Hivi Chid Benz alikuwa analishwa nini huko sober?

Uko sahihi kabisa
 
State mbaya kiafya kuliko ya mwanzo wakati anatumia sumu mazee unaijua sumu au unaisikia tu..
Mazeee... sumu siyo tu ile inayoua haraka kama cyanide.

Kuna sumu zinazoua taratibu na mafuta ya tumbo ni mojawapo. Unaposema “sumu” ni mbaya kuliko “kitambi,” unadhani mwili wa binadamu ni calculator ya kujumlisha madhara?

Hebu tuweke hili jambo sawa kwa maelezo mafupi

  • Addiction ya madawa ya kulevya ni sumu ya akili, mishipa, na tabia.
  • Kitambi kisicho na muscles ni sumu ya metabolic kinachochochea kisukari, shinikizo la damu, na magonjwa ya moyo.
  • Kwa hiyo, kusema “amepona sumu” halafu kupongeza mwili unaoashiria sumu nyingine ni sawa na kutoka kwenye moto na kuruka kwenye tanuri.
 
Mmh.. ata kuongea now anaongea km mtu isee amechange kwa 25%
Sawa tunaweza kupongeza hatua za mabadiliko za kuachana na addiction ila huo mwili haiwezi kuwa sehemu ya hizo pongezi.
 
Atakuwa madhara ya madawa ya kulevya anayasikia tu hewani..
Ku overcome drug addiction ni jambo lingine, na ku maintain mwili wa kiafya ni jambo jingine.

Sikushangai kuufurahia mwili wa aina hiyo kwasababu una reflect fikra halisi za watu wengi katika jamii yetu.
 
Chid kanenepa hadi nami natamani niende huko kutengeneza shavu😂🤣😂🤣
Ni side effects ya dawa wanazotumia baada ya muda atarejea kua sawa,
Mkipata wasaa muwe mnatembelea sober houses ni moja ya charity lakini pia mtajifunza vingi
 
Nadhani,alipendelea afe kabisa.
Hoja yako inaonyesha udhaifu mkubwa wa fikra na kutokuwepo kwa tafakuri ya kina kuhusu afya ya binadamu.

Unapojaribu kupima hali ya kiafya kwa kutumia kipimo cha “kitambi vs madawa ya kulevya,” unatelezesha mantiki na kuingia kwenye logical fallacy ya false equivalence, yaani kulinganisha vitu viwili visivyolingana kwa msingi usio sahihi.

Kwasababu kama sumu ya madawa ya kulevya ni ya kiakili, kihisia na kimwili. Inaharibu mfumo wa fahamu, tabia na uwezo wa kufanya maamuzi.

Inabidi ukumbuke pia kuwa hata kitambi kisicho na miuscles (minyama uzembe kama Chid) ni sumu ya kimetabolic. Inaongeza hatari ya kisukari, shinikizo la damu na magonjwa ya moyo.

Kwa hiyo kuunga mkono kauli ya “state mbaya kiafya kuliko ya mwanzo” ni sawa na kusherehekea mtu aliyekwepa ajali ya gari kwa kuruka kwenye mto wenye mamba. Afya ni zaidi ya kuonekana ni mlingano wa kimwili, kiakili, na kitabia.
 
Ushauri wako ni upi hapo?
 
Lakini mimi nimeangalia kwa jicho tofauti, inaweza kuwa maradhi hayo. Maana kafumuka tena kwa muda mfupi tu
Yeah nami nimewaza hivi mkuu usikute ndiyo yale yale ya maradona
Good thinking...
 
Ushauri wako ni upi hapo?
Ushauri wangu unajikita kwenye kutofautisha mabadiliko ya muonekano wa mwili na hali halisi ya kiafya.

Tunapomjadili Chid Benz, ni muhimu tusibaki kwenye pongezi za nje tu, bali tuangalie kwa kina muktadha wa kiafya unaoweza kuambatana na mabadiliko hayo.
 
