na historia ambayo haina ukweli?

Hiki ndicho kiichokusudiwa mwanzo walipofuta historia ya kweli ya TANU na kupachika nyingine?
Mzee Mohamed kwa namna unavyoongelea mchango wa Mwl kwenye harakati za Uhuru unamdunisha mno licha ya kwamba aliongoza mapambano ya Uhuru kwa akili nyingi na uweledi mkubwa sana hata kuwa mwenyekiti wa TAA, Rais wa kwanza wa Tanu, waziri mkuu wa kwanza wa Tanganyika huru, Rais wa kwanza wa Tanganyika huru na baadae Tanzania.

Ila umemwelezea kama mtu aliyekuja mjini akapokelewa na 'wajanja wa mji' waliompa maisha na yeye kusafiria nyota yao.

Huku pia ukimlaumu kwa kuhujumu umma wa kiislamu kwa makusudi, hili linaudhi wachangiaji wengi.
 
Mohamed Said anataka tuiamini zaidi Historia isiyoandikiwa, hadithi alizosimuliwa zaidi na wazee wake, ni vigumu sana kuiamini Historia ya aina hiyo hata kama kuna ukweli fulani kwenye maelezo yake ya Historia na kasoro nyingi kwenye Historia yenye mkono wa TANU.
Anatulazimisha tuamini kuwa uhuru wa Tanganyika uliletwa na "wazee" wake na kwa miwani ya kiislamu.
Anafikiri kwingine wazee wetu walikuwa wamelala.
Wazee wa wazee wetu, kina Mkwawa, Melele, Mputa Mbano Songea, Meli na Sina anafikiri hawakuwepo.
 
Mzee Mohamed kwa namna unavyoongelea mchango wa Mwl kwenye harakati za Uhuru unamdunisha mno licha ya kwamba aliongoza mapambano ya Uhuru kwa akili nyingi na uweledi mkubwa sana hata kuwa mwenyekiti wa TAA, Rais wa kwanza wa Tanu, waziri mkuu wa kwanza wa Tanganyika huru, Rais wa kwanza wa Tanganyika huru na baadae Tanzania.

Ila umemwelezea kama mtu aliyekuja mjini akapokelewa na 'wajanja wa mji' waliompa maisha na yeye kusafiria nyota yao.

Huku pia ukimlaumu kwa kuhujumu umma wa kiislamu kwa makusudi, hili linaudhi wachangiaji wengi.
Proved,
Hushangai kuwa historia ya wazee wangu ilifutwa?
Unasemaje kuhusu hili?
 
Mzee Mohamed kila pande za hii nchi zilishiriki kwa namna fulani kwenye harakati za Uhuru ndio maana kuna wadau wameelezea mchango wa vyama vilivyokuwepo huko Kilimanjaro, Mwanza n.k

Hivyo michango mingi sana ya makundi mengi haijaandikwa (ikiwemo mchango wa wazee wako).... nadhani hatukuwa making kuandika historia ya nchi yetu, ila kama 'ilifutwa' kwa makusudi siwezi kuthibitisha hili.
 
Anatulazimisha tuamini kuwa uhuru wa Tanganyika uliletwa na "wazee" wake na kwa miwani ya kiislamu.
Anafikiri kwingine wazee wetu walikuwa wamelala.
Wazee wa wazee wetu, kina Mkwawa, Melele, Mputa Mbano Songea, Meli na Sina anafikiri hawakuwepo.
Maso...
Mimi siwezi kulazimisha chochote katika uandishi wa historia ya uhuru wa Tanganyika.
Huu ni uwanja huru kila mtu ana haki ya kuingia na kuandika.

Kwengine wazee walikuwa katika harakati za TANU na kote nimefika katika kutafiti na nimeandika historia zao.

