Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Alva...Nasubir mwendelezo
Muendelezo wa jambo lipi.
Tafadhali nifahamishe ili nikuwekee.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alva...Nasubir mwendelezo
Hao wengine ndio tunataka kujua historia zao na michango yao,mpaka tunapata uhuru!Mwalimu ndo' mzalendo no 1 wa Taifa hili.Hakuna mwengine wa kuchukua hiyo no,baada ya yeye ndo wanafuata wengine.
Mohamed Said , unafahamika unajadili kutokea wapi.... Angle moja waislam , hata hao uliowaandika ni mule mule waislam.. Kwani wasio waislam hawakufanya mchango..Hata kma utaweka majina machache bado mwisho wa siku miwani yako ni waislam. Hicho ndio hoja kuu.. Vua miwani hiyo..Newazz,
Hayo usemayo yote yamo kwenye kitabu cha Abdul Sykes.
Mtafute kitabu umsome Mama bint Maalim, Bi. Halima Selengia, Yusuf Olotu hawa kutoka Moshi.
Umsome Yusuf Chembela, Salum Mpunga, Bi.Sharifa bint Mzee na Sheikh Yusuf Badi wa Lindi.
Umsome Haruna Taratibu na Omari Suleiman kutoka Dodoma.
Usiingie katika mjadala bila kuwa na uelewa wa kinachojadiliwa.
Ni sawa , lakini wakati ana uthubutu huo, asififishe ukweli mwingine, kuonekana ni watu fulani tu, wa mitaa ya Kariakoo.. Alikuwa ni babu yangu.. Je watoto wa wengine wakija ? Wapo wengi Rupia, Kyaruzi, Kinjekitile ... Asiweke historia kwenye milango ya ukariakoo, magomeni ... Tanzania ni zaidi ya hayo.Japokua ni kweli ila kama Mzee Mohamed Said asingekua na uthubutu wa kusema hayo michango ya hawa watu ingekua imefutika kabisa katika historia.
Kabisa kila kitu kuhusu historia yetu lazima kiandikwe. Biasness ya Mzee Mohamed ni kama biasness ya wale walioandika historia yetu iliyopo kwenye mitaala, muhimu atokee muandishi atakaeandika historia pasi na kua na ajenda binafsi.Ni sawa , lakini wakati ana uthubutu huo, asififishe ukweli mwingine, kuonekana ni watu fulani tu, wa mitaa ya Kariakoo.. Alikuwa ni babu yangu.. Je watoto wa wengine wakija ? Wapo wengi Rupia, Kyaruzi, Kinjekitile ... Asiweke historia kwenye milango ya ukariakoo, magomeni ... Tanzania ni zaidi ya hayo.
Historia hiyo ni mwiko (taboo) kwa watu wa aina ya Pascal Mayalla inawauma sana ikiwekwa bayana, kwa kuwa tu hawana cha kuhadithia cha wazee wao katika harakati za uhuru.Kuna siku Nyerere alikuwa akitoka nyumbani kwake magomeni akielekea sokoni Kariakoo kutafuta mahitaji ya nyumbani kufika maeneo ya faya akakutana na Mzee Mshume Kiyate na baada ya kujuliana hali ndipo Nyerere aliposema anaenda sokoni lakini cha ajabu fedha aliyokuwa nayo ilikuwa ni kidogo sana ndipo Mzee Kiyate alipomuongeza pesa na kumuahidi toka siku hiyo ni yeye ndiye atawajibika kupeleka vyakula nyumbani kwake na kweli ikawa hivyo hadi pale Nyerere alipoingia Ikulu na kuanza kuhudumiwa na Serikali, Je wakati huo huyo Rupia wako unayedai alimpa guarantee ya kumuwezesha mwalimu pale alipoacha kazi alikuwa wapi? Acha unafiki ndugu
Hakuna wa kumfikia au kumkaribia Mwl Nyerere hata mkija na story kutoka kuzimu bado Mwl anaendelea kubaki juu
Paschal,Kwa hili la ufadhili nakubaliana na wewe hatuwezi ku quotify kwa kupitia viwango nani alitoa nini, lakini ndani ya wafadhili hao, kulikuwa na mfadhili mkubwa kabisa aliyetoa kitu kikubwa kuliko wote, bila hata kujitaja ni nani, huyu ni Mzee John Rupia, huyu ndie alitoa guarantee kwa Mwalimu kuacha kazi ya mshahara serikalini because he had a guarantee na the guarantor ni Mzee John Rupia.
