Uchaguzi 2020 Hivi bado tunaamini nyomi kubwa kwenye mikutano ya kampeni ndio dalili za ushindi?

Bavicha ukiwaambia walete picha kama hizi wanakutukana matusi ya nguoni kabisa
 
Kwanini huu upuuzi wako haukuuandika juzi kwenye ufunguzi wa kampeni wa chama chakavu Pale Dodoma.
 
Mkuu unachosema ni kweli kabisa,nyomi ni kwaajiri tu ya kuvuguruga fikra za watu ili mtu aonekane anapendwa.Hii inatumiwa zaidi na CCM kwa sababu ni kibaya kinachojitembeza,wako tayari wawatoe watu Moro,pwani na Lindi ilimradi tu waonekane wanaungwa mkono na wanapendwa sana Dar.pesa na nguvu wanayoitumia kujaza watu hilo kwao si issue,issue ni uwanja ujae waonekane wanapendwa.Mambo ni mabaya zaidi kwa huyu incompetent wao magu
 
Mkuu hapa JF wewe ni mmoja wa watu nasoma sana michango yako mbona unajishusha kwa hii comment. Tulia kaa chini soma between the lines nlichoandika uone kama utakuja na hii conclusion yako.
Dah samahani sana! Yaishe tuendelee na mjadala wetu! Shukrani kwa kusoma michango yangu!
 
CCM na Tume ya Uchaguzi, upenda kuwaadaa watu kwamba wanaenda kwenye mikutano ya wapinzani huwa hawapigi kura. Hii siyo kweli kwa sababu;
1. Awamu ya pili ya Kikwete, watu wengi walienda kwa Slaa na awamu hiyo Slaa alishinda lakini referee ambaye ni mchezaji mahiri wa CCM(Tume) alikipa chama cha CCM ushindi.
2. Mwaka 2015 watu wengi walienda kwenye mikutano ya Lowassa, Lowassa alimgaragaza Magufuli tena by far, lakini kama kawaida referee akafanya yake.
This time around, Tume inahaha sana sababu imeanza gundua kwamba tunamaanisha tunaposema sasa basi.
 
Nyomi zikiwa Chadema mnatuletea changanuzi mfu? Mbona ya magufuli hamsemi hayo mnayosema kwa TL, Kwa kawaida wingi wa watu ni ishara ya kukubalika. Vyama vya TLP,CUF,NCCR nk umeshawai kushuhudia wakiwa na nyomi la watu?
 
Kisiasa, hasa siasa za kampeni nyomi ni propaganda muhimu kuwa nayo.
Nyomi ni dalili za mwanzo za chama kukubalika mbele ya wapiga kura.
Kwa kutambua umuhimu wa nyomi ndiyo maana baadhi ya vyama hukodisha magari ili kusafirisha wafuasi wake kuhudhuria kwa wingi mikutano yao.
Kwahiyo si jambo jema kuwakatisha tamaa wafuasi wanaojazana kwenye mikutano ya vyama vyao
 
Kwakipindi hiki cha kutoa faraja kwa baadhii ya wagombea, nimuhimu saana watuwajitokeze kwa wingiiii, bila kufanya hivyokunawatendewa miujizaaa hali itakua mbaya zaidiiiii.
Huku kungine tunapewa book tano si haba angalau mtu akirudi home ananunua kauzu
 
It’s official Dar Es Salaam is the first swing vote region in Tanzania, maana yake nini? wapiga kura wengi wameelimika zaidi na wenye kuangalia maslahi kwa uhalisia.

Wakati wa Lowassa ilikuwa yeyote kwao bora kuliko CCM. Leo upepo umebadilika Magufuli wanamwelea kweli.

Hakuna mtu mwenye akili zake Dar atapoteza kwenda kusikiliza ahadi za mishahara, kulipa mafao na upuuzi mwingine anao ongelea Lissu wakati bado budgeting ‘limiting factor’ ya makusanyo ipo pale pale.

Ni huko mikoani ndio kuna watu wanaweza amini upuuzi anao ongea Lissu.
 