Nimemwandika Ally Migeyo (Kanda ya Ziwa), Yusuf Olotu, Mama bint Mwalimu, Halima Selengia, Lucy Lameck na Amina Kinabo (Kilimanjaro), Msham Awadh (Mikindani), Salum Mpunga, Yusuf Chembera, Suleiman Masudi Mnonji, Shariffa bint Mzee, Sheikh Yusuf Badi (Lindi), Sheikh Abdallah Rashid Sembe, Mohamed Kajembe, Hamisi Kheri, Peter Mhando (Tanga) hawa ni wachache.

Orodha ni ndefu sana.
Hawa wote historia zao zilikuwa hazijulikani.

Mimi si mtu wa wewe leo kukebehi Waislam katika historia ya TANU na kudai uhuru.
Hivi ndivyo ilivyokuwa historia hiyo.

Kama wewe hupendi kwa nini ilikuwa hivyo hilo ni jambo lingine na haiwezekani kubadili historia.

Wote hawa wamo katika kitabu cha Abdul Sykes.

1648579485638.png
 
Mzee Mohamed kila pande za hii nchi zilishiriki kwa namna fulani kwenye harakati za Uhuru ndio maana kuna wadau wameelezea mchango wa vyama vilivyokuwepo huko Kilimanjaro, Mwanza n.k

Hivyo michango mingi sana ya makundi mengi haijaandikwa (ikiwemo mchango wa wazee wako).... nadhani hatukuwa making kuandika historia ya nchi yetu, ila kama 'ilifutwa' kwa makusudi siwezi kuthibitisha hili.
Proved,
Hakika baada ya TANU kuasisiwa Dar es Salaam majimboni wananchi wakawa sasa wanasajili matawi na nimefika katika hayo matawi wakati wa utafiti na wale walikuwa hai nimewahoji na historia zao nimeandika.

Jopo la Chuo Cha CCM Kivukoni lililokuwa linaandika historia ya TANU walipelekewa ''notes,'' za Abdul Sykes na mwanajopo mwenzao Hassan Upeka.

Kiongozi wa jopo Dr. Mayanja Kiwanuka alikataa kuzipokea kwa kudai kuwa historia ya TANU haina uhusiano wowote na Abdul Sykes.

Nilimuuliza Hassan Upeka ambae alikuwa Afisa wa Usalama kama naweza kumnukuu kwa jina lake katika kitabu cha Abdul Sykes na aliniruhusu.

Dr. Kiwanuka yu hai unaweza kupata uthibitisho kutoka kwake.
 
Haiwezekani kwamba asilimia 99 ya watu "walioutafuta" uhuru wa nchi hii walikuwa watu wa kanzu na baraghashia.
Historia ya aina hiyo haitakubalika popote, itakuwa ni uongo mkubwa propoganda tupu.
Maso...
Mimi siwezi kulazimisha chochote katika uandishi wa historia ya uhuru wa Tanganyika.
Huu ni uwanja huru kila mtu ana haki ya kuingia na kuandika.

Kwengine wazee walikuwa katika harakati za TANU na kote nimefika katika kutafiti na nimeandika historia zao.

Nimemwandika Ally Migeyo (Kanda ya Ziwa), Yusuf Olotu, Mama bint Mwalimu, Halima Selengia, Lucy Lameck na Amina Kinabo (Kilimanjaro), Msham Awadh (Mikindani), Salum Mpunga, Yusuf Chembera, Suleiman Masudi Mnonji, Shariffa bint Mzee, Sheikh Yusuf Badi (Lindi), Sheikh Abdallah Rashid Sembe, Mohamed Kajembe, Hamisi Kheri, Peter Mhando (Tanga) hawa ni wachache.

Orodha ni ndefu sana.
Hawa wote historia zao zilikuwa hazijulikani.

Mimi si mtu wa wewe leo kukebehi Waislam katika historia ya TANU na kudai uhuru.
Hivi ndivyo ilivyokuwa historia hiyo.

Kama wewe hupendi kwa nini ilikuwa hivyo hilo ni jambo lingine na haiwezekani kubadili historia.

