Ukimya nao ni jibu!.
Hoja karibu zote zimejibiwa
Ni kweli uwezaji wa DPW, utaleta tija.
It's true hoja za ubatili hazina majibu, ila hata kama kuna ubatili, IGA sio mkataba ni MoU tuu ya makubaliano kuiruhusu Tanzania kuingia mkataba na DPW. Mkataba ni HGA, utakuwa mzuri, japo kisheria, kukiisha tokea issues za ubatili, then ubatili huo unakuwa void ab initio, ila sisi huu ubatili wa mkataba huu tumeufanya kuwa ni ubatili wa voidable ambao unarekebishika.
Maadam wawakilishi rasmi wa Watanzania ni Bunge letu Tukufu, kama Bunge letu limeridhia, ni Watanzania tumeridhia.
Mfumo wetu wa utawala ni kupitia representation, Bunge letu ndio wawakilishi wetu, wakisema ndio, ni ndio, wewe Mwananchi huwezi kusema sio!. Itakubidi usubirie miaka 5, umfute kazi mwakilishi wako!.
Kilicho ridhiwa ni IGA, ni MoU ya makubaliano kuiruhusu Tanzania kuingia mkataba na DPW kutuendeshea Bandari zetu. Mkataba wa uendeshaji unaitwa HGA, hii HGA bado haijaingiwa, serikali yetu imepokea maoni ya Watanzania na itayajumuisha kwenye HGA, hivyo HGA itakuwa ni nzuri.
Sii kweli, sii yote, kuna mambo mengi, makubwa mazuri ya mkataba huu tumeyakubali, na machache mabaya wananchi tumeyakataa ila wawakilishi wetu, wabunge wetu na Bunge letu limekubali kila kitu.
Ukomo hauwepogi kwenye international treaties!, IGA ni MoU tuu sio mkataba, ukomo utakuwepo kwenye HGA ambayo ndio mkataba.
Mfumo wetu wa utawala ni spoon fed top down, serikali ikisema ni imesema, wewe Mwananchi huwezi kuikatalia.
Hata tukipuuzwa hatuwezi kuchukua hatua zozote zaidi ya kusubiria 2025 tuiadhibu CCM kwa kui vote out!. Hili pia haliwezekani kwasababu hata tukii vote out CCM, aje nani?, kwa vile hakuna mtu mbadala wa kuja, then tutaendelea na CCM mpaka atakapopatikana mbadala.
Mama anatakiwa kunyamaza kimya kabisa huku kazi nzuri ikiendelea.
P