Hivi CHADEMA wamemuelewa kweli Rais wetu? Kwamba hicho wanachozunguka kukihubiri ni ukiukaji wa malengo ya kuruhusu mikutano ya hadhara



Umesema Serikali iliacha kukusanya maoni ya wananchi juu ya mjadala wa Bandari za Tanganyika na mwekezaji DP World kwa sababu CHADEMA walianza kuzungumzia, hao CHADEMA sio sehemu ya wananchi?

Maoni yao sio Sawa na maoni ya watanzania wengine?

Wanachama wa CHADEMA na viongozi wao sio wananchi wa Tanzania?



Kwanza huo mkataba si ulivuja?

Kwani Serikali iliuleta lini kwa wananchi? Kabla ama baada ya kisainiwa?

Mkataba wa 2022 unakusanywa maoni ya wananchi 2023?







Unasema CHADEMA wanatumia vibaya pesa zao za Ruzuku.

Unashauri wakae watulie wasifanye mikutano ya hadhara ili wapate pesa za kuwalipa vijana wanaotumika katika uchaguzi pesa Nzuri ili kuwaepusha kuhongwa laki 5 na CCM?

Kumbe ndio huwa kinatokea mpaka CHADEMA kuibiwa kura na kushindwa kila Mwaka wa uchaguzi?





Unawazuiaje CHADEMA kuyasemea haya yanayoendelea katika nchi waliyomo kihalali?

Kazi ya CHADEMA ni Siasa, unataka leo waanze kuzunguka na kuelezea Sera na Malengo ya Chama, kwani kupinga Ufisadi sio sehemu ya Siasa?

Kutetea maslahi ya wananchi sio Siasa?

Kusimamia na kulinda rasilimali na maliasili za nchi sio sehemu ya Siasa?





Wakati Rais Samia anakaa chini na viongozi wa vyama vya upinzani na kukubaliana kusonga mbele na kuruhusu wafanye Siasa za majukwaani, aliwapangia ya kuongelea na ambayo sio ya kuongelea?


Rais Samia sio mgeni hapa nchini, anawajua vizuri CHADEMA na kipindi cha uongozi wa Rais mstaafu Jakaya alikuwepo Ikulu na mwenendo wa Siasa zao anaujua, kipi kilimfanya aamini kwamba sasa watafanya tofauti kwenye hili la DP World kama walivyofanya kwenye lile la Richmond?



Kosa pekee wanalofanya wanasiasa (unfortunately wa pande zote) ni kutoa maneno machafu na kuitana majina ya kutweza Utu.

Na hii inapelekea wote kutokutaka kushindwa na matokeo yake mara nyingi huwa ni mabaya maana casualties wa Siasa chafu huwa ni wengi na wananchi ndio wahanga wakubwa.
 
Duniani kote upinzani unaikosoa serikali, kama SSH anategemea vyama vya upinzani watangaze sera zao bila kukosoa mapungufu ya serikali iliyopo madarakani basi nayeye anaviashiria vya udikteta.
Kwanza nawauliza Maccm: Kuna kipengele cha Sheria ya vyama vya siasa au Sheria ya uchaguzi inayowalazimisha wapinzani mikutanoni au sehemu nyingine kuzungumzia sera zao tu na si kukosoa mapungufu ya serikali?
 
Kukubali upumbavu na ujinga basi na wewe utakuwa mpumbavu na mjinga.
 
Hatutaki Mkataba wa DP World Tanganyika.
 
Pole sana ndugu yangu, kumbe hujui tofauti ya vyama vya siasa na vikundi au vyama vya wanaharakati (activists). Goja nijaribu kukuelewesha:

Vyama vya siasa hufanya kazi kwa utaratibu niliouelezea hapo juu kwa kuzingatia sheria na kanuni za nchi pamoja na mila, desturi na maadili ya wananchi.

Kama likitokea jambo linaloelekea kutokuwa na masilahi ya taifa, hususani hili la mkataba wa IGA; chama hufanya kwanza utafiti wa kina wa kisayansi wakitumia watalaamu wao mahili. Baada ya hapo vikao vya chama (CC na NEC) hukaa kuchambua kwa makini utafiti huo na kutoa tamko la chama lililosheheni weledi mkubwa kuhusu jambo hilo pamoja na maoni na mapendekezo ya utatuzi wake. Vyama vya siasa huwa havikurupuki. Upinzani wa kisiasa siyo sawa na mchezo wa ngumi wa kurushiana makonde. Upinzani wa kisiasa ni wa kushindanisha nguvu za hoja na siyo hoja za nguvu.

