Hivi Chid Benz alikuwa analishwa nini huko sober?

Hivi Chid Benz alikuwa analishwa nini huko sober?

Vidonge gani mshana? Kwa uelewa wangu mdogo tangu nilivyoona muonekano wake nikawaza labda anatumia vidonge vya Yale mambo maana ndo hua yananenepesha mtu ghafla Sana

Ila nikaona kukaa kimya ni hekima pia
 
Hakuna Cha ajabu, ukianza kumeza methadone au arv lazima mwili uje hii ni scientifically proven

Sober lazima alikua anakula methadone
 
Nimejiuliza SANA. Huenda ni vidonge maalumu VYA lishe huwa vinanenepesha SANA, nilipokua ARUSHA Kuna maza Fulani ALIKUA navo, nikajua ni VYA ukimwi nilivo soma content zake NDO nikafahamu ni VYA lishe

Kwishaaaa
 
Hii nayo ni roho mbaya
Tunatofautiana mawazo

Ongezeko la mwili kama huo husuani pale tunaporejea mwili wake tuliouzoea ambao wote tunaweza kukubaliana kwamba hakijaptia kipindi kirefu tangu apate mwili huu mpya.

Mwili huu hauwezi kuchukuliwa kama jambo zuri kiafya kwasababu tunajua matatizo ya metabolic kama kisukari, shinikizo la damu au tatizo la ini.

Naongea hivi with personal experience silopoki tu na wala sipo hapa kutoa fagio kwa kila kitu hata kwenye vitu ambavyo ukivipima kwenye mizania ya afya unaona vina side effects kubwa.

Kupona uraibu ni jambo jingine, na kujenga afya endelevu ni jambo jingine.

Kwa kifupi mwili wa Chid wa sasa ni ushahidi wa mabadiliko ya maisha lakini sio ushahidi wa afya bora. Nyinyi mnaosema huo mwili ni afya ndio mnaompoteza.
 
Kisukari na kitambi wapi na wapi wee ushaona wapi? Tumpongeze kwa kitambi hiyo ni dalili amerudi kwenye normal eating habits sio mteja tena. Sasa anachangamoto ya kawaida ya watu wote kuchoma mafuta ya kukata kitambi which is easier kwake sababu ni mtu wa matizi
Kitambi na Kisukari ni mutual inclusive

Kisayansi inafahamika kuwa kitambi cha chini (kama cha Chid) ni kiashiria kikuu naomba hapa nissitize tena, kitambi kama hicho ni kiashiria KIKUU cha Insulin resistance

Kwa mtu kama Chid Benz ambaye amekuwa kwenye uraibu wa madawa kwa muda mrefu, mabadiliko ya ghafla ya uzito yanaweza kuashiria metabolic dysregulatio, yaani mwili hauwezi tena kudhibiti vizuri matumizi ya sukari na mafuta.

Kuacha matumizi ya dawa za kulevya of course ni jambo la heri na la kupongeza lakini lazima kama tunataka kumjenga Chid Benz lazima tumuambie ukweli na ajue kuwa kupona afya ni mchakato mpana unaousisha lishe bora, mazoezi, ushauri wa kiafya pamoja na ufuatiliaji wa VIASHIRIA VYA AFYA

Mwili wa Chid Benz unaonyesha mabadiliko ya nje, lakini bila ushahidi wa vital signs kama blood pressure, glucose levels, au liver function, hatuwezi kusema ameimarika kiafya.
 
We ni daktari kama sio sidhani ni shihi kuwa mashauri wa kiafya na matibabu
Logical fallacy of "Ad Hominem Fallacy" Kushambulia mtoa hoja badala ya hoja yenyewe

Unataka kuzima mjadala wa afya kwa kugeuza mwelekeo kuwa nani ana mamlaka ya kusema, badala ya kuchambua hoja zenyewe?

Kwa mantiki yako, mtu hawezi kusema maji ni mazuri bila kuwa mtaalamu wa kemia?

Basi tusijadili hata mpira bila ya kuwa na FIFA licensed coach.
 
Mi nawashangaa zaidi watu wanaompa hongera kwa huo mwili.

Wakati mimi nawaza tofauti, kwamba huwenda jamaa amepatwa na tatizo la kiafya and probably ni kisukari. Lakini watanzania wenzangu bado wanazidi kumpa hongera wana amini kitambi (mtumbo mkubwa) ni muonekano mzuri kiafya unaosadifu hali safi ya maisha.

