Hitimisho: Mkataba wa Tanzania na Emirati ya Dubai kupitia DP World tumeukataa!

Ukimya nao ni jibu!.

Hoja karibu zote zimejibiwa

Ni kweli uwezaji wa DPW, utaleta tija.

It's true hoja za ubatili hazina majibu, ila hata kama kuna ubatili, IGA sio mkataba ni MoU tuu ya makubaliano kuiruhusu Tanzania kuingia mkataba na DPW. Mkataba ni HGA, utakuwa mzuri, japo kisheria, kukiisha tokea issues za ubatili, then ubatili huo unakuwa void ab initio, ila sisi huu ubatili wa mkataba huu tumeufanya kuwa ni ubatili wa voidable ambao unarekebishika.

Maadam wawakilishi rasmi wa Watanzania ni Bunge letu Tukufu, kama Bunge letu limeridhia, ni Watanzania tumeridhia.

Mfumo wetu wa utawala ni kupitia representation, Bunge letu ndio wawakilishi wetu, wakisema ndio, ni ndio, wewe Mwananchi huwezi kusema sio!. Itakubidi usubirie miaka 5, umfute kazi mwakilishi wako!.

Kilicho ridhiwa ni IGA, ni MoU ya makubaliano kuiruhusu Tanzania kuingia mkataba na DPW kutuendeshea Bandari zetu. Mkataba wa uendeshaji unaitwa HGA, hii HGA bado haijaingiwa, serikali yetu imepokea maoni ya Watanzania na itayajumuisha kwenye HGA, hivyo HGA itakuwa ni nzuri.

Sii kweli, sii yote, kuna mambo mengi, makubwa mazuri ya mkataba huu tumeyakubali, na machache mabaya wananchi tumeyakataa ila wawakilishi wetu, wabunge wetu na Bunge letu limekubali kila kitu.

Ukomo hauwepogi kwenye international treaties!, IGA ni MoU tuu sio mkataba, ukomo utakuwepo kwenye HGA ambayo ndio mkataba.

Mfumo wetu wa utawala ni spoon fed top down, serikali ikisema ni imesema, wewe Mwananchi huwezi kuikatalia.

Hata tukipuuzwa hatuwezi kuchukua hatua zozote zaidi ya kusubiria 2025 tuiadhibu CCM kwa kui vote out!. Hili pia haliwezekani kwasababu hata tukii vote out CCM, aje nani?, kwa vile hakuna mtu mbadala wa kuja, then tutaendelea na CCM mpaka atakapopatikana mbadala.

Mama anatakiwa kunyamaza kimya kabisa huku kazi nzuri ikiendelea.

P
Ni wapi imeandikwa kwenye uendeshaji wa bunge kuwa Bungeni watajadili na kuupitisha MoU? Ni wapi mkataba ukakeuka MoU? Kwanini wasirekebishe kwanza MoU ndo waendelee kwenye Contract kuliko kukaza fuvu kuwa watafanya marekebisho mwenye Contract.
Lakini pia unajichanganya mara unaliita mkataba mara siyo mkataba...ueleweki kama Wabunge wetu walivyo, nina imani ungefanikiwa kuwa Mbunge kwenye ile uchaguzi wa 2020 pia ungeunga hoja kwa kuiiita mkataba.
 
Mshangao ni kuwa, Makubaliano ndiyo ina uchafu kiasi hiki tena inazo karatasi zisizofika 50. Fikiria uchafu itakayokwepo kwenye mkataba yenyewe wenye vipengele mablimbali.
Hivi hao viongozi wa serikali hawawezi kujifungia ata ndani ya hotel nzuri kwa kodi zetu wakachata nyaraka sentesi kwa sentesi alafu wakaanza discussion na upande wa pili?

Kama wahusika hawana uwezo watafute basi watu smart wenye uwezo wa kuyapitia neno kwa neno...toafuti na hapo wameongwa tu bila shaka.
 