Wote hawa wamo katika kitabu cha Abdul Sykes.

View attachment 2168627
 
Haiwezekani kwamba asilimia 99 ya watu "walioutafuta" uhuru wa nchi hii walikuwa watu wa kanzu na baraghashia.
Historia ya aina hiyo haitakubalika popote, itakuwa ni uongo mkubwa propoganda tupu.
Yoda,
Usiandike lugha za kifedhuli, ''bargashia,'' nk. haipendezi.

Hatari yake ni kuwa tutawakaribisha watu hodari kwa matusi mfano wa hayo na tutauharibu mjadala.

Sijui hiyo 99% ya Waislam kuwa walipigania uhuru wewe umeitoa wapi.

Nilichoeleza mimi katika kitabu cha Abdul Sykes na kwa hakika hili liko wazi ni kuwa Waislam walikuwa na mchango mkubwa katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Unaweza kuanza kuisoma historia hii kuanzia mwaka wa 1929 ilipoasisiwa Africa Association.

Na sababu zimeelezwa kwa nini historia imekuwa hivi.

Nadhani unajua kuwa Southern Province Kanisa lilikuwa linawatisha waumini wake wasijiunge, na TANU kwa kudai kuwa TANU ni chama cha Waislam wanataka kuleta Maji Maji nyingine safari hii dhidi ya Waingereza.

Haya yamo katika historia ya safari ya kwanza ya Nyerere Lindi alikofika hadi Mikindani, Masasi na Nachingwea.

Ujumbe makhsusi ulitumwa New Street TANU HQ kuja kueleza uongozi wa TANU matatizo yaliyokuwa yanaikabili TANU Southern Province.

Unaweza kuyasoma haya katika kitabu cha Abdul Sykes (1998) na halikadhalika katika kitabu changu, ''Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika 1,'' (2019).

Katika kitabu hiki utawasoma Ali Ibrahim Mnjawale na Salum Mpunga kutoka Lindi waliyokuja Dar es Salaam kuhudhuria mkutano wa kwanza wa TANU 1955 wakiwa na ujumbe kuhusu hii bugdha iliyokuwa inakabili TANU.

TANU ikawapeleka Nyerere, Ali Mwinyi Tambwe na Rajab Diwani Southern Province kwenda kupambana na propaganda hii mbaya.

Kama mtu anaona kuwa mimi naandika propaganda hii ni bahati mbaya kwake lakini ukweli utabakia pale pale kuwa hawa wazalendo walikuwapo na halikadhalika matatizo haya yalikuwapo.

1648586079689.png
 
Zamani ulikuwa na akili nyingi sana.
Hili ni swali zuri sana; kwa kweli siyo changamoto kama unavyoiona na ni changamoto ambayo naamini itakuja kujibiwa na Waislamu wengine. Toka mwanzo wa historia yetu yamekuwepo makundi mbalimbali ya kisiasa. Hata kwenye suala la dini ni hivyo hivyo. Kitu ambacho wengi tumefanikiwa katika mjadala huu ni kuonesha kuwa:

a. Ulichoandika katika kitabu hiki siyo historia bali ni simulizi tu ambalo halina ushahidi wa historia zaidi ya hisia.
b. Unatumia dini kuangalia historia na kuweka tafsiri ya kidini kwa kutumia historia na kudai "wazee" wako si kwa sababu ni wazee wa historia yetu bali ni kwa sababu ya kuwa unakubaliana nao kuwa ni dini moja.
c. Wapo watu ambao nina uhakika nao wazee wao walikuwa ni Waislamu na walikuwa upande mwingine kabisa wa kina Takadir na kina Sheikh Amir.

Hivyo watakuja Watanzania ambao wataiokoa historia yetu kutoka mikononi mwa mtazamo wa kidini na kuiweka mahala pake hasa. Wale ambao watawaunganisha wazee wetu katika umoja wao na uzalendo wao siyo kwa dini zao bali kwa Utanganyika na Utanzania wao. Litakapotokea hilo kitabu chako kitabakia kama simulizi la majaribio tu na mapungufu yake yatawekwa bayana. Ninatumaini hili litatokea mapema zaidi.
 