Kitu ambacho nakubaliana na wewe ni thamani ya huo ufadhili, mfano kwa vile Mzee John Rupia ndio alikuwa tajiri kupita wote (hapa naomba msilete ubishi), thamani ya mchango wake hata akichangia shilingi milioni mia moja kati ya Bilioni moja na yule mama muuza maandazi aliyechangia thumuni kati Shilingi moja yake, yule mama ndio ametoa zaidi.
Kuna wachingiaji wa kuonekanika na invisible donors waliochagia pakubwa in kind kuliko hata nominal values, mfano aliyemfundisha Mama Maria kupika chapati na kuokoa fedha za kitafunio, ametoa mchango mkubwa kuliko yule anayemnunulia mkate.
P
Newazz,Mohamed Said , unafahamika unajadili kutokea wapi.... Angle moja waislam , hata hao uliowaandika ni mule mule waislam.. Kwani wasio waislam hawakufanya mchango..Hata kma utaweka majina machache bado mwisho wa siku miwani yako ni waislam. Hicho ndio hoja kuu.. Vua miwani hiyo..
Mzee wangu usikate tamaa, tunaosoma ni wengi na kujifunza.Newazz,
Ndiyo historia ya TANU ilivyokuwa si kama mimi nimeitengeneza iwe hivyo.
La unadhani kuwa mimi nimeandika uongo fanya utafiti hata mdogo katika mikoa na uje na majibu.
Najua inawachoma wengi historia hii maana naona jinsi Majlis ilivyogeuka na watu sasa wananitukana.
Ukweli ni kuwa baada ya kuchapwa kitabu changu London (1998) publisher akakitangaza kwingi katika vyuo Ulaya na Marekani na hakika kitabu kimebadili historia nzima ya uhuru wa Tanganyika.
Kitabu hiki kikasababisha mimi kutiwa kwenye miradi miwili ya kuandika historia.
Mradi wa kwanza ulikuwa wa Oxford University Press, Nairobi na wa pili wa Harvard na Oxford University Press, New York.
Miradi yote hii imekamilika na vitabu vimechapwa na vinasomeshwa.
Nakumbuka katika mhadhara niliofanya Northwestern University, Chicago kuhusu Abdul Sykes na wazalendo wengine ambao historia zao zilikuwa zimefutika Mkuu wa Idara ya Historia ya Afrika Jonathon Glassman ambae ndiye aliyenialika, katika kutoa neno la shukurani mwisho wa mhadhara alisema kuwa hawakujua kuwa uhuru wa Tanganyika na Nyerere kuwa kiongozi kulichangiwa sana na wazalendo kama Hamza Mwapachu, Abdul Sykes, Sheikh Hassan bin Ameir na kuungwa mkono na Waislam.
Kwa kuwa ghadhabu ziko juu na siwezi kujibu matusi nimeacha kufanya majadiliano na hawa walioghadhibika kama njia ya kuepusha shari nitaendelea na wale ambao wana hamu ya kujifunza historia hii ambayo haikuwapo kabla.
Acha kashfa mkuu!Watu walianza harakati za kudai uhuru wakati huo Nyerere anachunga ng'ombe kwao huko,acheni kumtukuza na kumfanya Mungu mtu mnampa mateso ya bure huko alipo
Mzee wangu usikate tamaa, tunaosoma ni wengi na kujifunza.
Sio lazima kila kitu kikubaliwe na wote.
Asante Kwa upande wangu!
