Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mfumo wa elimu wa Tanzania sio mbaya kama jinsi wengi wanavyoutizamia, tatizo lipo kwa wananchi na wanafunzi wenyewe ambao hawataki kusoma vitu vinavyoendana na mazingira ya nchi, mfano utakuta mwanafunzi anataka akasome Coz itakayompatia sifa mtaani na kwa ndugu zake badala ya kumpatia ajira, mfano wengi wanataka wasome Human Resources management wengine usafirishaji wengine wasome Sheria wengine social administration wengine civil engineering wengine uhandisi ambapo hizi ni coz ngumu kupata ajira au kujiajiri, Ila Tanzania ni nchi yenye rasilimali nyingi za asili mfano rasilimali watu, rasilimali ardhi, rasilimali maji, rasilimali madini na mbuga za wanyama pamoja na vivutio vingine vya utalii sasa kwanini wanafunzi wasichague coz kuendana na rasilimali zilizopo mfano kilimo, ufugaji, utalii, madini, na uvuvi pamoja na ujasiriamali?Wakuu habari,
Hivii Tanzania tuna soma ili iweje.Mataifa yote duniani elimu inatumika kumkomboa mwananchi kutoka mazingira duni na kuyaboresha , kuyatawala mazingira na si mazingira kumtawala mwanadamu.
Hapa nyumbani tuna baadhi ya vyuo venye kozi mbali mbali ambazo kwa macho ya nyama unaona zina tija lakini katika hali halisi vijana wanalalamika ajira hamna.
Na Wakati ajira zikionekana amna kuna utitiri wa mazao na rasilimali zinazolishwa Tanzania na kuuzwa njee kama malighafi na si bidhaa, nashindwa kuelewa sasa kama tuna wanafunzi wanaograduate kila siku na still amna innovations zinazotokana na elimu hizo au adaptation ya teknolojia kutoka nje ili kuongeza thamani malighafi zetu za ndani na ziuzwe njee kama bidhaa kamili sasa tunasoma na kutoa ela ndefu kwenye mikopo ili iweje?
Tanzania inajikuta katika changamoto kubwa za elimu na ajira, huku vyuo vikuu vikitakiwa kuwa injini ya mabadiliko ya kijamii na kiuchumi.
Hali hii inakinzana na dhima ya elimu duniani, ambayo ni kumkomboa mwananchi kutoka kwenye umaskini na kuboresha mazingira yake.
Vyuo vikuu nchini vinatoa kozi mbalimbali, lakini vijana wanalalamika kuhusu ukosefu wa ajira, wakati huo huo kuna utitiri wa malighafi zinazozalishwa Tanzania na kuuzwa nje kama malighafi tu, bila kuongeza thamani.
Kuna haja kubwa ya kubadilisha mfumo wa elimu ili kuchochea uvumbuzi na teknolojia, na kuongeza thamani ya malighafi za ndani ili ziuzwe nje kama bidhaa kamili.
Kutoa mikopo kwa wanafunzi ni hatua nzuri, lakini inapaswa kuelekezwa kwa njia ambayo itawawezesha kuanzisha miradi yao wenyewe na kuchangia katika maendeleo ya jamii.
Walimu wanapaswa kuwa mifano inayotoa mabadiliko ya kijamii, na elimu inayotolewa inapaswa kuhamasisha ujasiriamali na uvumbuzi.
Ni muhimu kuanzisha vituo vya uvumbuzi ndani ya vyuo vikuu ambavyo vitakuwa kazi yake kuvumbua majawabu ya changamoto za jamii kupitia wanafunzi wa taaluma husika.
Wanafunzi wanapaswa kupata fursa ya kutumia elimu yao kuleta mabadiliko katika jamii kwa kubuni suluhisho za changamoto za kitaifa na kimataifa.
Vyuo kama vile Chuo Kikuu cha Dodoma na Dar es Salaam vinaweza kuwa kiongozi katika kuleta mabadiliko ya kielimu na kijamii.
Elimu inapaswa kuwa chanzo cha tija na maendeleo, na wanafunzi wanapaswa kufundishwa kwa namna inayowawezesha kuwa nguvu ya mabadiliko katika jamii zao.
Tunapaswa kuwa na mtazamo mpya wa elimu na kuhakikisha inatoa thamani halisi kwa jamii yetu. Hii ndiyo njia ya kufikia lengo la kusoma ili kuwa na mabadiliko ya kweli nchini Tanzania na kuwa na vyuo vikuu vinavyochochea uvumbuzi na maendeleo endelevu..
Huwezi mlaumu nyerere hivyo hata wewe ungepewa nchi katika hali iliyokuwepo kwa wakati ule usingeweza kufanya kitu tumpe heshima yake alikuwa mbunifu kutumia wachache walioelimika katika kuiongoza nchi, ujinga wamekuwa nao wananchi wa Tanzania wa miaka ya hivi karibuni ambapo wasomi ni wengi na wanashindwa kubadili kitu cha aina yoyote wanabaki kuwa wanafiki kwa waliokosa nafasi ya kusoma,Nyerere ndo chanzo cha ujinga na elimu duni, isipo kua alikua anayaongea ongea nyerere alikua kiongozi mnafiki sanaa alipotezea baba zetu mda na ujinga wake wa ujaama.
Njia pekee ya kudhibiti embezzlement of the public funds ni kuwalipa viongozi kwa mfumo wa asilimi %.Hapa waziri ana masters anafumaniwa akiwa na hawara na mke wake wanatoroka akiendesha gari la serikali kodi yetu. Anapata ajali na kumuua hawara. Cha kushangaza second in command anamtembelea hospitalini kumpa pole. Amepona na amerudi kazini na kupwa lC300 nyingine mpya.
Wanafunzi wenyewe hawa wanakuja kuuliza kozi inahusu nini jamii forum na search engine na website za vyuo zipo kazi ipoNi mfumo wetu mbovu ndgu yangu.
Imagine mtu mpaka anafika form 6 hajui hata anasoma ili uweje, ikifika siku anatakiwa kuchagua course ya kusomea chuo. Anachagua ile anayohisi atapewa mkopo kirahisi.
Ingelikua walau mtu akiwa o-level basi anaanza kuspecialize kwenye jambo fulani.
Ndio kazi za mitandao hiyo mkuu, sasa wamuulize nani na wao hizo course hawazijui na nyingi hata kuzisikia hawajawahiWanafunzi wenyewe hawa wanakuja kuuliza kozi inahusu nini jamii forum na search engine na website za vyuo zipo kazi ipo
Tatizo hiloNdio kazi za mitandao hiyo mkuu, sasa wamuulize nani na wao hizo course hawazijui na nyingi hata kuzisikia hawajawahi