Sasa ukishawekewa hayo unayoyadai hapo juu kwa Akili yako ndiko kuna prove nini!??
Unataka kusema kuwa binaadamu ambae hajakutana na na uovu au ubaya LAZIMA Akubali kuwa MUNGU YUPO??
We una reasons kama mtoto wa miaka mitano!
IQ yako kijana bado saaana!
Umeishiwa mpaka uwezo wa kufikiri!
Hujajibu swali.
Na kwa kutojibu swali, unachoniambia ni kwamba wewe unayesema unajua mungu yupo na mimi nisiyekubali kwamba mungu yupo wote hatuwezi kumuelezea huyu mungu.
Bora yangu mie siwezi kumuelezea kwa sababu simkubali.
Wewe unayemkubali, excuse yako ya kushindwa kumuelezea ni nini?
Kwa nini mungu alivyoumba ulimwengu hakuuumba uwe hauwezi kuwa na mabaya?
Mnasema uwezo alikuwa nao (ana uwezo wote) ujuzi alikuwa nao (ana ujuzi wote) na pia ana upendo kwa viumbe vyake (ana upendo wote).
Sasa imekuwaje akaumba ulimwengu ambao unaruhusu viumbe wake wateseke?
Wengine hata hawajui chakula watapata wapi, wengine wana magonjwa ya ajabu hata kupumua tu shida, wengine wanauana kwa ujinga tu (kwa jina lake yeye mungu).
Kwa nini mungu ambaye ana uwezo wote, ukiwa pamoja na uwezo wa kuumba ulimwengu usio na uovu kaumba ulimwengu huu uliojaa uovu?
Sijaona jibu la swali hili.
Na kama huwezi kujibu swali hili, wewe na mimi hatuna tofauti kubwa.Tofauti yetu ni kwamba mimi nakubali huyu mungu ha make sense, wewe hukubali hata unaposhindwa kujibu maswali basic kabisa.
Post yako ulivyoiandika hapo unaonekana huwezi hata kuelewa swali nililokuuliza linalenga nini.
Wewe ni kama yule samaki aliyeishi maisha yake yote ndani ya maji, hata ukimwambia "wewe unaishi ndani ya maji, huko nje kuna bara lina jangwa, jangwa ni sehemu ambayo haina maji" atakuangalia kama mwehu na kukuuliza "maji ndiyo kitu gani hicho?".
Hujaelewa hata swali nililokuuliza mantiki yake ni nini.
Swali dogo tu, huwezi kujibu.
Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe ulimwengu wenye maovu kama huu?
Baba wa kibinadamu tu, asiye ujuzi wote, uwezo wote wala upendo wote, anataka awafanyie wanawe mazuri kwa kadiri ya uwezo wake.
Huyu mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote, upendo wote kwa nini kaumba ulimwengu ulio chini ya standards za baba wa kibinadamu anayetaka mazuri tu kwa wanawe?
Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe ulimwengu ambao mabaya na maovu yanawezekana?
Hujajibu swali.