Jambo la kwanza hii lugha ya "kupigania" uhuru sio sahihi sana kwa mazingira ya jinsi Tanganyika ilivyoupata uhuru wake. Sisi uhuru wetu ulikuwa ni wa mazungumzo zaidi na wakoloni wetu jinsi ambavyo tungeendesha nchi yetu baada ya uhuru, lugha ya kufaa zaidi ni kutafuta uhuru.

Pili hakuna mtu anayeijua historia ya nchi hii atapinga kwamba Waislamu walikuwa na mchango katika kuutafuta uhuru wa nchi hii, Waislamu walikuwa sehemu ya nchi hii wakati uhuru unatafutwa, wameendelea kuwa sehemu ya nchi na wataendelea kuwa sehemu ya nchi hii kwa muda mrefu vivyo hivyo Wakristo.

Jambo linalopingwa na ambalo halitakubalika ni kutaka kuiwasilisha na kuitafsiri historia ya nchi hii kwa mrengo wa wazee wako tu kama madereva waliotufikisha kwenye uhuru na wengine wote waliobaki walikuwa abiria ambao walikuwa hawajui hata wanaelekea wapi. Huu ni upotoshaji mkubwa, kwa akili za kawaida tu kujadiliana na wakoloni au mabeberu wa kizungu mezani ilihitaji watu wenye elimu nzuri na wewe unafahamu vizuri kundi gani la jamii lilikuwa na elimu nzuri wakati huo.

Jambo lingine huonyeishi dhahiri sababu gani hasa zilimfanya Mwl aliwafute "wazee wako" katika historia, kama ni kweli Nyerere aliwafuta wazee wako ambao wengi kama sio wote ni wa mrego mmoja basi aliwafutwa kama sehemu ya "power struggle" ndani ya chama chake na pia ni sawa tu na ambavyo aliwafuta maswahiba wake wengine nje ya chama wakiwemo wasomi, waandishi, vyama vya upinzani, matajiri mabepari n.k Siuoni msingi wa malalamiko yako kuhusu hawa "wazee wako" tu.
Yoda,
Usiandike lugha za kifedhuli, ''bargashia,'' nk. haipendezi.

Hatari yake ni kuwa tutawakaribisha watu hodari kwa matusi mfano wa hayo na tutauharibu mjadala.

Sijui hiyo 99% ya Waislam kuwa walipigania uhuru wewe umeitoa wapi.

Nilichoeleza mimi katika kitabu cha Abdul Sykes na kwa hakika hili liko wazi ni kuwa Waislam walikuwa na mchango mkubwa katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Unaweza kuanza kuisoma historia hii kuanzia mwaka wa 1929 ilipoasisiwa Africa Association.

Na sababu zimeelezwa kwa nini historia imekuwa hivi.

Nadhani unajua kuwa Southern Province Kanisa lilikuwa linawatisha waumini wake wasijiunge, na TANU kwa kudai kuwa TANU ni chama cha Waislam wanataka kuleta Maji Maji nyingine safari hii dhidi ya Waingereza.

Haya yamo katika historia ya safari ya kwanza ya Nyerere Lindi alikofika hadi Mikindani, Masasi na Nachingwea.

Ujumbe makhsusi ulitumwa New Street TANU HQ kuja kueleza uongozi wa TANU matatizo yaliyokuwa yanaikabili TANU Southern Province.

Unaweza kuyasoma haya katika kitabu cha Abdul Sykes (1998) na halikadhalika katika kitabu changu, ''Watu Mashuhuru Katika Uhuru wa Tanganyika 1,'' (2019).

