Hivi Bongo tunasoma ili iweje?

Hivi Bongo tunasoma ili iweje?

Nafikiri waafrika wengi wamefuata mkumbo tu kuwa watoto wasome mpaka Chuo kikuu lakini kiuhalisia hawajui maana ya kusoma kabisa

Wanapewa vyandarua kama msaada wanafurahia ila uwezo wa kutengeneza hakuna sasa shule mnaenda kusomea nini
Ulaya vijana wa 6 form wanatengeneza madawa ya binadamu kwa ubunifu wao maabara
Sisi maabara mnahangaika na chura
 
Wewe ndio huelewi hata Transition ya Elimu yetu

Mwl. Nyerere si ndiye aliyeleta Elimu ya Ujamaa na Kujitegemea?

Wakati wake si ndio tulipata Mabwana Shamba na Mabibi Shamba wabobezi, Ma carpenter wazuri, Washonaji wazuri wa nguo mpaka batiki

Si ndiye alisisitiza kuwepo na vyuo vya ufundi kina Arusha Tech, Mbeya Tech na Moshi Tech?

Angalia waliosoma Middle School walivyokuwa vizuri

Sasahv elimu ndio imekuwa hovyo
Ukiangalia lawama anazopewa Nyerere utadhani alikuwa ndiye mkoloni.Na aliasa mapema tu kwamba kama alifanya ya hovyo yaachwe na yachukuliwe mazuri.Sasa leo hii miaka karibu 40 tangu aachie madaraka analaumiwa.
 
It's complicated.

Huwenda mtu akadhani jibu la swali lako ni kwamba watu waache kusoma, hapana bali tunatakiwa tusome zaidi ili tuweze kujikomboa kutokana na ujinga.

Bado kuna ujinga umetamalaki ndio maana hatuoni hata tija ya elimu.
Kinachotakiwa ni kuipata elimu sahihi kulingana na dunia inavyokwenda.
 
Kijana km una ujuzi usiufiche km una kipaji usikifiche kionyeshe na ujuzi wako uonyeshe show them what you can do
 
Ajira zipo Ila nyingi zimishikiliwa na wasiosoma walichonacho ni uzoefu tu wa kazi baasi
Kwanini tusiosoma tusije na brand zetu kutokea vyuoni kwa msaada wa vyuo kusaidia upatikanaji wa mikopo toka serikalini yenye riba nafuu kama ile ya halmshauri
 
It's complicated.

Huwenda mtu akadhani jibu la swali lako ni kwamba watu waache kusoma, hapana bali tunatakiwa tusome zaidi ili tuweze kujikomboa kutokana na ujinga.

Bado kuna ujinga umetamalaki ndio maana hatuoni hata tija ya elimu.
Kinachotakiwa ni kuipata elimu sahihi kulingana na dunia inavyokwenda.
Sawaa kabisaa sasa kwanini wenye dhamana awaji na suluhisho kuleta mabadiliko ya elimu ya sasa
 
Nafikiri waafrika wengi wamefuata mkumbo tu kuwa watoto wasome mpaka Chuo kikuu lakini kiuhalisia hawajui maana ya kusoma kabisa

Wanapewa vyandarua kama msaada wanafurahia ila uwezo wa kutengeneza hakuna sasa shule mnaenda kusomea nini
Ulaya vijana wa 6 form wanatengeneza madawa ya binadamu kwa ubunifu wao maabara
Sisi maabara mnahangaika na chura
nini kifanyike?
 
Ukiangalia lawama anazopewa Nyerere utadhani alikuwa ndiye mkoloni.Na aliasa mapema tu kwamba kama alifanya ya hovyo yaachwe na yachukuliwe mazuri.Sasa leo hii miaka karibu 40 tangu aachie madaraka analaumiwa.
Unataka asilaumiwe kwa aliyofanya ?
 
It's complicated.

Huwenda mtu akadhani jibu la swali lako ni kwamba watu waache kusoma, hapana bali tunatakiwa tusome zaidi ili tuweze kujikomboa kutokana na ujinga.

Bado kuna ujinga umetamalaki ndio maana hatuoni hata tija ya elimu.
Kinachotakiwa ni kuipata elimu sahihi kulingana na dunia inavyokwenda.
Wajinga na ujinga ni bado tatizo kuu nchi hii, elimu ya kujikomboa inahitajika sana lakini iliyopo inafaulisha tu na si kutoa weledi na ujuzi pamoja na ukombozi wa kifikra ndani ya vichwa vya watu kwanini tusiachane na misingiya elimu hii ya sasa?
 
Wakuu habari,

Hivii Tanzania tuna soma ili iweje.Mataifa yote duniani elimu inatumika kumkomboa mwananchi kutoka mazingira duni na kuyaboresha , kuyatawala mazingira na si mazingira kumtawala mwanadamu.

Hapa nyumbani tuna baadhi ya vyuo venye kozi mbali mbali ambazo kwa macho ya nyama unaona zina tija lakini katika hali halisi vijana wanalalamika ajira hamna.