Watanzania tumezungumza. Tumezungumza kwa kauli zetu kalikali kama msumari na waziwazi kuliko utandawazi. Tumezungumza kupitia Wanasheria, Maprofesa, Maaskofu, Masheikh, Wanasiasa, Wasomi hadi wananchi wa kawaida. Tumeuzungumza mkataba wa DP World kuliko hata Bunge letu.

Tumeuzungumza makataba kwa kuukosoa-kulingana na vifungu vyake. Tumepuuza hoja zisizo na haja za viongozi wa kiserikali na kichama waliojaribu kututoa kwenye hoja. Tumewapuuza kwa kuendelea kutetea tunachokiamini na tulichokiona kimkataba.

Najua kuwa Serikalini na chamani anasakwa 'mchawi' wa jambo lote hili. Yule aliyetuwekea wazi Mkataba wa DP World na Tanzania juu ya Bandari. Ilipangwa jambo hili lifanywe kimyakimya. Liiishe kimyakimya. Baada ya kubumburuka na kuanza kujadiliwa, tunaambiwa kuwa tunatoa maoni na yatazingatiwa. Inashangaza!

Hadi sasa, pamoja na ukimya wa Rais na Mwenyekiti wetu wa CCM juu ya hili, hakuna kiongozi yeyote wa Serikali au CCM aliyajibu hoja za haja za wakosoaji wa mkataba. Nguvu kubwa imeelekezwa kwenye kuuaminisha umma kuwa uwekezaji Bandarini utaleta tija. Hoja zetu ni juu ya ubovu na ubatili wa mkataba. Hizo hazina majibu.

Ni rahisi kuhitimisha bila kutisha kuwa Mkataba wa DP World tumeukataa. Na mambo yake yote tumeyakataa. Kukosekana kwa ukomo na maslahi ya kimkataba tumekukataa. Maelezo ya Serikali na viongozi wa CCM tumeyakataa. Tunasubiri tupuuzwe sauti zetu ili tuchukue hatua zetu!

Rais na Mwenyekiti wangu Mama Samia, huna lolote juu ya Mkataba wa DP World la kutuambia?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Igoma, Mwanza)
Leo tarehe 14/07/2023 siku ya ijumaa,Waziri na Wanasheria wa Wizara ya Miundo Mbinu wametoa ufafanuzi wa mkataba kifungu kwa kifungu mbele ya vyombo vya habari.Nakuomba utafute maelezo hayo ili yakusaidie kujenga hoja yenye nguvu.Kwa hivi ulivyo-present bandiko lako,huna points,ni kama udaku tu.
 
Watanzania tumezungumza. Tumezungumza kwa kauli zetu kalikali kama msumari na waziwazi kuliko utandawazi. Tumezungumza kupitia Wanasheria, Maprofesa, Maaskofu, Masheikh, Wanasiasa, Wasomi hadi wananchi wa kawaida. Tumeuzungumza mkataba wa DP World kuliko hata Bunge letu.

Tumeuzungumza makataba kwa kuukosoa-kulingana na vifungu vyake. Tumepuuza hoja zisizo na haja za viongozi wa kiserikali na kichama waliojaribu kututoa kwenye hoja. Tumewapuuza kwa kuendelea kutetea tunachokiamini na tulichokiona kimkataba.

Najua kuwa Serikalini na chamani anasakwa 'mchawi' wa jambo lote hili. Yule aliyetuwekea wazi Mkataba wa DP World na Tanzania juu ya Bandari. Ilipangwa jambo hili lifanywe kimyakimya. Liiishe kimyakimya. Baada ya kubumburuka na kuanza kujadiliwa, tunaambiwa kuwa tunatoa maoni na yatazingatiwa. Inashangaza!

Hadi sasa, pamoja na ukimya wa Rais na Mwenyekiti wetu wa CCM juu ya hili, hakuna kiongozi yeyote wa Serikali au CCM aliyajibu hoja za haja za wakosoaji wa mkataba. Nguvu kubwa imeelekezwa kwenye kuuaminisha umma kuwa uwekezaji Bandarini utaleta tija. Hoja zetu ni juu ya ubovu na ubatili wa mkataba. Hizo hazina majibu.

