Historia ya uhuru kama ilivyoandikwa na Ramadhani Makero

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
HUYU NDIYO ALLY SYKES MZEE WA FITINA.

Na.Ramadhan Makero

UHURU wa Tanganyika haukuwa kazi rahisi kupatikana kama ambavyo wengi wanadhania.

Ili kuwa ni shughuli pevu iliyohitaji kujitoa kwa hali na mali ili kuhakikisha Waafrika kutoka Tanganyika ambalo lilikuwa koloni la Uingereza, wanajitawala.

Jitihada hizo zilifanywa na wapigania uhuru mbalimbali waliounganishwa kupitia chama cha Tanganyika National Unioni (TANU), kilichoundwa na na watu waliojawa na shauku la kujitoa kwenye makucha ya kikoloni.

Ally Kleist Sykes mzaliwa wa Mtaa wa Gerezani, Kariakoo Dar es Salaam, ni miongoni mwa waasisi waliopigania uhuru wa Tanganyika ambaye ana mengi ya kukumbukwa.

Mzee huyo aliyezaliwa Oktoba 10 mwaka 1926 kisha kufariki Dunia Mei 19 mwaka 2013 alikuwa mzalendo aliyeanza harakati za kisiasa kwenye miaka ya 1950.

Ally Sykes ndiye aliyemwandikia na kumkabidhi Hayati Mwalimu Julius Nyerere kadi ya TANU namba moja.

Pia alikuwa miongoni mwa waasisi wa TANU, kati ya wazee watu saba waliokuwa katika kamati ya TAA iliyounda TANU.

Alikuwa miongoni mwa wafadhili wakuu wa TANU, huku akiwa tegemeo la chama hicho katika kutekeleza mikakati hatari dhidi ya utawala wa Uingereza.

Katika siasa za sasa Mzee Ally Sykes anaweza akaelezewa kama "Mzee wa fitna" kwani alikuwa majukumu ya kuwagombanisha wananchi dhidi ya serikali ya kikoloni.

Majukumu hayo aliyatelekeza kwa kuchapa karatasi ambayo Waingereza waliyaita ya kuchochea ghasia kwani majasusi wa serikali ya kikoloni walimfahamu kwa uhodari wa kutengeneza mambo.

Waingereza walipata wakati mgumu kumkabili kwani licha ya uhodari wa kisiasa aliokuwa nao, Ally Sykes pia alikuwa na medali ya mlenga shabaha mahiri, aliyopata kwenye Vita Kuu vya Pili ya Dunia.

Kwenye vita hiyo Ally Sykes alikuwa kwenye bataliani ya sita (Battalion 6 Burma Infantry) King's African Rifles (KAR)

Hakika Ally Sykes alikuwa mzalendo, mweledi wa mambo na miongoni mwa waasisi muhimu wa TANU ambaye sahihi yake ndio iko katika kadi ya TANU ya Mwalimu Nyerere.

Umaarufu wake ni kama aliurithi kutoka kwa Baba yake Mzee Kleist Sykes aliyekuwa watu mashuhuri Dar es Salaam katika miaka ya 1900 hadi alipofariki mwaka 1949.

Baba yake alikuwa maarufu kwa kuwa alilelewa na Affande Plantan aliyekuwa askari kiongozi katika jeshi la Wajerumani lilokuja Tanganyika na Herman Von Wissman.

Kleist alikuwa ndiye katibu muasisi wa African Association mwaka 1929 chama kilichokuja baadae kujibadili na kuwa TANU ambacho Ally Sykes akiwa mmoja wa waasisi.

Pia baba yake aliasisi Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) na kupitia jumuia hiyo akajenga shule ya kwanza ya Kiiislam Dar es Salaam, ambayo ilisomesha Qur’an pamoja na elimu ya kimagharibi.

Jumuiya hiyo ilichangia vijana wengi wa kiislamu kuingia kwenye siasa za TAA na TANU katika harakati za kudai uhuru.

AKUTANA NA NYERERE

Ally Sykes na kaka yake Abdulwahid Sykes ndio watu wa mwanzo kumpokea Mwalimu Nyerere alipokuja Dar es Salaam mwaka 1952.