Huku kungine tunapewa book tano si haba angalau mtu akirudi home ananunua kauzu
Nimatumiziii tyuuuu. Bora ataizooo buku tano tunakula kuliko kukiki za kufanya miujiza na kujiumiza bureee, ilikutafuta huruma na uraisi uwekifuta machozii.
 
Nimatumiziii tyuuuu. Bora ataizooo buku tano tunakula kuliko kukiki za kufanya miujiza na kujiumiza bureee, ilikutafuta huruma na uraisi uwekifuta machozii.
Mkuu sijakuelewa.hata hivyo mkuu kwangu Mimi katiba mpya ni kila kitu na kwa sababu hiyo Lissu ana kura yangu same way nilivyompa Lowassa.Na ikitokea vurugu za kuitoa ccm kwa nguvu Mimi nitakuwemo humo
 
Mkuu sijakuelewa.hata hivyo mkuu kwangu Mimi katiba mpya ni kila kitu na kwa sababu hiyo Lissu ana kura yangu same way nilivyompa Lowassa.Na ikitokea vurugu za kuitoa ccm kwa nguvu Mimi nitakuwemo humo
Hongera saaanaa mfarijiiiii. Tena akiona apamtandaoni umesema utampa kuraa, atatengamaaa zaidiii. Endeleeni kumfarijiii, tena jitokezeni kwa wingiii.
 
Nyomi zikiwa Chadema mnatuletea changanuzi mfu? Mbona ya magufuli hamsemi hayo mnayosema kwa TL, Kwa kawaida wingi wa watu ni ishara ya kukubalika. Vyama vya TLP,CUF,NCCR nk umeshawai kushuhudia wakiwa na nyomi la watu?
Hata nyomi za ccm hazina tija. Watu wanaenda kuangalia wasanii wakitumbuiza. Au kumuona Raisi. Nani asiependa kumuona Raisi wake. Hata wewe unamchukia Magu ila akija kwako kukusalimia utato meno kama yote.
So swala la nyomi uwingi wake sio tija kwa chama chochote kiwacho
 
Mkuu umeongea point sana kuliko wachangiaji woote. Ilaaa.... Lau kama nyomi ilikua factor zile kura zetu tulizompa lowasa zisingeenda kiduwanzi. Yule mzee alikua akijaza aisee. Halafu hata kuongea hawezi kachokaaa.
 
Kwanini huu upuuzi wako haukuuandika juzi kwenye ufunguzi wa kampeni wa chama chakavu Pale Dodoma.
Mkuu hii mada inapiga kote kote. Sijasema mimi ni sisiem lkn. Au nimesema? Au hiyo kumtaja lowasa?!
 
Huku Dom juzi yalipita mabasi yamebeba nyomi kutok kibaigwa huko sijui huko vijiji gani kuja kumwagwa Hapo Jamuhuri
 
Mkuu hii mada inapiga kote kote. Sijasema mimi ni sisiem lkn. Au nimesema? Au hiyo kumtaja lowasa?!
Ukichunguza kwa makini utagundua kuwa toka Lissu arudi nchini tabia ya mh Jiwe ilibadilika ghafla; akawa mpoleeeeee.

Huyu jamaa atakuwa mpole zaidi akienda Bukoba kwa Wahaya kuomba kura!! Akidhania wamesahau matusi aliyowatukana baada ya tetemeko.
 
Kama kuna kitu Magufuli kufanya uharibufu ndani ya hii miaka mitano, ni kwenye eneo la siasa. Leo hii hakuna anayehoji sera ama ilani ya chama chochote, bali watu wengi wanahoji nyomi! Kibaya zaidi udhaifu huu wa kuhoji nyomi unafanywa mpaka na wasomi. Yaani uimara wa chama kwa sasa haupimwi kwa utendaji, ilani ama sera, bali nyomi ndio uimara wa chama! Tulitegemea kuwe na midahalo ya nguvu kwenye TV, tuone watu wakitoa ufafanuzi wa ubora wa sera na ilani na jinsi ya kuzitekeleza. Lakini kwenye TV mjadala ni Simba na Yanga, na huku mitandaoni ni nyomi. Hakuna anayedili kwa kina kuhusu uchaguzi huu. Hili jambo ni aibu kubwa kama taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…