Hitachukua miaka 100 kumpata mchezaji hatari kama huyu Tanzania

Smart codetz

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2023
Posts
218
Reaction score
875
Nchini Uganda 1990's katika daladala 10 za kubeba abiria basi 5 kati ya hizo zilikua na picha/jina LUNYAMILA. Moja kati ya vipaji vikubwa kuwahi kutokea katika historia ya mpira.

Kuna show aliwapiga Mamelodi Sundowns pale CCM KIRUMBA 2001 mpaka kocha anauliza huyu ni Mtanzania?

Mwaka 1997 wakati George Weah yupo kwenye ubora wake akiwa na tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia (96) pale Shamba la Bibi huyu Weah aliuliza Lunyamila anacheza ligi gani? FT : Stars 1-1 Liberia. Mwanasoka bora duniani hakuamini alichokiona kwenye miguu ya huyu kiumbe.
456DDFF5-8D70-4E8B-BCD0-9B300F54AFBC.jpeg
E0A05B51-CAD9-4DA1-B9C9-1DCD4BC2D8ED.jpeg
 
wachezaji hatari na wenye vipaji vikubwa Tanzania walikuepo wengi.
Wachezaji ni Wengi ila uwezo unatofautiana sana huyu jamaa alikuwa na kipaji kikubwa sanaa aliwaacha mbali wenzie mpaka wapo ambo awajifikia uwezo wa Lunyamila,mohamed mmachinga,chambua na Sunday manara ila Lunyama alikuwa hatar zaidi yao
 
wacha wee.

mimi sikubishii kwasababu wewe umepata kumjua zaidi Lunyamila.ila wachezaji wazuri walikuepo wengi.

Edibili Jonas Lunyamila.
Said Maulidi"smg"
Michael Paul"Nailoni"
Makumbi Juma"Bongabonga"
Khamis Thobias"Gaga"
Abdallah Kibadeni"King"
Zamoyoni Mogela.
Maulid Kambi"Mandemla"
Maulid Dilunga.
Twaha Masiment.
Kitwana Manara.
Saleh Zimbwe.n.k

👆hao ni baadhi tu ya wachezaji wenye vipaji vikubwa waliowai kutokea Tanzania,kila miaka inavyosogea vipaji navyo vinapotea tunabaki na wachezaji wakukaba na kukimbia tu ila kutoa pasi na kupokea pasi ni shida,kumiliki mpira shida basi ilimradi tu bola liende.
 
Nchini Uganda 1990's katika daladala 10 za kubeba abiria basi 5 kati ya hizo zilikua na picha/jina LUNYAMILA. Moja kati ya vipaji vikubwa kuwahi kutokea katika historia ya mpira.

Kuna show aliwapiga Mamelodi Sundowns pale CCM KIRUMBA 2001 mpaka kocha anauliza huyu ni Mtanzania? Mwaka 1997 wakati George Weah yupo kwenye ubora wake akiwa na tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia (96) pale Shamba la Bibi huyu Weah aliuliza Lunyamila anacheza ligi gani? FT : Stars 1-1 Liberia. Mwanasoka bora duniani hakuamini alichokiona kwenye miguu ya huyu kiumbe.
View attachment 2573855View attachment 2573857
malizia kwa kusema ni kati ya wachezaji wachache wa miaka hiyo ambao mpira haukuwatoa kimaisha.
 
yap kiukweli wengi wao mpira aukuwatoa ni kama walipoteza muda, ingawa pia wapo wachezaji wa kileo nao wapo hohehahe awana kitu wamefulia.
maisha hayana mwenyewe.
 
Edibily ilikua asajiliwe Simba lkn nahodha wa zamani wa Simba Ramadhani Lenny Maufi 'Abega' (RIP) alimwambia mfadhili wa wakati huo 1992Azim Dewji,"hiki kitoto bwana kiakimbia kimbia sana hakichezi mpira wetu!" Lunya hayo maneno alisikia wakati huo wakiwa kambini Timu ya Taifa Chuo Kikuu(UDSM) hapo Azim alikua anawasainisha George Masatu na Hussein Amani Masha!!

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Ilikua aende Simba,gulamali akapanda ndege kwenda kwa baba yake lunyamila,akamfungulia duka la spea za baiskeli akamtia na mkwanja,mtoto akatua jangwani
 
alitokea kwenye umiseta
Alisoma Buhangija Sekondari Shinyanga na kusajiliwa na Yanga moja Kwa moja akitokea Biashara ya Shinyanga ambayo aliichezea akiwa bado mwanafunzi wa Sekondari wakati rafiki yake Nteze John Lungu akichezea timu pinzani ya Kurugenzi Shinyanga na kusajiliwa Pamba kisha Simba.
 