Katika kitabu hiki utawasoma Ali Ibrahim Mnjawale na Salum Mpunga kutoka Lindi waliyokuja Dar es Salaam kuhudhuria mkutano wa kwanza wa TANU 1955 wakiwa na ujumbe kuhusu hii bugdha iliyokuwa inakabili TANU.

TANU ikawapeleka Nyerere, Ali Mwinyi Tambwe na Rajab Diwani Southern Province kwenda kupambana na propaganda hii mbaya.

Kama mtu anaona kuwa mimi naandika propaganda hii ni bahati mbaya kwake lakini ukweli utabakia pale pale kuwa hawa wazalendo walikuwapo na halikadhalika matatizo haya yalikuwapo pia na hawa wazalendo walikuwapo.

View attachment 2168689
 
Jambo la kwanza hii lugha ya "kupigania" uhuru sio sahihi sana kwa mazingira ya jinsi Tanganyika ilivyoupata uhuru wake. Sisi uhuru wetu ulikuwa ni wa mazungumzo zaidi na wakoloni wetu jinsi ambavyo tungeendesha nchi yetu baada ya uhuru, lugha ya kufaa zaidi ni kutafuta uhuru.

Pili hakuna mtu anayeijua historia ya nchi hii atapinga kwamba Waislamu walikuwa na mchango katika kuutafuta uhuru wa nchi hii, Waislamu walikuwa sehemu ya nchi hii wakati uhuru unatafutwa, wameendelea kuwa sehemu ya nchi na wataendelea kuwa sehemu ya nchi hii kwa muda mrefu vivyo hivyo Wakristo.

Jambo linalopingwa na ambalo halitakubalika ni kutaka kuiwasilisha na kuitafsiri historia ya nchi hii kwa mrengo wa wazee wako tu kama madereva waliotufikisha kwenye uhuru na wengine wote waliobaki walikuwa abiria ambao walikuwa hawajui hata wanaelekea wapi. Huu ni upotoshaji mkubwa, kwa akili za kawaida tu kujadiliana na wakoloni au mabeberu wa kizungu mezani ilihitaji watu wenye elimu nzuri na wewe unafahamu vizuri kundi gani la jamii lilikuwa na elimu nzuri wakati huo.

Jambo lingine huonyeishi dhahiri sababu gani hasa zilimfanya Mwl aliwafute "wazee wako" katika historia, kama ni kweli Nyerere aliwafuta wazee wako ambao wengi kama sio wote ni wa mrego mmoja basi aliwafutwa kama sehemu ya "power struggle" ndani ya chama chake na pia ni sawa tu na ambavyo aliwafuta maswahiba wake wengine nje ya chama wakiwemo wasomi, waandishi, vyama vya upinzani, matajiri mabepari n.k Siuoni msingi wa malalamiko yako kuhusu hawa "wazee wako" tu.
Yoda,
Unakumbuka nilikueleza kuwa soma kitabu cha Abdul Sykes?

Hukusoma umefanya haraka ya kurejea hapa kujadili ikiwa hujui yaliyotokea baada ya uhuru.

Hili la "kupigania," halina sababu ya kukuhangaisha ni "semantics" tu.
Muhimu kwako ni kusoma kwanza.

Utakutana na "Nyaraka za Waikela," alizificha kwa miaka takriban 20 hadi zikanifikia.

Kwa nini alizificha?
Utasoma kwenye kitabu.

Nikasafiri hadi Tabora kwenda kufanya mahojiano na yeye.

Waikela anasema kama EAMWS isingekuwa na mipango ya elimu na kujenga Chuo Kikuu ingedumu hadi hii leo.

Utasoma kuhusu Muslim Congress ya 1962 na 1963.

Ujenzi wa shule za Kiislam nchi nzima na Chuo Kikuu ndicho kilichosababisha EAMWS ivunjwe mwaka wa 1968 na Mufti Sheikh Hassan bin Ameir akamatwe na kufukuzwa Tanzania Bara.

