Hivi Corona bado ipo?

Pole aise
 
Achen uoga ni hali ya kawaida pale mvua inapoanza mix tangawiz na asali na limao kunywa ni mafua makali na kichwa huuma kwa siku ila kinapona au tafuta rub
 
Huu mzigo upo mjini,
wiki iliyopita nimepigwa na mafua hayo ya hatari sana.
 
Pole mkuu..

Hizi dalili hizii zinanipa mawazo sana usikute ni mzee mzima 19
sure,
day one kifua ilinibana kama nimevaa bulletproof ilonibana hadi moyo unauma ofisini niliwork for only 2hrs, nikaenda nyumbani sio hospital tena coz one week before nilienda for checkup na sikua na tatazo lolote.

Kichwa ilipozidi na mafua huku kifua ikapoa nikaanza kukohoa sasa na homa ikalipuka mara baridi mara joto, uzalendo ukanishinda nikajongea hospital, wakanipima wakaniambia hakuna kitu inashida...

wakanipa dawa ya maji ya kifua, ya mafua na ya maumivu,
 
Hiyo ni seasonal flu, ambayo hata ukienda hospitalini utagundua watu wengi wana dalili za mafua.
 
Mie week ilopita tu niliumwa the same plus homa kali sana, nilipoenda hospital wakaniambia nna infection ya kwenye damu...na kunipa midawa kibao...

nilichofanya nikaenda kununua Azuma zangu dozi 1, tangawizi na asali. nashkuru kwa sasa nipo fresh ingawa kifua bado wakati mwengine nakohoakohoa.

Nionavyo corona haijawahi kuondoka tunaiishi nayo tushaizoea tunaona kama maradhi ya mafua na kifua tu.
 
pole sana mkuu...hizo dawa za hospital utamaliza zote mkuu vyema kuchanganya na za mitishamba. hata kama hio tangawizi, malimao, asali, manjano na kujifukiza nyungu japo ya siku tatu

mie kuna dawa flani huwa nanunua ya kuchemsha hio ukipata siku 3 tu mjarab
 
Corona ipo na inaendelea kusababisha vifo kwa wingi. Takwimu za sasa nilizopata (past two months) at least kwa Zanzibar zinatisha ila mamlaka hawataki kuzitoa. Kwa upande wa afya ya jamii (public heath code) ni makosa makubwa sana kwa mamlaka kuficha takwimu halisi kwa jamii, jamii inatakiwa ipate takwimu sahihi, na kupewa ufahamu wa kutosha nini maana ya hizo takwimu (simple interpletation), zaidi waelezwe nini cha kufanya kuepuka madhara haya. Sasa sisi tumejikita kwenye vitu tofauti; jamii ina uelewa mkubwa sana kuhusu mechi za laliga, simba na yanga, betting, new song za Diamong na Alikiba. Anyway tutafika , ila tutakuwa choka mbaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…