Na Wakati ajira zikionekana amna kuna utitiri wa mazao na rasilimali zinazolishwa Tanzania na kuuzwa njee kama malighafi na si bidhaa, nashindwa kuelewa sasa kama tuna wanafunzi wanaograduate kila siku na still amna innovations zinazotokana na elimu hizo au adaptation ya teknolojia kutoka nje ili kuongeza thamani malighafi zetu za ndani na ziuzwe njee kama bidhaa kamili sasa tunasoma na kutoa ela ndefu kwenye mikopo ili iweje?

Tanzania inajikuta katika changamoto kubwa za elimu na ajira, huku vyuo vikuu vikitakiwa kuwa injini ya mabadiliko ya kijamii na kiuchumi.

Hali hii inakinzana na dhima ya elimu duniani, ambayo ni kumkomboa mwananchi kutoka kwenye umaskini na kuboresha mazingira yake.

Vyuo vikuu nchini vinatoa kozi mbalimbali, lakini vijana wanalalamika kuhusu ukosefu wa ajira, wakati huo huo kuna utitiri wa malighafi zinazozalishwa Tanzania na kuuzwa nje kama malighafi tu, bila kuongeza thamani.

Kuna haja kubwa ya kubadilisha mfumo wa elimu ili kuchochea uvumbuzi na teknolojia, na kuongeza thamani ya malighafi za ndani ili ziuzwe nje kama bidhaa kamili.

Kutoa mikopo kwa wanafunzi ni hatua nzuri, lakini inapaswa kuelekezwa kwa njia ambayo itawawezesha kuanzisha miradi yao wenyewe na kuchangia katika maendeleo ya jamii.

Walimu wanapaswa kuwa mifano inayotoa mabadiliko ya kijamii, na elimu inayotolewa inapaswa kuhamasisha ujasiriamali na uvumbuzi.

Ni muhimu kuanzisha vituo vya uvumbuzi ndani ya vyuo vikuu ambavyo vitakuwa kazi yake kuvumbua majawabu ya changamoto za jamii kupitia wanafunzi wa taaluma husika.

Wanafunzi wanapaswa kupata fursa ya kutumia elimu yao kuleta mabadiliko katika jamii kwa kubuni suluhisho za changamoto za kitaifa na kimataifa.

Vyuo kama vile Chuo Kikuu cha Dodoma na Dar es Salaam vinaweza kuwa kiongozi katika kuleta mabadiliko ya kielimu na kijamii.

Elimu inapaswa kuwa chanzo cha tija na maendeleo, na wanafunzi wanapaswa kufundishwa kwa namna inayowawezesha kuwa nguvu ya mabadiliko katika jamii zao.

Tunapaswa kuwa na mtazamo mpya wa elimu na kuhakikisha inatoa thamani halisi kwa jamii yetu. Hii ndiyo njia ya kufikia lengo la kusoma ili kuwa na mabadiliko ya kweli nchini Tanzania na kuwa na vyuo vikuu vinavyochochea uvumbuzi na maendeleo endelevu..
Nakuja kuchangia
 
Sawaa kabisaa sasa kwanini wenye dhamana awaji na suluhisho kuleta mabadiliko ya elimu ya sasa
Tunarudi palepale kwenye elimu na wasomi.

Hivi kwani hao wenye dhamana huwa wanaqualifications kabisa za kuwa katika hizo nafasi.

Yaani bado kuna mtu ameishia STD 7 halafu yupo katika chombo cha maamuzi, sisemi atakuwa hajui lolote, ila kuna mambo nyeti ya mustakabali wa taifa atashindwa kuyaadress kwa weledi maana elimu hana.

Hivyo tunahitaji wasomi.

Haya uliyoyasema hapa, sitaki kuamini kuwa umeishia la 7, halafu ukawa na ufahamu huu.

Nadhani utakuwa umeielewa point yangu.
 
Vyuoni kuna wasomi na idara zote zinasimamiwa na wabobevu tena wamesoma mataifa ya watu kwa gharama za serikali wengine, lakini bado ukiona namna mambo yanavoendeshwa uko inatia mashaka, ukienda idara inayoongozwa na mtanzania afu uhame uende idara inayo ongozwa na mtu kutoka india au uerope uta sense tu tofauti ata kwenye mazingira ya njee tu achana na uwajibikaji, hii shida inaletwa na msingi mbovu wa elimu yetu inaandaa watu wasio jua kuwajibika na wanaokosa ubunifu toka chini inapaswa kubadilika bora watu wafeli lakini wakifaulu tuone tofauti yao na watu wengine.
 
Wajinga na ujinga ni bado tatizo kuu nchi hii, elimu ya kujikomboa inahitajika sana lakini iliyopo inafaulisha tu na si kutoa weledi na ujuzi pamoja na ukombozi wa kifikra ndani ya vichwa vya watu kwanini tusiachane na misingiya elimu hii ya sasa?
Hili suala la kubadili mtaala linapigiwa kelele kila kukicha lakini hakuna kinachfanyika.

