Katiba sio hitaji kubwa kwasababu uzuri au ubaya wa katiba unategemea haiba ya jamii ya watu wanaotumia katiba hiyo. Katiba ni maelezo/maneno yaliyo katika makaratasi tu. Kuitii au kutoitii hakutegemei kilichopo kwenye hayo maneno bali "quality" ya watu husika namna walivyo tayari kukubaliana na kilichomo.
Labda nikuulize, tukiichukua katiba ya Marekani kama ilivyo na kubadilisha kwenye US kuweka Tanzania, je Tanzania tutafanya mambo kama Marekani?
Nikuulize swali lingine. Sheria za usalama barabarani Tanzania zipo kwa kila mtumiaji barabara. Polisi ndio wanaosimamia sheria hiyo barabarani, na polisi Wana slogan yao, tii sheria bila shuruti. Je ushawahi kuona gari ya polisi ikaheshimu alama za barabarani? Ushaona gari ya polisi imekamatwa kwa kuvunja sheria za usalama barabarani? Katika jamii ya watu kama hao, katiba mpya itasaidia nini?
Hitaji kubwa kabisa kwa watanzania kwa Sasa ni madarasa mazuri na ya kisasa, walimu wa kutosha na motisha kwa walimu. Tukiliweza hilo hata kwa miaka 100, litakuwa na msaada sana kwani ni jamii hiyo itakayoweza kutengeneza na kuitii katiba, sio hii jamii ya vibaka kuanzia bodaboda hadi top guys.