Nyerere alifika nyumbani kwa akina Sykes na ilijenga urafiki ambao ulipitiliza na kuwa udugu mkubwa wa mapenzi ya dhati si baina yao tu bali hata kwa wake na mama zao.

Mama yake Nyerere, Bi. Mugaya mara kwa mara alipenda kumtembelea nyumbani Bi Mruguru biti Mussa ambaye ndiye mama wa Sykes.

Pia Mama Maria Nyerere alikuwa mwenye urafiki wa karibu na Bi. Zainab ambaye ni mke wa Ally Sykes aliyekuwa akiishi Mtaa wa Kipata.

Wakati huo harakati za kuanzisha TANU zilikuwa zimepamba moto huku fitna za Waingereza kuwatokomeza viongozi shupavu wa TAA kama Hamza Mwapachu, Dk. Vedast Kyaruzi, Dk. Wilbard Mwanjisi, zilikivunja nguvu chama hicho.

Ndio maana TANU ilipokuja kuasisiwa mwaka 1954 Ally Sykes kadi yake ya TANU ikawa namba mbili, Nyerere namba moja, Abdulwahid Sykes kadi yake namba tatu, Dossa Aziz kadi namba nne na John Rupia kadi yake ilikuwa namba saba.

Kipindi hicho Ally Sykes alikuwa Katibu wa Tanganyika African Government Servants Association (TAGSA) na vilevile alikuwa mwakilishi wa chama hicho katika Kamati ya Uajiri ya Serikali (Government Establishment Committee).

Thomas Marealle ndiye alikuwa rais wa TAGSA na Rashid Kawawa alikuwa mwanakamati.

Wanasiasa hao walijipa jina la ‘’Wednesday Tea Club’’ wakikutana kila siku ya Jumatano kunywa chai pamoja na kupanga mikakati ya kuwang’oa Waingereza katika ardhi ya Tanganyika.

Kupitia Ally, Abdulwahid na Dossa Aziz, Nyerere aliweza kujuana na wenyeji wa Dar es Salaam maarufu baadhi yao ni Sheikh Hassan bin Amir, Mshume Kiyate, Jumbe Tambaza, Sheikh Suleiman Takadir, Clement Mtamila, Titi Mohamed na Tatu biti Mzee.

1567561457281.jpeg
 
View attachment 1197154

Itaendelea lini
 
Hakuna wa kumfikia au kumkaribia Mwl Nyerere hata mkija na story kutoka kuzimu bado Mwl anaendelea kubaki juu
Jambo la kujiuliza hapo ni vipi aliweza kuepa kutekwa katika kundi hilo?
Bila shaka mtafaruku huo ndio uliopelekea mambo yakawa kama yalivyo hadi sasa.

Sijui tungekuwa wapi kama Mwalimu angetekwa na kundi hilo!
 
Ngongo,
Si kama watu wanaandika historia hizi ambazo hazikuwako kwa nia ya kumshusha Mwalimu Nyerere na sijui kwa nini uhisi hivyo, historia hizi zinaandikwa kwa kumamilisha historia ya Mwalimu mwenyewe.

Hakuna atakaeweza kubisha kuwa mchango wa Nyerere ulikuwa mkubwa na ikiwa yeyote awaye yule ataandika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika kwa nia ya kumdogosha kalamu yake haitafika popote pale.

Badala ya kuchukia kwa nini zinaandikwa historia za wazalendo wengine kama hii ya Ally Sykes iliyoandikwa na ndugu yetu Ramadhani ni wajibu wetu sisi kutia hima kila mwenye uwezo wa kutafiti na kuandika historia kama hizi akafanya hivyo.
 
HUYU NDIYO ALLY SYKES MZEE WA FITINA.
Mkuu Sky Eclat, asante sana kwa hii mada hii mujarab, swadacta, hii ni simulizi nzuri, hapa emmelezewa kama ni mmoja miongoni mwa wafadhili wakuu wa TANU,japo mfadhili mkuu wa TANU ni Mzee John Rupia, yeye hatajwi tajwi sana kutokana na..., anyway sio lazima kumtaja mfadhili Mkuu, hata wale waliochangia zile fedha zenye tundu enzi hizo ni fedha, nao pia ni wafadhili.

