Historia ya uhuru kama ilivyoandikwa na Ramadhani Makero

Mwalimu ndo' mzalendo no 1 wa Taifa hili.Hakuna mwengine wa kuchukua hiyo no,baada ya yeye ndo wanafuata wengine.
Hao wengine ndio tunataka kujua historia zao na michango yao,mpaka tunapata uhuru!
 
Mohamed Said , unafahamika unajadili kutokea wapi.... Angle moja waislam , hata hao uliowaandika ni mule mule waislam.. Kwani wasio waislam hawakufanya mchango..Hata kma utaweka majina machache bado mwisho wa siku miwani yako ni waislam. Hicho ndio hoja kuu.. Vua miwani hiyo..
 
Japokua ni kweli ila kama Mzee Mohamed Said asingekua na uthubutu wa kusema hayo michango ya hawa watu ingekua imefutika kabisa katika historia.
Ni sawa , lakini wakati ana uthubutu huo, asififishe ukweli mwingine, kuonekana ni watu fulani tu, wa mitaa ya Kariakoo.. Alikuwa ni babu yangu.. Je watoto wa wengine wakija ? Wapo wengi Rupia, Kyaruzi, Kinjekitile ... Asiweke historia kwenye milango ya ukariakoo, magomeni ... Tanzania ni zaidi ya hayo.
 
Kabisa kila kitu kuhusu historia yetu lazima kiandikwe. Biasness ya Mzee Mohamed ni kama biasness ya wale walioandika historia yetu iliyopo kwenye mitaala, muhimu atokee muandishi atakaeandika historia pasi na kua na ajenda binafsi.

Lakini pia tuliaminsihwa watu wa pwani hawakua na mchango wowote katika ukombozi wa Tanganyika huenda ndio anakanusha dhana hiyo
 
Historia hiyo ni mwiko (taboo) kwa watu wa aina ya Pascal Mayalla inawauma sana ikiwekwa bayana, kwa kuwa tu hawana cha kuhadithia cha wazee wao katika harakati za uhuru.

Hao wamekuta watu wamechagua mchele wakaengua chuya wakatayarisha nyama wakasafisha viungo wakaandaa kuni, shaba na karamu ikaandaliwa. Wakatandikiwa wakala sasa wameshiba badala ya kusifia wapishi wanajisifia wao kuwa, aah pilau tumeikomesha.

Hawana kheri hao, ni kama punda tu ambao fadhila yao ni mateke.

Sifahamu kinachowauma ni nini? Kutajwa hao wazee waliokuwa mstari wa mbele kwenye harakati za Uhuru au Uislam wao?

Huyo paschal mayalla mwenyewe bila ukarimu wa Waislam wa Dar. Asingekuwa hapo alipo.

Labda awe amewasahau kina Abdallah Jabir na Shariff Mehboub Al Haddad na kina Alioki waliomtoa tongotongo za ushamba.
 
Hakuna wa kumfikia au kumkaribia Mwl Nyerere hata mkija na story kutoka kuzimu bado Mwl anaendelea kubaki juu

Mimi binafsi naamini katika elimu ya kitaa.. Hii ninyi mnaiita elimu rasmi ni ..........., mtoa post endelea kutupa mambo tuliyofichwa
 
Paschal,
Kwa kuwa tunajadili wafadhili wa TANU na harakati za kudai uhuru ngoja nikuwekee hapa hstoria ya Rashid Ali Meli uone kuwa ingawa kulikuwa na wazalendo hawakuwa na uwezo wa fedha kama Mzee Rupia, Dossa Aziz na Sykes Brothers lakini walikuwa na moyo wa kujitolea nafsi zao:

Huyu Rashid Ali Meli alikuwa mmoja kati watu takriban hawazidi 20 waliohudhuria mkutano wa kwanza wa TANU Ukumbi wa Arnautoglo.

Rashid Ali Meli alikuwa mweka fedha Dar es Salaam Municipal Council.

Ilipodhihirika kuwa mfuko wa kumpeleka Nyerere New York UNO una matatizo yeye akaenda kwenye sefu yake kazini akafungua akatoa fedha kwa siri akamkabidhi Iddi Faiz atie katika safari ya Nyerere kwa makubaliano kuwa TANU itarejesha hizo fedha haraka.

Siku ya pili baada ya Rashid Ali Meli kutoa fedha zile na kuzipeleka TANU wakaguzi wakafika ofisini kwake kufanya ukaguzi.

Walijuaje?

Waingereza walikuwa na mtu wao katika uongozi wa juu wa TANU pale New Street akiwapa taarifa zote kila zinapotokea.

Huyu mtu wao alikuwa huyu mzee wangu.

Yako mengi sana katika historia ya TANU ya hawa, ''nyoka wa vichwa saba,'' chembelecho Maalim Faiza.
 
Newazz,
Ndiyo historia ya TANU ilivyokuwa si kama mimi nimeitengeneza iwe hivyo.

La unadhani kuwa mimi nimeandika uongo fanya utafiti hata mdogo katika mikoa na uje na majibu.

Najua inawachoma wengi historia hii maana naona jinsi Majlis ilivyogeuka na watu sasa wananitukana.