Huyo Mzee wako alikiri alikuwa 'kachero' wa waingereza na mpinga Uhuru? Baada ya uhuru alifukuzwa kazi?Waingereza walikuwa na mtu wao katika uongozi wa juu wa TANU pale New Street akiwapa taarifa zote kila zinapotokea.
Huyu mtu wao alikuwa huyu mzee wangu.
Proved,Huyo Mzee wako alikiri alikuwa 'kachero' wa waingereza na mpinga Uhuru? Baada ya uhuru alifukuzwa kazi?
Mada nzuri, ni vyema kujua tulikotoka. Inatisaidia kuthamini mambo ambayo kwa wakati fulani tunayachukulia kwa wepesi. Kwa sisi wa miaka ya late 80s umetufungua macho.HUYU NDIYO ALLY SYKES MZEE WA FITINA.
Na.Ramadhan Makero
UHURU wa Tanganyika haukuwa kazi rahisi kupatikana kama ambavyo wengi wanadhania.
Ili kuwa ni shughuli pevu iliyohitaji kujitoa kwa hali na mali ili kuhakikisha Waafrika kutoka Tanganyika ambalo lilikuwa koloni la Uingereza, wanajitawala.
Jitihada hizo zilifanywa na wapigania uhuru mbalimbali waliounganishwa kupitia chama cha Tanganyika National Unioni (TANU), kilichoundwa na na watu waliojawa na shauku la kujitoa kwenye makucha ya kikoloni.
Ally Kleist Sykes mzaliwa wa Mtaa wa Gerezani, Kariakoo Dar es Salaam, ni miongoni mwa waasisi waliopigania uhuru wa Tanganyika ambaye ana mengi ya kukumbukwa.
Mzee huyo aliyezaliwa Oktoba 10 mwaka 1926 kisha kufariki Dunia Mei 19 mwaka 2013 alikuwa mzalendo aliyeanza harakati za kisiasa kwenye miaka ya 1950.
Ally Sykes ndiye aliyemwandikia na kumkabidhi Hayati Mwalimu Julius Nyerere kadi ya TANU namba moja.
Pia alikuwa miongoni mwa waasisi wa TANU, kati ya wazee watu saba waliokuwa katika kamati ya TAA iliyounda TANU.
Alikuwa miongoni mwa wafadhili wakuu wa TANU, huku akiwa tegemeo la chama hicho katika kutekeleza mikakati hatari dhidi ya utawala wa Uingereza.
Katika siasa za sasa Mzee Ally Sykes anaweza akaelezewa kama "Mzee wa fitna" kwani alikuwa majukumu ya kuwagombanisha wananchi dhidi ya serikali ya kikoloni.
Majukumu hayo aliyatelekeza kwa kuchapa karatasi ambayo Waingereza waliyaita ya kuchochea ghasia kwani majasusi wa serikali ya kikoloni walimfahamu kwa uhodari wa kutengeneza mambo.
Waingereza walipata wakati mgumu kumkabili kwani licha ya uhodari wa kisiasa aliokuwa nao, Ally Sykes pia alikuwa na medali ya mlenga shabaha mahiri, aliyopata kwenye Vita Kuu vya Pili ya Dunia.
Kwenye vita hiyo Ally Sykes alikuwa kwenye bataliani ya sita (Battalion 6 Burma Infantry) King's African Rifles (KAR)
Hakika Ally Sykes alikuwa mzalendo, mweledi wa mambo na miongoni mwa waasisi muhimu wa TANU ambaye sahihi yake ndio iko katika kadi ya TANU ya Mwalimu Nyerere.
Umaarufu wake ni kama aliurithi kutoka kwa Baba yake Mzee Kleist Sykes aliyekuwa watu mashuhuri Dar es Salaam katika miaka ya 1900 hadi alipofariki mwaka 1949.
Baba yake alikuwa maarufu kwa kuwa alilelewa na Affande Plantan aliyekuwa askari kiongozi katika jeshi la Wajerumani lilokuja Tanganyika na Herman Von Wissman.
