Hivi haiwezekani dunia nzima tukaungana tukaivamia North Korea kupitia UN na kumtoa Kim Jong Un madarakani?

Hivi haiwezekani dunia nzima tukaungana tukaivamia North Korea kupitia UN na kumtoa Kim Jong Un madarakani?

Mtanzania kashindwa kuuvamia umasikini katika nchi yake, anakaa anajadili mambo ya kufikirika

Mkuu kama unataka habari za mambo ya umasikini wa watanzania unaweza kwenda kwenye jukwaa la siasa au habari na hoja mchanganyiko.

Tupo hapa kuongelea na kupashana mambo ya kimataifa kama jukwaa lisemavyo.

Sasa ulifuata nini kwenye hili jukwaa kama unajua Tanzania ina umasikini?

Na kuongelea mambo ya North Korea inaingilianaje na mambo ya uchumi wa Tanzania? Kwamba tusipoongelea mambo ya North Korea ndo umasikini utaisha Tanzania?
 
Kwa hizi akili za Kim Jong Un na namna ambavyo anahangaika kutafuta vita na the Western world ni dhahir kuwa nchi imemshinda na tusipokaa vizuri mjinga huyu atatupeleka kwenye WWIII

Kwanza Kim ndo anaongoza kwa kuwa na hostages wengi zaidi in the world kwani anaongoza watu Milioni 26 ambao hawana uhuru wa kufanya chochote.

Kim ni Psycho. Hivi kwanini UN Security Council isikae chini ikavote kumtoa huyu maniac madarakani?

Ikafanyika coup flani hivi ya kibabe ikiongozwa na Western countries ili North Korea iwe huru?

Au ipitishwe UN resolution tu kuamua kwamba dunia nzima tunaunda jeshi la kumtoa Kim madarakani?

Kama ni nyuklia hata US anazo. Nini kinasababisha tusiweze kumdhibiti huyu kiumbe?

Hizi ni baadhi ya headlines zinaoonesha jinsi Kim anavyotafuta vita ya tatu ya dunia kwa nguvu.

pole sana mtu wangu, dunia haiendeshwi hivyo, sheria za kimataifa zipo ata serikali yenu huko mumeiba kura sana lakini bado mupo madarakani na mpango wenu wa kubiba kura bado ni ule ule tu maana ndo hakuna namna
 
Hakuna China ya Xi Jinping.

Unaufahamu uhusiano wa China na NK una maslahi gani makubwa kwa China ?

Uhusiano wa China na North Korea hauna relation na tunachokizungumzia hapa.

Sisi Watanzania kuanzia mwaka 1969 mpaka 1985 tulikuwa na urafiki mkubwa na wachina.

Walitusaidia nini tulipokuwa tunapigana na nduli Iddi Amin?

If you think kwamba China will be ready to leave and forsake its economic benefit kwa sababu dunia inapigana na Kim then kuna kitu hukifahamu kuhusu China.

China is not the United States mjomba!
 
Uhusiano wa China na North Korea hauna relation na tunachokizungumzia hapa.

Sisi Watanzania kuanzia mwaka 1969 mpaka 1985 tulikuwa na urafiki mkubwa na wachina.

Walitusaidia nini tulipokuwa tunapigana na nduli Iddi Amin?

If you think kwamba China will be ready to enjoy its economic benefit kwa sababu dunia inapigana na Kim then kuna kitu hukifahamu kuhusu China.

China is not the United States mjomba!
Unafananisha uhusiano wa China na Tanzania na uhusiano wa China na Korea.

Hivi hata ramani ya China na Korea umeitazama ?

Wewe na China mna mkataba wa kulindwa pale ukivamiwa ?

Ndio maana nikakuuliza unafahamu uhusiano wa China na NK una maslahi gani makubwa kwa China ? Kushindwa kujibu kwa hili swali inaonesha kwa namna gani ulivyo ufahamu chochote.

Kasome kwanza uhusiano wa China na North Korea toka mwanzo mpaka sasa una maana gani kwa China.
 
pole sana mtu wangu, dunia haiendeshwi hivyo, sheria za kimataifa zipo ata serikali yenu huko mumeiba kura sana lakini bado mupo madarakani na mpango wenu wa kubiba kura bado ni ule ule tu maana ndo hakuna namna

Umeenda nje ya mada mkuu.

Sisi Tanzania ni tishio kwa World Peace? Je sisiemu inatuweka kwenye concetration camps kama Kim anavyofanya kwa wananchi wake?

Uhuru wakuabudu je? Lini ulisikia sisiemu imepiga mtu risasi kwa sababu mtu anataka aondoke nchini?

Kuifananisha Tanzania na North Korea unakosea sana mkuu!
 
Unafananisha uhusiano wa China na Tanzania na uhusiano wa China na Korea.

Hivi hata ramani ya China na Korea umeitazama ?

Wewe na China mna mkataba wa kulindwa pale ukivamiwa ?

Ndio maana nikakuuliza unafahamu uhusiano wa China na NK una maslahi gani makubwa kwa China ? Kushindwa kujibu kwa hili swali inaonesha kwa namna gani ulivyo ufahamu chochote.