Umeeleza hali.Ushauri wako ni upi kwa Chidibenzino!?
 
Huo si unene wa kawaida, km ini halijaharibika basi figo…!!
 
Umeeleza hali.Ushauri wako ni upi kwa Chidibenzino!?
Ushauri wangu kwa Chid Benz ungejikita kwenye kujenga afya ya kudumu, si tu kuondoka kwenye uraibu.

Ningemshauri afanye vipimo vya damu, ini, figo na moyo. Hii ingemsaidia kugundua mapema matatizo ya metabolic yanayoweza kujificha nyuma ya unene.

Pia ningemshauri azingatie lishe yenye uwiano mzuri. Mafuta mengi na sukari kupita kiasi kwenye mlo wake ningemshauri aachane navyo Badala yake aongeze ulaji wa mbogamboga, matunda, protini safi na maji ya kutosha.

Kingine ambacho ndio cha muhimu zaidi ni kuzingatia MAZOEZI. Chid benz wa zamani alikuwa na mwili wa mbavu uliojengeka kimazoezi. Ama kweli angerudi na mwili huu ningeungana na wengi kutoa pongezi kwasababu ni mwili unaokubalika katika mizania ya kiafya.

Ushauri wa mwisho ningemwambia ajiepushe na sifa zisizo na msingi ambazo anapewa na watu kuhusu transformation ya mwili wake. Asikubali sifa zenye chembe chembe ya fikra duni ya kijamii zimpotoshe na akubali kuamini huo mwili ni mzuri kiafya.

Kukubali huko kunaweza kumjengea confidence itayomfanya azembee kuchukua hatua sahihi na mwisho kujikuta yupo kwenye abyss ya magonjwa hatari kama kisukari.

Kwa kifupi, pongezi kwa kuacha madawa ni hatua ya kwanza. Lakini afya ya kweli inahitaji kujitunza kwa consistency. Kama jamii, ni wajibu wetu kumtia moyo kwa njia sahihi kwa kumwelekeza kwenye afya endelevu, si kumshangilia kwa mabadiliko ya nje pekee.
 
Huo si unene wa kawaida, km ini halijaharibika basi figo…!!
Kuna mwamba hapa mtaani alikuwa anauza matunda, alikuwa na mwili wa wastani lakini baada ya kipindi kifupi tu akafutuka.

Nikawa namwambia ndugu yangu huo mwili sio wa kuufurahia kafanye checkup. Akawa anacheka tu kwa masihara.

Baada ya kama mwezi mmoja nikakuta kwenye ofisi yake kuna mtu mwingine, nikauliza yuko wapi jamaa (maana alikuwa ni shabiki wa Yanga namimi nilikuwa mtani wake) dogo akanijibu kuwa yupo Hospitali anaumwa kisukari.

Ilikuja kubainika kuwa jamaa alikuwa na kisukari ila alichelewa kugundua, so siku alipoona hali imekuwa mbaya alipoenda hospitali ndio akaambiwa kuwa amechelewa. Baada ya siku 4 jamaa alifariki.
 
😥 Akili za kimaskini za kujua maisha tumeyapatia kumbe ndani kuna magonjwa..!!
 
Unaweza kuwa sahihi kabisaaa. Unene mwingine yaweza kuwa hata dalili ya kufeli kwa figo
 
😥 Akili za kimaskini za kujua maisha tumeyapatia kumbe ndani kuna magonjwa..!!
Na ndio maana kuna umuhimu kuusurubu mwili kwa mazoezi maana kama kuna shida kama hizo za figo sijui nini ZITAJIBU HARAKA SANAAAAAA ,magonjwa hayapendi usumbufu kabisaa. Yatajisema mapema tuu
 
Ukimwangalia vizuri pia anaonekana dhaifu siyo yule wa kabla ya drugs

Kuna shida kwa mwamba imefichwa tu
​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…