JumaKilumbi
JF-Expert Member
- Sep 7, 2022
- 432
- 507
Katika uzi nilioufungua jukwaani hapa nilioutumia kuwaalika Atheists kuleta hoja za kuthibitisha kuwa Mungu hayupo ili tujifunze kuhusu misingi yao, wachache hawakunielewa kwa kudhani nilitaka mabishano, ila nimepata hitimisho lifuatalo
HITIMISHO LANGU;
Awali nilidhani Atheists wana hoja za kusikiliza linapokuja suala la Mungu, lakini nimegundua wao wamejawa mashaka, hawana majibu ila maswali ambayo wanayakataa majibu yake, wengi wanakariri hoja na hawako tayari kupokea mabadiliko.
Hivyo basi, ninaamini Mungu yupo kwa mujibu wa Quran aliyoletewa Muhammad (PBUH)
Nimalize kwa nukuu ya Profesa nguli Jordan B. Peterson
“You can only find out what you actually believe (rather than what you think you believe) by watching how you act. You simply don’t know what you believe, before that. You are too complex to understand yourself.”
Jordan B. Peterson
- Baadhi ya Atheists wanashindwa kuelewa Mungu huyu (kama atajavyo na Quran na Biblia) anawezaje kuwepo wakati sifa zake zinajikanganya. Mfano kuwa na hasira na kuwa na huruma, kuwa muweza wa vyote n.k
- Atheists hawana maelezo mbadala yanayokubalika juu ya asili ya Dunia hii na UIlimwengu kwa ujumla.
- Atheists baadhi wanatatizwa na uwepo wa matatizo hapa Duniani, hivyo wanaona Mungu muweza wa vyote hayupo. Kwa maana angekuwepo angeyaondoa haya matatizo
- Baadhi hawana uhakika juu ya uwepo wa Mungu wanataka kumjua zaidi lakini si kwa kupitia hizi ‘mainstream religion’ kwa maana kwao wanaona ni uzushi.
- Baadhi wamechanganyikiwa, wanashindwa kuielewa hata kidogo dhana ya Mungu.
- Atheists wengi wako ‘on offensive’ wanashambulia hoja za Waumini na unapowaweka mazingira ya kuwalazimu kuthibitisha hoja zao inakuwa mtihani.
- Atheists wengi hupata chochote cha kusema kwa kushambulia hoja za waumini Dini wengi wao hawana hoja ukiacha kushambulia za waumini Dini.
- Wachache sana ni wakweli, na wana fikra huru.