Vikundi ama vyama vya wanaharakati havina sheria wala kanuni na taratibu za kufanya kazi yao. Wao hufanya kazi kwa matukio. Havifanyi utafiti. Wao wakisikia jambo lo lote lililofanywa au kukusudiwa kufanywa na serikali, hulirukia na kuishambulia serikali kwa nguvu kubwa bila hata uthibitisho wa kile walichokisikia. Huropoka maneno makali na mabaya kwa serikali na kwa viongozi wa serikali yakiwamo matusi na maneno mengine machafu. Hushambulia serikali ndani ya nchi na nje ya nchi na taasisi za kimataifa hususani European Union, World Bank na kadhalika. Lengo ni kuichafua nchi na kuitishia iwekewe vikwazo vya kimataifa kwa kile serikali ilichofanya. Wanaharakati hawatambui kwamba nchi yetu ni sovereign state yenye uhuru wa kuendesha mambo yake. Hawa wanaharakati hupeleka haraharaka mambo yetu BBC na Al Jazera na kadhalika. Wanaamini Tanzania inatawaliwa na mabeberu wa Ubiligiji, Ujerumani, USA na EU.

Chama cha chadema kiko kundi hili la wanaharakati. Hakina tofauti yo yote na vikundi vingine vya wanaharakati hususani kile cha Sauti ya Watu kinachoendeshwa na Maria Sarungi ambacho Dr Slaa kajiunga. Raisi Salmia kawaelekeza wanachotakiwa kufanya cha siasa. Sidhani kama wamemuelewa. Maamuzi ni ya kwao, waendelee kuwa chama cha wanaharakati au wajirekebishe na kurudi kuwa chama cha siasa kama vile chama cha Zitto Kabwe au kile cha Prof. Lipumba. Wakiendelea kuwa wanaharakati wasitegemee kupata ha mbunge mmoja 2025.
 


Please, don’t insult my intelligence due to your own misapprehension.



CHADEMA ni Chama cha Uanaharakati? Toka lini? Una uthibitisho juu ya hili?


Kwahiyo Msajili wa vyama vya siasa hapa nchini nae hana ufahamu kiasi hicho? Mbona hajakifutilia mbali?


Rais Samia pia hajui tofauti kati ya Chama cha Siasa na uanaharakati? Kwanini analalamika badala ya kufanya maamuzi magumu?




Hivi umejiuliza endapo Kama CHADEMA wangehudhuria Mkutano wa jana, hotuba ya Rais Samia ingekua tofauti kiasi gani?
 
Kwani walipangiwa cha kuhutubia?
 
Kumbe ndio huwa kinatokea mpaka CHADEMA kuibiwa kura na kushindwa kila Mwaka wa uchaguzi?
Sasa wewe au mwakilishi wako hayupo kwenye kusimamia upigaji wa kura na kuhesabu kura, unategemea kipi? Utabaki unalaumu bure tume ya uchaguzi, kwani hiyo tume inakuwaga ipo kwenye vituo vya kupigia kura? Utalaumu bure wakurugenzi wa halmashauri, kwani wanakuwagapo kwenye vituo vya kupigia kura?

Kwanza Tume ya Uchaguzi ina watu saba tu. Hawa kazi yao wakishirikiana na wakurugenzi wa halmashauri ni kuhakikisha vifaa vya kupigia kura vinakuwepo vya kutosha kwenye vituo vyote nchini vya kupigia kura. Zoezi la kupiga kura na kuhesabu kura vituoni linasimamiwa na wawakilishi wa kila chama cha siasa hapo kwenye kituo. Matokeo ya kura hutangazwa pale pale kituoni mara tu baada yakuhesabu kura na hubandikwa pale kituoni kwa kutumia Form A ambayo wawakilishi wa kila chama wamesaini kukubali matokeo hayo.