Ni rahisi kuhitimisha bila kutisha kuwa Mkataba wa DP World tumeukataa. Na mambo yake yote tumeyakataa. Kukosekana kwa ukomo na maslahi ya kimkataba tumekukataa. Maelezo ya Serikali na viongozi wa CCM tumeyakataa. Tunasubiri tupuuzwe sauti zetu ili tuchukue hatua zetu!

Rais na Mwenyekiti wangu Mama Samia, huna lolote juu ya Mkataba wa DP World la kutuambia?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Igoma, Mwanza)
Uukatae wewe kama nani?
 
20141018_MAP004_0.jpg
 
Paskali Mayala nimeamini wewe ni mchumia tumbo, kuna kitu unahitaji wewe ni chawa mjanja mjanja na ndio maana Magufuli alikukataa hadharani tena kwa kukutolea maneno ya kejeli
 
Ukimya nao ni jibu!.

Hoja karibu zote zimejibiwa

Ni kweli uwezaji wa DPW, utaleta tija.

It's true hoja za ubatili hazina majibu, ila hata kama kuna ubatili, IGA sio mkataba ni MoU tuu ya makubaliano kuiruhusu Tanzania kuingia mkataba na DPW. Mkataba ni HGA, utakuwa mzuri, japo kisheria, kukiisha tokea issues za ubatili, then ubatili huo unakuwa void ab initio, ila sisi huu ubatili wa mkataba huu tumeufanya kuwa ni ubatili wa voidable ambao unarekebishika.

Maadam wawakilishi rasmi wa Watanzania ni Bunge letu Tukufu, kama Bunge letu limeridhia, ni Watanzania tumeridhia.

Mfumo wetu wa utawala ni kupitia representation, Bunge letu ndio wawakilishi wetu, wakisema ndio, ni ndio, wewe Mwananchi huwezi kusema sio!. Itakubidi usubirie miaka 5, umfute kazi mwakilishi wako!.

Kilicho ridhiwa ni IGA, ni MoU ya makubaliano kuiruhusu Tanzania kuingia mkataba na DPW kutuendeshea Bandari zetu. Mkataba wa uendeshaji unaitwa HGA, hii HGA bado haijaingiwa, serikali yetu imepokea maoni ya Watanzania na itayajumuisha kwenye HGA, hivyo HGA itakuwa ni nzuri.

Sii kweli, sii yote, kuna mambo mengi, makubwa mazuri ya mkataba huu tumeyakubali, na machache mabaya wananchi tumeyakataa ila wawakilishi wetu, wabunge wetu na Bunge letu limekubali kila kitu.

Ukomo hauwepogi kwenye international treaties!, IGA ni MoU tuu sio mkataba, ukomo utakuwepo kwenye HGA ambayo ndio mkataba.

Mfumo wetu wa utawala ni spoon fed top down, serikali ikisema ni imesema, wewe Mwananchi huwezi kuikatalia.

Hata tukipuuzwa hatuwezi kuchukua hatua zozote zaidi ya kusubiria 2025 tuiadhibu CCM kwa kui vote out!. Hili pia haliwezekani kwasababu hata tukii vote out CCM, aje nani?, kwa vile hakuna mtu mbadala wa kuja, then tutaendelea na CCM mpaka atakapopatikana mbadala.

Mama anatakiwa kunyamaza kimya kabisa huku kazi nzuri ikiendelea.

P
Mungu wangu paschal,unaandika haya ukiwa umelewa?Hivi mwanasheria aliyefuzu Sheria anaweza akaaandika maneno kama haya?[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]Hivi,huu upumbavu wa kutaka kuwaaminisha watu kuwa ccm ikitoka madarakani hakuna mbadala wake unatokana na nini?kiburi,ujinga au ulevi tu wa madaraka? Paschal,ukilewa usiwe unashika key board.Zingatia ushauri huu
 
Mungu wangu paschal,unaandika haya ukiwa umelewa?Hivi mwanasheria aliyefuzu Sheria anaweza akaaandika maneno kama haya?
Mkuu Mwami Ntale , sio tuu mimi ni mwanasheria niliyefuzu, LL.B yangu ni LL.B ya UDSM, na sio LL.B plain, ni LL.B (Hons)!, ila kusomea sheria na kufuzu ni one thing, na ku practice sheria kuwa a competent lawyer is quite another!.