Kilichofuatia ni kuundwa kwa BAKWATA.
Ikiwa hutasoma historia hii utabakia kwenye ujinga kuwa unajadili jambo usilolijua.

1648610143959.png
 
Nimemwandika Ally Migeyo (Kanda ya Ziwa), Yusuf Olotu, Mama bint Mwalimu, Halima Selengia, Lucy Lameck na Amina Kinabo (Kilimanjaro), Msham Awadh (Mikindani), Salum Mpunga, Yusuf Chembera, Suleiman Masudi Mnonji, Shariffa bint Mzee, Sheikh Yusuf Badi (Lindi), Sheikh Abdallah Rashid Sembe, Mohamed Kajembe, Hamisi Kheri, Peter Mhando (Tanga) hawa ni wachache.

View attachment 2168627
Kwa orodha kama hii ya Waislamu watupu unaowajua wewe, kila kukicha unataka kutuaminisha ni Waislamu tu ndiyo walipigania Uhuru wa nchi hii. Hii imekuwa dhana yako siku zote. Ukweli ni kwamba walikuwapo watu wa kila imani na rika Tanganyika nzima waliochangia kupatikana kwa Uhuru, lakini wewe mzee umeng'ang'ania watu wa imani yako tu!! Na isitoshe, umekiri mwenyewe kuwa unachoandika ni vitu kwa kuhadithiwa tu na wazee wako bila ya kufanya utafiti wa kina.
 
Gold...
Kawaida ninaposoma, ''Wewe Mzee,'' najua kuwa mtu kaghadhibika kwa hiyo huchukua tahadhari kidogo nikasubiri hadi atulie ndipo tuendeleee na mjadala.

Sijapatapo kusema ni Waislam tu ndiyo waliopigania uhuru.

Ninachosema ni kuwa historia ya TANU iliyoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni (1981) imewafuta wazee wangu katika historia yake.

Sijakiri kitu chochote na sijui unakusudia nini kusema ''nimekiri.''

Kwa hakika mimi nimejifunza historia ya Dar es Salaam kutoka kwa baba yangu vinginevyo nisingejua mengi.

Labda kama unaona kwa kuwa kuna mambo nimehadithiwa basi ni uongo.
Ikiwa hivyo mengi katika historia ya dunia yatakuwa hayana ukweli.

Hakukuwapo Auschwitz, Poland kwenye mtanuri ya gesi yaliyotumika kuwaaangamizi Wayahudi.
Waliokuwapo wameihadithia dunia na tumejua kilichotokea.

Lakini hebu kaangalie kitabu cha Abdul Sykes na hesabu nyaraka nilizosoma na kufanya rejea achilia mbali vitabu.

Unajua baada ya kitabu kutoka na mchapaji publisher kuanza kukifanyia ''promotion,'' haraka sana kikaingizwa katika Cambridge Journal of African History na hapa Afrika ya Mashariki kilifanyiwa, ''serialisation,'' katika The East African.

Si lazima uamini niliyoandika kila mtu ana uhuru wa kuamini apendacho.
Usijitaabishe.
 
Asijitaabishe bure!!😁
 
Mzee Mohamed kwa namna unavyoongelea mchango wa Mwl kwenye harakati za Uhuru unamdunisha mno licha ya kwamba aliongoza mapambano ya Uhuru kwa akili nyingi na uweledi mkubwa sana hata kuwa mwenyekiti wa TAA, Rais wa kwanza wa Tanu, waziri mkuu wa kwanza wa Tanganyika huru, Rais wa kwanza wa Tanganyika huru na baadae Tanzania.

Ila umemwelezea kama mtu aliyekuja mjini akapokelewa na 'wajanja wa mji' waliompa maisha na yeye kusafiria nyota yao.