Nakala za matokeo ya kila kituo hupelekwa jimboni kufanyiwa majumulisho. Hapo jimboni wawakilishi wa kila chama husimamia upokeaji na ujumulishaji wa hizo form. Sasa kama chadema kinakusanya vibaka wa mitaani kuwa wawakilishi wao na hawawalipi cho chote cha maana, unategemea nini? Huyo kibaka hapo kituoni si anatarajia kuwachomoa simu au pesa mfukoni hao wapiga kura. Si anatarajia kuwauzia kura CCM ambao ni chama tajiri, kila kura ya chadema anawauzia ccm buku tano au hata buku moja. Akifanikiwa kuuza kura 100 kwa buku tano tano anatoka na kibunda cha laki 5 ambacho hajawahi kukipata maishani yake. Ataishukuru chadema kwa kumpa fursa hiyo ya ulaji na ataimba Piiipoziiiii Pawa! Hata ungalikuwa wewe au mimi tungalifanya hivyo hivyo. Wewe mlinzi nyumbani kwako kama humpi mshahara wake, akikuibia atakuwa hajafanya kosa kwani kachukua ujira wake. Muache kushutumu Tume ya Taifa ya Uchaguzi wala hao wakurugenzi wa halmashauri kwa sababu ya uzembe wenu.
 
Everybody knows this except you and likes. Rais kawapa onyo, hamukumuelewa kwa sababu katumia lugha ya kiungwana ambayo kwenu ni ngumu kuielewa. Angalikuwa Jiwe angaliwaambia kwa lugha mnayoijua na kuwapiga ban ya kufanya mikutano ya hadhara mara moja, mkashitaki huko kwa mabeberu wenu.

Mkiendelea na huo uanaharakati wenu hata raisi huyu atawachoka na kuwapiga ban kufanya hiyo mikutano, na ana uwezo wa kukifuta hiko chama mkashitaki kwenye hiyo mnayoiita dunia. Hakuna anayewaogopa. Bahati nzuri Mr Mbowe ameshajirekebisha kwa kiwango kikubwa, hata katibu mkuu wenu. Amebakia hasa Bw. Tundu Lissu, yeye anaweza kudhibitiwa pekee yake.
 


Naona unafanya siasa za mduara.

Nilichouliza Mimi na unayoeleza wewe ni Sawa?



Turudi kwenye swali la msingi….

Kuhusu hizo laki 5 CCM inazowahonga vijana wasimamizi wa CHADEMA wakati wa uchaguzi, ndio mojawapo wa kisababishi cha kushindwa kwa CHADEMA kila chaguzi?

Ni utaratibu wa Chama kuhonga vijana wa upinzani ili kufanikisha malengo yao?

Sera ya Chama na Serikali inasemaje kuhusu Rushwa?
 

Let me stop you right here!

“hamukumuelewa “ “ kwenu “ “ mnayoijua nyie” “mabeberu wenu” “mkiendelea” ……..


You seem like a reasonably bright fella, hapo juu hao unaowazungumzia kwa kuni-quote Mimi ni akina nani? Mimi na nani?


Are insinuating that I’m part of CHADEMA? Una tatizo la projection?


Umenisoma vizuri kabla ya kunijibu? Umerudia angalau mara mbili?


Kwahiyo yeyote muuliza maswali/ mtoa hoja inayokugusa tofauti na upendavyo ni CHADEMA?


Siasa ni sayansi, jibu hoja ya mada uliyoweka mezani.
 
Lini rushwa ilishaisha duniani? Lini wizi na ufisadi ulishaisha duniani? Hujasikia kama hata huko Amerika kura zinaibiwa hadi wanafikishana mahakamani na kurudia kuhesabu kura manually. Kura zinaibiwa licha ya kuweka sophisticated electronic election systems zenye kila ulinzi wa ki electronic. Sasa sembuse hizi za chadema zinazolindwa na vibaka. Yaani wala ccm siyo wezi, wanachukua tu kidogo zile ambazo zimeachwa peke yake bila ulinzi. Wakati mwingine vibaka hawa walioaminiwa na chadema huzitembeza na kuwashawishi wanachama wa ccm wazinunue hapo kwenye kituo cha kupigia kura.

Kama ni ufisadi nadhani chadema ndiyo inashika namba one kwenye vyama vya siasa nchini. Pesa wanayokusanya kwenye michango ya wanachama wakati wa mikutano yao huwa haiwekwi wazi. Ile wanayoipata kutoka kwa washirika wao ughaibuni huwa haiwekwi wazi. Hata ile ruzuku wanayopokea kutoka serikalini haiwekwi wazi. Kiasi kikubwa cha pesa hiyo bila shaka hutumbukia kwenye matumbo ya viongozi wa chama.
 


Ungekua unajibu hoja kwa hoja ingekua poa sana, tatizo unauzunguka mbuyu!

Unaogopa nini?



Kwahiyo Kama mpaka Amerika kuna Wizi na Ufisadi ndio CCM imehalalisha hizo laki 5 kwa vijana wa CHADEMA ili kuvuruga chaguzi kila mara?