P
 
Pascal,
Hili la ufadhili mkuu si rahisi kulieleza kwa uhakika na kusema kuwa fulani alimzidi mwenzake katika kuchangia.

Wafadhili wa TANU pale New New Street walikuwa John Rupia, Dossa Aziz Abdul na Ally Sykes na kila mtu alitoa kwa nafasi yake na kwa njia nyingi tofauti.

Kutajwa katika ufadhili kunategemea na kile kilichotolewa kwa wakati gani na kilikuwaje cha kuonekana au cha faragha.

Dossa Aziz alitoa gari nzima kuipa TANU kwa matumizi ya Mwalimu Nyerere.

Abdul Sykes nyumba yake ndiyo ilikuwa kama ofisi ya pili ya TANU kwa shughuli nyingi za chama na kwa ajili hii saa 24 watu wakiingia na wageni wakifikia kwake kutoka sehemu tofauti za Tanganyika kuanzia machifu hadi watu wa kawaida na wengine ilibidi wakae kwake.

Nyumbani kwa Abdul Sykes, Mzee Abdallah aliyekuwa mhudumu wa ofisi ya Abdul Kariakoo Market anasema kuna nyakati alikuwa anachinja hadi kuku 20 kwa siku kupeleka nyumbani kwa Abdul kwa ajili ya kitoweo.

Dossa Aziz yeye alikuwa akitoa matumizi ya siku kwa siku ya ofisi ya TANU na yeye na Mzee Rupia, Abdul na Ally ndiye pia wakilipa bili zote za chakula na vinywaji katika kila shughuli ya TANU kwa siku za mwanzo hadi walipokuja kusaidiwa na Baraza la Wazee wa TANU mfadhili mkubwa akiwa Mshume Kiyate.

Si rahisi kusema fulani yeye alitoa zaidi ya fulani kwa kuwa wafadhili wa TANU wote walisaidiana.

Iko siku In Shaa Allah nitaeleza kisa cha ''sanduku la fedha la Bwana Abdul'' kama nilivyoelezwa na mkewe mama yetu Bi. Mwamvua.

Historia ya TANU ina mengi sana.
 
Jambo la kujiuliza hapo ni vipi aliweza kuepa kutekwa katika kundi hilo?
Bila shaka mtafaruku huo ndio uliopelekea mambo yakawa kama yalivyo hadi sasa.

Sijui tungekuwa wapi kama Mwalimu angetekwa na kundi hilo!
Kalamu1
Nifafanulie kuhusu ''kundi,'' na ''kutekwa.''

Katika TAA hadi kufikia TANU nijuavyo mimi hapajapatapo kuw ana kundi lolote.

Nijuavyo mimi kulikuwa na kamati ndani ya kamati wakati inafanywa mipango ya kuunda TANU na Nyerere alikuwa bado hajafika Dar es Salaam.

Kulikuwa na TAA Political Subcommittee na wajumbe wake walikuwa Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, John Rupia na Steven Mhando.

Ndani ya hii kamati kulikuwa na kamati ndani ya kamati hii ya Abdul na Ally Sykes, Hamza Mwapachu, Dossa Aziz na Earle Seaton.

Sijaweza kuelewa hii Nyerere kutekwa una maana gani na nani wamteke na kwa sababu zipi?
 
Pascal,
Hili la ufadhili mkuu si rahisi kulieleza kwa uhakika na kusema kuwa fulani alimzidi mwenzake katika kuchangia.

Wafadhili wa TANU pale New New Street walikuwa John Rupia, Dossa Aziz Abdul na Ally Sykes na kila mtu alitoa kwa nafasi yake na kwa njia nyingi tofauti.

Kutajwa katika ufadhili kunategemea na kile kilichotolewa kwa wakati gani na kilikuwaje cha kuonekana au cha faragha.

Dossa Aziz alitoa gari nzima kuipa TANU kwa matumizi ya Mwalimu Nyerere.

Abdul Sykes nyumba yake ndiyo ilikuwa kama ofisi ya pili ya TANU kwa shughuli nyingi za chama na kwa ajili hii saa 24 watu wakiingia na wageni wakifikia kwake kutoka sehemu tofauti za Tanganyika kuanzia machifu hadi watu wa kawaida na wengine ilibidi wakae kwake.