Kleist alikuwa ndiye katibu muasisi wa African Association mwaka 1929 chama kilichokuja baadae kujibadili na kuwa TANU ambacho Ally Sykes akiwa mmoja wa waasisi.
Pia baba yake aliasisi Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) na kupitia jumuia hiyo akajenga shule ya kwanza ya Kiiislam Dar es Salaam, ambayo ilisomesha Qur’an pamoja na elimu ya kimagharibi.
Jumuiya hiyo ilichangia vijana wengi wa kiislamu kuingia kwenye siasa za TAA na TANU katika harakati za kudai uhuru.
AKUTANA NA NYERERE
Ally Sykes na kaka yake Abdulwahid Sykes ndio watu wa mwanzo kumpokea Mwalimu Nyerere alipokuja Dar es Salaam mwaka 1952.
Nyerere alifika nyumbani kwa akina Sykes na ilijenga urafiki ambao ulipitiliza na kuwa udugu mkubwa wa mapenzi ya dhati si baina yao tu bali hata kwa wake na mama zao.
Mama yake Nyerere, Bi. Mugaya mara kwa mara alipenda kumtembelea nyumbani Bi Mruguru biti Mussa ambaye ndiye mama wa Sykes.
Pia Mama Maria Nyerere alikuwa mwenye urafiki wa karibu na Bi. Zainab ambaye ni mke wa Ally Sykes aliyekuwa akiishi Mtaa wa Kipata.
Wakati huo harakati za kuanzisha TANU zilikuwa zimepamba moto huku fitna za Waingereza kuwatokomeza viongozi shupavu wa TAA kama Hamza Mwapachu, Dk. Vedast Kyaruzi, Dk. Wilbard Mwanjisi, zilikivunja nguvu chama hicho.
Ndio maana TANU ilipokuja kuasisiwa mwaka 1954 Ally Sykes kadi yake ya TANU ikawa namba mbili, Nyerere namba moja, Abdulwahid Sykes kadi yake namba tatu, Dossa Aziz kadi namba nne na John Rupia kadi yake ilikuwa namba saba.
Kipindi hicho Ally Sykes alikuwa Katibu wa Tanganyika African Government Servants Association (TAGSA) na vilevile alikuwa mwakilishi wa chama hicho katika Kamati ya Uajiri ya Serikali (Government Establishment Committee).
Thomas Marealle ndiye alikuwa rais wa TAGSA na Rashid Kawawa alikuwa mwanakamati.
Wanasiasa hao walijipa jina la ‘’Wednesday Tea Club’’ wakikutana kila siku ya Jumatano kunywa chai pamoja na kupanga mikakati ya kuwang’oa Waingereza katika ardhi ya Tanganyika.
Kupitia Ally, Abdulwahid na Dossa Aziz, Nyerere aliweza kujuana na wenyeji wa Dar es Salaam maarufu baadhi yao ni Sheikh Hassan bin Amir, Mshume Kiyate, Jumbe Tambaza, Sheikh Suleiman Takadir, Clement Mtamila, Titi Mohamed na Tatu biti Mzee.
View attachment 1197154
Hawa wazee kumbe walikuwa wakizungukana pia wao kwa wao? Ila unaposema baada ya uhuru hawa wasaliti waliachwa kufanya kazi na wale waliokuwa wanawahujumu inashangaza pia.Huyu Mzee Wangu alibaki katika ''service,'' na asingejulikana mpaka mimi nilipoelezwa na Mzee Wangu mwingine aliyekuwa Special Branch na akabaki katika utumishi chini ya Mwalimu Nyerere.
Duh...!.Paschal,
Waingereza walikuwa na mtu wao katika uongozi wa juu wa TANU pale New Street akiwapa taarifa zote kila zinapotokea.
Huyu mtu wao alikuwa huyu mzee wangu.
Yako mengi sana katika historia ya TANU ya hawa, ''nyoka wa vichwa saba,'' chembelecho Maalim Faiza.