Mimi nimesomea tuu sheria just for the love of it!, nimefuzu vizuri tuu, sasa ni mwanasheria na wakili ila sija practice, hivyo mimi as a lawyer, I'm not a competent lawyer at all!, in terms of law practice, but maandiko yangu..., kama unauwezo wa kusoma hoja za kisheria, angalia hoja zangu za kiisheria kuhusu DPW, Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee! kisha tafuta hoja za Prof. Shivji, na hoja za TLS, utanipa maua yangu!
Hivi,huu upumbavu wa kutaka kuwaaminisha watu kuwa ccm ikitoka madarakani hakuna mbadala wake unatokana na nini?
kiburi,ujinga au ulevi tu wa madaraka?
Kuna two types of people, the wishful thinkers and the realist. The wishful thinkers they just wish, some lives in utopia thinking wataamka one day wakute CCM haipo!.

The realist ni wale wanaokubali ukweli halisi uliopo hata uwe mchungu vipi!. Mimi ni realist, na nilisema Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!. kwasababu CCM sio tu ni chama tawala, bali pia ni chama Dola! na nikasema Wenye Matumaini na Upinzani Kushika Dola! Sahauni! CCM Inajiandaa Kuua Kabisa na Kuuzika Jumla
Paschal,ukilewa usiwe unashika key board.Zingatia ushauri huu
Asante sana, nitauzingatia, ushauri wako huu
Thanks.
P
 
Wangefanya demonstration hata ya kutoka huko kwny maandamano wanayoyahamasisha Kila siku tungeona kwli wanamaanisha....lakini wanabaki kubwekea tu hmu mitandaoni....halafu wanaposema watanzania wameukataa...ni lini ilipigwa hata kura kusema asilimia kubwa hawataki.....kiongozi wa dini au mwanasiasa kusema hataki au anakubali kitu flani haimaanishi amewasilisha mawazo ya watu woote anaowaongoza....kama Wana uchungu saana waingie barabarani kilazima alaf tuone...sio kubwekabweka Kila siku hmu ndani thread mpya Kila dakika
Unadhani ni kwanin ccm inatumia nguvu kubwa kuelimisha wananchi juu ya huo mkataba, kwani huo mkataba ndio wa kwanza?
 
Watanzania tumezungumza. Tumezungumza kwa kauli zetu kalikali kama msumari na waziwazi kuliko utandawazi. Tumezungumza kupitia Wanasheria, Maprofesa, Maaskofu,
Mmeukataa na nani. Sijakutuma unisemee. Jisemee mwenyewe. Hutulipii kodi ya nyumba.
 
Mkuu Mwami Ntale , sio tuu mimi ni mwanasheria niliyefuzu, LL.B yangu ni ya UDSM, na sio LL.B plain, ni LL.B (Hons)!, ila kusomea sheria na kufuzu ni one thing, na ku practice kuwa competent is another!. Mimi nimesomea, nimefuzu, ni wakili ila sija practice, hivyo mimi as a lawyer, I'm not competent at all!.

Kuna two types of people, the wishful thinkers and the realist. The wishful thinkers they just wish, some lives in utopia thinking wataamka one day wakute CCM haipo!.

The realist ni wale wanaokubali ukweli halisi uliopo hata uwe mchungu vipi!. Mimi ni realist, na nilisema Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!. kwasababu CCM sio tu ni chama tawala, bali pia ni chama Dola! na nikasema Wenye Matumaini na Upinzani Kushika Dola! Sahauni! CCM Inajiandaa Kuua Kabisa na Kuuzika Jumla

Asante sana, nitauzingatia,
Thanks.
P
Ila mda mwengine ukisoma sana unakuwa ..ma..y au mercenaries na mtumwa wa elimu. Sisi yetu macho maana akuna jambo lisilo na mwisho. # Pascal Mayalla vijana wa ......... 😂😂😂
 
Back
Top Bottom