Hivi hakuna kabisa uwezekano wa kuzungumza kuhusu Mungu nje ya msamiati wa kiyahudi?

unadhania haya ni masihara, kuna wenzio walikufa huku wamesimama, kutukana vitu wasivyovijua, endelea tu
 
Naomba unipe faida hapo kidogo. Hivi wayahudi wanamuelezea vipi Mungu mpaka wewe ukawaona ni bora katika jambo hilo. Ukinipa na mifano utakuwa umenisadia sana mimi na wale mfano wangu.
 
Naomba unipe faida hapo kidogo. Hivi wayahudi wanamuelezea vipi Mungu mpaka wewe ukawaona ni bora katika jambo hilo. Ukinipa na mifano utakuwa umenisadia sana mimi na wale mfano wangu.
tunasubiria jibu
 
Kumbe mmetumwa.... Ndio maana hizi thread za kumkana mungu zimekuwa nyingi. Kwa hiyo na nyinyi mliotumwa mmekuja kumtangaza mungu wenu??
 
Wazo chazo, Ama concept
Je unafikiri maana hiyo ni kamilifu ?

Dhana ni ni tamko litokanalo na kitendo "Dhania" ,kwa maana hiyo dhana ni jina lenye maana ya kutokuwa na uhakika juu ya kile unakizungumza au kufikiria,na mara nyingi humoelekea mtu katika kukosea.

Je kwa maana hiyo huoni unakosea katika matumizi ya hilo neno ?
 
Hapa nakubaliana na wewe kabisa. Mara nyingi watu wanaamini dhana ya Mungu waliyokuzwa nayo, na hawajishughulishi kutafuta ukweli zaidi.
Hivi kaka tutumie nyenzo gani au tupite njia gani ili tuupate huo ukweli ?
 
Kwanza kwa nini tumfate mungu Wa Israel wakati yeye atujui kabisaa Wa Israel awataki ata sikumoja kumsikia mtu mweusi wana tubagua vibaya mno hivi sis Wa Africa mbona atuyaoni wanao tufanyia awa watu. Papa mzungu kwa nini ajawai kuwa Mchina au muafrica.
 
Hapana, dhana ni fununu kuhusu maana, it's relative, but component and integral part of the absolute truth, Ama maana kuu, ingizo katika jumla kuu
 
kila wanachokifannya wameiga
 
Wanadamu baada ya kukosa majibu ya baadhi ya vitu ndipo wakamuumba Mungu vichwani mwao.

Ndio! Wapo wachache wanaoujua ukweli lakini wakadhamiria kabisa kutengeneza Mungu wao wa kufikirika ili waipishanishe jamii ya wengi na ukweli halisi
 
Wanadamu baada ya kukosa majibu ya baadhi ya vitu ndipo wakamuumba Mungu vichwani mwao.

Ndio! Wapo wachache wanaoujua ukweli lakini wakadhamiria kabisa kutengeneza Mungu wao wa kufikirika ili waipishanishe jamii ya wengi na ukweli halisi
Asante sana
 
Mimi siamini sana katika dini bali naamini katika MUNGU MMOJA TU MWENYE KUAMRISHA UPENDO, HAKI, WAJIBU NA HUKUMU. Ukiamini sana katika dini kunaleta utengano mkubwa sana maana waislam wanaabudu kivyao, wakristo kivyao na wayahudi kivyao lkn hizi dini tatu zina mzizi mmoja wa Ibarahim!!!

Ukiingia kwa wakristo nao wana madheheby chungu nzima, waislam pia sijui kwa wayahudi. Cha ajabu wao kwa wao utashangaa wanakufurishana mara huyu anakufuru mara yule anakufuru ili mradi kila mtu anataka kujitafutia wafuasi licha ya kuwa wote wana mzizi mmoja Ibrahim. Kwa mtu mwenye fikra huru ukisoma vitabu vyote vinavyotumiwa na dini hizo tatu utagundua Mwenyezi MUNGU hakuleta dini yoyote bali alileta mfumo wa maisha kwa ajili ya ustawi wa wanadamu duniani na baada ya mauti yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…