Kama kuna kitu Magufuli kufanya uharibufu ndani ya hii miaka mitano, ni kwenye eneo la siasa. Leo hii hakuna anayehoji sera ama ilani ya chama chochote, bali watu wengi wanahoji nyomi! Kibaya zaidi udhaifu huu wa kuhoji nyomi unafanywa mpaka na wasomi. Yaani uimara wa chama kwa sasa haupimwi kwa utendaji, ilani ama sera, bali nyomi ndio uimara wa chama! Tulitegemea kuwe na midahalo ya nguvu kwenye TV, tuone watu wakitoa ufafanuzi wa ubora wa sera na ilani na jinsi ya kuzitekeleza. Lakini kwenye TV mjadala ni Simba na Yanga, na huku mitandaoni ni nyomi. Hakuna anayedili kwa kina kuhusu uchaguzi huu. Hili jambo ni aibu kubwa kama taifa.