Hivi Bongo Movie kuna mtu ana elimu ya kiwango cha shahada(Degree)?

Macelebrity wa Bongo wote mwenye elimu ni Le mbebez tu, ye alisomea uinjinia wa meli.
 
Mzee CHILO ana digrii ya dini CHUO KIKUU CHA KIISLAMU MADINA
Ha[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
David Otunga huyu km nampata hiv alikuwa WWE baadae nikamuona anatangaza na sasa sijui yuko wapi.
Bongo movie kitambo sana sijawahi kuangalia sbb za movie zao hazieleweki. Sijajua mkuu ngoja waje watazamaji
Sio ndio yule self proclaimed "punga" kweli?
 
Wewe na hiyo degree yako ni kipi cha maana umekifanya kinaachoweza kukutofautisha na wengine wenye taaluma kama yako angalau Barani Afrika?!

Let's assume kuajiri mfanyakazi ingekuwa ni rahisi kama ku-download/pirate movie! Now, let's assume wewe umewekwa kundi moja na Wakorea, Wamarekani, Wahindi na Wachina na wote gharama zenu ni sawa!

Hivi unaamini kabisa huyo mwajiri wako angekuajiri wewe na kuwaacha hao wengine?!

Watu kama nyinyi hamna lolote zaidi ya ulimbukeni wa elimu! Miongoni mwenu kuna walimu lakini wanafunzi kila siku wanafeli pamoja na degree zao... sasa tofauti yao ni ipi na hao Bongo Movie?!

Wengine ni Wanasheria na Mawakili lakini bado wana historia mzuri ya kushindwa kesi... sasa wana tofauti gani na hao Bongo Movie?!

Wengine ni mabwana shamba na mabwana mifugo lakini sekta ya kilimo bado inazorota... so, what's the difference?!

Ni sekta ipi Tanzania hii miongoni mwa hizo sekta mlizojaa wasomi ambazo mnaweza kupita kifua mbele kwamba mpo very successful kulinganisha na nchi zingine duniani au angalau hata Afrika?!

UDSM ndicho the best university in the country! But by academic ranking, hakipo hata miongoni mwa Top 30 Africa... sasa na wenyewe wana tofauti gani na Bongo Movie?!

Now assume access to universities ingekuwa as simple as accessing a variety of movies in the internet... nani angeenda kusoma UDSM, SUA, Mzumbe n.k?!

Ni ushamba na ulimbukeni kujaribu kukashifu kundi la hustlers kwa kutumia kigezo cha elimu wakati inafahamika wazi nchi hii hapajawahi kuwa na formal education in film production!
 
culture gal,

Degree za Uigizaji zipo sana lakini tatizo ni kwamba zinapatikana nje ya nchi sawa na film production kwa ujumla. Na hapa ndipo Watanzania tunaposhindwa kuelewa! Leo hii mtu anaweza kuringa kwamba ana degree ya sheria na kumkashifu Bongo Movie asiye na degree!!!

Anachosahau ni kwamba, wakati yeye hiyo degree yake ya sheria ameipata hapa hapa nchini tena kwa pesa za serikali, kwa upande mwingine hapakuwa na degree ya film production/acting (sina hakika kama sasa zipo) na matokeo yake watu wanalazimika kutumia vipaji vyao peke yao!!

Wanasahau kwamba, kama serikali isingekuwa inatoa hizo degree za sheria, ualimu, uhasibu, uchumi hapa hapa nchini basi hata na wao wenyewe leo hii wangekuwa ni sawa na hao Bongo Movie kwa sababu, ni wachache tu wangekuwa na ubavu wa kwenda kusoma nje!

Na ukweli huu unaweza kuonekana kwa wazee wetu wengi ambao zamani walikuwa wanaajiriwa wakiwa ni darasa la saba tu kwa sababu serikali haikuwa na uwezo wa kutoa elimu ya juu kwa wengi. Hiyo ni kama ambavyo hata baada ya miaka kadhaa baadae serikali iliposhindwa kutoa elimu kwenye fani za film production kwa sababu bado hazijawa kipaumbele!

Kwahiyo suala la film production and acting ni tatizo la kisera zaidi kuliko kuona ni tatizo la Wasanii waBongo Movie.

Film Production ni taaluma ambayo watu wanatakiwa kupata formal education na vyuo vyake ni very expensive.

Lakini vile vile kuwakejeli Bongo Movie ni kushindwa kuchungulia makalio yetu wenyewe!! Hata hawa wanaoringa na degree zao kwenye sekta zingine, wala hakuna cha kutisha wanachofanya kwenye maeneo yao ya kazi. Ndo vile tu majority kazi zao hazihitaji ubunifu wowote zaidi ya kurudia rudia kile kile walichofanya jana na mwaka jana kitu ambacho ni tofauti na filamu! You always, have to come with something new!
 
hapo kwenye red, that's why we say mwende shule kabla ya kuanza kuigiza. ni ranking ya wapi Africa, na mwaka gani ambayo udsm haipo ndani ya 30s? wakati kuna kipindi ilishashika nafasi ya 11 Africa, vyuo 9 vikiwa vyote vya Africa kusini, kimoja Misri na kingine somewhere kama sikosei. go to school bro ndio urudi kuigiza.
 
Tunashukuru hata kama hawana elimu ya juu, lkn wanaedesha maisha yao
 
Tunashukuru hata kama hawana elimu ya juu, lkn wanaedesha maisha yao
lakini kile wanachoigiza ujue wanahamishia kwenye maisha halisi ya watoto wa kitanzania. wao ni kioo cha jamii. wajifunze kwa wenzao wa Nigeria, wanaigiza lakini wana degree.
 
Emmanuel Myamba "Pastor Muyamba" ni mhitimu wa Degree ya Sociology pale UDSM mwaka 2009.
 
Emmanuel Myamba "Pastor Muyamba" ni mhitimu wa Degree ya Sociology pale UDSM mwaka 2009.
yaani degree za kutafutiza?hahahaha, siwacheki kwasababu hawajasoma, kwasababu hata mimi nimesoma kwa neema ya Mungu tu kulingana na uchumi wa familia yangu ulivyokuwa....lakini hawa bongo movie wanapata hela nyingi tu lakini hawataki hata kujiendeleza. wametia aibu sana kweney script zao wanazotafsiri toka kiswahili kwenye kiingereza, ni aibu tupu, na wana hela lakini hawataki hata kuajiri mtu anayejua lugha awasaidie, kila kitu anafanya mtu mmoja, mmiliki wa movie, kuanzia director hadi mwigizaji, hani msanifu..everything. na movie moja inakamilika ndani ya miezi mitatu. wanakuambia ndani ya mwaka mmoja wanao uwezo kutengeneza movie tatu (kwa jinsi wanavyoona wanafanya kazi kwa bidii), wakati marekani movie moja inatumia miaka kadhaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…