Historia ya uhuru kama ilivyoandikwa na Ramadhani Makero

Historia ya uhuru kama ilivyoandikwa na Ramadhani Makero

Nimeipenda hii historia fupi na iliyoshiba.
Nyerere alikuwa ni mfungaji wa goli la ushindi, ila si vibaya kuwajua wachezaji wengine kwenye hiyo game je walikuwa wakina nani na walicheza namba ngapi, maana bila kupewa assist na wenzake sizani kama angefunga hilo goli.
Na lazima tumjue je man of the match alikuwa nani?
Hiyo timu ilifumuliwa, ikaundwa timu nyingine iliyoleta ushindi.
Timu hiyo aliyoanza nayo Mwalimu isingetufikisha popote.
 
Hiyo timu ilifumuliwa, ikaundwa timu nyingine iliyoleta ushindi.
Timu hiyo aliyoanza nayo Mwalimu isingetufikisha popote.
Kalamu!
Unasema mambo usiyoyajua.

Ungewatoa hao fedha za kuendesha chama zingetoka wapi?

1953 mara baada ya Mwalimu kuchukua uongozi TAA ilikufa na si kwa kuwa Mwalimu hakuwa na uwezo wa kuendesha la hasha morali ya baadhi ya wajumbe katika kamati zilikwenda chini.

Abdul alipokuwa Rais alitia rangi katika vikao na vikao vikapendeza na kutakata.

Mwalimu hakuwa na uwezo wa kufanya yale ambayo baadhi ya wajumbe waliyazoea kutoka kwa Abdul.

Hata TANU ilipokuwa imeshaundwa vikao vingi vya "retreat" vikifanyika nyumbani kwa Abdul Sykes ingawa Mwalimu alikuwa na nyumba yake Magomeni Majumba Sita.

Bila ya kuungwa mkono na watu hawa Mwalimu asingefika popote.

Unakijua kisa cha taharuki iliyokumba nyumba ya Abdul Sykes siku ilipohofiwa Nyerere kalishwa sumu nyumbani kwake Abdul baada ya chakula cha mchana walipokuwa kwenye retreat?

Unajua kwa nini Abdul alipewa jina "The Sweet," na Dossa, "The Bank?"

Someni kwanza historia ya TANU ndipo mzungumze.
 
Paschal,
Mimi singependa kubishana na wewe katika hili kwa kuwa si muhimu hivyo ila nitakueleza kitu kimoja.

John Rupia alikuwa na lori lake moja linaitwa, "Msichoke," mmoja kati ya wafanyakazi wake mimi ni mjomba wangu Rajab Athmani Matimbwa na yu hai anaishi Sungwi.

Dossa alikuwa na malori saba aloyorithi kwa baba yake.

Soma historia ya Mzee Matimbwa hapo chini:


Paschal,
Mimi nimeishi ndani ya historia hii wahusika wengi ni wazee wangu.

Wewe ni mtu baki hawa huwajui.
"Wewe ni mtu baki hawa huwajui "

Hii statement ina ukakasi sana

Na Paskali akisema Rupia ni mzee wake na wewe kwa Rupia ni mtu baki hakuna unalojua kuhusu ufadhili wake TANU utambishia ?
 
"Wewe ni mtu baki hawa huwajui "

Hii statement ina ukakasi sana

Na Paskali akisema Rupia ni mzee wake na wewe kwa Rupia ni mtu baki hakuna unalojua kuhusu ufadhili wake TANU utambishia ?
Yamakagashi,
Zungumza mengine.

Mimi nimezaliwa Dar es Salaam Mtaa wa Kipata.

Historia yetu Dar es Salaam Gerezani inarudi nyuma sasa miaka 100 na naijua.

Babu yangu Salum Abdallah nyumba yake ilikuwa Mtaa wa Mbaruku na Congo jirani na nyumba ya Aziz Ali baba yake Dossa Aziz.

Contemporary wake ni Ali Jumbe Kiro, Hassan Machakaomo, Kleist Sykes, Ibrahim Hamisi, Abdallah Simba Liwali wa Songea, Ali Said Mpima, Sheikh Hassan na Hussein Juma, Nassoro Kiruka, Mzee bin Sudi na baadhi ya hawa nimewawahi na kuwaona kwa macho yangu.

Baadhi ya hawa wazee ni kutoka Batetera Union chama cha Wamanyema.

Paschal anaweza kuyajua mengine lakini si haya ya Dar es Salaam ya 1950s.

Unajua kwa nini Mzaramo Sheikh Said Chaurembo aliyekuwa Liwali Mahakama ya Kariakoo alijenga lile ghorafa lake Mtaa wa Msimbazi?

Kama unalijua gorofa la Mzee Rupia na hili la Sheikh Chaurembo utaona yamefanana.

Sheikh Chaurembo alijenga jumba lile kuweka heshima ya wenye mji wao.

Huyu Sheikh Chaurembo alikuwa katika TAA Political Subcommittee 1950 pamoja na Mufti Sheikh Hassan bin Ameir.
 
Yameshakuwa
Na wengine watakuja waseme Marealle alionewa...
 
Hizi ngonjera wengine hazitusumbui kabisa.
Kalamu1,
Hakika una haki ya fikra zako zonavyokuelekeza.

Ikiwa unaona nielezayo ni "ngonjera," kwangu ni sawa kwani wapo watu wananufaika na elimu hii.
 
Back
Top Bottom