Nyumbani kwa Abdul Sykes, Mzee Abdallah aliyekuwa mhudumu wa ofisi ya Abdul Kariakoo Market anasema kuna nyakati alikuwa anachinja hadi kuku 20 kwa siku kupeleka nyumbani kwa Abdul kwa ajili ya kitoweo.

Dossa Aziz yeye alikuwa akitoa matumizi ya siku kwa siku ya ofisi ya TANU na yeye na Mzee Rupia, Abdul na Ally ndiye pia wakilipa bili zote za chakula na vinywaji katika kila shughuli ya TANU kwa siku za mwanzo hadi walipokuja kusaidiwa na Baraza la Wazee wa TANU mfadhili mkubwa akiwa Mshume Kiyate.

Si rahisi kusema fulani yeye alitoa zaidi ya fulani kwa kuwa wafadhili wa TANU wote walisaidiana.

Iko siku In Shaa Allah nitaeleza kisa cha ''sanduku la fedha la Bwana Abdul'' kama nilivyoelezwa na mkewe mama yetu Bi. Mwamvua.

Historia ya TANU ina mengi sana.
Kwa hili la ufadhili nakubaliana na wewe hatuwezi ku quotify kwa kupitia viwango nani alitoa nini, lakini ndani ya wafadhili hao, kulikuwa na mfadhili mkubwa kabisa aliyetoa kitu kikubwa kuliko wote, bila hata kujitaja ni nani, huyu ni Mzee John Rupia, huyu ndie alitoa guarantee kwa Mwalimu kuacha kazi ya mshahara serikalini because he had a guarantee na the guarantor ni Mzee John Rupia.

Kitu ambacho nakubaliana na wewe ni thamani ya huo ufadhili, mfano kwa vile Mzee John Rupia ndio alikuwa tajiri kupita wote (hapa naomba msilete ubishi), thamani ya mchango wake hata akichangia shilingi milioni mia moja kati ya Bilioni moja na yule mama muuza maandazi aliyechangia thumuni kati Shilingi moja yake, yule mama ndio ametoa zaidi.

Kuna wachingiaji wa kuonekanika na invisible donors waliochagia pakubwa in kind kuliko hata nominal values, mfano aliyemfundisha Mama Maria kupika chapati na kuokoa fedha za kitafunio, ametoa mchango mkubwa kuliko yule anayemnunulia mkate.
P
 
Ngongo,
Si kama watu wanaandika historia hizi ambazo hazikuwako kwa nia ya kumshusha Mwalimu Nyerere na sijui kwa nini uhisi hivyo, historia hizi zinaandikwa kwa kumamilisha historia ya Mwalimu mwenyewe.

Hakuna atakaeweza kubisha kuwa mchango wa Nyerere ulikuwa mkubwa na ikiwa yeyote awaye yule ataandika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika kwa nia ya kumdogosha kalamu yake haitafika popote pale.

Badala ya kuchukia kwa nini zinaandikwa historia za wazalendo wengine kama hii ya Ally Sykes iliyoandikwa na ndugu yetu Ramadhani ni wajibu wetu sisi kutia hima kila mwenye uwezo wa kutafiti na kuandika historia kama hizi akafanya hivyo.
Asante mkuu! Kuna baadhi miongoi mwetu tunapenda sana kutafsiri hata kama baadhi ya maswala hayahitaji tafsiri. Tuvumiliane tu!
 
Uzalendo wake ulikuwa wa nini wakati Uhuru tulikuwa bado hatujapata?
 
Kwa hili la ufadhili nakubaliana na wewe hatuwezi ku quotify kwa kupitia viwango nani alitoa nini, lakini ndani ya wafadhili hao, kulikuwa na mfadhili mkubwa kabisa aliyetoa kitu kikubwa kuliko wote, bila hata kujitaja ni nani, huyu ni Mzee John Rupia, huyu ndie alitoa guarantee kwa Mwalimu kuacha kazi ya mshahara serikalini because he had a guarantee na the guarantor ni Mzee John Rupia.