Hakuna sehemu nimekuuliza ni Chama gani kinaongoza kwa ufisadi na Rushwa kiasi useme Chadema inashika namba moja.


Nimekuuliza Kama Chama na Serikali vinabariki utoaji wa hongo za laki 5 kwenda kwa vijana wa CHADEMA ili kuvuruga chaguzi?


Sera za Chama na Serikali zinasemaje kuhusu Rushwa?


Jitahidi sana kukaa kwenye mstari wa mada uliyoanzisha mwenyewe.
 
Samia sio katiba. Tena CCM komeni kutumia kauli ya Rais kuruhusu mikutano ya hadhara yeye hana ruhusa ya kukataa wala kukubali. Sheria ipo wazi.
 
Ila kutawaliwa na Zanzibar ni sawa siyo?
 
Samia sio katiba. Tena CCM komeni kutumia kauli ya Rais kuruhusu mikutano ya hadhara yeye hana ruhusa ya kukataa wala kukubali. Sheria ipo wazi.
Jiwe alikataa katiba mpya na alipiga marufuku hiyo mikutano ya hadhara na mliufyata.

Ila kutawaliwa na Zanzibar ni sawa siyo?
Wewe unaona kutawaliwa na Moshi au Mwanza au Bagamoyo ni sawa?




Sera za Chama na Serikali zinasemaje kuhusu Rushwa?
Sera za vyama vya siasa, sheria za nchi, tekinolojia na hata imani na mahubiri ya dini mbali mbali hazijaweza na hazitaweza kukomesha wizi wa aina yo yote tangia mwanzo wa dunia. Katika bustani ya Adeni, ibilisi alimshawishi Eva kuiba lile tunda la Mungu na alifanya hivyo, akaliiba, akakamatwa na kuadhibiwa yeye na Adamu wake. Tangia hapo wizi unaendelea kwa ushawishi wa ibilisi, wanaokamatwa huadhibiwa, wengi hawakamatwi na dini zinahubiri adhabu yao wataikuta huko ahera watakapoenda.


Kwahiyo Kama mpaka Amerika kuna Wizi na Ufisadi ndio CCM imehalalisha hizo laki 5 kwa vijana wa CHADEMA ili kuvuruga chaguzi kila mara?
Nimekudokeza tu mfano rahisi wa mbinu moja wapo inayoweza kutumiwa kama chadema hawaweki mawakala thabiti wa kusimamia upigaji kura na uhesabu kura kwenye hivyo vituo. Mbinu ziko nyingi tu duniani za kuibiwa kura ukizembea. Huo ni mfano tu (abstract) wa great thinker, usiuchukulie kama ni wa ukweli na kwamba mimi ndiyo shahidi. Kwanza mimi si mwanachama wa chama cho chote cha kisiasa.

Ulisikia na kuona huko Kenya kwenye chaguzi zao walivyolalamika kura zao kuibiwa juu kwa juu kwa njia ya kidijitari za mtandao wakati wa transmission za data kwenda National Election Commission. Walifikishana hadi Mahakama ya juu lakini ikawa ngumu kuthibitisha wizi huo wa mtandao beyond reasonable doubt.

Bila shaka ulisikia huko USA wakilalamika jinsi Russia ilivyobadili electronically kura za Mama Clinton na kumwezesha rafiki yao Trump kuwa rais wa USA.

Leo umemsikia mwanaharakati wa kimataifa, Bw. Tundu Lissu alivyotorokea USA/ Belgium kutokea Ngorongoro hadi Nairobi International Airport baada ya alichotumwa kufanya huko Ngorongoro Crater na Tanzania kwa ujumula kusitishwa na jeshi la Wambura. Ameenda kutoa ripoti ya kile alichoweza kukikusanya hapa Tanzania. Huyu mtu nyie mnamuita ni mwanasiasa. Wenye akili wanamuita ni mwanaharakati na jasusi wa nchi za ulaya na Amerika. Ni kibaraka wa hao wazungu wanaotaka kumsimika awe raisi wa Tanzania kwa masilahi yao.
 
Hao wanaelewa sana lakini dini zao na mila zao ni za kudidimiza wanawake, haiwaingii akilini mwanamke kuwa Mkuu wao. Ni wajinga wajinga tu.

"It's easy to learn but very difficult to unlearn".
 
Kama unaamini tuna bunge basi wewe ni punguani wa kiwango kisichoelezeka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…