Kasome kwanza uhusiano wa China na North Korea toka mwanzo mpaka sasa una maana gani kwa China.

Again. If you think China itakuwa tayari kukosana na dunia yote kisa North Korea huijui vizuri China.
 
Mkuu inaonekana unapenda vita,Kim anatuhusu nini,sasa nchi za kiafrika zikaungane na hao wamagharibi kumpiga kim kwa faida ya wamagharibi sis tuapate faida gan maana hata sasa tu hao wamagharibi wanatutawala
 
Marekani amezungushia fensi wananchi wake wasitoke nchini?

Marekani unauliwa kwa sababu unaamini kwenye imani fulani?

Kim inabidi aondoke and North Korea needs to be a normal nation.

I dont understand how Kim is able to put 26 million people as prisoners na bado international community inamuangalia tu
Je unadhani ni sahihi kwa Putin kuja kuipiga Marekani kwa kigezo cha kwamba anataka Kurudisha maisha yawe normal! Aondoe mambo ya Diversity and equality!?? Unadhan Urusi akisema kuwa anataka alone Marekani ikiwa na watu wasio na mental illness ni sawa!??
 
Umeenda nje ya mada mkuu.

Sisi Tanzania ni tishio kwa World Peace? Je sisiemu inatuweka kwenye concetration camps kama Kim anavyofanya kwa wananchi wake?

Uhuru wakuabudu je? Lini ulisikia sisiemu imepiga mtu risasi kwa sababu mtu anataka aondoke nchini?

Kuifananisha Tanzania na North Korea unakosea sana mkuu!
World Peace? unadhani uhalifu utafanana kutokana na mazingira?
Nyinyi si mnateka watu huko na kuwauwa na kuwatupa, mara ngap imetokea kipindi cha mkkapa si wananchi walimiminiwa risasi kutoka kwenye ndege wao wakiwa kwenye maandamano, ushenzi ni mwingi uliko huko, Kim naye anafanya on the other way .
 
Kakufanya nini wewe personaly!? Au humpendi sababu habari za kusikia! Na je umeishafika kule kwa nchi yake ukadhibitisha hayo unayoyasema?....au unataarifu ukitokea wapi!?
 
Je unadhani ni sahihi kwa Putin kuja kuipiga Marekani kwa kigezo cha kwamba anataka Kurudisha maisha yawe normal! Aondoe mambo ya Diversity and equality!?? Unadhan Urusi akisema kuwa anataka alone Marekani ikiwa na watu wasio na mental illness ni sawa!??

Hapana mkuu si sawa kwa sababu marekani hauwi watu because wanataka kuondoka nchini wala ukikutwa unaangalia filamu za North Korea nchini Marekani haupigwi risasi.

Kwa hiyo Russia hana uhalali wa kuipiga Marekani based on those premises na ndo maana nikichukua a normal person from any country atachagua kwenda Marekani kuliko North Korea.

Na ndio maana in 2021 to 2024 kuna watu Milioni 10 wameingia Marekani. Kuna watu wangapi wameenda North Korea?

Au mku unataka kusema kuua watu kwa sababu wamekutwa na Biblia au kwa sababu wanaagalia series za nchi nyingine ni value ya ku-adopt?

Nikikuletea mfumo wa Marekani na wa North Korea utachagua upi tuadopt hapa Tanzania? Mfumo upi unatesa zaidi wananchi?
 
Kakufanya nini wewe personaly!? Au humpendi sababu habari za kusikia! Na je umeishafika kule kwa nchi yake ukadhibitisha hayo unayoyasema?....au unataarifu ukitokea wapi!?

Wewe unayemtetea na kumpenda umeshafika kwenye nchi yake?

Kama haujafika kwanini unamtetea?
 
World Peace? unadhani uhalifu utafanana kutokana na mazingira?
Nyinyi si mnateka watu huko na kuwauwa na kuwatupa, mara ngap imetokea kipindi cha mkkapa si wananchi walimiminiwa risasi kutoka kwenye ndege wao wakiwa kwenye maandamano, ushenzi ni mwingi uliko huko, Kim naye anafanya on the other way .

Ukifanya hivyo Tanzania sheria zinasema unatakiwa uwajibishwe.

Nani North Korea anaweza kumuwajibisha Kim?

Kwanini unafananisha mifumo miwili tofauti mkuu
 
Umeandika upuuzi mtupu,kiss lake nini kwenda kumsaidia Putin?mbona huyo Ukraine anasaidiwa na NATO hauoni?

With boots on the ground? Lini Marekani wamepeleka wanajeshi wake wakapigane Ukraine?

Na wamefika fikaje?
 
MODS acheni ubaguzi. Huu uzi ungekuwa unaizungumzia Tanzani au nchi za EAC mngeuacha? Nakumbuka nilishakula ban kitambo kidogo kwa maudhui yanayofanana na haya kipindi cha JK. Hivyo basi huu uzi UFUTWE mara moja
 
Back
Top Bottom