Umejibubwapi? Nitajuaje umejibu na si jwamba unakimbia swali tu? Unajuaje kwamba jibu lako halina makosa? Unaweza kuweka link hapa kwenye jibu lako?
Jibu langu halikuwa na makosa na halitakuwa na makosa sababu ni ukweli mtupu. Sababu siwezi kuweka kwa muda huu.
Kwa kuokoa muda ngoja nikujibu kwa ufupi. Kwanza uwepo wa Mola aliyetuumba unathibitishwa kwa hoja za kiakili yaani kwa kutumia akili (Hapa inaingia milango ya fahamu) na ushahidi wa kimaandiko (Sababu mimi ni muislamu natumia Qur'an,hadithi na kauli za waja wema walio tangulia). Hapa nafafanua kidogo,hapa ni akili ndio inatakiwa kuyatafakari maandiko.
Yaani yana anza maandiko kisha akili. Kwa ushahidi wa kimaandiko Mola wetu sisi alituambia katika Qur'an tuyaangalie maumbile ya mbingu na ardhi vyote vilivyomo humo tutapata kujua na kuamini uwepo ila watajua hilo na kuamini hilo wale wote wenye kutumia akili na kuzingatia juu ya yale yaliyomo katika ulimwengu huu.