Huku pia ukimlaumu kwa kuhujumu umma wa kiislamu kwa makusudi, hili linaudhi wachangiaji wengi

Kumbe sio mimi pekeyake ninayeona hivyo.
Mzee na Mheshimu ana staa walakin
 
Mag3: Nakubaliana na hoja zako mbili watu wachangie hii hoja.Uongo ukijirudia sana unakuwa ukweli.Hii limesukuma wengi kulijadili hili suala, tunaiona hatari iliyo mbeleni
Hii kauli huwa naisikia sana, sijui watu wameihakiki kwa namna gani. Uongo ukijirudia unakuwaje ukweli ?
 
Kwa orodha kama hii ya Waislamu watupu unaowajua wewe, kila kukicha unataka kutuaminisha ni Waislamu tu ndiyo walipigania Uhuru wa nchi hii. Hii imekuwa dhana yako siku zote. Ukweli ni kwamba walikuwapo watu wa kila imani na rika Tanganyika nzima waliochangia kupatikana kwa Uhuru, lakini wewe mzee umeng'ang'ania watu wa imani yako tu!! Na isitoshe, umekiri mwenyewe kuwa unachoandika ni vitu kwa kuhadithiwa tu na wazee wako bila ya kufanya utafiti wa kina.
Unaweza kututajia hao watu unao wasema kiongozi wangu ?
 
Asijitaabishe bure!!😁
Mokaze,
Hakika hana sababu ya kujitaabisha.
Kwa ni i nasema hivyo?

Yeye kaishi miaka chungu mzima akiamini historia iliyokuwapo kama ilivyoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni.

Akiishi raha mustarehe.
Mara anakuja huyu Mohamed Said anasema historia hiyo si sawa na anaweka historia mpya.

Historia hii inamtaabisha kwa kuwa anasoma majina yeye hata siku oja hajapata kuyasoma wala kuyasikia popote pale.

Anasoma historia ya Iddi Faiz Mafungo kadi yake ya TANU no. 24.
Anasoma historia ya ndugu yake Iddi Tosiri kadi yake ya TANU no. 25.

Anasoma kuwa hawa walikuwa wanachama wa TANU wakitokea Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na Tanganyika Africa Association.

Anasoma kuwa hawa ndugu wawili walikuwa watu wa karibu sana na Nyerere.
Iddi Faiz ndiye alikuwa Mweka Hazina wa TANU na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Anaangalia picha anamuona kweli Iddi Faizi yuko na Nyerere Dodoma mwaka wa 1956 pamoja na Sheikh Mohamed Ramiyya Khalifa wa Tarika Kadiriyya, yuko na Saadan Abdu Kandoro na Haruna Iddi Taratibu.

Nyerere hapo kazungukwa na Wamanyema watupu.
Mohamed Said anasherehesha anawaeleza Wamanyema ni watu gani na zipi hulka zao.

Yeye mwenyewe Mohamed Said ni Mmanyema kizazi cha tatu kuzaliwa Tanganyika.

Historia hii inamuudhi.
Yeye akiipenda historia ya Kivukoni haina kitu na nyepesi sana kuielewa.

Nyerere kachukua uongozi wa TANU 1953 wala haielezwi kachukua uongozi kutoka kwa nani.

Nyerere kaunda TANU wala haielezwi fedha za kuunda chama na gharamza zote za kuendesha ofisi zimetoka wapi.

Kila kitu chepesi kushinda unyoya wa ndege shorwa.
Leo anataabishwa na historia mpya ya Mohamed Said.

1648618625812.png

Kushoto ni Iddi Faiz Mafungo, Sheikh Mohamed Ramiyya, Julius Nyerere, Saadan Abdu Kandoro na Haruna Iddi Taratibu
 
Huku pia ukimlaumu kwa kuhujumu umma wa kiislamu kwa makusudi, hili linaudhi wachangiaji wengi.
Hili linaudhi vipi wachangiaji ? Kwamba alichoandika ni uongo kama ni uongo sawa, lakini kama ameandika ukweli, aisee wachukie watakao chukia, sababu hii ndiyo tabia ya ukweli ilivyo.
 
Back
Top Bottom