Hivi Bongo tunasoma ili iweje?

Mfumo wa elimu wa Tanzania sio mbaya kama jinsi wengi wanavyoutizamia, tatizo lipo kwa wananchi na wanafunzi wenyewe ambao hawataki kusoma vitu vinavyoendana na mazingira ya nchi, mfano utakuta mwanafunzi anataka akasome Coz itakayompatia sifa mtaani na kwa ndugu zake badala ya kumpatia ajira, mfano wengi wanataka wasome Human Resources management wengine usafirishaji wengine wasome Sheria wengine social administration wengine civil engineering wengine uhandisi ambapo hizi ni coz ngumu kupata ajira au kujiajiri, Ila Tanzania ni nchi yenye rasilimali nyingi za asili mfano rasilimali watu, rasilimali ardhi, rasilimali maji, rasilimali madini na mbuga za wanyama pamoja na vivutio vingine vya utalii sasa kwanini wanafunzi wasichague coz kuendana na rasilimali zilizopo mfano kilimo, ufugaji, utalii, madini, na uvuvi pamoja na ujasiriamali?
Kwanini tusiende kwenye vyuo vinavyotoa coz ya kuchakata malighafi na kuzalisha Bidhaa ili kujiajiri wenyewe na kujikwamua kiuchumi kwasababu kilimo kipo nchini, na kwanini tusome Coz ambayo utategemea kuajiriwa tu ndy uone matunda ya elimu yako.

Watanzania tuache kuatafuta sifa mitaani tuonekane tumesoma vitu vikubwa ingawa ni vitu visivyo na tija, cha muhimu tutafute elimu yenye tija tukipata nafasi ya kusoma ili tuache kuilaumu serikali kwa ujinga wa watu wenyewe na ukiritimba uliotujaa vichwani wa kusoma ili tupate ajira maofisini huo ni kudumisha ukoloni akilini mwetu.
 
Nyerere ndo chanzo cha ujinga na elimu duni, isipo kua alikua anayaongea ongea nyerere alikua kiongozi mnafiki sanaa alipotezea baba zetu mda na ujinga wake wa ujaama.
Huwezi mlaumu nyerere hivyo hata wewe ungepewa nchi katika hali iliyokuwepo kwa wakati ule usingeweza kufanya kitu tumpe heshima yake alikuwa mbunifu kutumia wachache walioelimika katika kuiongoza nchi, ujinga wamekuwa nao wananchi wa Tanzania wa miaka ya hivi karibuni ambapo wasomi ni wengi na wanashindwa kubadili kitu cha aina yoyote wanabaki kuwa wanafiki kwa waliokosa nafasi ya kusoma,

Wasomi wa Tanzania ni wasaliti wengi wakiwa mtaani wanaongea vya mana kweli ila wakishapata nafasi serikalini hawazungumzi wala hawahoji kitu wala hawaleti mabadiliko yoyote ispokuwa wanageuka chawa wa raisi ili wazidi kupata nafasi za juu na kupata mishahara minono tu. Nyerere ni Baba na babu wa taifa la Tanzania hilo halipingiki na heshma yake itakuwepo milele.
 
Njia pekee ya kudhibiti embezzlement of the public funds ni kuwalipa viongozi kwa mfumo wa asilimi %.

Yaani kwa mfano kwa taifa zima kabla ya kuandaa bajeti ya mwaka wa fedha kuandaliwe malengo ya Taifa zima kwa ujumla ndani ya huo mwaka, alafu kila wizara ipewe jukumu la kutimiza lengo la taifa ndani ya huo mwaka kufuatana na dira ya taifa, alafu kila wariziri wa wizara husika awe na report maalumu ya utendaji wa utekelezaji wa wizara husika itakayosaidia kujua asilimia za utekelezaji wao kulingana na asilimia walizopatiwa na Taifa.

Mfano kwa mwaka wizara ya elimu inatarajia kujenga shule 1000 kuajiri asilimia 50% ya salimu na kufaulisha kwa asilimia angalau 89% kwa mwaka na inapaswa kuhakikisha yote waliyoagizwa yanatimizwa na kama ikishindwa kutimiza basi zinaangaliwa asilimia walizofanikiwa kuzifikia hapo ndio tunapata asilimia za kutoa mishahara.

Hapo kila waziri mwenye dhamamana angehakikisha wizara yake inafanya kazi kwa umakini ili kufikia malengo na asilimia kubwa ya utekelezaji ili kulinda kiwango cha mishahara yao.

Maana wakitekeleza kwa asilimia ndogo mshahara wao nao unakuwa mdogo.
 
Ni mfumo wetu mbovu ndgu yangu.

Imagine mtu mpaka anafika form 6 hajui hata anasoma ili uweje, ikifika siku anatakiwa kuchagua course ya kusomea chuo. Anachagua ile anayohisi atapewa mkopo kirahisi.

Ingelikua walau mtu akiwa o-level basi anaanza kuspecialize kwenye jambo fulani.
 
Wanafunzi wenyewe hawa wanakuja kuuliza kozi inahusu nini jamii forum na search engine na website za vyuo zipo kazi ipo
 
Wanafunzi wenyewe hawa wanakuja kuuliza kozi inahusu nini jamii forum na search engine na website za vyuo zipo kazi ipo
Ndio kazi za mitandao hiyo mkuu, sasa wamuulize nani na wao hizo course hawazijui na nyingi hata kuzisikia hawajawahi
 
Hii hii elimu, na mapungufu yake yote,lakini imetoa ma injinia, mafundi kibao, wamejaa Vodacom, Tigo, Airtel, ttcl,migodini, na wana maisha mazuri tu, (nimefanya kazi hizo sekta kwa miaka 15),
Wengine walistaafu, walifungua makampuni makubwa tu yametoa ajira Nyingi kwa vijana, kampuni kama BV engineeeing, Horizon, zimejengwa na vijana waliosoma hapa bongo, tena st kayumba, kwa uzoefu wangu TZ hakuna fulsa, serikali na sekta binafsi haziwezi kuajili waalimu wote, wahandisi wote, ma dokta wote, mafundi wote, sekta yetu ya manufacturing ni ndogo Sana, ukiacha viwanda vya wahindi vya nguo, hakuna kiwanda chenye kuzalisha bidhaa za ki tekinolojia kama tairi za gari, vipuri vya magari, electronics goods nk,
Sehemu pekee kijana kutoka chuo, ataweza kutengeneza maisha na kuishi vzr, ni migodini, makampuni ya simu,
Sasa cha kufanya, kwa vijana tafuta degree yako, lakini kichwani weka kabisa kuwa wewe ni raia wa dunia, ukishindwa kupata issue bongo, kwea pipa nenda nje(sio Kenya huko, nao wana shida kama zetu).
Jifunze kizungu vzr, sio hiki cha kuombea maji, namaanisha kile chenyewe,kama wanavyobonga Kenya na Uganda,
Tafuta passport, kwea pipa, omba hata uraia huko nje,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…