Uhusiano kati ya kufa na pumzi kukatika ni kwamba pumzi ikikatika damu inakosa oxygen na rigor mortis ina set in. You don't need a soul there.
Umesoma mental conditions zote na kuzimaliza?
Hata hujaelewa swali unasema umelijibu mara kibao.
Wewe swali unalotaka kulijibu ni lile la kwa nini kuna maovu. Kwa mfano, kwa nini mungu anaachia watu wanakufa kwa UKIMWI. Explanation yako ni kwamba watu wenyewe ndio wanaofanya zinaa.Na hivyo ndio wanaojisababishia UKIMWI (ingawa hata hili jibu halitoshi, kwa sababu kuna watoto wadogo wanazaliwa na H.I.V bila ya kufanya zinaa yoyote)
Kwa hiyo tunaona kwamba, ingawa swali ulilojibu si nililouliza, hata hilo ulilojibu halijibu swali uliloamua kulijibu kikamilifu.
Umesema maovu ni matokeo ya matendo yetu, wakati wengine wanapatwa na maovu kabla hata hawajapata akili ya kutenda maovu wao useme yamewarudia kutokana na matendo yao.
Mtoto mdogo anapopatawa na mabaya anapatwaje na mabaya kwa makosa yake?
Lakini kama nilivyosema mwanzo, hili swali, ingawa umeliboronga, si lile nililouliza.
Swali nililouliza ni, je, pale mungu alipokuwa anauumba ulimwengu huu, kwa kuwa yeye ni mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na mwenye upendo wote, kwa nini hakuuumba ulimwengu ambao hauruhusu mabaya, hauruhusu maovu, kiasi kwamba hata huyo binadamu mnayemlaumu kwamba mabaya yanampata kwa sababu yeye anafanya mabaya asiweze kufanya mabaya in the first place?
Kwa sababu ukifikiria sana haya mambo, utajiuliza kwa nini binadamu anafanya mabaya?
Utasema, anafanya mabaya kwa sababu mbalimbali, malezi, DNA, ujinga, shetani etc. Kwa mujibu wa mapokeo yenu mnamuweka mbele sana shetani kama baba wa ubaya.
Lakini swali linakuja, huyu shetani katokeaje? Kajiumba mwenyewe au kaumbwa na mungu?
Kama kajiumba mwenyewe basi mungu si muumba vyote na muweza yote.
Kama kaumbwa na mungu, basi mungu ndiye katuletea huyu shetani, na alimjua atakavyokuwa hata kabla hajamuumba, kwa sababu kwa mujibu wenu mungu anajua yote.
Sasa kwa nini alikubali kumuumba huyu shetani wakati akijua kwamba huyu shetani ataleta mabaya duniani?
In fact I will go a step further back.
Kwa nini mungu, kabla ya kumuumba shetani, aliumba ulimwengu ambao shetani na mabaya yote yanayowezekana kufamnyika leo, yawezekane?
Kwa nini mungu hakuumba ulimwengu ambao zinaa na UKIMWI haviwezekani?
Alishindwa au hakutaka tu?
Kama alishindwa, basi si muweza yote.
Kama aliweza ila hakutaka tu, basi hana upendo hivyo, kwa sababu alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu usio na mateso, lakini hakuutumia.
Kwa nini huyu mungu wenu alipokuwa anaumba ulimwengu hakutaka kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kufanyika?