Kitu ambacho nakubaliana na wewe ni thamani ya huo ufadhili, mfano kwa vile Mzee John Rupia ndio alikuwa tajiri kupita wote (hapa naomba msilete ubishi), thamani ya mchango wake hata akichangia shilingi milioni mia moja kati ya Bilioni moja na yule mama muuza maandazi aliyechangia thumuni kati Shilingi moja yake, yule mama ndio ametoa zaidi.

Kuna wachingiaji wa kuonekanika na invisible donors waliochagia pakubwa in kind kuliko hata nominal values, mfano aliyemfundisha Mama Maria kupika chapati na kuokoa fedha za kitafunio, ametoa mchango mkubwa kuliko yule anayemnunulia mkate.
P
Paschal,
Mimi singependa kubishana na wewe katika hili kwa kuwa si muhimu hivyo ila nitakueleza kitu kimoja.

John Rupia alikuwa na lori lake moja linaitwa, "Msichoke," mmoja kati ya wafanyakazi wake mimi ni mjomba wangu Rajab Athmani Matimbwa na yu hai anaishi Sungwi.

Dossa alikuwa na malori saba aloyorithi kwa baba yake.

Soma historia ya Mzee Matimbwa hapo chini:

Paschal,
Mimi nimeishi ndani ya historia hii wahusika wengi ni wazee wangu.

Wewe ni mtu baki hawa huwajui.
 
Wanalazimisha tuwatambue wehu wengine waliokuwa wanashinda kwenye bao wakati mwalimu yupo busy kuweka mikakati ya kuikomboa Nchi

Hawa wazee ni kuwaacha tu wanamatatizo mengi
Tatitzo kubwa ni udini umeathiri fahamu zao
Hakuna wa kumfikia au kumkaribia Mwl Nyerere hata mkija na story kutoka kuzimu bado Mwl anaendelea kubaki juu
 
Nimeipenda hii historia fupi na iliyoshiba.
Nyerere alikuwa ni mfungaji wa goli la ushindi, ila si vibaya kuwajua wachezaji wengine kwenye hiyo game je walikuwa wakina nani na walicheza namba ngapi, maana bila kupewa assist na wenzake sizani kama angefunga hilo goli.
Na lazima tumjue je man of the match alikuwa nani?
 
Kwa hili la ufadhili nakubaliana na wewe hatuwezi ku quotify kwa kupitia viwango nani alitoa nini, lakini ndani ya wafadhili hao, kulikuwa na mfadhili mkubwa kabisa aliyetoa kitu kikubwa kuliko wote, bila hata kujitaja ni nani, huyu ni Mzee John Rupia, huyu ndie alitoa guarantee kwa Mwalimu kuacha kazi ya mshahara serikalini because he had a guarantee na the guarantor ni Mzee John Rupia.

Kitu ambacho nakubaliana na wewe ni thamani ya huo ufadhili, mfano kwa vile Mzee John Rupia ndio alikuwa tajiri kupita wote (hapa naomba msilete ubishi), thamani ya mchango wake hata akichangia shilingi milioni mia moja kati ya Bilioni moja na yule mama muuza maandazi aliyechangia thumuni kati Shilingi moja yake, yule mama ndio ametoa zaidi.

Kuna wachingiaji wa kuonekanika na invisible donors waliochagia pakubwa in kind kuliko hata nominal values, mfano aliyemfundisha Mama Maria kupika chapati na kuokoa fedha za kitafunio, ametoa mchango mkubwa kuliko yule anayemnunulia mkate.
P
Reference tafadhali
 
Wanalazimisha tuwatambue wehu wengine waliokuwa wanashinda kwenye bao wakati mwalimu yupo busy kuweka mikakati ya kuikomboa Nchi

Hawa wazee ni kuwaacha tu wanamatatizo mengi
Tatitzo kubwa ni udini umeathiri fahamu zao
Mikocheni,
Hajalazimishwa mtu chochote.

Nimeandika kitabu cha historia ya TANU watu wamekipenda na sasa tunakwenda toleo la nne.

Wengi mmeguswa na kitabu hiki mnakuja hapa Majlis kukipinga na ndiyo huu mjadala.

Kutokana na hii mijadala kitabu kimepata umaarufu mkubwa na mauzo yameongezeka sana.
 
Back
Top Bottom