Hivi Bunge linaweza kukataa kuidhinisha jina la Waziri Mkuu linalopendekezwa na Rais?

Hivi Bunge linaweza kukataa kuidhinisha jina la Waziri Mkuu linalopendekezwa na Rais?

Mzalendo Uchwara

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2020
Posts
4,437
Reaction score
13,836
Hii haina uhusiano wowote na kikao cha Bunge kinachofuata.

Nilitaka kujua tu, hivi wabunge wetu hawa ambao wengi walipita kwa mgongo wa Hayati JPM, ikitokea mmoja 'miongoni mwao' anapigwa chini u PM halafu linapelekwa jina lingine, wanaweza kulikataa?

Maana wanasema mwenzako akinyolewa wewe tia maji, sasa kama 'mmoja wenu' atatendewa hivi na wao wakaidhinisha, Si mwendo utakuwa huo huo 2025 kule majimboni? Wote 'watanyolewa'!

Ikitokea wamegoma kuidhinisha jina jipya itakuwaje? Bunge linavunjwa?? Tunaenda kwenye uchaguzi mkuu?

Ni tafakuri tu.
 
Mafisadi na wezi wa mali za umma mnaumizwa sana na utendaji kazi wa waziri mkuu wetu.
Na bado tunamuomba mama akifanikiwa kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 amteuwe tena Majaliwa aendelee hadi 2030.
Mimi binafsi namkubali sana waziri mkuu wetu, kama nilivyosema haina uhusiano na waziri mkuu wetu.

Ni swali tu juu ya mamlaka ya bunge letu tukufu, wanaweza kukataa pendekezo la rais? Na wakikataa nini kinafuata?
 
Kupatikana kwa Waziri Mkuu (WM)
Katiba ya Jamhuri, Sehemu ya tatu, Ibara ya 51, ibara ndogo za 1-6

Kikatiba Rais ana mamlaka ya kuteua jina la WM (waziri mkuu) toka kwa wabunge wa kuchaguliwa toka kwenye chama cha siasa chenye wabunge wengi.

• Jina hilo litawasilishwa bungeni ambapo Bunge litatakiwa aidha kupitisha au kupiga kura ya hapana kwa jina husika (kura ya ndiyo inapaswa kuwa nyingi kuliko hapana, na kinyume chake).

• kitokea kura ya ndiyo zikawa nyingi basi mwenye jina atakuwa WM, na ikitokea kinyume chake basi jina litarudishwa kwa Rais ambaye atalazimika kuchagua jina lingine kwa sharti zile zile nilizoeleza hapo juu na mchakato utakuwa hivyo hivyo mpaka Jina husika lipate kura ya ndiyo kwa ‘majority vote’

Ikiwa Wabunge hawana imani na WM
Ili kumuondoa;
• Ni lazima WM awe ameshtakiwa kwa makosa ambayo itaonekana kakiuka maadili ya kiuongozi

• Ni lazima miezi 6 iwe imepita tangu kuchaguliwa kwake

• Ni lazima miezi 9 iwe imepita tangu kuitishwa kura ya kutokuwa na imani nae

• Ni lazima 20% au zaidi ya wabunge wamuandikie Spika kuomba kuitisha kura ya kutokuwa na imani na WM

• Spika akiona sharti zote zimetimia ataitisha kura hiyo mara moja, na ili WM aondoke lazima kura ya kutokuwa na imani nae ziwe nyingi.

Ikiwa kura za kutokuwa na imani nae ni nyingi kuliko za kuwa na imani nae Spika atamtumia rais azimio hilo, ambae atalazimika kupendekeza jina lq mbunge mwingine kuwa WM, huku WM atatakiwa kuachia madaraka ndani ya siku mbili.

HALI ZITAKAZOMLAZIMU RAIS AVUNJE BUNGE NA KURUDI KWENYE UCHAGUZI MKUU
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 🇹🇿, ibara ya 90, ibara ndogo ya 2a-e

- ikiwa maisha ya Bunge yameisha (ile miaka mitano mitano) kwa mujibu wa Ibara ya 65 ya Katiba au wakati wowote ndani ya miezi kumi na miwili ya mwisho ya uhai wa Bunge, isipokuwa tu ikiwa Spika atapata taarifa rasmi chini ya Ibara ya 46A ya Katiba hii inayopendekeza kuundwa kwa Bunge. Kamati Maalum ya Uchunguzi kwa lengo la kumshtaki Rais;

- ikiwa Bunge litakataa kupitisha bajeti iliyopendekezwa na Serikali;

- iwapo Bunge litashindwa kupitisha Mswada kwa mujibu wa masharti ya Ibara ya 97(4);

- iwapo Bunge litakataa kupitisha mswada ambao ni muhimu sana kwa sera za Serikali na Rais akaona kwamba suluhu si kumteua Waziri Mkuu mwingine bali kuitisha uchaguzi mkuu;

- iwapo, kwa kuzingatia uwiano wa uwakilishi wa vyama vya siasa katika Bunge, Rais anaona kwamba si halali tena kwa Serikali iliyo madarakani kuendelea na wadhifa wake, na haiwezekani kuunda Serikali mpya.

Zinapotokea hali hizi basi bila shaka tutarudi kwenye kampeni na uchaguzi mkuu.
 
Ikitokea wamegoma kuidhinisha jina jipya itakuwaje? Bunge linavunjwa?? Tunaenda kwenye uchaguzi mkuu?

Ni tafakuri tu.
Mkuu Mzalendo Uchwara,
Rais wa Tanzania ni sehemu ya Bunge, ndiye analiunda, anateua watendaji wakuu wa Bunge, anaidhinisha sheria zote zinazotungwa na Bunge, na kulivunja Bunge.

Bunge likitunga sheria, kwa mujibu wa Ibara ya 97 ya katiba, rais asipoipitisha, atairudisha Bungeni kwa mara ya kwanza, wairekebishe. Sheria iliyokataliwa na rais inaporudishwa Bungeni, Bunge likijiona sheria hiyo iko sawa, hivyo linamlazimisha rais aipitishe, litairudisha kwa mara ya pili, Rais asipokubali kuipitisha, rais atalivunja Bunge kwa kuitisha uchaguzi Mkuu wa wabunge tuu.

The same process applies kwa Bunge likiataa kupitisha jina la Waziri Mkuu, watalirudisha kwa rais, ili abadilishe, rais asipobadilisha, atalivinja Bunge, na kuitisha uchaguzi wa wabunge.

Na kuvunjwa kwa tatu kwa Bunge ni likigoma kupitisha bajeti kuu ya serikali

Kuvunjwa kwa nne kwa Bunge, ni likikataa kupokea ripoti ya CAG.

Rais hawezi kulivunja Bunge, likitumia ibara ya 46A kumuondoa rais madarakani.
P
 
Mkuu Mzalendo Uchwara,
Rais wa Tanzania ni sehemu ya Bunge, ndiye analiunda, anateua watendaji wakuu wa Bunge, anaidhinisha sheria zote zinazotungwa na Bunge, na kulivunja Bunge...
Asante mkuu, umenifungua mancho.

Kwa taratibu hizo basi bunge letu tukufu haliwezi kwenda kinyume na matakwa ya Rais hata siku moja.
 
Hii haina uhusiano wowote na kikao cha Bunge kinachofuata.

Nilitaka kujua tu, hivi wabunge wetu hawa ambao wengi walipita kwa mgongo wa Hayati JPM, ikitokea mmoja 'miongoni mwao' anapigwa chini u PM halafu linapelekwa jina lingine, wanaweza kulikataa...
Hizi ni ramli chonganishi!
 
Back
Top Bottom