Coach Slamah Hamad
JF-Expert Member
- Nov 12, 2014
- 3,740
- 4,938
Baada ya bunge kuridhia mkataba tata wa IGA kati ya JMT na DP World, tarehe 10 June 2023, watanzania wengi wa nyanja mbali mbali walijitokeza kujadili suala hili. Mjadala ulipamba moto na serikali kuamua kukusanya maoni yaliyokuwa yanatolewa na wananchi kusuhu mkataba huu kwa lengo la kuyafanyia kazi. Mjadala uliendelea vizuri kwa takribani miezi miwili. Ghafla chadema wakadandia na kupoka mjadala huu na kuufanya kuwa sera yao kwenye mikutano ya hadhara waliyokuwa wakiifanya sehemu mbali mbali ya nchi. Hivyo sakata la bandari likawa ni la mapambano ya kisiasa kati ya chadema na serikali ya ccm. Hii ikasababisha wananchi kusitisha mjadala waliokuwa wanafanya wa kutoa maoni yao kwa serikali. Kwani sasa mwananchi akipinga mkataba huu, alionekana ni mwana chadema na yule aliyekubaliana na mkataba huu alionekana ni mwana ccm! Mjadala ukafa na serikali ikaacha kukusanya maoni ya wananchi kwani serikali haiwezi kukusanya maoni ya chadema au wanachadema.
Hivyo ndivyo chadema ilichofanya kwa katiba mpya na wamasai kuhama kwa hiari kutoka Ngorongoro Crater ili kuepuka kupotea kwa hifadhi hiyo kutokana kuongezeka sana kwa shughuli za kibinadamu kwenye Crater hiyo ambayo iliorodheshwa kwenye Seven Wonders of the World.
Wafuate sheria, kanuni na taratibu za nchi yetu, pamoja na kuzingatia maadili ya mtanzania, mila na desturi za mtanzania. Maoni na mapendekezo yao yawakilishwe bungeni kupitia kwa wabunge wao wa kuchaguliwa na wananchi na wale wa viti maalum vyao wasiowapenda.
Wakazane kutumia hiyo fursa waliyopewa ya mikutano ya hadhara kukijenga chama chao kwa kunadi sera za chama chao (kama wanzo), ili itakapofika mwaka 2025 waweze kuwa na wabunge wengi bungeni. Ikiwezekana washinde hata hicho kiti cha uraisi. Wahakikishe wanajipanga vizuri kulinda kura zao kwa kuweka mawakala waaminifu na wanaowalipa vizuri katika kila kituo cha kupigia kura. Uzoefu wa nyuma umeonesha kuwa chadema hutumia vijana waganga njaa kama mawakala wao na huwa hawalipwi hata senti moja na chama chao kusimamia kura kwenye vituo. Hivyo huwa ni rahisi sana kununuliwa na CCM kwa pesa kidogo cha kama laki tano tu. Chadema watunze hiyo ruzuku ili muda utakapofika waweze kuwalipa hawa mawakala wao angalao Sh. million tatu kila mmoja. Sasa hivi wanatumia vibaya ruzuku hii kwa kulipana posho ya kuzunguka ovyo ovyo kila mahali. Watajikuta wakati ukifika hawana risasi aka posho kwa mawakala wa kulinda kura zao na kuambulia kifo cha mende.
Nguvu ya chama cha siasa chochote inatokana na wingi wa wabunge wao ndani ya bunge kwani bungeni ndipo mahali pekee pa maamuzi ya yote serikali inayopaswa kuyafanya. Hivyo hizo ndoto zao za katiba mpya na mengine zitawezekana tu kama watakuwa na majority bungeni na kushinda kiti cha uraisi. Hivyo kwa sasa zibaki tu kuwa ndoto na wasitake kushinikiza CCM yenye majority bungeni kutekeleza ndoto zao, hilo haliwezekani po pote duniani na hata huko ahera.
Umesema Serikali iliacha kukusanya maoni ya wananchi juu ya mjadala wa Bandari za Tanganyika na mwekezaji DP World kwa sababu CHADEMA walianza kuzungumzia, hao CHADEMA sio sehemu ya wananchi?
Maoni yao sio Sawa na maoni ya watanzania wengine?
Wanachama wa CHADEMA na viongozi wao sio wananchi wa Tanzania?
Kwanza huo mkataba si ulivuja?
Kwani Serikali iliuleta lini kwa wananchi? Kabla ama baada ya kisainiwa?
Mkataba wa 2022 unakusanywa maoni ya wananchi 2023?
Unasema CHADEMA wanatumia vibaya pesa zao za Ruzuku.
Unashauri wakae watulie wasifanye mikutano ya hadhara ili wapate pesa za kuwalipa vijana wanaotumika katika uchaguzi pesa Nzuri ili kuwaepusha kuhongwa laki 5 na CCM?
Kumbe ndio huwa kinatokea mpaka CHADEMA kuibiwa kura na kushindwa kila Mwaka wa uchaguzi?
Unawazuiaje CHADEMA kuyasemea haya yanayoendelea katika nchi waliyomo kihalali?
Kazi ya CHADEMA ni Siasa, unataka leo waanze kuzunguka na kuelezea Sera na Malengo ya Chama, kwani kupinga Ufisadi sio sehemu ya Siasa?
Kutetea maslahi ya wananchi sio Siasa?
Kusimamia na kulinda rasilimali na maliasili za nchi sio sehemu ya Siasa?
Wakati Rais Samia anakaa chini na viongozi wa vyama vya upinzani na kukubaliana kusonga mbele na kuruhusu wafanye Siasa za majukwaani, aliwapangia ya kuongelea na ambayo sio ya kuongelea?
Rais Samia sio mgeni hapa nchini, anawajua vizuri CHADEMA na kipindi cha uongozi wa Rais mstaafu Jakaya alikuwepo Ikulu na mwenendo wa Siasa zao anaujua, kipi kilimfanya aamini kwamba sasa watafanya tofauti kwenye hili la DP World kama walivyofanya kwenye lile la Richmond?
Kosa pekee wanalofanya wanasiasa (unfortunately wa pande zote) ni kutoa maneno machafu na kuitana majina ya kutweza Utu.
Na hii inapelekea wote kutokutaka kushindwa na matokeo yake mara nyingi huwa ni mabaya maana casualties wa Siasa chafu huwa ni wengi na wananchi ndio wahanga wakubwa.