Unambiwa yanga walimsubiri nje ya chumba cha mitiani , alipomaliza tuh akajiunga hii ni baada ya kumuona kwenye umiseta
 
Edibily ilikua asajiliwe Simba lkn nahodha wa zamani wa Simba Ramadhani Lenny Maufi 'Abega' (RIP) alimwambia mfadhili wa wakati huo 1992Azim Dewji,"hiki kitoto bwana kiakimbia kimbia sana hakichezi mpira wetu!" Lunya hayo maneno alisikia wakati huo wakiwa kambini Timu ya Taifa Chuo Kikuu(UDSM) hapo Azim alikua anawasainisha George Masatu na Hussein Amani Masha!!

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
Mnamsingizia Lenny, Lunyamila wakati anasajiliwa timu ya Taifa iliweka kambi Arusha Kwa wiki 2 na kumalizia Dar Kwa siku 4 za mwisho. Gari la Abbas Gulamali lilimchukua Lunyamila toka Buhangija Sekondari baada tu ya kumaliza mtihani wa form 4.
 
Nchini Uganda 1990's katika daladala 10 za kubeba abiria basi 5 kati ya hizo zilikua na picha/jina LUNYAMILA. Moja kati ya vipaji vikubwa kuwahi kutokea katika historia ya mpira.

Kuna show aliwapiga Mamelodi Sundowns pale CCM KIRUMBA 2001 mpaka kocha anauliza huyu ni Mtanzania? Mwaka 1997 wakati George Weah yupo kwenye ubora wake akiwa na tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia (96) pale Shamba la Bibi huyu Weah aliuliza Lunyamila anacheza ligi gani? FT : Stars 1-1 Liberia. Mwanasoka bora duniani hakuamini alichokiona kwenye miguu ya huyu kiumbe.
View attachment 2573855View attachment 2573857
Kitu cha kusikitisha kabisa na nakishuhudia mara kwa mara kwa macho yangu, Edibily Lunyamila tupo nae sana maeneo ya Mbezi kwa yusufu amechoka na hana uwezo wowote kifedha. Maisha yake yamekuwa ya kuungaunga kwa wadau. Amekuwa mlevi sana mtu wa kuombaomba bia kwenye mabaa. Kama ilivyo desturi ya wachezaji wa zamani kiukweli maisha ya Lunyamila yanasikitisha sana.
 
Halafu akaishia kucheza yanga , shida ilikuwa nini maana mchezaji kuishia kucheza yanga inafikirisha kama alikuwa mkali sana au machachari.
 
Nchini Uganda 1990's katika daladala 10 za kubeba abiria basi 5 kati ya hizo zilikua na picha/jina LUNYAMILA. Moja kati ya vipaji vikubwa kuwahi kutokea katika historia ya mpira.

Kuna show aliwapiga Mamelodi Sundowns pale CCM KIRUMBA 2001 mpaka kocha anauliza huyu ni Mtanzania? Mwaka 1997 wakati George Weah yupo kwenye ubora wake akiwa na tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia (96) pale Shamba la Bibi huyu Weah aliuliza Lunyamila anacheza ligi gani? FT : Stars 1-1 Liberia. Mwanasoka bora duniani hakuamini alichokiona kwenye miguu ya huyu kiumbe.
View attachment 2573855View attachment 2573857
Ni mwaka huo wa 1993 Yanga hii utopolo ilibeba kombe la vilabu Africa mashariki na kati. Hatari sana sana na mwaka huo huo Simba SC the football genius club tulifika final ya kombe la washindi la CAF hatari sana Azim Dewji aliuza mechi alihonga wachezaji kadhaa wetu ili tusibebe kombe asipate mzigo wa kutoa zawadi ya gari aina ya KIA muundo Kama wa canter za mizigo.
 
Kitu cha kusikitisha kabisa na nakishuhudia mara kwa mara kwa macho yangu, Edibily Lunyamila tupo nae sana maeneo ya Mbezi kwa yusufu amechoka na hana uwezo wowote kifedha. Maisha yake yamekuwa ya kuungaunga kwa wadau. Amekuwa mlevi sana mtu wa kuombaomba bia kwenye mabaa. Kama ilivyo desturi ya wachezaji wa zamani kiukweli maisha ya Lunyamila yanasikitisha sana.
Yanga kwan wasimpe hata kiasi kadhaa kumsitiri.
 
Ni mwaka huo wa 1993 Yanga hii utopolo ilibeba kombe la vilabu Africa mashariki na kati. Hatari sana sana na mwaka huo huo Simba SC the football genius club tulifika final ya kombe la washindi la CAF hatari sana Azim Dewji aliuza mechi alihonga wachezaji kadhaa wetu ili tusibebe kombe asipate mzigo wa kutoa zawadi ya gari aina ya KIA muundo Kama wa canter za mizigo.
Lile halikuwa Kombe la Washindi bali lilikuwa linaitwa Kombe la CAF ambalo kwa sasa limefutwa! Zama zile kulikuwa na Michuano ya Club Bingwa, Kombe la Washindi, na Kombe la CAF. Baada ya kufutwa Kombe la CAF likabaki Club Bingwa na Kombe la Washindi ambalo ndilo hivi sasa linaitwa Confederation Cup
 
Back
Top Bottom