Lakini swali ni je, tunao hao wataalamu wakutubadilishia huo mtaala uendane na dunia inavyokwenda sasa?
Walimu wenye weledi ambao wataufundisha huo mtaala?
Na je viongozi wanaopewa dhamana ya kusimamia wizara kama ya elimu, je wanaweledi wa kusimamia wizara hiyo, ili walete mabadiliko?

Maana kiongozi ananafasi kubwa sana katika kuleta mabadiliko katika hili.
 
viongozi awana maono na nia ya dhati kulikomboa Taifa kazi zinafanyika kama business as usual. Maswali yako yote yanahitaji majibu kabla ya kuamua kutoka tulipo na majibu yapo ila sioni mwenye nia wala haja hiyo.
 
nini kifanyike?
Najua hatuna wataalamu na wabunifu ila tunataka vijana wa kuweza kutengeneza bidhaa na kila kitu
Kwa kufanya hivyo badala ya viongozi wetu wasiokuwa na akili kutwa kwenda kuomba hela na misaada na kuwa ombaomba kila siku
Badala yake wayaombe hayo mataifa makubwa ambayo yana balozi zao hapo kwetu kwa kupeleka vijana wetu kusomea ufundi wowote

Hiki ndio kifanyike waache ujinga wa kuomba hela na badala yake waombe NDOANO
 
sidhani kama kupeleka vijana njee itasaidia kwasababu ubunifu sio kitu kinafundishwa tuna ma wasomi wengi wamesoma vyuo vikuu vikubwa nje lakini sio watu wa vumbuzi na watatua changamoto ,kwangu nachukulia ni kama tabia au uwezo ambao unajengwa kwa muda mrefu sio miaka miwili mitatu, wataalamu wa njee wanaweza kuletwa ndani kwa muda fulani wasaidie tu na kuongoza njia wapo wanafunzi na vijana nje ya mfumo wa elimu wana mawazo yao mazuri ila awana wa kuwapa njia na kuwasimamia kwasababu walimu wenyew wengi hata awajawahi kuwa wabunifu na wavumbuzi awawezi kuona mawazo ya kivumbuzi na kuyaongoza kutimiza adhma ya wazo husika
 
Elimu huwa na tija kubwa kwenye nchi zenye mifumo makini ya uchumi na maendeleo. Mifumo ambayo sekta zote za uchumi na maendeleo (the industry) ziko imara na vipaumbele vya taifa ni kuboresha tija, uzalishaji na maendeleo ya teknolojia (modernisation).

Nchi za namna hiyo zinahamasisha wasomi na wanataaluma mbali mbali kujiimarisha kielimu ili kuwa wabunifu na kuchagiza maendeleo katika kila sekta na fani. Na kawaida, sekta hasa za kibiashara, uzalishaji na huduma (industry) ndizo “zinazolipa” sana na hivyo kuhitaji na kuvutia wanataaluma wengi huko kwa ajira na hata fursa za kuanzisha miradi ya kisomi ya kujiajiri.

Tatizo la Tanzania na nchi za Afrika (SSA), viongozi wameweka kipaumbele kwenye siasa na mifumo ya utawala wa nchi (overheads) kuliko kwenye sekta za kiuchumi. Wamerundika maslahi makubwa huko na kuhakikisha sehemu kubwa ya bajeti na rasilimali za taifa inaelekezwa huko. Halafu sifa kuu za kupata nafasi/fusra muhimu katika sehemu hizo sio umahiri wala utendaji kitaaluma bali ni utii na kujikomba kwa viongozi.

Matokeo, unakuta maprofesa wa vyuo vikuu, wahandisi, madaktari, wanasheria wabobezi, n.k. wanakimbikilia kwenye siasa au teuzi. Na wakienda huko wana tabia ya kukiuka na hata kupingana na kanuni kuu za taaluma zao. Siasa inalipa kuliko sekta zote za maendeleo ya taifa. Hata wanaoitwa wafanyabiashara unawakuta bungeni au wanahangaika na “connection” za kisiasa!

Wasomi wanaambiwa “wajiajiri”. Wapi? Wakati sekta zinazowiana na elimu zao ni kama hazipo? Mnaua sekta za maendeleo (industry), mnatukuza fursa za kisiasa, halafu mnataka wasomi wajiajiri - kwenye bodaboda? Umachinga? Fremu? Vigenge? Kilimo cha mkono? Lazima elimu na taaluma ziumie na kupoteza umuhimu wake taratibu.

Kuna ujinga mwingine. Nilimsikia mhubiri mmoja akiponda elimu inayotolewa Tz kwamba haina maana yoyote. Akatoa mfano wa nchi moja huko Asia kuwa wanafunzi wa sekondari wanafundishwa mambo yenye tija kama kuunda simu za mkononi wakati huku kwetu unakuta vijana wanahangaika kujifunza “principles of physics”! Eti zitawasaidia nini wakimaliza shule! Ndio yale mambo ya waliomaliza std7 au fm4 kuunda helicopter au EVs. Sijui tunaielewaje elimu na tunatarajia nini!
 
Back
Top Bottom