Hitaji kubwa la Tanzania ni Katiba Mpya

Hitaji kubwa la Tanzania ni Katiba Mpya

Poa 2

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2019
Posts
1,317
Reaction score
1,320
Mikutano ya hadhara imeruhusiwa, japo ilizuiwa kinyemela na yule dikteta uchwara.

Raisi Samia yupo hapo kwa makusudi mema ya Mungu na kwa mujibu wa katiba japo kifungu hicho cha katiba hakina afya Tena kwa taifa lililo makini.

Hatupigi hatua kimaendeleo mpaka Sasa kwa sababu ya katiba mbovu Kila raisi anayeingia madarakani anakuja na vipaumbele vyake na wakati mwingine kutoendeleza miradi au mipango au vipaumbele vya mtangulizi wake, hili ni tatizo sana japo tunaliipuuza.

Huu ndio wakati mwafaka wa chama cha upinzani kuhubiri habari za katiba MPYA kwa nguvu na maarifa yenu yote, msituangushe tumewaamini sana.

Mungu awatangulie na kuwalinda mkafanye siasa safi yenye nguvu.

CCM imeshindwa kutuvusha watanzania mda wa mabadiliko ya kweli ni Sasa.
Elimu kubwa ilishatokewa kwa wanacpnchi kipindi cha mchakato wa kuipata mapendekezo/ Ukusanyaji wa maoni kwa Sasa wanachohitaji ujasiri wa viongozi katika kudai katiba Mpya.
La muhimu ni kwamba Katiba Mpya na nzuri haitapatikana kwa mazungumzo ya mezani.
CCM wanavuta mda tu kwa kichaka cha mazungumzo. Katiba Mpya na nzuri itapatikana kwa shinikizo na maandamano yaani nguvu ya imma.
Viongozi wa upinzani nguvu kubwa ni kuwashawishi wananchi kuandamana nchi nzima na wananchi wako tayari wanasubiri amri ya viongozi wao.
 
Hitaji kubwa ni shibe, watu waondolewa njaa ya chakula na kipato. Katiba isubiri
 
Hiyo katiba ataisimamia nani? au itajisimamia yenyewe?
 
Wanasiasa wamewaaminisha watu kwamba wanahitaji katiba mpya, ila sidhani kama ni kweli Watanzania wanahitaji hiyo katiba mpya. Kwani tulio nayo haifai kuongezewa vipengele vipya au kurekebisha vipengele vya sasa?

Hii nchi bana imekaa kimaslahi sana, kila mtu anapigania maslahi yake, wapinzani nao wana jambo lao kwenye huo mchakato. Mchakato wa zamani ulioanzishwa na Mh. Kikwete ulikwama kwasababu, wapinzani hawakufanikishiwa jambo lao la serikali tatu, hapo ndipo nilipojua hawa wapinzani sio watu wa kuwaamini. Rasimu ilikua na mambo mengi ya msingi lakini wakayakataa hayo yote kwasababu tu hoja yao ya serikali 3 haikupewa nafasi.

Hatuhitaji katiba mpya ispokua tunataka mabadiliko katika sekta ya elimu, ili vijana wetu waendane na kasi ya maendeleo ya sayansi na teknologia. Tunataka elimu iwaandae vijana wetu jinsi ya kujitegemea zaidi kuliko kuajiriwa, tunayaona mambo hayo yakitekelezeka chini ya uongozi huu. Hatutaki kua na maandamano kila kukicha, hatutaki vurugu na fujo zilizo chochewa na wanasiasa kwa ajili ya maslahi yao binafsi na vyama vyao.
 
Acha ujinga wa kutumia mawazo ya wanasiasa uchwara kijana. Hivi ni siku gani mtatumia akili zenu wenyewe?

Kila siku ni kudandia mawazo ya wanasiasa wenu hata kama mawazo yenyew hayana maana yoyote kitaifa.

Maendeleo ya nchi hayaletwi na katiba bali yanaletwa na uchapakazi wa wananchi husika, mipango madhubuti ya kuinua uchumi, elimu nk.

Malawi wana katiba nzuri tu, imewasaidia nini kuondokana na umasikini mkubwa waliokuwa nao?

Marekani wana katiba moja lkn kila raisi huja na sera zake. Mfano Trump kaja na sera za kufukuza wahamiaji na ku ban some countries, Biden kaachana na mikakati ya Trump badala yake kaja na sera ya vita vya Ukraine nk.

So kinachohitajika ni maono ya viongozi pamoja na wananchi kujua wajibu wao wa kufanyakazi kwa bidii, kulipa kodi nk. Sio ukae barabarani ukipiga zogo huku ukitegemea kuwa katiba mpya itakuletea ugali nyumban kwako.

Swala la katiba ni la wanasiasa ambao wanalengo la kupiga pesa kupitia vikao vya katiba.
 
Ngoja uvccm waje 🤣🤣🤣 hii kitu hawataki hata kuisikia!!! Utasikia bibi kule kijijin katiba mpya itamsaidia nn 🤣🤣🤣
 
hiyo katiba ataisimamia nani? au itajisimamia yenyewe?
Watasimamia watu hili ya Sasa ni ngumu kuisimamia kwa sababu Ina mianya inayoruhusu wachache kufanya chochote bika kuchukukiwa hatua
 
Wanasiasa wamewaaminisha watu kwamba wanahitaji katiba mpya, ila sidhani kama ni kweli Watanzania wanahitaji hiyo katiba mpya. Kwani tulio nayo haifai kuongezewa vipengele vipya au kurekebisha vipengele vya sasa?

Hii nchi bana imekaa kimaslahi sana, kila mtu anapigania maslahi yake, wapinzani nao wana jambo lao kwenye huo mchakato. Mchakato wa zamani ulioanzishwa na Mh. Kikwete ulikwama kwasababu, wapinzani hawakufanikishiwa jambo lao la serikali tatu, hapo ndipo nilipojua hawa wapinzani sio watu wa kuwaamini. Rasimu ilikua na mambo mengi ya msingi lakini wakayakataa hayo yote kwasababu tu hoja yao ya serikali 3 haikupewa nafasi.

Hatuhitaji katiba mpya ispokua tunataka mabadiliko katika sekta ya elimu, ili vijana wetu waendane na kasi ya maendeleo ya sayansi na teknologia. Tunataka elimu iwaandae vijana wetu jinsi ya kujitegemea zaidi kuliko kuajiriwa, tunayaona mambo hayo yakitekelezeka chini ya uongozi huu. Hatutaki kua na maandamano kila kukicha, hatutaki vurugu na fujo zilizo chochewa na wanasiasa kwa ajili ya maslahi yao binafsi na vyama vyao.
Umeandika kizuzu sana, sidhani kama zinakutosha
 
Unahitaji katiba mpya ili CCM ijifie wewe jamaa vipi?Hujui katiba mbovu ndio ponapona ya CCM kung'oka madarakani?
 
Unahitaji katiba mpya ili CCM ijifie wewe jamaa vipi?Hujui katiba mbovu ndio ponapona ya CCM kung'oka madarakani?
Tunahitaji kulikomboa taifa hili na ni lazima sisiem ife kwanza ndio ukombozi kamili uwadie
 
Watasimamia watu hili ya Sasa ni ngumu kuisimamia kwa sababu Ina mianya inayoruhusu wachache kufanya chochote bika kuchukukiwa hatua
kenya na afirka kusina wanakatiba nzuli sana lakini ufisadi mtindo 1 raiya wako hoi mtu mweusi hawezi kujiongoza
 
Back
Top Bottom