Wanasiasa wamewaaminisha watu kwamba wanahitaji katiba mpya, ila sidhani kama ni kweli Watanzania wanahitaji hiyo katiba mpya. Kwani tulio nayo haifai kuongezewa vipengele vipya au kurekebisha vipengele vya sasa?
Hii nchi bana imekaa kimaslahi sana, kila mtu anapigania maslahi yake, wapinzani nao wana jambo lao kwenye huo mchakato. Mchakato wa zamani ulioanzishwa na Mh. Kikwete ulikwama kwasababu, wapinzani hawakufanikishiwa jambo lao la serikali tatu, hapo ndipo nilipojua hawa wapinzani sio watu wa kuwaamini. Rasimu ilikua na mambo mengi ya msingi lakini wakayakataa hayo yote kwasababu tu hoja yao ya serikali 3 haikupewa nafasi.
Hatuhitaji katiba mpya ispokua tunataka mabadiliko katika sekta ya elimu, ili vijana wetu waendane na kasi ya maendeleo ya sayansi na teknologia. Tunataka elimu iwaandae vijana wetu jinsi ya kujitegemea zaidi kuliko kuajiriwa, tunayaona mambo hayo yakitekelezeka chini ya uongozi huu. Hatutaki kua na maandamano kila kukicha, hatutaki vurugu na fujo zilizo chochewa na wanasiasa kwa ajili ya maslahi yao binafsi na vyama vyao.