Ukweli ni kuwa baada ya kuchapwa kitabu changu London (1998) publisher akakitangaza kwingi katika vyuo Ulaya na Marekani na hakika kitabu kimebadili historia nzima ya uhuru wa Tanganyika.

Kitabu hiki kikasababisha mimi kutiwa kwenye miradi miwili ya kuandika historia.

Mradi wa kwanza ulikuwa wa Oxford University Press, Nairobi na wa pili wa Harvard na Oxford University Press, New York.

Miradi yote hii imekamilika na vitabu vimechapwa na vinasomeshwa.

Nakumbuka katika mhadhara niliofanya Northwestern University, Chicago kuhusu Abdul Sykes na wazalendo wengine ambao historia zao zilikuwa zimefutika Mkuu wa Idara ya Historia ya Afrika Jonathon Glassman ambae ndiye aliyenialika, katika kutoa neno la shukurani mwisho wa mhadhara alisema kuwa hawakujua kuwa uhuru wa Tanganyika na Nyerere kuwa kiongozi kulichangiwa sana na wazalendo kama Hamza Mwapachu, Abdul Sykes, Sheikh Hassan bin Ameir na kuungwa mkono na Waislam.

Kwa kuwa ghadhabu ziko juu na siwezi kujibu matusi nimeacha kufanya majadiliano na hawa walioghadhibika kama njia ya kuepusha shari nitaendelea na wale ambao wana hamu ya kujifunza historia hii ambayo haikuwapo kabla.


Northwestern University, Evanston Chicago
 
Mzee wangu usikate tamaa, tunaosoma ni wengi na kujifunza.

Sio lazima kila kitu kikubaliwe na wote.

Asante Kwa upande wangu!
 
Watu walianza harakati za kudai uhuru wakati huo Nyerere anachunga ng'ombe kwao huko,acheni kumtukuza na kumfanya Mungu mtu mnampa mateso ya bure huko alipo
Acha kashfa mkuu!
 
Mumby,
Hiyo si adabu ya mjadala huwezi kutumia lugha kama hiyo Mwalimu Nyerere kwa umri wake aliokuwanao wakati anasuhubiana na wazee wetu alikuwa makamo yao na wengine kawapita kwa hiyo huyu ni sawa na baba zetu achilia mbali heshima yake kama Baba wa Taifa.

Mzee wangu usikate tamaa, tunaosoma ni wengi na kujifunza.

Sio lazima kila kitu kikubaliwe na wote.

Asante Kwa upande wangu!
 
Waingereza walikuwa na mtu wao katika uongozi wa juu wa TANU pale New Street akiwapa taarifa zote kila zinapotokea.

Huyu mtu wao alikuwa huyu mzee wangu.
Huyo Mzee wako alikiri alikuwa 'kachero' wa waingereza na mpinga Uhuru? Baada ya uhuru alifukuzwa kazi?
 
Jumong,
Hakika lazima ziwepo ikhitilafu katika maoni hili haliepukiki.
 
Jumong,
Hakika lazima ziwepo ikhitilafu katika maoni hili haliepukiki.
 
Huyo Mzee wako alikiri alikuwa 'kachero' wa waingereza na mpinga Uhuru? Baada ya uhuru alifukuzwa kazi?
Proved,
Jana nimetembelewa na rafiki yangu kutoka Harvard kaja niona kuhusu utafiti wake mpya.

Swali lake la kwanza kataka kujua historia ya Mzee Wangu.

Huyu Mzee Wangu alibaki katika ''service,'' na asingejulikana mpaka mimi nilipoelezwa na Mzee Wangu mwingine aliyekuwa Special Branch na akabaki katika utumishi chini ya Mwalimu Nyerere.

Huyu Mzee Wangu iko siku Insha Allah nitaeleza historia yake hapa Majlis.

Safari ya kwanza Nyerere 1955 anatoka Dar es Salaam kuitangaza TANU Mzee Wangu yuko mkono wa kulia wa Mwalimu.

Huyu Mzee Wangu alikuwa mtu wake sana Abdul Sykes na wakiishi mtaa mmoja.
Historia ya TANU ina mambo.

Mzee Wangu huyu alinisaidia sana katika kuandika kitabu hiki lakini kwenye kitabu sikiweza kumshukuru kwa sababu zilizo wazi.

Siku moja katika mazungumzo na mwanangu wa mwisho akaniangushia ''bomb shell,'' akanambia, ''Baba nikimaliza chuo nataka nijiunge na Intelligence.''
 
Mada nzuri, ni vyema kujua tulikotoka. Inatisaidia kuthamini mambo ambayo kwa wakati fulani tunayachukulia kwa wepesi. Kwa sisi wa miaka ya late 80s umetufungua macho.
 
Huyu Mzee Wangu alibaki katika ''service,'' na asingejulikana mpaka mimi nilipoelezwa na Mzee Wangu mwingine aliyekuwa Special Branch na akabaki katika utumishi chini ya Mwalimu Nyerere.
Hawa wazee kumbe walikuwa wakizungukana pia wao kwa wao? Ila unaposema baada ya uhuru hawa wasaliti waliachwa kufanya kazi na wale waliokuwa wanawahujumu inashangaza pia.
 
Duh...!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…