VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Watanzania tumezungumza. Tumezungumza kwa kauli zetu kalikali kama msumari na waziwazi kuliko utandawazi. Tumezungumza kupitia Wanasheria, Maprofesa, Maaskofu, Masheikh, Wanasiasa, Wasomi hadi wananchi wa kawaida. Tumeuzungumza mkataba wa DP World kuliko hata Bunge letu.
Tumeuzungumza makataba kwa kuukosoa-kulingana na vifungu vyake. Tumepuuza hoja zisizo na haja za viongozi wa kiserikali na kichama waliojaribu kututoa kwenye hoja. Tumewapuuza kwa kuendelea kutetea tunachokiamini na tulichokiona kimkataba.
Najua kuwa Serikalini na chamani anasakwa 'mchawi' wa jambo lote hili. Yule aliyetuwekea wazi Mkataba wa DP World na Tanzania juu ya Bandari. Ilipangwa jambo hili lifanywe kimyakimya. Liiishe kimyakimya. Baada ya kubumburuka na kuanza kujadiliwa, tunaambiwa kuwa tunatoa maoni na yatazingatiwa. Inashangaza!
Hadi sasa, pamoja na ukimya wa Rais na Mwenyekiti wetu wa CCM juu ya hili, hakuna kiongozi yeyote wa Serikali au CCM aliyajibu hoja za haja za wakosoaji wa mkataba. Nguvu kubwa imeelekezwa kwenye kuuaminisha umma kuwa uwekezaji Bandarini utaleta tija. Hoja zetu ni juu ya ubovu na ubatili wa mkataba. Hizo hazina majibu.
Ni rahisi kuhitimisha bila kutisha kuwa Mkataba wa DP World tumeukataa. Na mambo yake yote tumeyakataa. Kukosekana kwa ukomo na maslahi ya kimkataba tumekukataa. Maelezo ya Serikali na viongozi wa CCM tumeyakataa. Tunasubiri tupuuzwe sauti zetu ili tuchukue hatua zetu!
Rais na Mwenyekiti wangu Mama Samia, huna lolote juu ya Mkataba wa DP World la kutuambia?
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Igoma, Mwanza)