Kwa huo mwili ilikuwa ni wa kumpa pole, huo sio mwili mzuri na haipendezi kujitamba kumiliki mwili wa namna hiyo.

Kwa huo mwili inawezekana kwa asilimia kubwa kuwa Chid yupo kwenye state mbaya kiafya kuliko alivyokuwa mwanzo.
Hujui ubaya wa addiction ndo maana unaleta ujuaji wa kijinga. Huo mwili ni kazi rahisi kuuondoa kuliko uraibu wa madawa ya kulevya. Karibu watu wote wanaotoka sober house hunenepa.
 
Lack of Discipline ,

Chidbenz anakosa nidhamu ya kila kitu kuanzia kula , kufanya Kazi n.k

Nidhamu means self control au kuwa na kiasi.

Nadhani watu wa karibu either hawamsaidii au yeye hawasikilizi.

Kwakuwa alibidi kuwa healed Ila hakustahili kuwa na huo Mwonekano.

Maaana kwa age yake na huo unene ni hatari anaweza kupata magonjwa kama kisukari , Pressure n.k
Punguza ujuaji wewe Dr Hayawani.
 
Hujui ubaya wa addiction ndo maana unaleta ujuaji wa kijinga. Huo mwili ni kazi rahisi kuuondoa kuliko uraibu wa madawa ya kulevya. Karibu watu wote wanaotoka sober house hunenepa.
Ni lini kitambi kikawa tiba ya uraibu?

Au tuseme, kwa mtazamo wako, kuongezeka uzito ghafla ni cheti cha afya bora?

Kusema “kitambi ni kazi rahisi kukIondoa” ni sawa na kusema “kuvaa suti ni tiba ya malaria.”

Au ni sawa na kusema “kuondoa jengo ni rahisi kuliko kuondoa tetemeko la ardhi.” Unapuuza kabisa muktadha wa kiafya, mabadiliko ya mwili, na sababu zinazopelekea unene ghafla.

Ni hoja ya kijinga inayodhihirisha ujinga wa kimfumo au mkumbo uliojengeka kwenye jamii, ambapo muonekano wa nje unapewa sana uzito kuliko viashiria vya ndani vya afya.
 
Wewe ni mtu mjinga uliyeamua kubisha kama mwehu. Fuatilia kwanza mchakato mzima wa matibabu ya watu waliokuwa mateja na side effects zake kabla ya kuja kujibu siasa za kipumbavu hapa.
 
Mi nawashangaa zaidi watu wanaompa hongera kwa huo mwili.

Wakati mimi nawaza tofauti, kwamba huwenda jamaa amepatwa na tatizo la kiafya and probably ni kisukari. Lakini watanzania wenzangu bado wanazidi kumpa hongera wana amini kitambi (mtumbo mkubwa) ni muonekano mzuri kiafya unaosadifu hali safi ya maisha.

Kwa huo mwili ilikuwa ni wa kumpa pole, huo sio mwili mzuri na haipendezi kujitamba kumiliki mwili wa namna hiyo.

Kwa huo mwili inawezekana kwa asilimia kubwa kuwa Chid yupo kwenye state mbaya kiafya kuliko alivyokuwa mwanzo.
Mmh.. ata kuongea now anaongea km mtu isee amechange kwa 25%
 
Mi nawashangaa zaidi watu wanaompa hongera kwa huo mwili.

Wakati mimi nawaza tofauti, kwamba huwenda jamaa amepatwa na tatizo la kiafya and probably ni kisukari. Lakini watanzania wenzangu bado wanazidi kumpa hongera wana amini kitambi (mtumbo mkubwa) ni muonekano mzuri kiafya unaosadifu hali safi ya maisha.

Kwa huo mwili ilikuwa ni wa kumpa pole, huo sio mwili mzuri na haipendezi kujitamba kumiliki mwili wa namna hiyo.

Kwa huo mwili inawezekana kwa asilimia kubwa kuwa Chid yupo kwenye state mbaya kiafya kuliko alivyokuwa mwanzo.
State mbaya kiafya kuliko ya mwanzo wakati anatumia sumu mazee unaijua sumu au unaisikia tu..
 
Back
Top Bottom