Hivi haiwezekani dunia nzima tukaungana tukaivamia North Korea kupitia UN na kumtoa Kim Jong Un madarakani?

Mabwana zenu USA wenyewe hawauwezi moto wake nyie makapuku mtaweza wapi
Hakuna maslahi yoyote ,USA hawaogopi nchi kama hii yenye itikadi ya mtu mmoja yaani sio ya kitaifa au kisera hivyo akifa huyo kama asipo ridhi ndungu basi na haina nguvu kiuchumi hata ukipigana na yo haiwezi sustain vita vya muda mrefu zaidi ya kuitishia marekani na korea kusini tu juzi juzi walituma mabaloon ya.mavi
 
Mkapeleke amani kama mliopeleka syria na uhuru au sio?
Hivi ulishawahi kusoma story halisi ya Marekani alichokifanya pale Korea Kaskazini?
Ushawahi kusoma Marekani alichokuwa anajaribu kufanya pale vietnam?
Waacheni Korea Kaskazini na mambo yao na nyie pambaneni na ya kwenu.
 
Itoshe kusema wewe ni miongoni wajinga wengi tulionao hapa nchini. Pambania maisha yako, okoa kizazi chako achana na ndoto za kipuuzi.
 
Mumvamie mtu ambaye anaongoza taifa lake kwa utashi wake? Are you mad! Lile ni taifa huru mwacheni afanye anachotaka kumvamia ndio kutafta majanga sababu yule kurusha nuclear hajiulizi mara mbili

North Korea sio taifa huru. Thats the whole point! Kim ndo yuko huru, wananchi wake hawapo
 

Kuna utofauti mkubwa sana kati ya TZ na North Korea.

Wale jamaa hawaruhusiwi kuangalia series za nchi nyingine, kutoka nchi nje ya nchi, kusoma vitabu, hakuna utawala wa sheria n.k

Kuna shida gani tukiwasadia hawa wananchi Milioni 26 walipo kwenye utawala dhalimu wa Kim?
 
Kaa ufahamu hakuna dola iliyowahi kudumu milele.

Huyo ataondolewa na wakorea wenyewe tu muda ukifika.

Jamaa watamchoka na vitimbi vyake watamuondoa trust me.
 
Wewe kama Mtanzania, North korea kakuathili vipi mpaka uwe na wazo la kupigananae?
 
Baba Yako amekutelekeza wewe na mama Yako. Unataka eti polisi wamkamate warudishe nyumbani. Hicho ndio umetuambia.

North Korea ni nchi huru, watu wake wanampenda Kiongozi wao na style ya maisha yao sio lazima yafanane na Yako.

Mfano rahisi ni Libya walikua na maneno kama Yako Leo Libya Iko wapi, same to Iraq.

Kwanza nani alisema lazima Kila mtu aishi kama hao wazungu wako wanavyotaka(westerners). Kumbuka Kila nchi na mfumo wake wa maisha hivyo watapata viongozi kulingana na mfumo wao.

Hivi Uingereza ni lini watapiga kura kumchgua King or Queen?
 
The Axis Of Evil. Wote hao wanatakiwa wang'olewe!
Wanatakiwa wang'olewe waliberali wakiongozwa na chama cha Democrats kwa kuanzia Kamala piga chini ,babu Biden akalelewe nyumba ya wazee ,,,maupinde wote wasafishwe
 

Kama wana raha na kiongozi kwanini kila mwaka kuna thousands of North Koreans wanaingia South Korea?

Wewe mwenyewe ukiambiwa ukakae North Korea utaweza mkuu?
 
Hilo sio jambo jema hata kidogo. Huyo na Hao wenzake ni muhimu sana kwa wao kuwepo. Hawapo kwa bahati mbaya -la hasha. Siku watakapokosekana ndo utajua umuhimu wao. Ni hayo tu.
 
Huyu na yule Khamenei wa Iran ni machizi na Putin,wangefaa kuwa eliminated by any means
Dah! Mkuu; Kwani wamekutenda nini ww hadi wastahili kuwa eliminated by any means?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…